Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,763
Waswahili wanasema kuwa ngooma ikivuma sana hupasuka. Mashindano ya Bss japo yapo kitambo sasa yameonekana hayana tija kwa upande wa washiriki ila ni mtaji kwa waandaaji. Nasema hivi kutokana na ukweli kuwa tangu haya mashindano yaanze miaka takriban 5 iliyopita hakuna bidhaa (msanii) ya kweli ambayo imeweza kuingia sokoni na kudumu japo miezi 6! Wengi huishia pale hela zao walizopewa zinapoisha.
Wapi Jumanne Iddi, wapi Misoji, wapi Leah Moudy, wapi Kassim, wapi Iddi Ramadhani. Hao nazungumzia wale washindi wa kwanza. Top ten nzima hakuna ambaye ameweza kuchomoza tangu mashindano kuanza. Kizuri zaidi ni kuwa hata Benchmark wanakiri hilo.
Matokeo yake tunashuhudia walioshindwa Bss wakikimbilia Tusker Project Fame. Hao ni pamoja na Peter Msechu, pamoja na wengine wanaoshiriki mwaka huu. Historia inaonyesha kuwa hata Project Fame nayo haina tija kwani tangu kipindi kile inafanyika South Africa, Lindiwe (mwanadada mwenye sauti kumshinda Whitney) wa Zambia aliibuka mshindi. Yuko wapi? Kulikuwa na Dare wa Nigeria mwenye sauti kama Luther Vandross. Yuko wapi?
Tusker project fame imehamia Kenya lakini nayo imeshindwa kutoa wasanii waliotegemewa kufanya vyema zaidi ya kutengeneza majina kwa usiku mmoja. Bss imeshindwa kutimiza lengo ikaamua kubadili malengo ya mashindano kwa kusema kuwa wanawawezesha vijana kujitegemea kimaisha hata kama si kupitia muziki. Ingekuwa hivyo basi ungebuniwa mradi mwingine kama ilivyo kwa Big Brother au iliyokuwa yetu ya Maisha Plus.
Kwa kiasi kikubwa hili la kujenga wasanii limeweza kutekelezwa na Tanzania House of Talents (THT). Hawavumi ila wapo sana. THT inatoa wasanii wengi wa aina tofauti lakini wa muziki ndio zaidi, na kizuri zaidi wameweza kuwepo kwenye tasnia kwa kitambo huku wakiendelea kuimarika.
Msanii kama Amini, Barnaba na Mataruma kipindi hicho nawaona kwenye Jenerali on Monday sikujua kama ndio hawa wa sasa japo walikuwa na dalili za wazi za kuonyesha kuchomoza.
Kilichonifanya kuandika haya yote ni baada ya kuona mahojiano ya msanii Rachel (aka Ray c), pamoja na kuona wimbo wake mpya videoni. Ishu si video bali mpangilio wa sauti na ubora wa sauti yake. Nikasema ninawiwa kusema chochote juu ya THT.
THT imeweza Kutoa wasanii wengi na wazuri na wanaoonekana kudumu kwenye tasnia kwa muda mrefu, tangu kina Mwasiti, Barnaba, amini, Linah, Rachel na wengine wengi. Nina hakika hawa wangepitia BSS leo hii tusingewasikia katika ramani ya muziki wetu.
Kilicchobaki ni kuanza kutafuta ni nini hasa kinachofanya hawa wanaopitia BSS washindwe kabisa kufanya vyema kwani tangu kuingia kambini hadi siku ya fainali, ni kwamba wamepikwa hadi wakapikika. Wana walimu wazuri, vifaa, wanakula vizuri, wanalala pazuri... Kwa nini washindwe kutokelezea?
Sababu ni deni walilo nalo kwa watanzania au hofu ni ile publicity wanayopata? Au sababu ni media kuwabania? BSS nao wangekuwa na radio na tv yao inawezekana wasanii wanaotokana na Bss wangepata air time ya kutosha na kuwafanya kuwika? Haya ni mambo ya kuhoji.