THT vs BSS

Mkuu kwa soko letu la "bongofleva" usiyumbe na nyimbo kuingia topten!
Laiti ukielewa yaliyofichika nyuma ya mapazia ya "ustaa wa bongo" utakubali kuwa ni mambo ya ajabu!
Nikupe kisa, wiki mbili zilizopita tukiwa mtaani jamaa akawa anampiga mziga Temba (Mh Temba) Temba akamwambia sina kitu nlkuwa na laki 5 nimewapa clouds kwaajili ya promo ya "kichwa kinauma"....
Unaona ?

Suala sio redio zingine zifanye kama clouds mkuu, hii kauli ya kufifisha mjadala utafikiri wabongo wengine mnapojadili matatizo ya rushwa anakwambia kwani we ukipewa hutakula!

Suala ni kuwa na soko imara la music lenye kuruhusu vipaji na uwezo wa waimbaji na idara zingine za music.

Mbaya sana ni kuwa matatizo mengi yanajijengea mizizi kiasi kwamba yanastawi kama ni mazoea ya kila siku hvyo hujenga tabia.

Tunapojadili tumefikaje hapo kwenye platform hzi ni namna tunaweka kumbukumbu sawa kuwa ni vipi tunaweza kutoka!

Ok, kwa mkao wa jamii yetu ambapo ni rahisi sana kubomoa kuliko kujenga wakati mwingine tiba inayobaki ni MUDA tu.
Mpaka pale wasanii watakapo nyonywa mpaka wabaki mifupa mitupu, huenda watasaidia mabadiliko kutoka ndani kabisa.

Ila kwa mpaka sasa sioni cha maana kwa hao wasanii wa THT kuwafunika wenzao wa BSS (tena tuishie hapohapo kwa BSS tuziache TPF na zingine za kimataifa)!

Unamtaja Leah Moudy mbona hujamtaja Grace Matata?
 
Utakuwa na maslahi kwenye tasnia hii ndugu yangu. Maslahi ambayo kwa namna fulani yanawekewa kiwingu na watu fulani. Huo ni mtazamo wangu. Nimeshasema sijajua yakiyoko nyuma ya pazia kama unavyofahamu wewe. nauliza, kwa nini Temba akatoe laki 5 kwa ajili ya promo? Huu ndio udhaifu ninaouzungumzia. Temba amekaa kwenye gemu kwa muda gani? TMK wana management chini ya Fella, ila sijui ina mipaka gani. kwa nini management isifanye kazi ya kutosha kuhakikisha kuwa wasanii wake wanapata kile wanachostahili? kama wanaona kuna mizengwe ni kwa nini management haiweki haya wazi?

Nasema hivi, wacha waendelee kunyonywa hadi wabaki mifupa maana wao ndio wanaruhusu haya. Kama wanamtegemea mnyonyaji wakati kuna mbadala ni nani awahurumie? Ni wapi wanayasemea haya kwa uwazi zaidi ya kulalamika chini kwa chini? tatizo lao kubwa ni kuwa hawana alimu ya kutosha! Wengi wanaoingia katika muziki ni wale wenye vipaji tu na mwisho wa siku wanakutana na vultures ambao kwa bahati mbaya hawana huruma. Kenya na Uganda wasanii wana elimu ya kutosha. wahuu kwa mfano ana shahada ya Hesabu. Utamchezea kivipi? wakati mwingine suala la kudai haki linaendana na upeo wa kielimu. Na ndio maana wengi wa bongo huishia kufanya show za ndani kwa kuwa mawasiliano ya kimataifa pamoja na network ni hafifu. Hizo nyenzo wanazo wale wanaowatumia.

Clouds Media wanatumia rasilimali walizo nazo kupata wanachohitaji, na kwa faida! Labda tatizo ni pale wanapotaka zaidi.

Taito inasema BSS na THT. Grace Matata sijajua chanzo chake kwani nimeanza kumsikia tu from nowhere, and all over sudden sijamsikia tena. Yawezekana aina ya muziki anaoimba (sijui ni jazz au Afro Pop) hauna mvuto kwa walaji, ila anajua muziki.

Ninachosema kuhusu BSS ni kuwa wasitake kubadili lengo la wao kuanzisha mashindano hayo pale wanapoona kuwa malango yao ya kuzalisha wanamuziki bora hayatimii. Kitakachotokea sasa ni washiriki nao kushiriki kikamilifu mwanzo mwisho ila malengo yao yakiwa ni kupata hela tu na kisha kurudi katika maisha yao ya kawaida. malengo yao yangekuwa yanafikiwa, washiriki wasingetoka tena na kwenda TPF. Kwangu mimi huku ni kudhalilisha mashindano ya BSS, kwamba hayana uwezo wa kuwafikisha washiriki pale wanapotaka. Tena ingefaa kwa kila anayetaka kwenda TPF wala asifikirie kupitia BSS. Hili kama hajalijua, ndio mianya ya udhaifu katika kufikia malengo husika.
 
Utakuwa na maslahi kwenye tasnia hii ndugu yangu. Maslahi ambayo kwa namna fulani yanawekewa kiwingu na watu fulani.

Huu sio mtazamo sahihi tena Mkuu wangu,
Kwamba kila mtu anayepinga ujinga fulani kwenye jambo fulani basi eti amekosa ulaji au amekoseshwa tonge!!
Ndio yale ya Mkapa kuwaambia wapinga rushwa kuwa waache wivu wa kike.... huu ni mtazamo mbaya sana Kaka.
JF tunajadili Tz tunayoitaka katika masuala yote.

Mimi nina maslahi na Music kwa ujumla, katika fuatilia yangu ya music kuna vitu naamini ni vizuri zaidi na watz wanastahili kuvijua na kupata na naamini kutokea hapo watu watapa vingi sana na kufurahia zaidi music na pia wanamusic wetu wafanye music kwa uwezo wa kipaji chao na utashi wao wote huku wakifurahia haki yao stahiki...

Mkuu wangu Raia Fulani music halisi kwa maana ya music ni mtamu sana asikwambie mtu, natamani hii segment ya utamu wa music nimkaribishe Sikonge akusimulie utamu wa music!

Nimekutajia Grace Matata kwa mfano tu Mkuu kuwa usikariri kuwa eti wanamuziki wote wa THT wana "mafanikio"...

Narudia tena kuwa sio sahihi kulazimisha mwanamuziki aimbe aina ya music asiyo na utashi nayo wala hisia eti ili awe maarufu tu hapana sababu haiwezekanai mashabiki wote wa music kupenda kila aina ya music, ndio maaana kuna aina nyingi za music kwaajili ya wapenzi wa aina nyingi!!!

Na pia ni haki ya wapenzi wote wa music za aina zote kuridhishwa na aina ya music wanayoipenda toka kwa mwanamuziki wa aina husika......

HAIWEZEKANI WATU WOTE WAIMBE BONGOFLEVA!!!!!!!!!!!!!

Kushindwa kwa aina nyingine za music ni kushindwa kwa "wadau" waliojipa uhusika wa music.....
Sababu music haiendeshwi na "wadau" bali ni wanamuziki wenyewe..
Naomba hapa ieleweke ni wanamuziki hasa,

Kwa mfano hata kwenye evolution ya music toka enzi za Disco, wasimamizi wakuu walikuwa ni Ma-DJ wenyewe, wadau wapo kwenye mazingira tu kwaajili ya ku-support na kufuata maelekezo
(ndio maana mwanzo nkakupa mfano wa biashara ya uinjinia na mainjinia)..

Hata nikitoa mfano wasasa, rais wa Deff Jam ni Jay-Z, huyo ni mwanahiphop wa hasa aliyetokea kwenye tawi la "real hardcore hiphop"...

Sijui kama point yangu imeeleweka Mkuu??

Mi najaribu kueleza tu kile ninachoona kama ni kiini cha music yetu kuwa kama ilivyo!!

Hayo ya TMK na Fella ni kichekesho tu kama kibwagizo cha habari eti management....
Wakina Temba wakashtaki wapi sasa?? Wakati huo ni utaratibu ulio"rasmi"....
Wakashtaki kwani wao hawataki ulaji kwa maana ya matamasha??

Je! hawaogopi kupotezwa kwenye soko kama yalivyowakutaga wakina Inspector Haroon na SUGU kwa kukataa kujiunga na Smooth Vibes Project??

Mimi ni mjumbe huru tu bro!
 
Mkuu yawezekana ni mjumbe huru lakini kwa staili yako ya majibu ni kuwa kuna zaidi ya mjumbe huru. Mi hoja yangu kubwa hapa ni kwa vipi kila mtu ang'ang'anie clouds media kwa ajili ya kutoka?

Suala lingine ni kuwa kama kuna aina nyingi ambazo wadau wameshindwa kuvaa uhusika, imewezekanaje clouds media kuvaa uhusika? Kama jazz haipendwi mdau atamlazimishaje mlaji kuipenda? Na kama wadau wameshindwa, wanamuziki wetu wamewezaje kuendesha tasnia yao hadi kupendwa? Hapa tunawazungumzia kina Kitime na Kinasha. Yako wapi mafanikio yao katika kuongoza tasnia yao kama si wadai kina Mawingu kufanikiwa japo kuufikisha muziki hapo ulipo?

Unazungumzia hip hop ya USA. Wale walikuwa wanaimbia maisha yao na ndio maana ikawa rahisi kwa muziki huo kuweza kukubalika. Umemzungumzia Jay z lakini hukumtaja co founder wa def jam- Russell. Unajuaje kama bila Russell Jay z angesimama? Hujamtaja Marion Suge knight. Huyu ni CEO wa Death Row. Hapa unajuaje kama Dr Dre angesimama bila Marion? Kwa hiyo ishu si mwanamuziki asimamie kazi zake bali lazima kuwepo na specialization. Kujua kuimba si kujua soko, na ndio maana 'wadau' wakawepo.

Nami nasema, haiwezekani kwa kuwa tu haiwezekani kila mmoja aimbe bongofleva, basi tuimbiwe na aina ya miziki ambayo haipenyi masikioni. Hao wanaotafuta hizo variatiea watapotezwa tu na soko! Muziki tunaoujua Tz ni dansi, taarab, gospel, mnanda, mchiriku, bongofleva...

20% yuko/alikuwa THT? Ben Pol, Diamond, ali Kiba, Prof J, Weusi... Hawa nao wako THT? ndio ujue pia kuwa kizuri kinajiuza. Nawe kwa kuijua tasnia ilivyo ni hatua zipi ulizochukua, mkuu kujaribu kuwasaidia hawa kina Temba?
 
20% yuko/alikuwa THT? Ben Pol, Diamond, ali Kiba, Prof J, Weusi... Hawa nao wako THT? ndio ujue pia kuwa kizuri kinajiuza. Nawe kwa kuijua tasnia ilivyo ni hatua zipi ulizochukua, mkuu kujaribu kuwasaidia hawa kina Temba?


Sasa hapa mbona unatoka nje ya maada yako??

BSS vs THT!!!!!

Kumbe umeona na unafahamu "mafanikio" ya msanii yanategemea sana soko lilivyo...

Kwa kuweka kumbukumbu sawa Ben Pol ni THT kaka lol!!

Sasa unasema tuimbiwe hizo aina nyingine za music halafu hapo hapo unasema wanaotafuta hizo varieties (za music) watapotezwa tu na soko....Sasa ni nini hiki??

Kweli miziki mlioizoea wabongo wengi ni hiyo uliyoitaja....

Lakini RF unaposema "bongofleva" ni aina ya music, hebu nisimulie ni music ya namna gani ki-maadhi na ladha yake?? Huo ndio mgogoro wangu tu.... Hizo aina zingine kama ulivyotaja kama Dansi, taarab, mnanda na mchiriku naziheshimu sana na wala sina tatizo nazo....
Ndio ninachotaka hicho, tuvunje hilo kapu la bongofleva ndani yake zitoke aina nyingi tu za uimbaji watu wajifunze wajenge vipaji kwenye hizo aina zifanyiwe utafiti ziwe na upigaji wake "instrumentals"..

Gospel Mkuu sio aina ya music pia, kama uansikiliza "gospel" utanielewa!
Huwezi ukasema eti fulani anaimba gospel lol only in Tz!!

Sijakuelewa unaposema US wanaimba maisha yao...!
Nilimtaja Jigga sababu tu ulikuwa ni mfano wa sasa ndio maana nilisema kwa sasa!
Nilijua tu utamtaja Russel hivyo nikakuweka kipolo lol, kwani Russel sio mwana-hiphop?? Si unakumbuka RUN DMC???
Russel ni mwanamziki Kaka oohhh sababu hajarekodi mda mrefu au sababu huzijui kazi zake kama Kinasha hahahahaha...

Suge ni mwana-hiphop pia real hustler, maisha aliyokulia na hata alipoitoa Death Row ni hiphop tosha.....
Mkuu kuwa mwanamuziki ni zaidi ya kupanda jukwaani na kushika mic au gitaa au kinanda.... ni suala la passion zaidi..!

Mi nazungumzia UKWELI tu, hata kama huo ukweli hamna anayeusikiliza au jamii nzima imekuwa ya kipuuzi...
Media ifanye kazi za media na iishie hapo...

Naona umewakomalia sana wakina Kitine na Kinasha....
Hebu waache aisee, wao ni wanamuziki na wanfanya music hata kama sio katika level unayoitamani wewe ila wanakidhi utashi wao na hadhira wanayoiimbia na wengine tunashiriki shuguli wanazozaindaa kama "Sauti za Busara" nk nk basi, Natamani next time nikupitie twende wote Zanzibar kwenye hilo Tamasha labda unaweza kuona utamu wa Music lol

Haya mawazo ninayoyaota mimi ya ku-over haul ya music industry yetu ni kitu kikubwa sana sio rahisi kama ninavyosema na wala sio suala la Kinasha afanyaje, sababu anachokifanya tu ile kusimamia misimamo yake katika music ni kitu kinachofaa sana kwa kuanzia, na sio lazima awe na ndoto kama zangu hivyo naomba usiwahukumu kabisa.

Kila mtu ana wang'ang'ania hao jamaa sababu wao ndio wamejipambanua kuwa ndio wadau wakuu wa burudani huku wakisimika mizizi hadi kwenye ngazi ya serikali kuu....

Mkuu narudia tena mimi ni mjumbe huru tu ninayetumikia music ninayoipenda na mwenye uwezo wa kuingia show ya aina ya music ninao upenda hata nikiwa peke yangu na nika-enjoy hiyo show kwa kadiri muimbaji na timu yake walivyoleta kazi yao!
 
Mkuu nashukuru kwa michango yako. Wakati mwingine kuna njia nyingi za kuuliza jambo. Ila kwa kila kilichozungumziwa hapa hakuna sehemu niliyotoka nje ya mada. Mifano si kutoka nje ya mada.

Kuhusu variaties hujanisoma. Nimesema kwa kuwa wewe unasema tuwe na variaties, kwa hiyo tuletewe hata aina zingine za muziki ambazo hazipenyi masikioni?

Sasa pamoja na kujua yote haya kuna sehemu ukusema hujui nini kifanyike. Kujua jambo si tatizo hata kidogo kwani hayo mambo ya kujua ni suala tu la kutafuta hizo taarifa, pamoja na kuwa na fursa ya kuishi mazingira ya kile unachokijua kwa undani. Suala hapa ni kujua namna ya kutatua haya ili mwisho wa siku mambo yakae sawa na tuwe na kina Mawingu wengi na mwisho wa siku pawepo na ushindani. mathlani mimi sasa nimejipanga kuingia rasmi katika tasnia ya filamu. najua kuna changamoto nyingi huko lakini ukijua namna ya kuogelea maji hayakusumbui.

Kadhalika sitaweza kuacha kuzungumzia kuhusu hawa wanaoitwa 'magwiji' kwa kuwa jamii haitambui ugwiji wao uo wapi hasa. Utasema mimi pekee ndio sijui wanachofanya.

Sauti za busara, Ziff vyote hivi vinafanyikia huko. Ingekuwa ni fursa kwa hawa 'magwiji' nao kuonyesha michango yao dhahiri ili tujue kuwa kuna kazi wanaifanya na ambayo inaonekana. Sasa kuitwa kushiriki bado sijashawishika kukubali kuwa mchango wake umetosheleza. Kadhalika nimetazama achievements za sauti za busara tangu 2003 to date sijaona popote uhusika wa Kitime. Sanasana naona Bi kidude. mchango wake uko wapi katika muziki a Tanzania? hawa ndio tulitaka sasa tuwategemee.

Tuzungumzie sasa suluhu ya haya yanayoendelea maana matatizo yanajulikana ila suluhu ndio kizungumkuti.
 
Na katika kile kinachoonekana kukubali matokeo, sasa BSS itaitwa e(epiq)BSS. Nayo inaunganisha nguvu na clouds media maana nimesikia jingle ya 'Fungua njia' ikipigwa clouds fm. Na tusishangae kuona eBSS ikirushwa pia kupitia clouds tv. Hapa ndipo tunaanza kuamini kuwa kuna watu wenye nguvu kwenye hizi media, na kama unashindwa kupambana nao ungana nao... jouneGwalu unasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaha lol........

Tunatofautiana sana katika kuangalia haya mambo......

Muda ndio mganga wa kweli amabye hajawahi kushindwa.......

Nimepitia mengi sana Mkuu kwenye haya mambo ya music na wala sijawahi kuyumba kimsimamo hata watz wote mkiwa Clouds na mkihubiri injiri yao...........

Hawanitishi hata chembe.

Mitaa itaelewa tu!
 
Let me tell you one thing very serious. I am very sceptical to the whole issue that other media give in to pave a way in to this monopoly. I am ironically speaking that as far as they have failed to contain themselves and take their chances, let Mawingu have the industrial's lion's share! In the long run you will come to concur with me that I am objectively speaking on the issue at hand.

My concern is WHY Benchmark allied with Mawingu on its mission? With Zantel I have no problem. They are sopnsors. But why with cloud? So in the mean time, ironically speaking, you will agree with me that the Mawingu guys are playing it rough and tough. And Iam telling you, this season's eBSS winner shall make it!

Lakini bado hunielewi! Nini kifanyike tuondoe hii monopoly?
 
Let me tell you one thing very serious. I am very sceptical to the whole issue that other media give in to pave a way in to this monopoly. I am ironically speaking that as far as they have failed to contain themselves and take their chances, let Mawingu have the industrial's lion's share! In the long run you will come to concur with me that I am objectively speaking on the issue at hand.

My concern is WHY Benchmark allied with Mawingu on its mission? With Zantel I have no problem. They are sopnsors. But why with cloud? So in the mean time, ironically speaking, you will agree with me that the Mawingu guys are playing it rough and tough.
And Iam telling you, this season's eBSS winner shall make it!

Lakini bado hunielewi! Nini kifanyike tuondoe hii monopoly?


Hapo kwenye
bold underlined red

Haki ya Mungu tutaona......
Ntaingia kwenye sala maalum ya kuomba uzima kwa ajili ya kushudia hilo lol.....

Mkuu wangu Raia Fulani...

Sina cha kukuambia eti tufanye moja mbili tatu ndio ujue hiki ndio kifanyike......

Anayefanya ukweli afanye ukweli, na anayeuongopea umma azidi kudanganya....

Nafanya kinachonipasa kufanya.... tunajenga empire mbili za ki-music ya ukweli itadumu mpaka mwisho ya uongo itaanguka....

Sio suala la nini kifanyike, tayari kuna kitu kinafanyika sema sio katika mfumo mliouzoea wa "wajanja wa clouds" hivyo bahati mbaya sana hampati taarifa ila Dunia inajua kinachoendelea.

Na show inaendelea Africa nzima.....!

Ok tuachane na haya, hebu na wewe niambie vipi juzi ulienda ubalozi wa Ufaransa kwenye "european Film Festival"

Kwenye filamu nawaonea wivu sana!!

 
Last edited by a moderator:
ulidanganya kuwa wewe si mdau wa muziki. Sasa naona kile nilichohisi. Sikukosea. Hicho kinachofanyika kuzunguka dunia juu ya muziki wa kitanzania huku watanzania hawafahamu ni kipi? Msije mkatuletea tu utamaduni mpya.

Kuhusu hiyo festival kiukweli nimeisikia ila hiyo ni kwa ajili ya wazungu waishio nje ya bara lao hivyo wakapate fleva ya kile walichokosa. Hata hivyo si vibaya kuhudhuria kwani kuna mengi ya kujifunza, hasa namna ya uchukuaji wa picha, n.k.

Na hiyo kusema unaona wivu unamaanisha nini? Maana nachelea kukubaliana na wewe kama kweli unaona wivu wa dhati. Filamu bongo ni potential opportunity kwa anayejua nini maana ya kuwekeza katika filamu. Kama utakuwa interested let's team together to formalize this sector.

Kwa sasa bado kuna mengi ya kufanya kuondoa magugu yanayoziba uhalisia wa tasnia yenyewe. Haina tofauti na muziki japo msanii wa filamu anaonekana kunufaika zaidi
 
Mkuu RF achaga mauoga na wewe....

Kuna watu kama wakina Awadi, N'ndou, 'Tuku, Wainaina, Massamba nk nk nk hao ni waafrika wanaofanya music katika mahadhi ya ki-africa yaliyotukuka.... Na wanazunguka dunia...

Hivyo niliposema kuzunguka dunia usidhani kuna jipya sana!

Kwenye Music kuna kazi ngumu sana, maranyingi huwa nachanganyikiwa kabisa.....

Ila uzuri wangu mi ni mlevi wa sanaa kwa ujumla hivyo music ikinidatisha filamu zinaniliwaza....

Pia sikuweza kwenda kwenye lile Tamasha nilichelewa kupata mualiko

Ila nilipata taarifa ya nini kilitokea pande ile....

Kuna vingi vya kujifunza kwa jamaa zetu wale...

Ok, ahsante kwa mualiko
 
soon nitakualika kwenye filamu. Kuna baadhi ya mambo naweka sawa kwanza
 
nimeufatilia mjadala wenu...hapa kulikuwa na pande mbili 1.wale wasiofahamu chochote kuhusu hali halisi ya soko la muziki wetu.
2.wale wanaofahamu hali halisi ya soko la muziki wetu,na wanatamani kila mmoja aione picha halisi na kusapot changes.
Gwalu yupo kundi la pili..

Siku moja nilikuwa pande flani nikakutana na Doto(wa Mapacha) tukawa tunaongea izi ishu za soko letu la muziki kwa kweli hali inazidi kuwa mbaya,hawa jamaa wa Mawingu wanavuka mipaka sasa,wanatia hasira sana....ila nilimwambia kitu kimoja D alicheka sana,nilimwambia nyie mnavyowakomalia hawa machoko kuna watu wanawaona kama machizi uko mtaani.
 
nimeufatilia mjadala wenu...hapa kulikuwa na pande mbili 1.wale wasiofahamu chochote kuhusu hali halisi ya soko la muziki wetu.
2.wale wanaofahamu hali halisi ya soko la muziki wetu,na wanatamani kila mmoja aione picha halisi na kusapot changes.
Gwalu yupo kundi la pili..

Siku moja nilikuwa pande flani nikakutana na Doto(wa Mapacha) tukawa tunaongea izi ishu za soko letu la muziki kwa kweli hali inazidi kuwa mbaya,hawa jamaa wa Mawingu wanavuka mipaka sasa,wanatia hasira sana....ila nilimwambia kitu kimoja D alicheka sana,nilimwambia nyie mnavyowakomalia hawa machoko kuna watu wanawaona kama machizi uko mtaani.


Poa Mkuu wangu ma2mbo...!!

Ila kunakitu wabongo wengi hawakioni, hao jamaa mawingu wala sio wa kuwahofia kabisa, kwanza miradi yao mingi sio ya mda mrefu na kwa kudhibitisha hilo hebu waulize mashabiki wao ule mchezo wa "uzinduzi" wa album umeishia wapi??

Ulienda kwa kasi mwishowe ukaangukia mbali huko, walianza na uzinduzi wa diamond jubilee bongofleva ilipozidi kuwa bubble gum zinduzi zikahamia bilcanas bongofleva ilipozidi kupoteza radha kabisa zinduzi zikahamia mikoani....
Hali imekuwa mbaya kabisa sasahivi ndio hamna kabisa cha uzinduzi wala wanabongofleva sijui kama wanafanya album, sasa kama hamna ufanyaji wa album kuna muziki hapo??

Watanitajia Diamond...... well kazindua.... then??

Jamaa wamebakiwa na matamasha mepesi na siasa za redioni perepeche kibaooo!!!
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati nakasirika pale ninapoona kuwa kuna watu wanatukanwa bila ya wale wanaotukana kuwa na sababu ya msingi ya kufanya hivyo ikiwa wana nyenzo muhimu za kuweza kuwa sawa na wanaotukanwa. Clouds nawasifia kwa machungu ili wanaotukana nao wakasirike wapate akili ya kuondokana na matusi waanze nao ushindani wa kimantiki na si wa mipasho. Kama ni mipasho, wale jamaa wako full. Ishu hapa ni kuwa na sekta katika soko huria ambazo zina wadau wanaojua nini cha kufanya. We are not talking about invisible hands hapa kama Gwalu unavyotaka tuamini, kwamba kuna mambo yanafanyika. Where?

Mnasema yale waliyoanzisha yanakufa. Yako wapi mliyoanzisha yakadumu? Kama malengo yao yalitimia wana haja gani tena ya kuumiza vichwa? Kama kweli kuna watu wana uchungu na muziki hakuna sababu ya kulia na sijui Basata. Sekta binafsi zinaweza kusimama zenyewe na ndio maaana kuna vitu kama PPP-Public Private Partnership. Hii ni kwenye sekta zote. Sio muda wa kulia na watu fulani. Kwa nini kama mtu unalijua vyema soko la muziki unashindwa kufanya jambo?

Gwalu, man and the fellas, you know very well about the industry. Stop crying because your tears are of a fish. Just stand and do something as they do, or otherwise you better accept a defeat
 
nimeufatilia mjadala wenu...hapa kulikuwa na pande mbili 1.wale wasiofahamu chochote kuhusu hali halisi ya soko la muziki wetu.
2.wale wanaofahamu hali halisi ya soko la muziki wetu,na wanatamani kila mmoja aione picha halisi na kusapot changes.
Gwalu yupo kundi la pili..

Siku moja nilikuwa pande flani nikakutana na Doto(wa Mapacha) tukawa tunaongea izi ishu za soko letu la muziki kwa kweli hali inazidi kuwa mbaya,hawa jamaa wa Mawingu wanavuka mipaka sasa,wanatia hasira sana....ila nilimwambia kitu kimoja D alicheka sana,nilimwambia nyie mnavyowakomalia hawa machoko kuna watu wanawaona kama machizi uko mtaani.

Kutukana sio suluhu. Utatukana na mwisho utakufa kwa stress na utaonekana mwehu tu. Ni machizi hadi Benchmark wameamua kujiunga nao kufanya kazi. Ni machizi hadi wanakuwa na ukaribu na Rais. Ni machizi hadi wanateka soko la muziki nchini. Hao wasanii watabaki kulia tu wakati wenzao wanachanja mbuga. Weusi wanatokea wapi? Na hao mapacha wanatokea wapi? Kama huna ladha nani atakukubali, ndugu? Au hao jamaa walitaka kujifananisha na P square? Endelea kufuatilia mjadala, kaka
 
Weusi wanatokea wapi? Na hao mapacha wanatokea wapi? Kama huna ladha nani atakukubali, ndugu? Au hao jamaa walitaka kujifananisha na P square? Endelea kufuatilia mjadala, kaka

kwenye maisha ya kawaida(kipato)huwezi kuwafananisha Mapacha na Weusi,usidanganywe na promo...Weusi ni moja ya wasanii maskini kabisa hapa bongo,Mapacha ni wajasiriamali na wanaharakati...wasanii wote wa Arusha ikiwemo Weusi wakija Dsm wamepitia kwenye malezi ya Mapacha,kuanzia kula mpaka kulala wakati wanaangaikia kutoka...nini faida ya muziki kama una jina kubwa lakini maskini?

Bado nafatilia mjadala,japo naona unaongea vitu ambavyo vya kufikilika sana...na nakuakikishia hii Empire soon itaanguka,watu wanadeal nao kisayansi sana sasa ivi.
 
kwenye maisha ya kawaida(kipato)huwezi kuwafananisha Mapacha na Weusi,usidanganywe na promo...Weusi ni moja ya wasanii maskini kabisa hapa bongo,Mapacha ni wajasiriamali na wanaharakati...wasanii wote wa Arusha ikiwemo Weusi wakija Dsm wamepitia kwenye malezi ya Mapacha,kuanzia kula mpaka kulala wakati wanaangaikia kutoka...nini faida ya muziki kama una jina kubwa lakini maskini?

Bado nafatilia mjadala,japo naona unaongea vitu ambavyo vya kufikilika sana...na nakuakikishia hii Empire soon itaanguka,watu wanadeal nao kisayansi sana sasa ivi.

Hata ulimwengu uliumbwa kwa fikra ndugu. Na yawezekana hao wanaolalamikia muziki hawafikiri. Sasa, hao mapacha waliwabeba weusi kwa kipato kilichotokana na nini? Kama ni muziki mbona leo waanze kulia? Kama ni ishu zingine kwa nini leo walilie muziki? Sijui kama huwa unapata muda wa kujiuliza haya.

Kadhalika haimaanishi kuwa kila afanyaye kazi serikalini kipato chake kinamtosha. Hivyo haimaanishi kuwa kila afanyaye muziki basi aendeshe benzi, maana ndivyo unavyotaka tuamini.

Kingine ninachokiona hapa ni suala la kufuata mkumbo kwa hawa wasanii. Kisa tu fulani kaimba basi nami naweza. Ukiacha hilo kuna suala la kudhani muziki ni kimbilio baada ya kukosa kwingine, hasa kutokana na kukimbia umande. Bangi na malengo wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom