Thread Maalumu Ya Kufichua Maeneo Yenye Njaa Na Kipindupindu (weka na ushahidi kama upo)

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Kuna tetesi kuwa viongozi wa wilaya na mikoa wanaficha taarifa za baa la njaa na kipindupindu ktk maeneo yao. Ndiyo maana kwa mfano, rais kwa ujasiri mkubwa anapinga kwa nguvu zake zote juu ya uwepo wa baa la njaa.

Kwa kuwa nchi hii ni yetu sote, basi tumsaidie mhe rais kumjulisha kupitia jukwaa hili juu ya uwepo wa mabalaa haya mawili kwa kuyataja maeneo husika. Na kama utakuwa na ushahidi wa picha, sauti, maandishi ama video tuwekee hapa.

KARIBUNI
 
Mkuu huu uzi ni wa watz wote, kama eneo lako na langu hakuna mabalaa haya basi tuwape nafasi wale ambao wako kwenye maeneo yenye shida hizo.

Ndiyo maana ya uzi huu mkuu Uta Uta.
 
Ndg Kirchoff, kama mahindi ni sh 500 kwa kisado haimaanishi kuna njaa. inaweza kuwa ni ongezeko la bei ya mazao tu. njaa ni ukosefu wa chakula na siyo kupanda kwa bei.
 
Ndg Kirchoff, kama mahindi ni sh 500 kwa kisado haimaanishi kuna njaa. inaweza kuwa ni ongezeko la bei ya mazao tu. njaa ni ukosefu wa chakula na siyo kupanda kwa bei.
Ongezeko LA bei linatokana na nini mkuu?
Ndo njaa yenyewe iyo.
 
Wale jamaa kule Dodoma walikuwa wanashindia viwavi na zambarau,kule Musoma walishindia kumbikumbi,hatujasikia hayo mwaka huu.
 
Back
Top Bottom