Thomas Muller, Raumdeuter wasamehe hawakujui

Nabii kibonge

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
277
308
Kiufupi mimi ni mfuatiliaji wa ligi mbalimbali tofauti na wadau wengi ambao kwao EPL ndio ligi. Na huwa wanazi-refer hizi ligi nyingine kama ligi za wakulima na hazina ushindani na sishangai wakisema hivyo.

Watakwambia hizo ligi hazina wachezaji wa kutisha na wenye changamoto lakini mda huo huo utasikia wanamsifia mchezaji kama Lingard, hao hao watakwambia Trent Alexander anatisha kuliko Cafu, watakwambia ndiye beki bora wapembeni duniani kwa sasa. Achana na hayo.

Thomas Muller, wajerumani wanamwita Raumdeuter huku wakimaanisha 'space intepreter' jina ambalo linatokana na uchezaji wake. Sio mtu wa kudrible sana kama unavyomwona Neymar, pia sio mtu anayehitaji akuonyeshe skills kama Marseile Turn ndio ujue ni hatari, lakini uwezo wake mkubwa wa kuusoma mchezo na good positioning ndio silaha kubwa ya mwanajeshi huyu wa Kijerumani

Kiufupi tu Thomas Muller akiwa na miaka 20 tu alimaliza na goli 5 world cup 2010. 2014 akamaliza na goli 5 tena. Nilikuwa natarajia angevunja record ya Miroslav Klose na kumpiku Ronaldo de Lima kwa magoli mengi ya World cup lakini imeshindikana 2018 na kwa hili namlaumu 100% Pep Guardiola

Siku zote katika kutafuta mrithi wa kocha aliyedumu kwa kipindi huku akiwa na mafanikio huwa ni shida kidogo, rejea hata David Moyes baada ya kibabu Fegi. Bayern waliingia kwenye dimbwi hilo hilo ni wazi Pep alikuwa anashinda mechi nyingi na winning rate kubwa tu maana alishinda mechi 22 katika 27 za mwanzo ila bila kuficha Pep alikuwa anaharibu soka natural la wajerumani

Tactics za Pep zinahusisha pasi nyingi na ndio maana alivyotua Bayern akaanza kuwanufaisha viungo wake kina Thiago Alcantara. Ni wazi soka la kijerumani la piga nikupe zile counter attacks, soka la kumfanya mpinzani mda wote awe na mashaka chini ya collabo ya Robben na Ribery lilipotea na hapo ndipo kiwango cha Thomas Muller kilianza kudorora na si Muller pekee, wapo wachezaji wengi tu

Kiujumla Thomas Muller ametwaa Uefa champions League, ametwaa World cup na ubingwa wa Bundesliga mara 9 na amehusika katika kutengeneza magoli 141 huku akifunga 162 kwa ngazi ya club na kwa national team kahusika kutengeneza mabao 54 katika timu ya taifa.

Kilichonisikitiaha zaidi ni kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyu hadi kuhusishwa na kuondoka katika kalbu hiyo. Lakini ujio wa kocha Hans Flick ambaye ninaamini ndiye mrithi wa Jupp Hynckess, Thomas Muller amerudi kwenye ubora wake na sasa ndiye Raumdeuter wa kweli

Msimu huu tu Thomas Muller ametoa assist 21 na kufunga mabao 8 huku akichangia zaidi ya 30+% ya magoli ya Lewandowiski aliyemaliza na mabao 31 bado Thomas Muller atakuoffer vitu mbali mbali ikiwemo defending kutokana na uwezo kwa kupora mipira akiwa eneo la mbele nadhani hata KDB hagusi hapa ila KDB anachomzidi muller ni uwezo wa kUtengeneza nafasi nyingi na kufunga magoli mengi lakin Thomas Muller ni mzuri katika kudefend pia.

Katika mafanikio ya sasa ya Bayern ni wazi utakuwa mchawi usipomtaja Thomas Muller lakini yote haya hayaonekani. Bayern anaonnekana tu Lewandowski na Gnabry huku wakisahau mtu wa muhimu Thomas Muller.

Ni wazi chini ya Hans Flick ambaye ameshinda mechi 27 kati ya 29 za mwanzo timu imeimarika na sasa naiona Bayern mpya inarudi chini ya usimamizi wa mwamba Oliver Khan

Bahati mbaya kwako Muller unacheza mpira katika zama za mpira ambazo watu wanaabudu maneno na ushabiki tu kwani anayeonekana anacheza mpira ni Bruno Fernandes, Greenwod, Alexander Anold na wajinga wenzao kina Dele Ali lakini Ujerumani wala Italia hamna mpira. Naamini hata Zlatan ambaye ameenda AC Milan dirisha dogo na katika mechi 18 ana magoli 10 na assist 6 huku akiwa ameanza mechi 16 tu ingekuwa England wangempa na uchezaji bora kabisa wa ligi.
 
Haina shida mkuu ww ndiye mwenye maandiko yenye point tupu

Nani umewahi kumsikia anatamka kwamba Lingard ni mchezaji bora?

Kuna mahali umeandika eti kuna watu wanasema TAA ni bora kuliko Cafu! Unaweza kuthibitisha?

Halafu watu wanakwambia ligi haina ushindani hutaki kukubali, for the last 10 years Bayern kachukua mara 8, Dortmund mara 2. Ushindani uko wapi?

Unakuja na mfano wa ligi ya Italy, for the last 10 years Juve kashinda Seria A mara 9, hapo kuna ushindani? Au ushindani maana yake ni nini?
 
Mkuu kumbe ndio point yako hio, em sema ukweli ligi yenye ushindani ndio mancity angemaliza na point 100????

Ni kwel bayern anachukua mar 9 mfululizo sawa na juve tu lakini unaona ushindani wanaoupata

Chukulia juve tu msim huu alivyoteswa na kina Lazio, Juve kadraw na Lecce tim inashka umwisho, kafungwa na Cagliari team ipo below top ten unataka ushindani upi mkuu?

Tunajua bayern alivyosumbuliwa na Frankfurt au Leverkusen. LIVER katangazwa bingwa bado mechi ngapi mkuu?? Msimu huu bayern katangazawa bingwa bado mechi mbili na uliona mwanzoni mwa msimu alivyoburuzwa

Mbona husemi katika miaka 10 man u alichukua ligi mara 7??? 1992-1999

Haya hizo timu zako zenye ushindani mbona zimeenda mashindano makubwa kama UEFA na bado zikawaprove wrong watu
 
Nani umewahi kumsikia anatamka kwamba Lingard ni mchezaji bora?

Kuna mahali umeandika eti kuna watu wanasema TAA ni bora kuliko Cafu! Unaweza kuthibitisha?

Halafu watu wanakwambia ligi haina ushindani hutaki kukubali, for the last 10 years Bayern kachukua mara 8, Dortmund mara 2. Ushindani uko wapi?

Unakuja na mfano wa ligi ya Italy, for the last 10 years Juve kashinda Seria A mara 9, hapo kuna ushindani? Au ushindani maana yake ni nini?
Kuhusu Lingard na TAA maneno yapo mengi tu toka kwa mashabiki na baadhi ya wachambuzi kama unapitia soçia networks utaona tu mkuu
 
Mbona husemi katika miaka 10 man u alichukua ligi mara 7??? 1992-1999

Tunazungumzia current issues bro, hiyo Italy tuloyoiweka hapo, miaka hiyo ilikuwa ni ligi ngumu, ushindani wa kutosha kutoka AC Milan, Inter Milan, Juventus na wengineo.

Swala la City kupata points 100 au Liverpool kuchukua ubingwa ikiwa imebaki game 7 ni swala la mara moja kwa kipindi, ndiyo maana kwa zaidi ya miaka 100 hilo limetokea mara moja tu, ndiyo maana ya record.

Nazungumzia Juve kuchukua mara 9 na Bayern mara 8 ndani ya misimu 10 ya hivi karibuni, hata kama ni kwa gap la points chache, huo ndiyo ushindani?

Msimu unaanza tayari unajua bingwa ni nani, huo siyo ushindani.

EPL leo ukiambiwa umtaje bingwa wa msimu ujao hutapatia, ila nina uhakika Juve na Bayern ni mabingwa msimu ujao.

Haya hizo timu zako zenye ushindani mbona zimeenda mashindano makubwa kama UEFA na bado zikawaprove wrong watu

For the last 10 years, Juve na Bayern (Seria A na Bundesliga) wamechukua UEFA ngapi?

EPL wamechukua UEFA ngapi?
 
Kuhusu Lingard na TAA maneno yapo mengi tu toka kwa mashabiki na baadhi ya wachambuzi kama unapitia soçia networks utaona tu mkuu

Unaweza kuweka ushahidi?

Nakushauri kitu bro, flow yako ya uandishi ni nzuri, lakini ili andiko lako livutie, jaribu kuweka mifano ambayo ni relevant.

Acha uandishi wa kizembe wa kina Edo Kumwembe, kwamba ili usifie kitu fulani ni lazima uponde kingine.

Unaweza kufikisha ujumbe vizuri sana kumuhusu Thomas Muller bila kuiponda EPL (tena kwa kumtaja Lingard), unaweza kumsifu Muller bila kumponda KDB na bado ukaeleweka.
 
Tunazungumzia current issues bro, hiyo Italy tuloyoiweka hapo, miaka hiyo ilikuwa ni ligi ngumu, ushindani wa kutosha kutoka AC Milan, Inter Milan, Juventus na wengineo.

Swala la City kupata points 100 au Liverpool kuchukua ubingwa ikiwa imebaki game 7 ni swala la mara moja kwa kipindi, ndiyo maana kwa zaidi ya miaka 100 hilo limetokea mara moja tu, ndiyo maana ya record.

Nazungumzia Juve kuchukua mara 9 na Bayern mara 8 ndani ya misimu 10 ya hivi karibuni, hata kama ni kwa gap la points chache, huo ndiyo ushindani?

Msimu unaanza tayari unajua bingwa ni nani, huo siyo ushindani.

EPL leo ukiambiwa umtaje bingwa wa msimu ujao hutapatia, ila nina uhakika Juve na Bayern ni mabingwa msimu ujao.For the last 10 years, Juve na Bayern (Seria A na Bundesliga) wamechukua UEFA ngapi?

EPL wamechukua UEFA ngapi?
Mkuu haijalishi wanachukua mara ngapi lakini hakuna ushindani??? Pia mwisho wa siku lazima tukubali bayern na juventus wana best teams kufananisha na team nyingine za ligi na hii inatokana na investment

Mkuu mbona madrid kabeba uefa mara 3 mfululizo je UEFA Na tim za ulaya kiujumla hazina ushindani au??????
 
Tunazungumzia current issues bro, hiyo Italy tuloyoiweka hapo, miaka hiyo ilikuwa ni ligi ngumu, ushindani wa kutosha kutoka AC Milan, Inter Milan, Juventus na wengineo.

Swala la City kupata points 100 au Liverpool kuchukua ubingwa ikiwa imebaki game 7 ni swala la mara moja kwa kipindi, ndiyo maana kwa zaidi ya miaka 100 hilo limetokea mara moja tu, ndiyo maana ya record.

Nazungumzia Juve kuchukua mara 9 na Bayern mara 8 ndani ya misimu 10 ya hivi karibuni, hata kama ni kwa gap la points chache, huo ndiyo ushindani?

Msimu unaanza tayari unajua bingwa ni nani, huo siyo ushindani.

EPL leo ukiambiwa umtaje bingwa wa msimu ujao hutapatia, ila nina uhakika Juve na Bayern ni mabingwa msimu ujao.For the last 10 years, Juve na Bayern (Seria A na Bundesliga) wamechukua UEFA ngapi?

EPL wamechukua UEFA ngapi?
Kuhusu UEFA mkuu unajua jinsi spain walivyodominate kwahiyo vp tuseme na EPL nayo ni farmers league au maaana madrid ana 4 barca ana 2 bayern 1 chelsea 1 na Liver 1 na inter 1 na hapo ukicheki uamtaona Epl na bundesliga na serie A bado level ile ile vp kwa hilo mkuu?
 
Mkuu haijalishi wanachukua mara ngapi lakini hakuna ushindani??? Pia mwisho wa siku lazima tukubali bayern na juventus wana best teams kufananisha na team nyingine za ligi na hii inatokana na investment

Mkuu mbona madrid kabena uefa mara 3 mfululizo je UEFA Na tim za ulaya kiujumla hazina ushindani au??????

Bayern na Juventus ni kweli wamefanya in investments. Kwa nini ligi nzima timu 1 tu ndiyo ifanye investment?

3 na 8/9 ni sawa?
 
Unaweza kuweka ushahidi?

Nakushauri kitu bro, flow yako ya uandishi ni nzuri, lakini ili andiko lako livutie, jaribu kuweka mifano ambayo ni relevant.

Acha uandishi wa kizembe wa kina Edo Kumwembe, kwamba ili usifie kitu fulani ni lazima uponde kingine.

Unaweza kufikisha ujumbe vizuri sana kumuhusu Thomas Muller bila kuiponda EPL (tena kwa kumtaja Lingard), unaweza kumsifu Muller bila kumponda KDB na bado ukaeleweka.
Sijui unataka relevance ipi??? Af pia uandishi kwa kufanya comparison sion kama kuna dhambi au violation yoyote ya principle za ushahidi
Pia ndio maana nlisema ukipita kwenye socia media utaligundua hilo toka kwa fans mbali mbali l
 
Bayern na Juventus ni kweli wamefanya in investments. Kwa nini ligi nzima timu 1 tu ndiyo ifanye investment?

3 na 8/9 ni sawa?
Kwa mashindano makubwa kama UEFA ambayo timu bora ulaya zinakutana unaona timu kuchukua mara 3 mfululizo unaona ni kawaida?
 
Kuhusu UEFA mkuu unajua jinsi spain walivyodominate kwahiyo vp tuseme na EPL nayo ni farmers league au maaana madrid ana 4 barca ana 2 bayern 1 chelsea 1 na Liver 1 na inter 1 na hapo ukicheki uamtaona Epl na bundesliga na serie A bado level ile ile vp kwa hilo mkuu?

Ukiamua kuiita hivyo inabidi uweke vigezo.

Hizo ligi za Ujerumani na Italy zimeitwa hivyo kwa sababu ni 1 horse race leagues.

Sasa kama EPL utaiita farmers league unatakiwa kuja na sababu.
 
Back
Top Bottom