secret file
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 5,839
- 8,652
Sasa ingia nyanjani ujionee!Salute kwenu mabibi na mabwana.
Mafanikio makubwa huja kwa ku-take risk kubwa vilevile. Ukikosa unakosa kweli unaweza usirudie tena lakini mzigo ukitiki unatoboa kweli kweli.
Sasa mpango mzima nimeshau-draft kila kitu hadi soko la mafuta ya alizeti nitakayokamua. Kilichobaki ni kusubiri mwezi wa kumi na mbili niingie site nikapambane.
Nimepanga kulima ekari 40 za alizeti mkoani singida. Ardhi ninayomiliki hadi sasa ni ekari 10 tu ila nipo kwenye hatua za mwisho kukodi ekari 30 ili zifike 40. Nitalima alizeti zote.
Michakato mingine kama trekta la kulimia inaenda vizuri na muda sio mrefu inakamilika.
Kuna mbegu moja ya alizeti inaitwa Hysun 33. Hii mbegu balaa lake sio la nchi hii. Inasemekana kwa ekari moja inaweza kutoa gunia 15-18 za alizeti za kilo mia mia. Inasemekana inavumilia hali zote za ukame na mvua nyingi, magonjwa n.k. Ni mbegu bora sana naona hata serikali ya mkoa imeipitisha rasmi which means huenda ipo vizuri. Bei yake kwa kilo ni 35000/=.
Nimepiga hesabu zangu za kilimo cha mtandaoni au kwenye makaratasi. Kwa ekari 40 nitaweza kupata gunia 400 (nimeassume ekari moja itatoa gunia 10 badala ya gunia 15 walizosema wataalam).
Kwa hizo gunia 400 nitakamua mafuta ya alizeti ambapo sasa watalaam wa mbegu ya Hysun 33 wamesema uhakika ni kupata dumu 2 za mafuta ya alizeti kwa kila gunia. Mimi nita-lower expectation zangu nipate average ya dumu moja kwa gunia moja). Hapo nitazungumzia habari ya kupata dumu 400 za mafuta.
Nitauza mafuta kwa bei ya 50,000/= kwa dumu moja la lita 20. Hapo nitapata 20M. Calculation zangu zinaonyesha kuwa running cost zote zitanigharimu 5M). Hapo nategemea net profit ya 15M.
Sina shaka na mahesabu yangu yote hapo juu. Hapo nimeweka minimum value sana ukilinganisha na maelekezo ya wataalam na wazee wa kijiji niliopata fursa ya kukutana nao hivi majuzi. Shida yangu ni moja tu: MVUA HAITANIANGUSHA KWELI? ukizingatia mkoa wa singida ni mkoa wa ukame ukame.
Naombeni maoni yenu kuhusu hii kitu. Nina uzoefu kidogo kwenye kilimo hiki kwani mwaka jana nililima ekari 2 ili nipate uzoefu. Nilipata gunia nane tu. Kosa langu la kwanza nilikua napiga simu na kutuma hela tu kijijini hadi muda wa mavuno sijakanyaga shambani. Mwaka huu nitakua mwenyewe shambani mwanzo mwisho nikishiriki kila kitu. Kosa la pili nilitumia mbegu za kienyeji. Mwaka huu nitatumia mbegu hybrid za Hysun 33.
Karibuni kwa mchango.
Hiyo running cost inahusisha na gharama za kukodi na kulima hayo mashamba? Technically costs zote ziwe 10 ml sawa unaweza jitahidi kufikia hiyo 20 maana michakato ni mingi kwenye kilimo.
Kuhusu mvua inabidi ufanye timing Sana kwa kuzungumza na wenyeji wa hayo maeneo.
Kuhusu bei ya alizeti sio kesi ni uhakika ila shida ni kufaulu uzalishaji.
Mwisho hizo mbegu xinapatikana wapi?
Kuna ma agents wa makampun flan huwa wanapitisha vijijini ikifika msimu wa uhitaji.Hizi certified mbegu xinapatikana wapi hasaa?
Maduka ya pembejeo na mawakala wao wanauza.Hizi certified mbegu xinapatikana wapi hasaa?
Hizi certified mbegu xinapatikana wapi hasaa?
MbeyaUpo mkoa gani?
Unaweza kuagiza hata toka mikoa mingine.
Mbeya mawakala kibao.Mbeya
mkuu kwema?Mkuu add number hii mimi niko dodoma njia ya kwenda kiteto +971555088703 nalima maeneo hayo
haters kazini. anataka kujua kushindwaNi takribani mwaka sasa, hebu tupe ushuhuda namna ulivyoangukia pua.
Manyoni hautatoboa mkuu.Nina subscribe uzi kwa sababu msimu ujao nitalima eka 50 za alizeti huko Manyoni. Sasa mkuu njoo utupe feedback, changamoto na mafanikio
natanguliza shukurani zangu mkuu.Manyoni hautatoboa mkuu.
Kuna maeneo ambayo ukilima ni umelima....
Ardhi ya pale haitunzi unyevu, so n very risk. Pia sio productive kiviiiile,. Nenda sehemu hzi; mwahu, kisisi, gawidu, ghalanyangu, dajamida. Huko utakuja kunishukuru.
Mkuu naomba mawasiliano yako tafadhaliNina subscribe uzi kwa sababu msimu ujao nitalima eka 50 za alizeti huko Manyoni. Sasa mkuu njoo utupe feedback, changamoto na mafanikio
Pamojanatanguliza shukurani zangu mkuu.
Hayo maeneo yapo wapi mkuuPamoja
Ni Singida kaskazini. Ukifika Singida mjini, nenda msufini, tafta gari za Ngamu (Obvious huwa n noah). Nadhan nauli n 4000 kama haijabadlika. Huko utakuwa in between hayo maeneo, so n rahisi zaid kupata mbili tatu kwa hicho unachokifikiria.Hayo maeneo yapo wapi mkuu
Nakupata mkuu MiquelNi Singida kaskazini. Ukifika Singida mjini, nenda msufini, tafta gari za Ngamu (Obvious huwa n noah). Nadhan nauli n 4000 kama haijabadlika. Huko utakuwa in between hayo maeneo, so n rahisi zaid kupata mbili tatu kwa hicho unachokifikiria.