Moja ya malengo ya kuanzisha TBC, iliyojulikana kama TVT hapo mwanzo ni KUELIMISHA na KUFAHAMISHA umma wa watanzania pamoja na KUKUZA LUGHA YA KISWAHILI. Haya ni malengo ya msingi TBC inayopaswa kuyatimiza.
Kipindi cha nyuma kulikuwa na mzozo kwanini inaitwa TBC? TBC ni Tanzania Broadcasting Corporation - Kwanini television ya Taifa iitwe kwa kiingereza kama lengo lake ni kukuza kiswahili?
Hichi kipindi cha "This week in perspective" pia nacho kilishazungumziwa sana tu, lakini huyu mzee mwenyewe Mzee Simbei ameonyesha kutopenda idea ya kukitangaza kwa kiswahili.
Ukweli ni kwamba, watanzania tumefika pahala hatujali tena "nani anajua kiingereza na nani hajui". Alimradi tu wewe unajua basi unadhani kila mtu anajua na hatuwajali wale wasiojua!
Hata matangazo muhimu kama ya UKIMWI au MALARIA etc mengine yapo kwa kiingereza, achilia mbali document nyingi za Serikali etc.
Tatizo jingine la hiki kipindi ni uwezo wa kujieleza wa interviewers kwa kiingereza. Kuna wakati unafika mtu ana struggle kutoa point, achilia mbali pronounciation mbaya .... so nashindwa hata mimi kuelewa ni kwa nini ung'ang'anie kiingereza pasipo sababu za msingi na wakati watanzania walio wengi wanafahamu kiswahili fasaha na si kiingereza.
Nimeguswa sana na mtazamo chanya wa proffesor Safari (ktk pindi la this week in perspective) kuhusu tendo la wabunge wa chadema ku-walk out bungeni.
Kiranga, niko na wewe kwenye hili, nilisema mahali 'Chadema Hawajajipanga!' walinishukia, simply because washabiki wao, wanapenda tuu Chadema kiimbiwe nyimbo za sifa na mapambio.Hii ni habari ya bilauri kuwa imejaa nusu au tupu nusu.
CHADEMA wanastahili pongezi kwa kuthubutu kusema uozo ulio katika katiba na mfumo mzima wa uchaguzi. Kwa hakika hili ni suala la kujivunia kwa wnamapinduzi wote, na limeweka rekodi mpya katika siasa za Tanzania, hili nataka niliseme kwanza kabisa ili chochote nitakachosema baadaye kisije kuchukuliwa kama kutoelewa umuhimu wa kitendo hiki.
Lakini wengine tunawalaumu kwa kutofanya cha kutosha wala kupanga vizuri mambo yao. Ukitaka kuonyesha msimamo tu unaweza kuonyesha msimamo mpaka utachoka, CCM kama hawana haya ya kubadilika kutokana na vitendo hivi vya kuonyesha msimamo watabaki hivyo.
Zaidi kinachohitajika ni hatua zenye mikakati ya kisheria na kisiasa, CHADEMA wana mkakati gani wa kutekeleza mikakati hii?
Siku hizi chache zilizopita zimenionyesha CHADEMA ambayo ilitaka kufanya kitu kikubwa (kutomtambua rais) ikashindwa ikabidi ianze ku fumble na kuunga unga huku inaenda, mara hatumtambui rais, mara tunamtambua lakini hatutambui matokeo (WTF ?). Mara wabunge wengine wamesusia kumsusia rais, ili mradi chama kinaonekana hakina ukomavu wa kutosha.
Ni kweli kwamba CHADEMA hawajavunja sheria katika kumsusia rais bungeni, lakini wengine wanaweza kusema hawajaweka sheria mpya vile vile.
Mimi ningeshukuru hata CHADEMA wangevunja sheria, kama sheria zenyewe ni dhalimu, ili mradi wauondoe udhalimu huu. Huwezi ku ininstall operating system ya computer wakati unaitumia hiyo hiyo OS, huwezi kuing'oa nyumba wakati uko ndani ya hiyo nyumba, huwezi kurusha roketi iende kwenye mwezi kwa kuheshimu na kutoipita nguvu ya uvutano ya dunia inayokufunga hapa duniani, huwezi kuushinda utawala dhalimu na katiba yake kwa kutumia katiba hiyo hiyo dhalimu.
Uhuru hauombwi, unachukuliwa. CHADEMA wamejiandaa kuchukua uhuru/ Ushindi wao (kama wanashinda) ? Au wanangojea mpaka CCM watake ? Na CCM wasipotaka kuleta mabadiliko ya katiba mpaka 2015 hali iwe hii hii CHADEMA watafanya nini ?
Kiranga, niko na wewe kwenye hili, nilisema mahali 'Chadema Hawajajipanga!' walinishukia, simply because washabiki wao, wanapenda tuu Chadema kiimbiwe nyimbo za sifa na mapambio.
Kiranga, natofautiana na wewe kidogo kwenye mambo mawili, la kwanza nakubaliana nawe huku nikitofautiana nawe ni hili la uhuru, ni kweli, uhuru hauombwi, kama ilivyo haki, wala hauletewi kwenye kisahani cha chai,Kiranga umesema uhuru unachukuliwi as if uko pale unakungojea wewe ujichukulie, mimi naongezea kuwa uhuru, unadaiwa na ikibidi unapiganiwa, hii sasa ndio iwe ajenda ya Chadema kwenye kudai katiba mpya.
Tofauti nyingine na wewe, ni kuwa unaamini ili upambane, ni lazima utoke nje, mtazamo wangu, ili kupambana sio lazima utoke nje, you can fight from within, yaani unapambana kuanzia ndani, ndio maana nimeipongeza Chadema kwa mafanikio iliyoyapata. Nimemuomba Dr. Slaa ajitokeze hadharani atuambie japo asante kwa hicho hicho kidogo kilichopatikana baada ya kuchakachuliwa. 'If you don't get what you want, just take what you get!', usisuse!.
Kwa kufuata mtazamo wako, Chadema walitakiwa kwanza kupambana wakiwa nje mpaka uwanja wa mapambano usawazishwe, ndipo waingie kwenye mapambano. Kitendo cha Chadema kuingia kwenye mapambano, huku kikijua fika kinagombea kisu huku mmoja ameshika mpini na mwingine kwenye makali, matokeo utayajua tuu hata kabla, hivyo wamefanya vema kukubali kuingia, na japo kisu kimewakata,wamefanikiwa kupunguza kidogo ile grip ya kwenye mpini, hivyo mshika mpini anaanza kuteleza na mwisho atapokonywa.
Sasa Chadema wanatakiwa kutumia hiyo nguvu yake Bungeni, japo ndogo, kupambana from within,japo watakumbana na vizingiti vingi vya uchache wao na hii fragmented opposition, lakini wananchi watawaelewa wanapigania nini na come 2015, watawakataa washika mpini kwa nguvu zote na watapokonywa hicho kisu!
Ndiyo maana nataka kujua kama utawala waCCM hautabadili kitu, CHADEMA itafanya nini?Sawa kabisa naunga mkono 100% lakini hili la katiba haifai 2015 kufanya uchanguzi na katiba hii,hii na NEC hii hii :thinking: