THIS SUNDAY ON TUONGEE ASUBUHI
Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''.
Wageni wanaweza kubadilika kutokana na ratiba binafsi za sikukuu
Yahya M
YAHYA,
Jeshi la police limepoteza hadhi yake kwa wananchi, hali hii huchangiwa zaidi na si polisi wenyewe bali ni matakwa fulani kutoka kwa 'waliowateua'. Vyombo vyetu vya dola kiujumla huwajibika tu kwa aidha kulinda mipaka ama pale mmoja wa vigogo/wafanyabiashara maarufu wanapokumbwa na dhoruba inayoegemea police..ndipo hutumika.
Nionavyo, Police imepoteza muelekeao kiujumla kwa wananchi. Hii ni hali ambayo hurithishwa baina ya IGP wa sasa na IGP ajaye, haya yote huchagizwa na utendaji unaoegemea upande fulani na kuwaacha walalahoi wakiangamia pasipo kupata ulinzi wa aidha POLISI JAMII, ULINZI SHIRIKISHI au hata ULINZI KAMILIFU WA POLISI.
Tumeshuhudia ktk chaguzi kuu za kila baada ya miaka 5, hali imekuwa ikiegemea kwa kuwanyooshe tu wapinzani kuwa ndio wenye kuwa na chembe za vurugu,, hebu tujiulize katika hili:-
- Je hao wapinzani wenye chanzo cha kuvuruga amani ya nchi..ni watanzania ama si watanzania?
- Je! wapinzani wanatoka katika jamii ya watanzania wapenda amani au kuna watanzania wasiopenda amani?
- Je! Ni wapinzani ndio wanaotoka katika tabaka la vurugu na wale wenye chama tawala ni miongoni mwa kizazi mithili ya malaika kwa wao kutokuwa na chembe za kufanya vurugu ndio maana POLICE hawathubutu kuwamulika na kutumia nguvu kwao?
- Je! Police hawana njia za dialogue katika ku-compromise mambo badala yake nguvu kubwa kutumika kuwazuia/kuwatawanya raia wakiwa katika demands zao za msingi kwa utawala.
- Je! Iwaje police itoapo vibali huja na hoja ya kwamba..tunazuia maandamano hayo kwani amani ya nchi itavurugwa',, kwa nini wasitoe ulinzi na ushirikiano murua ili ujumbe wa maandamano uwafikie wahusika?
Kiukweli, polisi inajitahidi ila kuna tabaka halisia la kushughulikia wananchi. Tabaka la walionacho ndio huongoza kwa kusikilizwa, kutafutiwa njia m'badala na hata condussive response kuchukuliwa kwa wale wenye kuchokoza aina ya hili tabaka shauri tu ya kuwa na UWEZO. Tabaka la pili ni lile la wasiokuwa nacho, tabaka hili hutafsiriwa kirahisi kama ni tabaka angamizi...Ya kwamba:-
- watu wa chini wanapohitaji misaada ya kipolisi hawapati kirahisi, bali wakijichukulia sheria mikononi hulaumiwa.
- watu wa hali ya chini huchoshwa wadhulumiwapo, mahitaji yao wapatapo majanga huambulia negative response toka katika jeshi.
- watu wa chini hawasahau yanayowakuta kupitia jeshi hili, na wapatapo mianya nao hujawa na ghadhabu nzito kwa adha iwakutayo.
NGUVU KUBWA:
Nchi yetu ni nchi ya demokrasia ambapo jamii husika iwapo na jambo basi hutumia njia bora za kuwasilisha kilio chao mathalani maandamano, kongamano, mikutano ya hadhara ama vinginevyo. Kutumia nguvu kubwa ni sawa na kuvundika bomu lililoshikiliwa na viumbe wananchi, ya kwamba muda ufikapo ni kulipuka tu. Kwa nini jeshi lisijenge imani kwa raia wake pale wanapoona haki haitendeki nao kuamua kuandamana, kwa nini wazuiwe ilhali mambo yanakuwa hadharani juu ya dhamira ya raia kufikisha ujumbe kwa jamii nzima na kwa watawala?
Itapendeza zaidi jeshi libadilike tena kuanzia sasa, raia wanapoomizwa na jeshi...je hii inakuwa ni expense ya nani kwa haya madhara, na je inajenga taswira gani ifikiapo wapinzani kuvunjwa mikono, kuumizwa, kupigwa virungu na yote haya hufanywa na police ? Inapoonekana ya kwamba kuna hali ya kupigwa virungu na kuvunjwa viungo...hii itapelekea kupandikiza fikra ya uhasama baina ya raia na jeshi la police,, na kwamba wananchi waendapo katika maandamano ya kudai haki zao nao watakuwa na vifaa vya kujilinda na virungu ambapo tayari amani haitokuwepo tena. Kutokeapo na jeshi kwenda mrama kwa kutumia nguvu kubwa zaidi kinyume na taratibu...basi waiombe jamii radhi hadharani (na huu ndio utawala bora na uliotukuka) na hii pia italijengea jeshi heshima na kurejesha imani kwa wananchi ya kwamba police wapo kwa ajili yetu na SI KUTUUMIZA NA KUTUATHIRI.
Sote tuipende nchi yetu, tuijenge, tujenge mahusiano mazuri baina ya police na wananchi bali polisi iepushe ya kwamba waonapo vurugu ndoogo tu kuamua kutumia nguvu...tubadilike kwa AMANI & MSHIKAMANO WA NCHI YETU. Tusipigane, tusivunjane bali TUHESHIMIANE KIMISINGI.