This Sunday 26 DEC 2010 on Star TV '' TUONGEE ASUBUHI''

Asante Yahya Mhoza kwa mada hii nzuri baada ya ile ya katiba wiki iliyopita tuliyoimaliza kwa mtu aitwae Mjuni George wakati sauti ni ile yam zee msekwa.

Kwanini polisi wanalazimika kutumia nguvu zaidi?

1. Mimi ni polisi niliacha kazi hiyo kwa sababu katika jeshi hilo kuna viongozi wake wengi wanaamini askari hawana akili na hawawezi kufikiri, lipo kundi kubwa la askari kinyume na sheria na kanuni za jeshi hilo linatumikishwa ndivyo sivyo kwa maslahi binafsi. Wanasema afande ndio mwenye akili na kwamba akisema twanga risasi wanategemea watwange.

2. Kuna matumizi mabaya ya madaraka ya watawala kutea makamanda wa polisi kwa rekodi ya kupiga mabomu wapinzani na siyo sifa ya utendaji. Kama inavyosemekana mahita alipewa kuwa IGP kwa kuwa alimpiga mabomu mh.mrema sasa andenyenge alikuwa mlinzi wa mahita anamategemeo makubwa kwa kumpiga Lema marungu atapewa cheo zaidi –mimi nadahani amepitwa na wakati.

3. Tunaelewa na tumefundishwa kwamba polisi anaweza kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anahatarisha maisha yake, au anagoma kutii amri halali mfano jambazi lina silaha itamlazimu polisi kutumia silaha kulidhibiti pamoja na kwamba haruhusiwi kuua. Sasa haingii akilini polisi anamvamia mbunge na virungu ndani ya ukumbi wa madiwani kisa OCD kamuru ili kumfurahisha RPC na Mkurugenzi ambao kwa vyovyote vile wanataka kuwafurahisha wabwana wakubwa na chama tawala.

4. Jeshi la polisi kwa ujumla imepoteza dira imekuwa kitengo ndani ya ccm na inafanya kazi kwa maslahi ya chama-mfano unawapiga wananchi wanaodai Matokeo kutoka kwa mkurugenzi aliyegoma kutangaza kisa anaogopa wakubwa hawatafurahi, hivi hapa anaevunja sheria ni nani? Mwananchi anaedai haki yake au mkurugenzi anayepora haki?

5. IGP Mwema amejitahi di kuleta chachu mpya lakini ili aweze kufanikiwa lazima asiwe achidodo asiwe ndumila kuwili asiwe kibaraka, asiwe tawi la ccm, polisi ya sasa inatumia nguvu sana kwa sababu haifuati kanini zake na sheria badala yake inafanya kazi kwa maslahi ya chama tawala, jeshi la polisi lifukuze makamanda kama andenyenge wapo wengi wanaosaka ukubwa juu ya migongo ya watanzania kwa kuwapiga mabomu. Kumpiga mbunge ni sawa na kuwapiga waliomchagua. Mwema awaruhusu polisi hawa waliogeuka watumwa na wajinga –kuwa na fikra na siyo kufanya kila kitu wanachoambiwa na mkubwa wao bila hivyo jeshi la polisi litaendelea kuwa adui wa watanzania. Polisi wanashida sawa na watanzania wengine hawana makazi, hawana Elimu nzuri, hawapati maslahi stahili, kwahiyo ni sehemu ya jamii.

6. Kitendo cha kumpiga Mbunge Lema kilinifanya nijisikie uchungu kiasi kwamba niliona kumeza bomu na kujilipua wanavyofanya wairaq ni kitu rahisi saana sehemu yenye chuki na maudhi kama hii ya kumpiga virungu mbunge kisa kadai haki, lakini pia sijawai sikia mbunge hata mmoja wa ccm amepigwa marungu hata pale alipovunja sheria mfano Yule mgombea wa maswa aliyempiga mtama OCD je angekuwa LEMA? INGEKUWAJE? SHAME ON RPC , OCD AND DED FOR ARUSHA, SHAME ON POLICE FORCE, SHAME ON ALL THESE INJUSTICE.
 
Kwani Mh. Godbless Lema ni mhalifu?

Au mimi sielewi maana ya uhalifu?

Bila Shaka ni Mhalifu wala hakuna DOUBT!

Ngoja nikusaidie Kiongozi wangu, pengine umeshtushwa na Neno Mhalifu: Neno hilo linatokana na shina HALIFU ambalo tumekopa kutoka kwa Waarabu kwa neno KHALIF, Ambapo maneno hayo (HALIFU na KHALIF) yana maana: Tenda Kinyume cha Kanuni; Sheria; Vunja Sheria; Kataa Kutii: Mtawala. 2. Kuwa Mkaidi; Kataza; Pinga Amri. (Kamusi Sanifu 1981: 73)

Kama ulitazama katika TV kwa kilichotokea pale Ukumbini doubt yako itakuwa solved Mkuu.

Merry XMAS
 
Nawashukuru sana STAR TV kwa kumulika maovu yanayofanywa polisi kama wafuasi wa CCM huu ni ukweli usiopingika. Natoa mfano mmoja ambao una ukweli usiopingika kuwa polisi watiifu sana wa CCM pale aliyekuwa mbunge wa Bariadi kumnasa kibao polisi, nasema kama angekuwa SHIBUDA nadhani angeuawa na kubambikiwa kesi ya mauaji. Polisi mtavuruga amani na sisi hatavumilia kabisa kuona haki haitendeki. Nawadhitishia hili halina mda mrefu Tanzani haitakuwa na amani tena ni hapo tu bunge likianza.
 
Bila Shaka ni Mhalifu wala hakuna DOUBT!

Ngoja nikusaidie Kiongozi wangu, pengine umeshtushwa na Neno Mhalifu: Neno hilo linatokana na shina HALIFU ambalo tumekopa kutoka kwa Waarabu kwa neno KHALIF, Ambapo maneno hayo (HALIFU na KHALIF) yana maana: Tenda Kinyume cha Kanuni; Sheria; Vunja Sheria; Kataa Kutii: Mtawala. 2. Kuwa Mkaidi; Kataza; Pinga Amri. (Kamusi Sanifu 1981: 73)

Kama ulitazama katika TV kwa kilichotokea pale Ukumbini doubt yako itakuwa solved Mkuu.

Merry XMAS

Kupambana na mtu anayevunja sheria ni kuvunja sheria?
 
Asilimia themanini ya Watanzania ni maskini kwa hiyo polisi wanapolinda matajiri maana yake msaada wao hautaonekana kwa raia ndio maana nathubutu kusema watanzania hawalindwi na polisi bali wanajilinda wenyewe. Janja ya polisi kusema Uslama wa raia haina ukweli!! Tuchukue mfano rahisi tu ........ Nani alishaona police patrol katika maeneo ya Mbagala; Manzese; Kwanjeka; Mabatini; Itezi na kwingine penye watu wa kawaida? Linganisha na maeneo ya Makzi walipo wenye kipato.

Kuhusu Mgomo ya Wanafunzi; Kama wanafunzi wamegoma kwa kucheleweshewa mikopo yao kwa nini Police wasimkamate Mwenyekiti/Mkurugunzi wa Bodi ya Mkopo wa kuhatarisha Amani kama walivyomkamata SHIBUDA kule kule Maswa? Kule shinyanga watu wengine walifanya vurugu badala yake akakamatwa Shibuda aliyekuwa two kilometers from the event. This should apply to the loan board! Badala yake police wanaenda kuua watu wasiokuwa na hatia ambao si chanzo cha matatizo!!!
 
Back
Top Bottom