This Sunday 26 DEC 2010 on Star TV '' TUONGEE ASUBUHI''

Yahya Mohamed

Verified Member
Oct 28, 2010
270
195
WanaJF

Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matukio ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year

Naomba Kuwasilisha

Yahya M
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,538
2,000
Ahsante sana Yahya.

Ngoja tujiandae na maswali hasa Nguvu iliyotumika Arusha kwa Lema vile vile kwa wanachuo wa Dodoma.
Naskia kuna Binti wa Kike kuvunjika Mguu, kule kule porini sasa mi nashindwa kuelewa pale alikuwa anahatarisha usalama wa nani wakati ni mbali sana na wananchi au maofisi.
 
Spencer
Ahsante kwa kulitaja tukio la Dodoma jana, na Morogoro pia Nguvu ilitumika. Natumai mengi yatakumbukwa katika hili. Looking forwad kwa mchango wako J2 Mkuu
Yahya
 
Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,809
0
WanaJF
Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.
Mada itakayojadiliwa ni '' Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matuki ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year
Naomba Kuwasilisha

Yahya M

Safi sana,
ngoja tukune vichwa kisha tuje na maangalizo/mitazamo.
 
STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,765
2,000
Ahsnte sana bwana Yahya, Sisi wanachi wa kawaida tunachotaka ni nyie waandishi kuwabana hawa jamaa vizuri kwa sababu, sisi wengine tunakuwa hatupati hizo line hadi muda unaisha.

Maoni yangu:

1. Muulize IGP kwa nini wampige mbuge ila hali hakuwa na silaha yeyote na alikuwa akikataa Mkurugenzi na Madiwa wa CCM kuendelea kuvunja sheria wakati aliapa kuilinda katiba ya JMT bungeni.

2. Inakuwaje hata siku moja polisi hawajawahi kumpiga au kumkamata na kumweka ndani mbunge na kiongozi yeyote wa CCM hata kama wanavunja sheria hadharani. mfano wakati wa kampeni tumeona matukio mengi na polisi wapo lakini utadhani kama hawapo vile.

3. Hivi polisi wanafahamu idadi ya watanzaia ambao wamechoshwa na utawala wa CCM siku wakianza kuwatafuta polisi moja moja wao polisi watakwenda wapi maana katika hali ya kwaidi hii inapunguza imani ya Raia kwa polisi wetu na ni kutokana na kutumiwa vibaya.

4. Ushauri wangu kwa IGP na viongozi wa jeshi la polisi ni kwamba hivyo vyeo vya muda na siku ikifika utakimbilia nchi gani maana kuwa na misimamo ya kichama kwenye kazi ya jeshi, uandishi wa habari, etc ni mbaya sana kwani ni watu wa kawaida wanaweza kupima utendaji wako.

5. Mngewaalika na wanasheria kutoka vyama vya upinzani ili wazungumzie hizo issues kwa hoja.

Ahsante.
 
jino kwa jino

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
766

yote umeandika points ila mkuu naweka tu msisitizo
 
Yahya Mohamed

Verified Member
Oct 28, 2010
270
195
This Sunday 26 DEC 2010 on Star TV '' TUONGEE ASUBUHI''
WanaJF

Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matukio ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Josephat Isango - CHADEMA Singida
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year

Naomba Kuwasilisha

Yahya M
 
Yahya Mohamed

Verified Member
Oct 28, 2010
270
195
THIS SUNDAY ON TUONGEE ASUBUHI

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''.

Wageni wanaweza kubadilika kutokana na ratiba binafsi za sikukuu

Yahya M
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,538
2,000
Yahya,

1: IGP alijifunza nini kwa Raia wa (MWANZA) Tanzania ktk mkutano wa Kampeni wa Mwiasho wa Dr Slaa licha ya hapo awali kuwapiga mabomu.
na pia polisi wakiwa wamesusa kutoa ulinzi?.
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,538
2,000
Yahya,

1: IGP alijifunza nini kwa Raia wa (MWANZA) Tanzania ktk mkutano wa Kampeni wa Mwiasho wa Dr Slaa licha ya hapo awali kuwapiga mabomu.
na pia polisi wakiwa wamesusa kutoa ulinzi?.[/QUOTE]

...............Mkutano kufanyika kwa amani na Utulivu licha Polisi kuususia?
 
Baiskeli

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
334
225
naomba mwambie mwema sina imani naye na jeshi lake kwa ujumla tena si mimi tu. mimi pamoja na familia yangu. nimemaliza.
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,697
2,000
Asante Yahya. Tunashukuru sana kwa jinsi unavyoishirikisha jamii kwa mstakabali wake. Star Tv hamlinanishwi...... Mungu akubariki sana. Ngoja niandae points za kuzungumza na Mh. sana Said Mwema. Polisi wanatukosea sana wananchi sijui tuanzie wapi. Naona wanaanzisha si kitu kingine bali serikali ya kipolisi. Baadae basi............
 
Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,809
0
THIS SUNDAY ON TUONGEE ASUBUHI

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''.

Wageni wanaweza kubadilika kutokana na ratiba binafsi za sikukuu

Yahya M

YAHYA,
Jeshi la police limepoteza hadhi yake kwa wananchi, hali hii huchangiwa zaidi na si polisi wenyewe bali ni matakwa fulani kutoka kwa 'waliowateua'. Vyombo vyetu vya dola kiujumla huwajibika tu kwa aidha kulinda mipaka ama pale mmoja wa vigogo/wafanyabiashara maarufu wanapokumbwa na dhoruba inayoegemea police..ndipo hutumika.
Nionavyo, Police imepoteza muelekeao kiujumla kwa wananchi. Hii ni hali ambayo hurithishwa baina ya IGP wa sasa na IGP ajaye, haya yote huchagizwa na utendaji unaoegemea upande fulani na kuwaacha walalahoi wakiangamia pasipo kupata ulinzi wa aidha POLISI JAMII, ULINZI SHIRIKISHI au hata ULINZI KAMILIFU WA POLISI.
Tumeshuhudia ktk chaguzi kuu za kila baada ya miaka 5, hali imekuwa ikiegemea kwa kuwanyooshe tu wapinzani kuwa ndio wenye kuwa na chembe za vurugu,, hebu tujiulize katika hili:-
  • Je hao wapinzani wenye chanzo cha kuvuruga amani ya nchi..ni watanzania ama si watanzania?
  • Je! wapinzani wanatoka katika jamii ya watanzania wapenda amani au kuna watanzania wasiopenda amani?
  • Je! Ni wapinzani ndio wanaotoka katika tabaka la vurugu na wale wenye chama tawala ni miongoni mwa kizazi mithili ya malaika kwa wao kutokuwa na chembe za kufanya vurugu ndio maana POLICE hawathubutu kuwamulika na kutumia nguvu kwao?
  • Je! Police hawana njia za dialogue katika ku-compromise mambo badala yake nguvu kubwa kutumika kuwazuia/kuwatawanya raia wakiwa katika demands zao za msingi kwa utawala.
  • Je! Iwaje police itoapo vibali huja na hoja ya kwamba..tunazuia maandamano hayo kwani amani ya nchi itavurugwa',, kwa nini wasitoe ulinzi na ushirikiano murua ili ujumbe wa maandamano uwafikie wahusika?
Kiukweli, polisi inajitahidi ila kuna tabaka halisia la kushughulikia wananchi. Tabaka la walionacho ndio huongoza kwa kusikilizwa, kutafutiwa njia m'badala na hata condussive response kuchukuliwa kwa wale wenye kuchokoza aina ya hili tabaka shauri tu ya kuwa na UWEZO. Tabaka la pili ni lile la wasiokuwa nacho, tabaka hili hutafsiriwa kirahisi kama ni tabaka angamizi...Ya kwamba:-
  • watu wa chini wanapohitaji misaada ya kipolisi hawapati kirahisi, bali wakijichukulia sheria mikononi hulaumiwa.
  • watu wa hali ya chini huchoshwa wadhulumiwapo, mahitaji yao wapatapo majanga huambulia negative response toka katika jeshi.
  • watu wa chini hawasahau yanayowakuta kupitia jeshi hili, na wapatapo mianya nao hujawa na ghadhabu nzito kwa adha iwakutayo.
NGUVU KUBWA:
Nchi yetu ni nchi ya demokrasia ambapo jamii husika iwapo na jambo basi hutumia njia bora za kuwasilisha kilio chao mathalani maandamano, kongamano, mikutano ya hadhara ama vinginevyo. Kutumia nguvu kubwa ni sawa na kuvundika bomu lililoshikiliwa na viumbe wananchi, ya kwamba muda ufikapo ni kulipuka tu. Kwa nini jeshi lisijenge imani kwa raia wake pale wanapoona haki haitendeki nao kuamua kuandamana, kwa nini wazuiwe ilhali mambo yanakuwa hadharani juu ya dhamira ya raia kufikisha ujumbe kwa jamii nzima na kwa watawala?
Itapendeza zaidi jeshi libadilike tena kuanzia sasa, raia wanapoomizwa na jeshi...je hii inakuwa ni expense ya nani kwa haya madhara, na je inajenga taswira gani ifikiapo wapinzani kuvunjwa mikono, kuumizwa, kupigwa virungu na yote haya hufanywa na police ? Inapoonekana ya kwamba kuna hali ya kupigwa virungu na kuvunjwa viungo...hii itapelekea kupandikiza fikra ya uhasama baina ya raia na jeshi la police,, na kwamba wananchi waendapo katika maandamano ya kudai haki zao nao watakuwa na vifaa vya kujilinda na virungu ambapo tayari amani haitokuwepo tena. Kutokeapo na jeshi kwenda mrama kwa kutumia nguvu kubwa zaidi kinyume na taratibu...basi waiombe jamii radhi hadharani (na huu ndio utawala bora na uliotukuka) na hii pia italijengea jeshi heshima na kurejesha imani kwa wananchi ya kwamba police wapo kwa ajili yetu na SI KUTUUMIZA NA KUTUATHIRI.
Sote tuipende nchi yetu, tuijenge, tujenge mahusiano mazuri baina ya police na wananchi bali polisi iepushe ya kwamba waonapo vurugu ndoogo tu kuamua kutumia nguvu...tubadilike kwa AMANI & MSHIKAMANO WA NCHI YETU. Tusipigane, tusivunjane bali TUHESHIMIANE KIMISINGI.
 
LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
WanaJF

Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matukio ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year

Naomba Kuwasilisha

Yahya M

Yahya..ahsante sana

Mimi ninaomba kumuuliza IGP .... je polisi kama chombo cha dola ni jeshi au taasisi ya kulinda amani na kuchunga sheria ndani ya mipaka ya nchi.....

mapendekezo yangu..... sheria zinazounda state organs zibadilishwe na polisi isiwe jeshi bali iwe ni taasisi ya kutoa huduma za usalama na ulinzi wa raia... mfano badala ya kuwa Tanzania Police Force iwe Tanzania Police Service... South Africa wana SAPS (South African Police Service) na its one of the best policing organs in the world...policing does not mean using force... using force will be the last resort like ...if the pain persist see a medical doctor..... haya mapendekezo yaingie moja kwa moja kwenye sheria mama inayoanzisha taasisi ya polisi katika mabadiliko na uanzishwaji wa katiba mpya..

Naomba mawazo haya yafike kwa muhusika

Nakutakia heri ya mwaka mpya
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,831
2,000
WanaJF

Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matukio ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year

Naomba Kuwasilisha

Yahya M

Kwani Mh. Godbless Lema ni mhalifu?

Au mimi sielewi maana ya uhalifu?
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
0
IGP Mwema, Tangu uanze kazi umejitahidi sana kuwa professional unlike mahita(bogus) askari wako hasa wa Dar wameanza kujiheshimu na inaelekea elimu imeanza kuingia hongera...sasa swali
1. Askari wa mikoa ni wasumbufu kupita kiasa bila sababu juzi walimkamata babangu kijijini (dodoma) eti wanaulizia leseni ya tractor ambayo iko juu ya mawe (haiko barabarani) akili kweli hiyo?
2. Pili embu wapeni uwezo askari vituoni hawana hata karatasi na kalamu jamani...kama tuandamane tudai haki za polisi ni mateso tupu.
 
Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,204
1,195
Ndg. Yahaya M.
Muulize saidi Mwema:-
1: Ilikuwaje au nani alitoa amri Jeshi la polisi kuingia kwenye ukumbi wa waheshimiwa madiwa ni wa Arusha, ili hali sheria ni sawa na za bungeni? yaani mtu ambaye siye Diwani haruhusiwi kuingia ukumbini mpaka sheria zitenguliwe? Tumeona hata nchi zingine Wabunge wakikunjana suti zao lakini hakuna polisi anaeingilia, inakuwaje Tz?

2: Jeshi la polisi lina mamlaka gani kisheria kuzuia maandamano/mikutano ya kisiasa wakati kazi yake ni kulinda amani tu kwenye mikusanyiko hiyo?

3: Imekuwa ni kawaida Jeshi la Polisi linapiga marufuku mikusanyiko halali ya kisiasa hasa kwa vyama vya upinzani kwa kisingizio kuwa hawana askari wa kutosha kwenda kulinda amani ama kuna dalili za uvunjifu wa amani (vigezo gani wanatumia) lakini pindi ikitokea kuna maandamano tayari utaona askari wanamwagika mpaka unashangaa! Je, haoni kama jeshi lake linatumika kwa manufaa ya chama tawala tu?

Yapo maswali mengi ila niachie na wengine waongezee!
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,697
2,000
Yahya, asante sana kwa kutupa nafasi ya kutoa mchango wetu katika mstakabali wa nchi yetu.
Kuhusu matumizi ya nguvu katika kukamata waharifu limekuwa ni jambo la kawaida sasa kuona kila mahali nguvu kubwa sana inatumika kuwatia nguvuni waharifu na kwa kweli mahali pengine nachelea kuwaita waharifu kwa sababu utagundua si waharifu.

Wakati mwingine huwa nashangaa sana nikiona mambo ambayo polisi wetu sasa wanayafanya hasa linapokuja suala la kumtia mtu nguvuni kwani hutumia nguvu na hata kupiga kama njia ya kuonyesha kwamba wanamtia nguvuni mtu hatakama mtu mwenyewe hakukataa kutii itikio la kuwa chini ya ulinzi. Mara nyingi utashangaa polisi hataki hata umuulize kwa nini anakutia nguvuni, na mambo mengine ya kisheria kabla hawajakupeleka kituoni.

Kwa mfano kwenye suala la Lema ambalo ni mfano mmojawapo tu ambalo kwa kweli tunawashukuru waandishi wa habari ambao walionyesha tukio zima. Utashangaa kwa nini askari walitumia nguvu kiasi hicho kwa kitu ambacho wala wao hawakutakiwa kutumia nguvu kiasi hicho. Polisi walifanya hivyo wakijua kwamba wanafanya kosa ndio sababu walimuachia baada ya kumpeleka kituoni lakini wakiwa wameshampiga. Kila mara viongozi wa vyama vya upinzani kila wakitoa malalamiko yao uonekana ni wakosaji mbele ya polisi. Si hilo tu, bali baadhi ya matukio wakati wa uchaguzi ni ushahidi kuwa polisi wetu wamekuwa wakifanya kazi kwa misukumo ya kisiasa. Na hapa najua wao polisi watakua ni wepesi kukataa lakini kwa kweli hata wakikataa jambo hili liko wazi kuwa wanafanya kazi zao kwa misukumo ya kisiasa.

Wakati nchi yetu ilipobadilika na kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa majeshi yote ikiwa ni pamoja na polisi walitakiwa kuwa nje ya siasa ya vyama. Lakini kwa sasa tunashuhudia maaskari wetu wakijihusisha na siasa za vyama nyuma ya pazia. Shida hii iko hasa kwa viongozi wakuu wa polisi. Hawa kwa kutumia vyeo vyao uhamrisha maaskari wa chini kupiga au kuwakamata wanachama wa vyama vingine vya siasa kwa visingizio mbali mbali. Na hili sio siri. Niliona kwa mfano wakati wa uchaguzi mkuu uliopita nilikwenda kituo cha polisi kwani nilikamatwa na askari wa usalama barabarani na nililipa faini lakini kwa bahati mbaya nilikuwa nimevaa mavazi ya chadema. Wakati natoka kituoni wale viongozi wa polisi waliokuwepo walikuwa wakinifuatilia sana kana kwamba nina kesi ya kuua. Kila mmoja alikuwa akiniangalia vibaya na kama ningekuwa na kesi kubwa nadhani nisingepata msaada kwao.

Tumeshuhudia kila wakati wa uchaguzi wapenzi na viongozi wa siasa wamekuwa wakikamatwa bila sababu za maana huku wakisingiziwa kuanzisha fujo hata pale ambapo kulikuwa na uhakika kuwa waanzilishi walikuwa chama cha mapinduzi. Polisi wamekuwa si wasikivu hata kidogo. Angalia leo kila kukiwa na maandamano ambayo mengi huwa ni ya amani kama ilivyoonekana juzi juzi pale UDOM askari huwa wanakuja na kuwapiga watu ambao hawana hata na siraha kwa kisingizio cha kutawanya maandamano. Sijawahi kuona maandamano ambayo kwao waliwahi kuona ni ya haki bali kwao maandamano yote ya kupinga lolote la serikali kwao huwa ni kosa la kusababisha kupiga watu. Maandamano ni haki yetu kama ni ya amani. Tumeshuhudia hata wale wazee wetu wa iliyokuwa Afrika mashariki ambao inajulikana wazi kwamba walikuwa wakitafuta haki yao walipigwa na kuburutwa barabani kwa aibu kubwa. Hili watu wanaona kama ni kitu cha kawaida na viongozi wetu wa polisi hawaoni shida. Tumeona viongozi wa vyama wakipigwa kama tulivyoshuhudia Professor Lipumba akipigwa mpaka kuvunjika mkono, lakini tumeshuhudia pia IGP aliyepita akieleza uongo kwenye vyombo vya habari kwamba chama cha CUF kiliingiza visu kwa ajili ya kudhuru watu huku akijua kuwa ni uongo. Jeshi la Polisi linapojihusisha na kubambika kesi kwa ajili ya siasa hili ni jeshi la polisi kweli? Si kazi ya polisi kuwachagulia watu maandamano bali ni kazi yao kulinda maandamano ili yawe ya amani.
Kwa ujumla wake utagundua polisi wetu sasa wanatumiwa na wanasiasa na hawafuati misingi ya kazi zao.

Mkuu wa jeshi la Polisi hapa atuambie ni lini watajiondoa katika ushabiki wa vyama vya siasa na kutenda kazi zao? Tumechoka kuona kuwa sasa jeshi la polisi limekuwa ni chombo cha kutumika kupiga wote wanaopingana na lolote linaloipinga serikali. Hii si kazi yao.
Hata kwenye nchi walizokwenda kulinda amani je wanapiga ovyo tu wananchi wa huko? Amani haiji kwa kupiga watu ovyo bali linaweza kuzalisha maafa kama yale ya Zanzibar.

Mie bado naunganisha matukio haya na udhahifu wa katiba yetu.
 
DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
WanaJF

Nichukue fursa hii kwanza kuwatakia Heri ya X-mas na pia kuendelea kushukuru kwa michango yenu Adhimu. Kwa kuzingatia mawazo ya Wadau, ninapost mapema mada ya wiki hii kuwapa muda kufanya utafiti wa Kina ili kuja na takwimu sahihi na hoja zilizoshiba kwa masilahi ya Umma.

Mada itakayojadiliwa ni ''Kuna Ulazima gani kwa Askari wa Jeshi la Polisi kutumia Nguvu za ziada wakati wa kuwakamata watuhumiwa au Wahalifu''. Matukio ya karibuni ni hili la Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Shabiki wa Soka aliyengia uwanjani wakati wa mechi ya Fainali ya CECAFA Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na IVORY COAST:

Wangeni watarajiwa
IGP - Said Mwema
Wakili Harold Sungusia - HLRC

Mwanza
Patrobas - SAUT
Political Analyst na Activist ICODM - Magoiga Samweli Nchagwa

Merry X-MAS and Happy New Year

Naomba Kuwasilisha

Yahya M

Asante Yahya Mhoza kwa mada hii nzuri baada ya ile ya katiba wiki iliyopita tuliyoimaliza kwa mtu aitwae Mjuni George wakati sauti ni ile yam zee msekwa.
Kwanini polisi wanalazimika kutumia nguvu zaidi?
1. Mimi ni polisi niliacha kazi hiyo kwa sababu katika jeshi hilo kuna viongozi wake wengi wanaamini askari hawana akili na hawawezi kufikiri, lipo kundi kubwa la askari kinyume na sheria na kanuni za jeshi hilo linatumikishwa ndivyo sivyo kwa maslahi binafsi. Wanasema afande ndio mwenye akili na kwamba akisema twanga risasi wanategemea watwange.
2. Kuna matumizi mabaya ya madaraka ya watawala kutea makamanda wa polisi kwa rekodi ya kupiga mabomu wapinzani na siyo sifa ya utendaji. Kama inavyosemekana mahita alipewa kuwa IGP kwa kuwa alimpiga mabomu mh.mrema sasa andenyenge alikuwa mlinzi wa mahita anamategemeo makubwa kwa kumpiga Lema marungu atapewa cheo zaidi –mimi nadahani amepitwa na wakati.
3. Tunaelewa na tumefundishwa kwamba polisi anaweza kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anahatarisha maisha yake, au anagoma kutii amri halali mfano jambazi lina silaha itamlazimu polisi kutumia silaha kulidhibiti pamoja na kwamba haruhusiwi kuua. Sasa haingii akilini polisi anamvamia mbunge na virungu ndani ya ukumbi wa madiwani kisa OCD kamuru ili kumfurahisha RPC na Mkurugenzi ambao kwa vyovyote vile wanataka kuwafurahisha wabwana wakubwa na chama tawala.
4. Jeshi la polisi kwa ujumla imepoteza dira imekuwa kitengo ndani ya ccm na inafanya kazi kwa maslahi ya chama-mfano unawapiga wananchi wanaodai Matokeo kutoka kwa mkurugenzi aliyegoma kutangaza kisa anaogopa wakubwa hawatafurahi, hivi hapa anaevunja sheria ni nani? Mwananchi anaedai haki yake au mkurugenzi anayepora haki???
5. IGP Mwema amejitahi di kuleta chachu mpya lakini ili aweze kufanikiwa lazima asiwe achidodo asiwe ndumila kuwili asiwe kibaraka, asiwe tawi la ccm, polisi ya sasa inatumia nguvu sana kwa sababu haifuati kanini zake na sheria badala yake inafanya kazi kwa maslahi ya chama tawala, jeshi la polisi lifukuze makamanda kama andenyenge wapo wengi wanaosaka ukubwa juu ya migongo ya watanzania kwa kuwapiga mabomu. Kumpiga mbunge ni sawa na kuwapiga waliomchagua. Mwema awaruhusu polisi hawa waliogeuka watumwa na wajinga –kuwa na fikra na siyo kufanya kila kitu wanachoambiwa na mkubwa wao bila hivyo jeshi la polisi litaendelea kuwa adui wa watanzania. Polisi wanashida sawa na watanzania wengine hawana makazi, hawana Elimu nzuri, hawapati maslahi stahili, kwahiyo ni sehemu ya jamii.
6. Kitendo cha kumpiga Mbunge Lema kilinifanya nijisikie uchungu kiasi kwamba niliona kumeza bomu na kujilipua wanavyofanya wairaq ni kitu rahisi saana sehemu yenye chuki na maudhi kama hii ya kumpiga virungu mbunge kisa kadai haki, lakini pia sijawai sikia mbunge hata mmoja wa ccm amepigwa marungu hata pale alipovunja sheria mfano Yule mgombea wa maswa aliyempiga mtama OCD je angekuwa LEMA? INGEKUWAJE? SHAME ON RPC , OCD AND DED FOR ARUSHA, SHAME ON POLICE FORCE, SHAME ON ALL THESE INJUSTICE.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom