This made my day...

This made my day...

naa

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
1,766
Reaction score
3,797
Anakuja Mzungu anasema anahitaji Ngedere, ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi wanakijiji wanahaha kusaka ngedere, wanawaleta Mzungu ananunua wote anasepa nao.

Anarudi tena anasema vipi, naona wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya 35,000 ngedere mmoja, wanakijiji wanaenda deep zaidi msituni, kamata ngedere, leta kwa mzungu, mzungu anasepa nao.

Alafu wiki mnayofuatia Mzungu anasema bado anataka ngedere, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji macho yamewatoka, hawana tena Ngedere.

Mzungu anasema basi ntaftieni kwa Laki na Nusu. Kesho yake inasikika kuwa kuna Mchagga anauza Ngedere kijiji cha pili, anauza kwa 100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta wanaenda nunua Ngedere wote wa kijiji cha pili. Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana ngedere wakijua watamuuzia mzungu fasta kwa laki na nusu, Mzungu hatokei Ng'oooo!!!!

Infact, yule mzungu alikuwa anawakusanya tu na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji hiki.

Mwenye macho na aone, mwenye masikio na asikie. Muwe na usiku mwema wakuu.
 
naa nimecheka sana....lakini nasikitika umeonyesha mzungu ana akili sana kuliko hao wanakijiji wote!!
 
Last edited by a moderator:
hahah cjui aliwaza nini alotunga hii but ina ujumbe ndani yake proNDO
 
Last edited by a moderator:
chadema nao wakichukua nchi itakuwa story kama hivi
 
Inatufundisha nini hii?

inafundisha mambo mengi,pia naona imekaa vzr kiuchumi.lyk Tz 2nauza malighafi z2 kwa bei cheee badaye cc wnywe 2nanunua vi2 vylvyo tngnzwa kwa maligf hzo kwa bei ya juu xana
 
  • Thanks
Reactions: naa
kwa uelewa wangu ni kwamba, unaweza sasa ukanunua kiwanja kwa bei ndogo ila ukakiifadh bila kujenga,baada ya miaka kadhaa unaweza ukauza kwa dau kubwa tofauti na ulivyonunua.. ni mtazamo wangu tu
 
Si ndio wanavofanya na almasi zetu, thahabu zetu, wanyama wetu na kadhalika. Miafrika ndivyo tulivyo- NN
 
Back
Top Bottom