This is pathetic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This is pathetic

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Sep 6, 2008.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Bukoba (BUWASA), Jackob Laizer, jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba akidaiwa kumsaidia mwanafunzi anayetuhumiwa kuwa na uhusiano naye wa mapenzi, kutaka kujiua kwa sumu ya thiodan.

  Tangu Septemba mosi mwaka huu, Laizer alikuwa anashikiliwa na Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kutaka kumuua kwa sumu mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari ya Mugeza mwenye umri wa miaka 16 anayesoma Kidato cha Pili. Jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Salewi, alipotafutwa na gazeti hili kuthibitisha kumshikilia meneja huyo, alisema:

  “Ndiyo tunamshikilia, na leo (jana) tumemfikisha mahakamani kwa kusaidia mtu kutaka kujiua… unajua alikuwa na kahawara kake mwanafunzi…” Awali, meneja huyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera chini ya uangalizi wa Polisi akidaiwa kusumbuliwa na ugonjwa ambao haukutajwa na aliugua baada ya kukamatwa.

  Inadaiwa meneja huyo alipeleka sumu hiyo ya kuulia wadudu ya thiodan shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa lengo la kumtaka ajiue kupoteza ushahidi wa kesi inayomkabili ya kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi huyo. Mwanafunzi huyo (jina tunalo) amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Kagera.

  Inadaiwa baada ya kupelekewa sumu hiyo na meneja huyo, aliipokea na kuweka katika chakula na kisha kuwapatia wanafunzi wenzake wawili waliotajwa kuwa ni Magdath Kafuba na Yakilila Ruta, wote wa Kidato cha Pili ambao ni marafiki zake. Kutokana na hali hiyo, mwanafunzi huyo na wenzake walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako wamelazwa hadi sasa katika wadi namba tano.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Henry Salewi, tukio hilo lilitokea Septemba mosi jioni wakati wanafunzi walipokuwa wakipata chakula cha jioni shuleni hapo. Hata hivyo, msichana anayedaiwa kuwa na uhusiano na meneja huyo amelazwa chini ya ulinzi wa Polisi pamoja na Laizer anayedaiwa kukabiliwa na shinikizo la damu na kuharisha damu, magonjwa ambayo yalijitokeza baada ya kukataliwa dhamana na polisi.

  Kamanda Salewi alisema kukamatwa kwa Laizer kumetokana na maelezo ya mwanafunzi huyo kumtaja kuwa ndiye alimpelekea sumu hiyo ajidhuru, kuepuka kuandamwa na vyombo vya dola na aibu kwa jamii na wanafunzi wenzake wanaodaiwa wamekuwa wakimzomea kuwa ana mpenzi wakati anasoma. Alisema baada ya kupewa dawa hiyo, hakutaka ionekane kuwa yeye ndiye amejiua hivyo kutokana na kuwa karibu na wenzake hao.

  Inadaiwa aliiweka sumu katika chakula na kushiriki nao kwa pamoja bila wao kujua kinachoendelea. Baada ya kula chakula hicho, watoto hao walianza kujigaragaza chini kwa maumivu huku wakiishiwa nguvu na kupoteza fahamu, ndipo uongozi wa shule ulipowakimbiza hospitalini kupata matibabu.

  Baba mzazi wa binti huyo, mkulima wa Nkwenda wilayani Karagwe, Ibrahimu Seleman alisema tangu awali amekuwa akiwasiliana na uongozi wa shule baada ya kujua taarifa za mwanawe kuendelea kuwa na uhusiano ya mapenzi na meneja huyo ambaye alifunguliwa kesi namba 257/2008 katika Mahakama ya Wilaya na kuachiwa kwa dhamana, lakini hakukoma kuendelea na mapenzi na binti huyo.

  Agosti 28, mwaka huu, baba huyo alipokea ujumbe wa simu kutoka kwa binti yake aliyedai anaumwa kichwa, na kutokana na ujumbe huo aliwasiliana na uongozi wa shule kujua kilichompata. Aliambiwa mtoto wake haumwi, bali alikuwa amenyang’anywa simu na mkuu wa shule iliyodaiwa kununuliwa na Laizer na kwa hasira mkuu huyo wa shule aliitupa chini na kuivunja vunja.

  Septemba mosi, baba huyo alisema alipokea simu kutoka kwa uongozi wa shule hiyo na uongozi wa Polisi wakimjulisha kuwa mwanawe amekula sumu na amekimbizwa hospitalini, hali iliyosababisha baba huyo kufunga safari kutoka wilayani Karagwe hadi Bukoba kumwona mwanawe. "Nilipata mshtuko kusikia mwanangu amekula sumu.

  Jana saa sita za mchana mimi na mamake tulifika hapa Bukoba kumwona, lakini sikukuta mgonjwa, bali nilikuta wagonjwa… inashangaza mwanangu sijazungumza naye, mama yake ndo anaongea naye kwa sababu kuna mengine labda hawezi kuniambia.Taarifa niliyosoma aliyoandikisha polisi inasikitisha,” alisema mzazi huyo. Juni mwaka huu, polisi walimkamata meneja huyo wa BUWASA kwa tuhuma za kubaka na kumweka kinyumba mwanafunzi huyo na alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba Julai 2, mwaka huu. Alikana mashitaka na aliachiwa kwa dhamana yenye thamani ya Sh milioni moja.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nachanganyikiwa; Alitaka kumsaidia kujiua au alitaka kumuaa? Kwa nini alimbaka wakatiw alikuwa na uhusiano wa kimapenzi?
   
 3. mohammedzahor

  mohammedzahor Member

  #3
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna refu lisilo na mwisho, hapo sheria ichukue mkondo wake mana inawezekana wamemtengenezea zengwe, siamini kama mtu mwenye akili zake amsaidie mwanafunzi kujiua. ila msema kweli ni mkono wa sheria.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Something is missing somewhere.... look like huyo mtoto hajatulia na kulichomplekea kunywa sumu ni huko kunyang'anywa simu. Baada ya noma kubumbuluka noma lote akamsukumia meneja.


  Its really pathetic!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nooooo, tumpe huyu meneja muda mpaka Juni mwakani amlishe chakula bora, kumtunza na kusafisha sumu ya huyu Mwanafunzi na tumuachie huru meneja kwa kufuata haki za ubinadamu kama tamko la Raisi kwa watuhumiwa wa EPA linavyosema!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  Wenye haki za binadamu ni mafisadi tu waliokuwa ndani ya chama au serikali ama mafisadi ambao ufisadi wao uliwashirikisha mafisadi toka chama na serikali, lakini kama hukuwa huko wewe huna haki za binadamu utasulubiwa mpaka ujute kuzaliwa.
   
 7. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Huyo mwanafunzi naye anaonekana ana akili pungufu (IQ ndogo) au anasumbuliwa na utaahira wa aina fulani. Itakuwaje apokee sumu na kukubali kuitumia kwa lengo la kuondoa maisha siyo yake tu, bali pamoja na wenzake wawili wasiyo na hatia?
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hauwezi kuwa na mapenzi na mtu aliye na umri chini ya miaka 16. Inaitwa ni statutory rape maana inaaminika kuwa hajafikia umri wa kujiamulia baya na zuri. Ukitembea na msichana au mvulana aliye chini ya umri huu. Umembaka, period.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana ukitembea na msichana wa umri huu inahesabika kuwa umembaka. Bado ni mtoto na ni rahisi kurubuniwa.
   
 10. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  sijaelewa! kubakwa zaidi ya mara moja? katika kanisa katoliki kuna dhambi ambayo ni ngumu kuithibitisha, nayo ni kubaka. inatakiwa anayebakwa apambane kufa na kupona na hata ikiwezekana ajeruhiwe na ikibidi afe kama shahidi kuliko kukubali dhambi hiyo ya udhinifu. sasa hili la dada zetu kudai kubakwa wakati amefanya hilo tendo kw akuridhika mpaka mara 4 au zaidi , halafu baadaye anadai amebakwa baada ya kunyimwa simu ndo sielewi.

  inatokea mwanaume anambaka msichana, kile cha kwanza halafu msichana anachia sauti ya furaha kabsaa... ahaaa, ahsante sanaaaaaa. kesho yake yuko mahakamani! sijui wanasheria nisaidieni.
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hauko pekeyako unaechanganyikiwa!mfano pale unapompa mimba mwanafunzi tumeona watu wamefungwa miaka 30! Yaani the unbornchild hatapata matunzo ya baba yake for the coming 30 years bora basi serikali ingekuwa inawagharimia hawa watoto baba zao wanao kula mvua thelathini lakini wapi! Hivi wenzangu mnaionaje hii?Hawachanganyi na nyie?
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  I beg to differ! Kwenye nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendela utakuta age of sexual consent ni miaka 16 na kuendelea. Cheki hapa http://www.ageofconsent.com/ageofconsent.htm

  Kwa hiyo, suala la kubakwa kiujumla halina uzito. Ile kwamba amepewa sumu, alijua kwamba ni sumu, na aliitumia kwa makusudi kwa lengo la kujiua yeye mwenyewe na isitoshe wenzake wawili wasiyohusika ni ishara tosha kwamba huyu denti lazima atakuwa na matatizo fulani ya akili.
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hakuanza naye leo. Aliishafunguliwa mashitaka lakini bado akaendelea na uhusiano! Kwa vile hatujui basdei yake ilikuwa lini basi wengine tunaassume kuwa uhusiano ulianza hata kabla hajaingia hiyo miaka 16! Sasa labda uniambie kuwa age of consent kwetu ni miaka 14!!!
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Huna sababu ya msingi ya ku-speculate mambo ambayo yapo beyond factual basis kulingana na taarifa husika. That said, let us limit ourselves to what is contained in the news article provided. That should be our only point of departure. Msichana ana miaka 16, na hatufahamu ana mimba ya muda gani. Inawezekana kabisa mhusika alianza uhusiano wa kimapenzi na huyo msichana baada ya binti kufikisha miaka 16... and he therefore deserves the benefit of the doubt. At any rate kama nilivyosema, hiyo siyo sababu ya msichana kukubali kupokea sumu ili ajiue wakati akijua kwamba ni sumu; na kutaka kuwaua wenzake wawili. Msichana yoyote wa miaka 16 ana akili tosha kuelewa kwamba hiyo si sawa.
   
 15. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu kina kosekana kwenye hii habari......

  Habari hii imechanganywa changanywa..
   
 16. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni umri gani kisheria mwanamke anakuwa sio mtoto tena na hivyo anaweza kujua baya na zuri ili kujiamulia kuolewa na kuanza kujamiwa kihalali na mumewe?
   
 17. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hiyo kusema kweli sina uhakika kisheria ni umri gani (it appears to be either 16 or 18-years-old depending on which source you choose to go with). All the same, argument yangu n kwamba independent of age of consent, binadamu wa wastani wa miaka 16 anategemewa kuwa na moral judgement inayotosha kumfanya aelewe kwamba si sawa kukubali kupokea sumu na kuitumia kuondoa maisha yake binafsi na wenzake wawili wasiyo na hatia.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Haya mwenye facts, tuambie huyu msichana alizaliwa lini? Swala si kuwa mtoto wa miaka 16 ana akili tosha au la, ni sheria inasemaje! Mbele ya sheria msichana wa miaka chini ya hii hana kibali cha kufanya mapenzi hasa na mtu aliye na umri zaidi ya hapa. Mbele ya sheria msichana aliyechini ya umri huu , (hata kama ana matiti na anapasua darasani) bado hawezi kutambua kikamilifu kati ya kitu kibaya na kizuri. Si kuwa ni mazezeta bali hawajakomaa.

  Hao prosecutors si wajinga kumshitaki mtu kwa kubaka kama alikuwa anatembea na mtu aliyevuka age of consent! Hii ni factual basis kulingana na taarifa husika!
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Pointi yangu ni kwamba: kumshitaki mtu kwa "kubaka" ni independent na mlalamikaji kujaribu wakati huohuo kuondoa maisha yake mwenyewe na wenzake wawili wasiyo na hatia, ambayo relatively speaking in fact ni makosa makubwa zaidi ya jinai (felonies) ukilinganisha na shitaka la kubaka in isolation, au siyo?
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu! Hata wapenda kunyonga wamarekani wamekubali kuwa mtu aliye chini ya miaka 16 hastahili kunyongwa hata akifanya nini! Huyu ni mtoto bado na si ajabu kwa akili zake alikuwa anaona ndiyo anaonyesha mapenzi kwa huyo jamaa. Nadhani kubaka nayo ni felony. Miaka 30 si mchezo katika jela zetu. Kwa upande ni sawa na hukumu ya kifo.
   
Loading...