This is my true story

This is my true story

Pole sana mawazo ya Mungu s ya mwanadamu wakati wewe unawaza mtakavokuwa mnazeeka pamoja Mungu alishajua n mda gani atamchukua,hyo hyo Mungu alikufanya uzoee mapema maumivu maana yangezid zaid kama bado mgekuwa wapenzi kuna vitu Mungu anatuepusha bila sisi kujua,ko endelea kumshukuru Mungu yeye ndo anajua
 
We boya kweli man

Unamsomesha mtu huna hata mkataba nae, na biashara ukamfungulia

Wenzako huwa wanazalisha kuanzia watoto wawili ndipo mwanamke anapelekwa shule.

Hayo matatizo ulijitakia mwenyewe uache kutulikia hapa.
Jamn muacheni mwenzenu tunatofautiana kwa jinsi walivokuwa ilikuwa halali yake kufanya hayo yote
 
Mkuu kwanza pole sana, but inaonekana ndio first time kuwa katika mahusiano lakini humu ndani wadau mbali mbali kila siku wanatoa mabandiko kuhusu suala la kusomesha mpenzi wengi wamelia na kusaga meno so watu tujifunze kupitia mabandiko aya ila ulijiwekeza sana kwa uyo janeth lakini hawa wanawake sijajua wana shida gani hatujui waliongea nini na shetani siku ile all in all tafuta mke oa maisha yaendelee
Yaan ukiona mwanaume yule mwenye mwanamke mmoja ujue amependa kwel sema tatizo moyo wa mtu n kichaka
 
Ungetia mimba kwanza walau uache chata au unfeoa then ndio uende kusoma. Mimi huwa siamini long distance relationship.

Bro mwanamke anahitaji afanyiwe maamuzi ya haraka haitaji kusubiri subiri ni wachache wenye uwezo huo wa kusubiri. Muda alokya anasoma ameshakusubiri vya kutosha yeye anamaliza chuo anajua kuna kitu anategemea kuja kukipata. Anategemea atakua free na wewe. Anategemea mtakua na muda mzuri pamoja. Anategemea hakutakuwa tena na zile discussion zilizokuwa zinambana mpaka akawa anakukosa. Sasa wakati yeye anawaza ivyo wewe ndio unanenda kusoma tena nje ya nchi. Anafahamu vizuri vyuo jinsi vilivyo kwa sababu hata naye amepita humo.

So mi nahisi yeye ndio aliona anaelekea kukupoteza na ndio maana alifanya uamuzi wa mapema aloona unamfaa yeye.

Mwisho pole sana. Piga moyo konde songa mbele mkuu.
Hilo nahis nalo lilichangia mtu anapokuwa amesoma amepata kazi kifatacho n familia sasa wakati unawaza hvo mwenzako ndo anadai kusoma tena ,hlo jambo la ww kusoma tena kuna jinsi lilimwaribu kichwa ogopa psychology kwa hyo na ww kuna namna ulichangia
 
Kilichoniuma hapa ni janeth kufa tu.

Yaliyobaki wacha yakupate, wanaume hamjui mnataka nini mkikutana na waliopambana wakajisomesha mnaleta nyodo

Kazi ya mwanaume ni kutoka mahari na sio kumsomesha Mke ambae huna uakika kama utamuoa.

Ahaaa mbavu zangu, eti mchumba yupo nje anasoma au anafanya kazi nikisikiaga huu upuuzi napatwa na hasira, jitu unalisubiri miaka yote kwa uaminifi mara unaskia ana mzungu, Mara mtoto.

Ndugu mwanasheria, wacha yakupate tugawane maumivu

Dhambi ya usaliti haiwezi mwacha mtu salama, janeth ulipendwa ilibidi upendeke, rip janeth.
We Mbona unakua katili kwa mtoto wa mwanamke mwenzako yaani unamcheka
 
Acha mambo ya kuweka shada la maua, utasababisha awe anakutukana tu huko aliko maana hakupendi.
 
Ndugu zangu mimi naishi Mwanza na nafanya kazi serikalini(Mimi sina wazazi na ni pekee kwa wazazi walionizaa na hata walionilea...pia walionilea walishatangulia mbele za haki).... nimeona leo nilete mkasa wangu wa mapenzi hapa ijapokuwa huwa sipendi kukumbuka haya machungu kwani huwa naumia sana kupita kiasi ila nimeona tu nilete kwani naamini wengi mtajifunza na kuwa makini kutokana na haya yaliyonikuta mm mwenzenu, huu mkasa ni wa kweli kabisa haya ndio yaliyonikuta mimi na kuniacha na jeraha la moyo milele, wema wng umegeuka kuwa moto wa kunichoma mimi...ninayoyaandika hapa yote ni ya kweli sijaongeza chochote na ni story ya kweli kabisa ya maisha yangu mimi....huwa namuomba MUNGU kila siku aniponye(Kwa ambao mnajua maana ya kupenda mtaelewa story yng ila ambao hamjui maana ya kupenda hamtanielewa)

Ndugu zangu kweli waliosema umdhaniaye kumbe siye hakika hawakukosea ilikuwa mwaka 2010 nlipoanza mahusiano na huyu msichana, hakika mwanzoni alionyesha sana kunipenda na mimi nilimpenda kwa dhati na kweli, nilimjali na kumthamini kwa moyo wangu wote, alichotaka nilimpa kwa wakati bila kuchelewa. Wanawake wote niliona hawana maana zaidi yake, kiukweli nilimpenda sana Janeth, kwa muda wote niliokuwa nae sikuwahi kuwa na msichana mwingine zaidi yake nilikuwa muaminifu kwake asilimia 100 huu ndio ukweli ndugu zangu ila kumbe mwenzangu alikuwa anakuja kubadilika daaahh....niliziba masikio kwa yote niliyokuwa nasikia juu yake mimi, nilipenda nikawa kipofu. Janeth mpenzi wng alimaliza kidato cha sita ila hakufanikiwa kufika kiwango cha kwenda chuo na alikaa nyumbani mwaka mzima kwakuwa nyumbani kwao hawakuwa na uwezo wa kumsomesha chuo bila mkopo, basi kwakuwa alikuwa ameshanitambulisha kwa mama yake(Alikuwa anaishi tu na mama yake na wadogo zake wawili) basi kwakuwa nilimpenda kweli nikaamua kumsomesha chuo diploma chuo cha St Augustine, alifurahi sana na kuniahidi kwamba atanipenda milele na atazidi kujitunza kwaajili yangu basi ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa kumi ndipo alipoanza chuo na alichukua kozi ya diploma in law(sheria) ambayo ndio fani yangu na alipenda kusomea nilichosomea....basi mapenzi yetu yaliendelea kama kawaida nikaamua kumfungulia duka la nguo za special na viatu karibu na stendi ya Nyegezi ili pia imsaidie kumuongezea kipato akiwa anasoma, na akiwa mwaka wa kwanza ada yote ya chuo nilifanikiwa kumaliza na ela ya matumizi na mambo mengine huwa nlikuwa nampa hata asiponiomba....kiukweli Janeth nilimpenda nikafa nikaoza mimi hata kwao mama yake nlikuwa namjali sana.
Nashukuru MUNGU maendeleo yake ya chuo yalikuwa mazuri alionyesha bidii hasa na hata biashara niliyomfungulia aliiendeleza vizuri ijapokuwa alimpa rafiki yake auze, nami kuona huyu mwanamke ana bidii nilifurahi sana na kuona kweli nimepata mke, basi nikaamua kumnunulia kagari tu kadogo kakutembelea(Toyota Spacio) ili imsaidie mizunguko yake ya hapa na pale nikampeleka driving school kila akitoka chuo jioni anaenda, alipomaliza driving school tu nikamkatia leseni. Sasa akawa akijisikia kuendesha gari langu anaendesha au la kwake hivyohivyo tu,tunabadilishana...mapenzi yalinoga tulipendana hadi tulifanana...hadi ninapoandika hapa naumia sana moyoni nikimkumbuka Janeth wng....miezi ikasonga ikafika mwaka 2013 akafanikiwa kumaliza chuo na akapata G.P.A ya 4.2 kiukweli alikuwa smart na ndipo nlipoamua kumpa zawadi ya kumfungulia tena biashara nyingine ya duka la vipodozi huku nikihangaika kumtafutia kazi ya alichosomea. Kiukweli MUNGU ni mwema nlifanikiwa kupata nafasi ya legal officer katika kampuni moja ya ulinzi hapa mwanza hiyo ilikuwa mwezi wa kwanza mwaka 2014 mwezi wa kwanza....ilipofika mwezi wa tano nliamua kuendelea kujiendeleza kimasomo kwa kuamua kwenda kuchukua masters degree nchini Marekani na nikamuahidi mpenzi wangu Janeth nikirudi tu tutafunga harusi rasmi..mpenzi wangu alilia sana na kunisihi nisiondoke, nakumbuka tangu nilipo mwambia hivyo alikosa kabisa hamu ya kula ila mm ni mwanaume nilimbembeleza sana na alinielewa.
Siku ilipowadia mimi kuondoka niliondoka huku nikimuacha mpenzi wangu akiwa na majonzi nami kwenye ndege nilijiona sijakamilika kuwa mbali na yeye ila nilipiga moyo konde kumbe bila kujua mpenzi wangu sitamuona tena daaahhh, kweli waliosema usilolijua ni usiku wa giza waliona mbali. Nilipoondoka Janeth nilimsihi sana awe makini na kazi, awe makini na biashara, mali zangu zote niliziacha chini ya uangalizi wake kwani kila kitu changu mimi nilikuwa nachukulia ni cha sisi wote na nyumba yangu nlimwachia.
Sasa kizaazaa kinaanzia hapa nikiwa masomoni mwanzoni tulikuwa tunawasiliana vizuri tu kwa video calls, chats za kawaida na kadhalika ila baada ya kama mwaka hivi Janeth wangu alianza kubadilika kitu ambacho kilinipa wakati mgumu sana, alikuwa hanitafuti hadi mm nianze kumtafuta, na tukichat ananijibu short tu na nikimuuliza nn tatizo mbona umechange hivyo kama kuna tatizo niambie ananiambia tu hamna tatizo nipo sawa basi nikaendelea tu kuvumilia hivyohivyo.
Sasa kuna rafiki yangu wa karibu sana nikawasiliana nae na nikampa kazi amfuatilie mpenzi wangu ili kama kuna cha tofauti ambacho anafanya huyu mpenzi wangu basi anijulishe...na kweli ndani ya wiki mbili huyu rafiki yangu MUNGU alimsaidia kujua ukweli kwa kufuatilia habari za mpenzi wangu kazini kwake na kuambiwa kwamba huyu mpenzi wangu Janeth anatembea na boss wake na zaidi ana mimba ya miezi 6......ndugu zangu acheni tu nilipopata hizo habari niliishiwa nguvu kiasi cha kupoteza fahamu na nilikimbizwa hospitali na nilikuja kuzinduka baada ya masaa mawili lkn nilipatiwa matibabu vizuri na kupata nafuu na niliamua kumfungukia Janeth na alipoona nimejua alikuwa mkali kupindukia akaniambia hanitaki tena mm tena nimkome niliumia sana kwakweli ndugu zangu maumivu niliyoyapata ni zaidi ya msumari wa moto uliowekwa kwenye kidonda kibichi..basi kwakuwa nampenda sana nlipoona amechukia kwasababu ya kumwambia hivyo nlijitahidi tu hata kujishusha tu na kumuomba msamaha ijapokuwa yeye ndio kanikosea ili tu tuendelee na uhusiano wetu kama mwanzo ila huwezi amini alikataa kata kata na kunitukania hadi wazazi wangu waliofariki na kusema mm simfai tena...basi nlikata tu simu huku nikiwa kwenye maumivu makali.
Baada ya siku kama tano hivi nilimtafuta tena kwenye simu bila mafanikio ila hakupatikana tena.
Basi nlijaribu tu kuwasiliana na huyu rafiki yangu wa karibu ili ajaribu tu kumtafuta mpenzi wng na aongee nae ili amshauri kurudiana na mimi ila huwezi amini rafiki yangu aliniambia alivyomgusia hilo suala tu alimtukana sana na kumpa onyo asimfuatilie maisha yake na ameamua kuachana na mimi na kesho yake alienda akamkabidhi huyu rafiki yangu funguo za nyumba yangu na akahamia rasmi kwa bosi wake wakaendelea kula maisha.
Basi tu nliendelea kumtafuta kwenye simu bila mafanikio,aliamua kubadilisha kabisa mawasiliano kwani aliona namsumbua. Basi kutokana na watu walivyonishauri na kuniombea niliimarika siku hadi siku na maumivu kupungua moyoni mwangu, huwezi amini ndugi yangu nilikonda kwa mawazo ila afya yangu ilirudi kidogokidogo na hatimaye nilimaliza masomo yangu na kurudi nyumbani Tanzania na kukuta habari ya kuhuzunisha zaidi kuhusu mpenzi wangu Janeth kwamba amefariki wakati wa kujifungua na mtoto pia alifariki na biashara zangu na zake nilizomuachia zote zimefilisika na huyo boss wake ambaye walikuwa wakiishi wote amefungwa kwa kosa la kutembea na kumpa mimba mwanafunzi(ambaye ni mtoto wa kigogo mmoja hapa Mwanza) hadi sasa yupo gerezani anatumikia kifungo
Ila kilichoniuma zaidi ni kumpoteza mpenzi wangu Janeth, nilimpenda sana kwa moyo wangu wote, mm siwezi kumuhukumu kwani siwezi jua nini kilimkuta au alifanyiwa nini hadi akanifanyia vile kwani dunia ina mengi ndugu zangu unaweza kukuta hazikuwa akili zake. Sijawahi kupenda kama nilivyokuwa nampenda Janeth hadi sasa.
Na kila ikifika tarehe 23 mwezi wa nane wa kila mwaka(Siku ambayo Janeth alifariki) huwa ni lazima nikaweke shada la maua juu ya kaburi lake na kufanya maombi.
HAKIKA SITAMSAHAU, MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.View attachment 1147007
Usihudumie K kama hujaiwowa au hujaifunga iwe yako wengine wale kwa macho
 
Mshukuru mungu alifariki ungekufa ww maana kwa stress za kumwona kapendeza alaf yupo na mtu mwingine
alaf muache uboya mchumba hasomeshwi mnakwama wap
 
Wacha weee, kwa hyo ninavyokuhudumia mm ni boya
Endelea kumhudumia tu maana hata wewe heshima unataka akupe kabla haujamuoa wakati maandiko yanasema mke anatakiwa amheshimu mume na siyo mchumba ila yeye anakuheshimu wakati bado siyo mume ni mchumba kwahiyo na wewe endelea kumhudumia tu mkuu
 
sijamaliza kusoma..paragrafu ya pili tu nimegundua ni yale yale..MCHUMBA HASOMESHWI.
 
Pole mkuu, ilikuwa inatakiwa anapomaliza diploma namimba awe nayo changa, ULIBUGI SANA KAMANDA WAZAMU
 
Pole Sana ila inabidi u let it go don't go to her grave delete all necessary reminder of her. Haikua liziki yako hiyo. Mungu hakukupangia wewe na Janet muwe mke na mme. Ila yupo mkeo ambaye Mola amekupangia lakini wewe ndio kikwazo .God is waiting for u to finish ur mourning ili akukutanishe na mkeo halisi ambaye mtatengeneza future together. Stop crying standup and move on.
 
Hii nkiandika movie lzima itauza sana,it's too emotional,pole lakini.
 
Mimi mke wangu simwamini na huwa namwambia kabisaa sijawahi kumwamini mtu wa aina yake katika maisha yangu...kwa hiyo anakaa mguu ndani mguu nje.
 
Back
Top Bottom