X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Kanuni ya pili ya Thermodynamics yakanusha Evolution
Evolution Deceit. com - This website is the interactive version of the book "Evolution Deceit" by HARUN YAHYA
KANUNI (Law) ya pili ya Thermodynamics ambayo inatambulika kama moja ya kanuni za msingi za sayansi ya fizikia, inaeleza kuwa katika hali ya kawaida, mifumo yote ikiachwa (bila uangalizi) huwa na kawaida ya kuvurugika, kutawanyika na kuharibika katika uwiano sawa na kiwango cha muda kitakachopita.
Vitu vyote, vyenye uhai na visivyo na uhai, huchakaa, hupungua, hupukutika na hatimaye huharibika na kuisha. Hii ndio khatma ya kila kitu. Na zaidi ya hivyo, kanuni hii inaeleza kuwa mweleko huu hauwezi kurudi nyuma.
Mfano, ikiwa gari jipya kabisa litapelekwa likatelekezwa Jangwani kwa miaka kadhaa, basi itakuwa ni jambo la kustaajabisha iwapo mtu atarudi baada ya miaka kumi na kulikuta liko katika hali nzuri kuliko lilipoachwa. Hii ni kwa kuwa mategemeo ni kulikuta lishachakaa, limejaa kutu, matairi yashapasuka, springi nyingine zimefyatuka, rangi imekoboka, na kadhalika. Ama kwa viumbe hai, basi hali huwa mbaya zaidi. Kazi ya kuoza ni kubwa na mara moja huyo kiumbe hupotea.
Kanuni hii ambayo pia hujulikana kama "kanuni ya Entropy" inaeleza kuwa ulimwengu wote unaelekea katika hali ya kuvurugika na kukosa mpangilio zaidi na zaidi kadri muda unavyopita.
Ukweli wa kisayansi wa kanuni hii umeshathibitika na nadharia hii ni yenye kukubaliwa na ulimwengu wote wa kisayansi. Albert Eistein ameeleza kuwa ndiyo "kanuni kuu ya sayansi yote".
Lakini hapa wa-Darwin wamekuwa kisiki cha mbanga kwani nadharia yao inakwenda kinyume na kupingana moja kwa moja na kanuni hii muhimu.
Kama ilivyoelezwa huko nyuma, nadharia ya mnyumbuliko wa viumbe inaeleza kuwa chembe za maada (atoms na molecules) zisizokuwa na mpangilio wala mfumo, zenye kutawanyika na zisizo na uhai zikajipangilia, zikaungana na kuunda chembe kuu zenye miundo ya hali ya juu na ya kustaajabisha kama vile chembe za protini, DNA na RNA. Kisha hizi zikajipangilia zikaunda chembe hai (cells) na baada ya hapo zikaibua mifumo ya hali ya juu ya viumbe hai vya wingi wa aina kwa mamilioni.
Navyo viumbe hivyo vikapangika katika mifumo ya maisha ya kustajaabisha yenye kuhusiana vizuri kabisa na mazingira yao na vyenyewe kwa vyenyewe. Kama vile nyasi kuwa chakula cha swala na swala chakula cha simba na simba chakula cha nyasi na kadhalika.
Maana yake ni kuwa kutokana na hali ya mvurugiko unapatikana mpangilio, tena wa hali ya juu kiasi kisichokadirika kiakili. Hivi leo, wanasayansi wa dunia, pamoja na wanafikizia wa fani mbalimbali za kitaaluma wanahangaika kutafuta njia ay kuondoa tatizo la kuharibika mazingira ya dunia yanayotokana na maendeleo yaliyoyaleta na wanashindwa kabisa. Matokeo yake mazingira yanazidi kuharibika. Lakini wa-Darwin na wa-Maada wengine wanaamini kuwa mifumo mizuri ya mazingira tuliyoikuta imeibuka yenyewe tu.
Lakini wa-Darwin wenyewe wanakiri kigingi hiki kinavyowakwaza. Wanasayanasi. Mwanamnyumbuliko, Roger Lewin anaeleza kama alivyonukuliwa na Dr. Harun Yahya katika Evolution Deceit: The Scientific Collapse of Darwinism and its Idiological Background, uk. 115. log to the website: http://www.evolutiondeceit.com/
"Tatizo moja linalowakabili wanabailojia ni ule mgongano unaoonekana baina ya "evolution" na kanuni ya pili ya thermodynamics. Mifumo inatakiwa ivurugike na kutoa mpangilio hafifu, sio mpangilio bora zaidi".
Naye George Stravropoulos amenukuriwa na Harun Yahya akieleza: "Mpaka sasa imeshindikana kuielezea photosynthesis na mifumo yote ya uhai na kwa mnasaba wa thermodyanamics, pamoja na lugha zenye kukanganya kutumika".
Baada ya kukwama huku, Wa-Darwin wamekosa njia. Lakini kwa U-Darwin si sayansi bali ni "dini", bado inang'ang'aniwa pamoja na kukanushwa na sayansi kwa mara nyingine tena. M-Darwin maarufu Jeremy Rifkrin anatangaza imani yake kwa lugha ya kifamaji kama ifuatavyo:
"Kanuni ya Entropy inasema kuwa Evolution ina kunywa nishati yote inayopatikana kwa ajili ya uhai katika sayari hii. Dhana yetu ya Evolutilon ni kinyume kabisa cha hivyo. Tunaamini kuwa kinamna fulani Evolution kimiujiza inaunda ubora mkuu zaidi na mpangilio hapa duniani".
Wanamnyumbuliko ni mabingwa wa kughushi:
http://www.evolutiondeceit.com/chapter9.php
Wakiwa wanaelewa vyema kuwa nadharia yao haina mashiko kisayansi, wana nadharia hawa hawakuishia kufanya juhudi kutafuta ushahidi wa kisayansi. Bali pale wanapokwama basi huwa tayari kutumia mbinu yoyote ili mradi kuipa uhai nadharia yao, na walau kuughilibu umma.
Kwa mfano, wananadharia hawa wana kawaida ya kutoa michoro ya uongo na ya kubuni ya viumbe vya kubuni wanavyodai kuwa eti viliishi zamani. Hawakukosa hata kughushi michoro na kuunda mafuu ya bandia katika majaribio yao ya kuuhadaa ulimwengu.
Miongoni mwa wa mwanzo kabisa kukamatwa katika njama hizi ni mwanasayansi wa zama za mwishoni mwa karne ya 19, Ernest Haeckel. Bwana huyu alibuni nadharia ya uongo kuwa vichanga vya viumbe hai matumboni mwao hupitia hatua zile zile ambazo viumbe hao walipitia katika historia ya kunyumbulika kwao.
Katika kuthibitisha nadharia yake hiyo, Bwana huyu alichora michoro ya uongo ya vichanga katika hatua mbalimbali ili kuonesha kitangulizi cha mimba (embryo) cha mwanadamu kwanza kilionesha hali ya samaki, kisha ujusi na hatimaye ubinadamu. Nadharia hii imeshathibitishwa kuwa ni upuuzi usio na maana. La kushangaza ni kuwa mpaka leo hii nadharia hii, ujulikanayo kama "Recapitulation" inafundishwa mashuleni hapa kwetu Tanzania.
George Geylord Simpson, mwana mnyumbuliko maarufu anaeleza katika An Introduction to Biology kilichochapishwa New York, uk. 241:
"Haeckel ameieleza visivyo kanuni husika ya "evolution". Imekwishathibitika bila shaka vichanga havipitii hatua za mnyumbuliko (za wazazi wao)".
Lakini Hackel alithibitika kuwa alighushi michoro yake katika uhai wake. Katika utetezi wake ulionukuliwa na Francis Hitching katika The Neck of the Giraffe: Where Darwin Went Wrong, New York, 1982, uk. 204 alieleza kama ifuatavyo:
"Baada ya kukiri kuwepo kwa "ghishi", ilibidi nijichukulie kuwa mwenye kuhiliki na kuangamia lau kama nisingekuwa na faraja ya kuwaona pamoja nami ndani ya kizimba wahalifu wenzangu, miongoni mwao wakiwemo wengi wa watafiti wenye kuaminika na wanabaiolojia wa kuheshimika. Mingi ya michoro yote katika vitabu bora kabisa vya bailojia, rejea na majarida vingestahili kutuhumiwa kwa ghishi kwa kiwango kile kile (ninachotuhumiwa), kwani yote hiyo si sahihi, na pia "imerekebishwa", imepindwa kwa makusudi na umeundwa (ili ilete sura zinazokidhi haja)."
Mfano mwingine wa visa vya wa-Darwin kughushi data za kisayansi ni ule wa fuu lijulikanalo kama "Piltdown man". Hili lilikuwa si chochote bali ni taya la Orang-utan lililounganishwa kwa makusudi na fuvu la mtu. Ulimwengu wa sayansi uliliamini fuvu hili ukiamini ni fuvu la mtu wa kale aliyekaribiana na masokwe watu. Kwa miaka 40 wa-Darwn walijitapa juu ya mafanikio yao katika kuthibitisha mnyumbuliko wa watu kutoka masokwe mtu.
Mgunduzi wa fuu hili alikuwa Dr. Charles Dawson mwaka 1912, si mbali sana na kipindi cha ghishi cha Haeckel, katika eneo la Piltdown huko Uingereza. Fuvu hili lilikuwa na mvuto mkubwa kwa wanasayansi. Jumla ya tafiti za shahada za udaktari (PhD) 500 zilifanywa juu ya fuvu hilo na maisha au kunyumbulika kwake zilifanywa katika vyuo vikuu mbalimbali duniani.
Ni mwaka 1953 ndipo ghishi hii ilipogunduliwa na kutangazwa. Fuvu hili lilikuwa la kichwa cha mtu aliyekufa miaka elfu kidogo iliyopita na taya la Orang-utan aliyekufa hivi karibuni. Meno ya fuu hilo yalikuwa ya Orang-utan bali yalisuguliwa kwa chuma ili yaelekeane na meno ya mtu. Meno hayo yalipangwa katika taya kwa ustadi mkubwa nyufa zikazibwa. Pia utafiti uliofanywa juu ya zana mbalimbali za "kale" zilizo "kutwa" pamoja na fuu hlo ulionesha kuwa hazikuwa bali ni ghishi zilizochongwa leo.
Baada ya ugunduzi huo, fuu hilo liliondolewa upesi upesi kutoka katika jumba la makumbusho la Uingereza(British Museum) lilimowekwa kwa miaka 40.
Darwin na kashfa za ubaguzi wa rangi
Katika kitabu chake The Descent of Man kilichochapishwa baada ya kile cha Origin of Species, Darwin anaeleza kuwa watu wa rangi tofauti wamo katika hatua tofauti za maendeleo ya viumbe. Na kwamba wazungu ndio walioendelea zaidi na bora zaidi, bali Waafrika na Aborigines wa Australia wao bado wako katika hatua za usokwe mtu.
Darwin aliamini kuwa watu wa makabila haya ya nyuma kimabadiliko hatimaye watafutiliwa mbali na wale walio mbele zaidi. Darwin alisema:
"Katika kipindi fulani kijacho, ambacho si mbali sana ukipimia kwa karne, makabila (races) ya kistaarabu bila shaka yoyote yatayafuta na kuchukua maeneo ya makabila ya kishenzi duniani kote... tofauti iliyopo baina ya watu walio bora zaidi, kama tunavyoweza kutaraji, zaidi hata kuliko nyani, badala ya ilivyo sasa katika Waafrika au a Australia na Magorilla."
Tazama: Charles Darwin katika The Descent of Man, chapisho la 2, 1874, uk. 178.