Theory ya Darwin imechangia kwa sehemu kubwa ubaguzi wa rangi

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Ubaguzi wa rangi ulikuwepo muda mrefu sana kabla ya Darwin na theory yake au kuja kuipa nguvu maana inasemekana yeye sio mwanzilishi, lakin pindi tu ilivyo kuja huyu bwana na habari zake ubaguzi wa rangi uliongezeka kwa kiwango kikubwa.

Katika kitabu chake cha 1871 The Descent of Man Darwin alikuja na kitu kinacho itawa ‘survive for the fittest. Akimaanisha kuwa maendeleo ya mabadiliko kwa viumbe yalitegemeana na uwezo wa kiumbe husika kupambana na mazingira yake.

’ Yaani aliyekuwa na nguvu ndiye aliyeishi, aliyeweza kuhimili misukosuko mbalimbali ndiye aliyeweza kubadilika kutokana na mazingira hayo na kuhama kutoka kiumbe kimoja kwenda kingine.

Pia akaonyesha kuwa mpambano huu ulikuwa hadi kwa makundi ya rangi mbalimbali ya binadamu. Hivyo inaonekana watu wa rangi fulani ni bora juu ya watu wa rangi nyingine kutokana na uwezo wao wa kuhimili mpambano.

Habari hii ikabeba dhana kuwa watu wa rangi nyeupe (wazungu) ndiyo kundi ambalo linaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana kushinda kwenye ‘fight for fittest ,’ wakati watu rangi nyeusi (waafrika) wakiwa wameachwa nyuma katika mpambano huo na hivyo kuashiria kuwa muda si muda watu weusi watafutika kabisa kutokana na kushindwa kwao na watu weupe.

Umeona kwa jinsi gani nadharia ya Darwin ilivyozaa ugonjwa mbaya sana, ugonjwa wa ubaguzi wa rangi, kwani watu wa bara la Ulaya kutokana na nadharia hii ni kuwa wao tayari wamesha fanikiwa na kuendelea katika hali ya ubinadamu kamili, wakati watu wa Afrika wameachwa nyuma na wapo kwenye hatari ya kufutika kama walivyo futika viumbe wengine.Hivyo wakaona kwao ni sawa na haki yao kuwabagua watu weusi kwasababu wapo kwenye 'survive for fittest '

Mwana anthropologist wa India Lalita Vidyarthi anaelezea ni namna gani nadharia ya Darwini ilivyo leta ubaguzi wa rangi kwenye fani ya sayansi ya jamii;

“Nadharia yake (Darwin) ya survive of the fittest ilikaribishwa na kukumbatiwa na wana sayansi ya jamii wa kipindi hicho, na waliamini kuwa binadamu amefanikiwa katika hatua mbalimbali za evolution, mafanikio ambayo yana onekana kwa watu weupe wa Ulaya (Wazungu). Katika nusu ya pili ya karne ya kumi na tisa ubaguzi wa rangi ulikubaliwa kama ukweli wa msingi na sehemu kubwa ya wanasayansi wa Ulaya”

Pia amesema John West, makamu wa rais na mwandamizi katika Taasisi ya Ugunduzi.

"Ubaguzi wa rangi una vyanzo vingi, ambavyo vingi vilimtangulia Darwin, lakini nadharia ya mabadiliko ilitoa nguvu kubwa kwa toleo la kisayansi ambalo bado linatuathiri hadi leo,"

Nawasilisha.

images (13).jpg
 
Adamu na Eva wao walikuwa kundi gani?
Swali hili kwa nani kwangu au wana-Darwinism, kama langu basi jibu langu ni kwamba hawakutokana na mabadiliko yeyote (evolution) na maanisha hawakuwa katika kundi lolote
 
Acha kuwadanganya watu, nadharia(theory) inaitwe Survival of the fitest.na sio survival for the fitest. Kwanza hii nadharia ni ya HEBERT SPENCER ,wala sio Charles Darwin .Theory ya darwin inaitwa NATURAL SELECTION(Preservation of favourable race during struggle for live). Ni kweli ya darwin itumika Adulf hilter Nazism. Lakn Survival of the fitest ilitumiwa na Spencer,karl marx, na communist na socialism.
 
Kwa kifupi theory ya Hebert spences ya Survival of the fitest, ina ondoa ubaguzi(ant-racism), ant-religion inatumiwa mataifa Urusi,china,ukomunist na ujamaa,pamajo vyama kama democratic ya Obama USA. Wakati Social darwinist .inatuka na chama cha repubrica cha D.Trump, US. ,UK, Japan, Ulaya nchi za kifalme.Adulf hilter aliwai sema Germanic super natural race,aliwaua wayahudi(jewish). Kwa hofu wayahudi kuwafuta wajerumani. Theory hii haiwatukuzi weupe bali wayahudi na waarabu ya asian(semic) race.refer God bless shem and extent japhat( white or european)
 
Back
Top Bottom