The World Justice Project Rule of Law Index-2019: Tanzania yashika nafasi ya 91 kati ya Nchi 126 katika Utendaji wa Utawala wa Sheria Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
The World Justice Project Rule of Law Index® inapima ni kwa namna gani Utawala wa Sheria unapatikana na kwa namna gani unavyotambuliwa na Umma kwa ujumla katika Nchi 126 na katika Mamlaka kwa ujumla Duniani kote kulinagana na na Uchunguzi uliofanywa kwenye Kaya 120,000 na Waatalum 3,800

Huku ikijumuisha Data za Msingi, WJP Rule of Law Index inapima Utendaji wa Utawala wa Sheria katika Nchi kwa kuangalia vigezo nane; Kupingana na Mamlaka ya Serikali, Kutokuwepo kwa Vitendo vya Rushwa, Uwazi wa Serikali, Haki za Msingi, Haki Jinai, Haki Madai, Utekelezaji wa Sheria na Maagizo na Usalama


Ripoti kwa Ufupi
Alama katika orodha Mpya WJP Rule of Law Index zinaonesha Nchi nyingi zinashuka kuliko kupanda katika Utendaji wa Utawala wa Sheria Kiujumla kwa mwaka wa pili mfululizo, kitendo kinachoonesha Nchi hizo ziznaelekea kwenye utawala dhaifu wa sheria Duniani

Katika ishara inayoashiria kuongezeka kwa udikteta, alama inayoonesha "Kupingana na Mamlaka ya Serikali" ilipungua katika nchi nyingi kuliko Vigezo vingine Duniani kote mwaka uliopita (Katika Nchi 61 Kupingana na Mamlaka kulipungua, Katika Nchi 23 kulibaki sawa, Katika Nchi 29 Kuliboreshwa)

Kigezo cha pili kilichoshuka katika utendaji wake kwa mwaka uliopita ni Haki Jinai, kikifuatiwa na Uwazi wa Serikali, na Haki za Msingi. Katika Muonekano chanya, Nchi nyingi zimefanya vizuri katika Kutokuwepo kwa Vitendo vya Rushwa kuliko kufanya vibaya kwa mwaka wa pili mfululizo

Nchi za juu zilizofanya vizuri katika Utendaji wa Utawala wa Sheria kwa Ujumla kwa mwaka 2019 ni Denmark (1), Norway (2), na Finland (3); Nchi zilizofanya vibaya na kushika nafasi tatu za mwisho ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (124), Cambodia (125), na Venezuela (126).


Jedwali hapa chini linaonesha alama na viwango vya WJP ya Kielelezo cha Utawala wa Sheria kwa Ujumla kwa mwaka 2019. Alama zinaanzia 0 hadi 1, na 1 inayoonesha kufanya vizuri katika Utawala wa Sheria


1.PNG

Jedwali hapa chini linaonesha alama na viwango vya WJP ya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Mapato ambapo Tanzania ipo katika kundi la Kipato cha Chini lenye nchi 20 ikiwa nafasi ya 7

1.PNG

Jedwali hapa chini linaonesha alama na viwango vya WJP ya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Kupingana na Mamlaka ya Serikali ambapo Tanzania ipo nafasi ya 72 katika Nchi 126

1.jpg

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Kutokuwepo kwa Vitendo vya Rushwa Tanzania ipo nafasi ya 85 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Uwazi wa Serikali, Tanzania ipo nafasi ya 104 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na uteolwaji wa Haki za Msingi, Tanzania ipo nafasi ya 102 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Maagizo na Usamala, Tanzania ipo nafasi ya 77 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Utekelezaji wa Sheria, Tanzania ipo nafasi ya 101 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Utolewaji wa Haki Madai, Tanzania ipo nafasi ya 82 katika Nchi 126

Alama na viwango vya WJP vya Kielelezo cha Utawala wa Sheria mwaka 2019 kulinagana na Utolewaji wa Haki Jinai, Tanzania ipo nafasi ya 83 katika Nchi 126

Kwa taarifa zaidi, soma;
 

Attachments

  • ROLI-2019-Reduced.pdf
    12.8 MB · Views: 1
Duh!, ila hivi ni vigezo vya mabeberu, inabidi Bara la Africa, tutoe African Chatter of African Democracy, African Justice, African Rule of law, na African Human Rights Standards.
P
 
Kumbe hatuko pabaya sana, wanaoangaliwa huwa ni wale watatu wa kwanza na wa mwisho, humo katikati unaweza kuogelea popote na usijulikane.
 
Kinachonishangaza ni kuwa dunia yote inajua kuwa sisi ni nchi ya uchumi hafifu (low income countries) na watanzania tunajua hivyo. Lakini ukiona matangazo ya Serikali hasa wakati wa uzinduzi wa miradi tunayotekeleza, tunajimwambafai kuwa SISI NI MATAJIRI. Hivi kwa nini tunajimwambafaia nani wakati nafsi zetu tunajua sisi ni nchi maskini?
 
Back
Top Bottom