The World is a flat plane and not a globe

The World is a flat plane and not a globe

Haya tunayojadili hapa hayajafafanuliwa na dini.kwa hyo niko free kujadili hapa.

Ingekuwadini yangu imeeleza kwa uwazi basi usingeniona hapa
Wewe si huamini kwasababu ya dini?

Mi nawe tushamalizana ulishanambia jambo lolote ambalo dini itasema we utafata bila kuhoji hata kama ingesema mwanaume aolewe wewe uko tayari kufata, sasa sembuse ushindwe kufata nadharia ya dunia bapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marejeo ya dini kwangu ni utopolo

Unaelewa utopolo ni nini?
Sielewi utopolo ni nini ?

Nimekuuliza kwako wewe marejeo ni nini ? Mathalani unaposema Dunia duara au labda Hakuna Mola muumba, huwa una rejea wapi ?
 
Kwamba mi ndo sielewi au

Jamaa huoni kasema ana marejeo yanayo support argument yake?
Nilichosema kuwa ile kauli ya wazi kusema kuwa dunia duara ama tufe hyo kauli haipo katika Qurani,huwenda kukawa na viashiria ambavyo mtu anaweza kuvitumia kuthibitisha upande wake.

Kama ambavyo mimi naamini kwa mujibu wa viashiria vya Qurani dunia sio kama mpira ni kama sahani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe macho yako tu unavyoona kila siku kipi kikubwa kati ya dunia na jua..?

Yani katika macho yako unavyoona kila siku simu na gari kipi kikubwa kwa unavyoona kila siku?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo macho yako yanavyoona basi kile kinachoomekana ndo sahihi?

Hakuna illusion?

Kuna watu wako bongo hapa wamefanana na jayz, kwaiyo tusitumie DNA tuhitimishe kua jamaa ni mdogo wa jayz kwasababu macho yanaonesha kua wamefanana?

Na rockets ambazo zinapaa angani umbali wa juu ambao huku chini tunaziona ndogo kama mjusi basi kwa kuona huko kulitakiwa tuzione hivyo hivyo hata zikitua ardhini
 
Kwa wenye uhakika na Umbo la Dunia mnaloliamini naomba majibu ya maswali haya. (Mnijibu kutokana na umbo la dunia mnaloliamini)

1. Kwanini tumefundishwa Umbo la Dunia?

2. Kwanini Tulifundishwa Jua limesimama ilhali Tunaliona likitembea?

3. Ni kwa nini Mito mirefu haibadirishi uelekeo wa maji yake? (Kwa waumini wa Dunia Mviringo)

4. Wanaosafiri kwenda anga za mbali, huwa wanaeleekea uelekeo upi, kati ya Kulifuata Jua, nyuma ya dunia kwauelekeo wa Jua lilipo au pembeni mwa dunia?

5. Juu au Chini ya Dunia ni Wapi?

6. Kuna mwenye ushahidi wa umbo la Dunia nje ya Vitabu au teknolojia za Mzungu?

Nitakuwa nimepata kitu hakuongezea uelewa wangu baada ya majibu haya, maana nimekua nikifuatilia Mada hizi ila mwisho wa siku wanaodai wana uelewa wa jinsi dunia ilivyo huwa hawapendi kuhojiwa ili wafunguke.





Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom