Nadhani baada ya Katiba pendekezwa kupitishwa katika Bunge la Katiba umefika wakati sasa kwa UKAWA kutumia busara na hekima za kutosha ili kuipata Katiba ya Wananchi kama ilivyopendekezwa na Jaji Warioba. Kwa mtazamo wangu sioni sababu ya hawa ndugu zetu wa Ukawa kutumia nguvu nyingi kutaka kupambana na mamlaka kwa jambo ambalo tayari limeshapitishwa kisheria ingawa halina uhalali wa kisiasa.
Cha kufanya:
Ukawa watulizane, wajifungie mahali na wafanye kazi ya kuipitia Katiba pendekezwa kwa jicho la kisiasa, kisheria na kisha warudi kwa wanachi kupitia majukwaa halali na kuwaeleza ni nini tofauti ya Katiba pendekezwa vs Rasimu ya Tume. Wawe wa kweli, naamini Katiba pendekezwa ina mazuri yake ingawa pia ina mapungufu ya kutosha, vivyo hivyo Rasimu ya Tume ina mazuri yake ingawa pia ina mapungufu.
Wawaeleze wananchi ni marekebisho yapi ambayo Rasimu ya Tume ilihitaji kufanyiwa ili ikidhi mahitaji ya sasa na ya baadae ya nchi yetu.
Na mwisho wa siku waibebe Rasimu ya Tume yenye marekebisho yao kama agenda ya uchaguzi mwaka ujao.
Nawasilisha