The Unsung Hero: Lipumba Hotuba yake nzito imeliunganisha Bunge

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,398
1,006
Prof Lipumba akitoa maoni yanayoaitwa ya wachache ambayo kimsingi ndiyo maoni ya wananchi ametoa hoja nyingi nzito miongoni mwake ni kuwa rasimu ya katiba ina misingi na kuikataa misingi ni sawa na kuikataa rasimu yenyewe mabayo ni maoni ya wananchi, na msingi wake ni serikali 3.

Kuikataa serikali 3 ni kuikataa rasimu kwani msingi wake umejengwa kwenye serikali 3. Lakini ameshangazwa na unafiki wa hali ya juu wa baadhi ya mawaziri wanaotoka ofisi ya waziri mkuu,ofisi ya makamu wa rais na wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotoa maoni ya serikali 3 kwenye tume halafu kwenye bunge la katiba wanatetea serikali 2,kwa kisingizio cha gharama.

Wakati katika mfumo wowote Tanzania tatizo sio gharama bali UFISADI.FEDHA ZETU ZINATOSHA KABISA KUENDESHA SERIKALI YOYOTE BILA MSAADA.IKIWA TU...IKIWA TUTAONDOA UFISADI.AMEELEZA VIZURI NA KWA MARA YA KWANZA WABUNGE WENGI KUTOKA MAKUNDI YOTE WAMEMPA HESHIMA KWA KUSIMAMA NA KUMPIGIA MAKOFI MAONI YANGU NI KUWA WABUNGE WAKIMTUMIA VIZURI WANAWEZA KUTOKA KATIKA MKWAMO HUU NA KUSONGA MBELE.HONGERA MH.LIPUMBA
 
Nimekikuta
ichi kichwa kikidadavua jinsi gani uchumi unavofujwa na mafisadi, asema
serekali tatu inawezekana kuendeshwa bila kuongezeka gharama ilimrad
inataka mising imara tu, alia na misamaha ya kodi, ataka mawazo ya wananch yaheshimiwe.
 
nimekoshwa sana na maelezo ya professor lipumba jioni ya leo huko bungeni dodoma.
nimemkubali .
ole sendeka ameonyesha upumbavu wake wa kutumika utafikiri amekuwa kondom.
kwa kifupi naunga mkono hoja za waliowachache kwenye bunge la katiba

waliowengi kwenye hilo bunge ni maadui wetu tuwazomeeni
 
Kwa hiyo ume-assume kwamba kila mtu anajua kile ambacho Lipumba na Ole Sendeka wamesema? Una tofauti gani na huyo Ole Sendeka?
 
Nimekikuta
ichi kichwa kikidadavua jinsi gani uchumi unavofujwa na mafisadi, asema
serekali tatu inawezekana kuendeshwa bila kuongezeka gharama ilimrad
inataka mising imara tu, alia na misamaha ya kodi, ataka mawazo ya wananch yaheshimiwe.

Watamtukana watasema ana uchu wa madaraka. Nchi hii kwani inahitaji professional? Wapi na wapi ukiwa na c mbili na m moja ndo watakuheshimu. Nchi ya ajabu kweli (kusadikika)
 
Tunahitaji serikali adilifu itakayokuwa na mikakati mizuri ya kukusanya mapato na kuyasimamia vizuri bila wizi tunaoushuhudia.
 
Mzee wa Simanjiro, Ole Sendeka ameipata ya moto baada ya kukutana na Zomea zomea ya ajabu pale alipotaka kufanya jitihada za kuzuia hoja kali za Prof Lipumba alizokuwa anazijenga alipokuwa akitolea ufafanuzi wa mapendekezo ya wajumbe wachache wa kamati namba kumi. Hoja za Lipumba zilikuwa zinaelekea kuwavua nguo wakubwa kwa jinsi alivyochambua mapato na matumizi ya serikali na ubadhirifu wa pesa hzo mpaka kuwaletea hofu ya kuzmudu serikali 3. Hapo Ole Sendeka akaona aokoe jahazi kwa kufifiza au kupunguza hoja za Lipumba kwa kuomba utaratibu wa kijinga na ndipo alipokutana na zomeazomea ya hali ya juu iliyotulizwa kwa nguvu kubwa ya mwenyekiti Sitta.
 
Hebu
funguka zaidi mkuu
alichokisema huyo Prof. maana wengine hatujapata wasaa wa kufuatilia
tunategemea Jf

Mimi nimemkuta mwisho akichangia kweny BLK, duh yani machozi yamenitaoka
kuwa na mtu km huyu lakin 2meshindwa kum2mia 2kaendelea badala yake 2na
hangaika na akina mchemba. Aliemuwah toka mwanzo atuambie kasemaje yani bunge zima limecharuka kwa furaha mpaka 6 ameacha mdomo wazi ilikua naomb Mungu atokee panya aingie mule mdomoni, akina john komba ata hawajuwi anasemaje?
 
Akitoa maoni yanayoaitwa ya wachache ambayo kimsingi ndiyo maoni ya wananchi ametoa hoja nyingi nzito miongoni mwake ni kuwa rasimu ya katiba ina misingi na kuikataa misingi ni sawa na kuikataa rasimu yenyewe mabayo ni maoni ya wananchi.na msingi wake ni serikali 3.kuikataa serikali 3 ni kuikataa rasimu kwani msingi wake umejengwa kwenye serikali 3.lakini ameshangazwa na unafiki wa hali ya juu wa baadhi ya mawaziri wanaotoka ofisi ya waziri mkuu,ofisi ya makamu wa rais na wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotoa maoni ya serikali 3 kwenye tume halafu kwenye bunge la katiba wanatetea serikali 2,kwa kisingizio cha gharama.wakati katika mfumo wowote Tanzania tatizo sio gharama bali UFISADI.FEDHA ZETU ZINATOSHA KABISA KUENDESHA SERIKALI YOYOTE BILA MSAADA.IKIWA TU...IKIWA TUTAONDOA UFISADI.AMEELEZA VIZURI NA KWA MARA YA KWANZA WABUNGE WENGI KUTOKA MAKUNDI YOTE WAMEMPA HESHIMA KWA KUSIMAMA NA KUMPIGIA MAKOFI MAONI YANGU NI KUWA WABUNGE WAKIMTUMIA VIZURI WANAWEZA KUTOKA KATIKA MKWAMO HUU NA KUSONGA MBELE.HONGERA MH.LIPUMBA

Ijapokuwa wakat kijana mwenzetu Kafulila wqkati anashusha nondo sikubahatika kumuona, ila nondo na uchambuzi MAKINI wa Prof. Lipumba umenipa FARAJA ya siku! Sendeka yaani ovyooo, nashukuru Mwenyekiti kampuuza, hakuwa na hoja zaidi ya kutokwa mapovu tu!
 
Kusema kweli nimemsikiliza Professor Lipumba, ana hoja mjarab kabisa. Anastahili asikilizwe bila ushabik wa vyama.

Mpaka nimemuonea huruma Ole Sendeka, kachapwa na nondo mfululizo mpaka kasimama kutoa taarifa akachanganyikiwa badala ya kutoa taarifa akaomba muongozo bila kujijuwa, lakini inaonesha hata Sitta alikuwa anaburudishwa na nondo za prof, zilimuingia akaamua kumtolea nje Ole Sendeka na kumuomba prof aendelee kumwaga hoja kwa mpangilio aujuao.

Kudos Professor.
 
Lipumba amesema kuwa kama wanaotaka serikali mbili hofu yao ipo kwenye gharama ya kuendesha serikali tatu, basi hofu hiyo waiondoe kwani mambo makuu makubwa yanayosababisha Nchi hii kuwa masikini ni Ufisadi, misamaha holela ya kodi na maadili ya uogozi .Mambo hayo yanaainishwa wazi wazi katika rasimu ya katiba na kama yakidhibitiwa basi serikali ya shirikisho itaendeshwa bila shida yoyote.
 
Mzee wa Simanjiro, Ole Sendeka ameipata ya moto baada ya kukutana na Zomea zomea ya ajabu pale alipotaka kufanya jitihada za kuzuia hoja kali za Prof Lipumba alizokuwa anazijenga alipokuwa akitolea ufafanuzi wa mapendekezo ya wajumbe wachache wa kamati namba kumi. Hoja za Lipumba zilikuwa zinaelekea kuwavua nguo wakubwa kwa jinsi alivyochambua mapato na matumizi ya serikali na ubadhirifu wa pesa hzo mpaka kuwaletea hofu ya kuzmudu serikali 3. Hapo Ole Sendeka akaona aokoe jahazi kwa kufifiza au kupunguza hoja za Lipumba kwa kuomba utaratibu wa kijinga na ndipo alipokutana na zomeazomea ya hali ya juu iliyotulizwa kwa nguvu kubwa ya mwenyekiti Sitta.
akili ndogo ilitaka kufundisha akili kubwa yaani ni form six anataka kumfundisha prof aibu yake kesho ajifunze
 
Kusema kweli nimemsikiliza Professor Lipumba, ana hoja mjarab kabisa. Anastahili asikilizwe bila ushabik wa vyama.

Mpaka nimemuonea huruma Ole Sendeka, kachapwa na nondo mfululizo mpaka kasimama kutoa taarifa akachanganyikiwa badala ya ktuo taarifa akaomba muongozo bila kujijuwa, lakini inaonesha hata Sitta alikuwa anaburudishwa na nondo za prof, zilimuingia akaamua kumtolea nje Ole Sendeka na kumuomba prof aendelee kumwaga hoja kwa mpangilio aujuao.

Kudos Professor.

OleSendeka aliumbuka aisee, anataka kushinda na mchumi Prof , yeye na elimu yake yakuunga unga
 
Kusema kweli nimemsikiliza Professor Lipumba, ana hoja mjarab kabisa. Anastahili asikilizwe bila ushabik wa vyama.

Mpaka nimemuonea huruma Ole Sendeka, kachapwa na nondo mfululizo mpaka kasimama kutoa taarifa akachanganyikiwa badala ya ktuo taarifa akaomba muongozo bila kujijuwa, lakini inaonesha hata Sitta alikuwa anaburudishwa na nondo za prof, zilimuingia akaamua kumtolea nje Ole Sendeka na kumuomba prof aendelee kumwaga hoja kwa mpangilio aujuao.

Kudos Professor.
Nimetafuta kitufe cha like sijakiona...itoshe kusema nimependezwa na mchango wako
 
Kusema kweli nimemsikiliza Professor Lipumba, ana hoja mjarab kabisa. Anastahili asikilizwe bila ushabik wa vyama.

Mpaka nimemuonea huruma Ole Sendeka, kachapwa na nondo mfululizo mpaka kasimama kutoa taarifa akachanganyikiwa badala ya ktuo taarifa akaomba muongozo bila kujijuwa, lakini inaonesha hata Sitta alikuwa anaburudishwa na nondo za prof, zilimuingia akaamua kumtolea nje Ole Sendeka na kumuomba prof aendelee kumwaga hoja kwa mpangilio aujuao.

Kudos Professor.

Kwa post hii inaonekana huwa unajitambua na unajua matatizo ya serikali ila unajifanyaga nunda tu.
 
Watanzania wengi tumepoteza uzalendo wetu kutokana ushabiki wa kisiasa.

Wanasiasa wengi fikra zao za vyama wanataka ziwe fikra za watanzania wote, hii katiba ni ya Tanzania siyo katiba ya chama chochote cha siasa.

Ole Sendeka, wakati mwingine angalia maslahi ya taifa kwanza, Prof. Lipumba, kaongea mambo ya msingi na ya ujenzi kwa taifa.
 
Back
Top Bottom