Hahahahahaaa nadhani Novemba ile nimeingia zangu Dom nikafikia lodge palipokucha kulikuwa na mdau wangu nikaacha mizigo yangu nikadandia boda nikapandisha chuo.... The very first day naenda kuregister,sasa baada ya kutoka utawala mkuu nikapanda boda nikaingia utawala social, sasa nikajikuta natakiwa nirudi tena utawala mkuu, nilivyoona daladala zinatoka humanities nikadandia chap kusevu hela maana nilipaona ni karibu mno kipindi naletwa na bodaboda mara paap naona tunapita geti kuu pale mara hamad tunaishusha ile down baada ya chimwaga pale, nikamtonya konda oya nishushe kituo kinachofuata, akaniuliza MAKULU? wakati sikijui nikamwambia ndio, kufika nikashuka nikazuga naingia shop kuchukua vocha then nikavuka upande wa pili wa kituo kurudi chuo nikadandia za education/ng'ong'ona bila kuuliza ila uzuri ilikuwa inapitia njia ya utawala mkuu haikunyoosha pale njia panda benki.. nikashuka naona lile libarabara lireefu jengo lipo mbali jua la Dodoma limeshachanganya nikanyakua hatua pale..




kumbukumbu nyingi sana nzuri UDOM nakihusudu sana kile chuo, ingawa kuna lecturer mmoja muhindi ***## yule popote pale alipo na pia walikuwa wanakera kwenye mazingira ya kutegeana ili tupigane mafine ya kukomoana kwenye time extension ya tafiti..
#Embracing Knowledge