The Two Generals' Paradox: mada fikirishi

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
Majeshi mawili ya sehemu moja yakiongozwa na majenerali tofauti yanajiandaa kuivamia kambi ya maadui sehemu fulani. Majeshi haya yameweka kambi karibu na mji wanaotaka uvamia lakini katika sehemu tofauti chukulia jeshi moja kusini mwa mji na jingine kaskazini mwa mji. Huku mji wanaouvamia ukiwa umetenganisha majeshi hayo kati, njia pekee ya majeshi haya mawili kuwasiliana ni kwa kutuma messenja (mpeleka taarifa) ambaye atakatisha njia ya kufika haraka upande wa pili tukichukulia ni katikati/pembeni ya maadui
Ubaya unakuja kuna chance kubwa mpeleka taarifa huyu (messenger) anaweza kamatwa njiani na taarifa ikashindwa fika upande wa pili. Kumbuka taarifa ni muhimu katika maamuzi ya kuuvamia mji huo ili isije tokea upande mmoja ukavamia na kushindwa wakati huo upande mwingine bado haujavamia. Hii itampa adui muda wa kujipanga kujilinda!.
Ingawa majenerali hawa wamekubaliana kuuvamia kwa pamoja lakini hawajakubaliana ni ndani ya muda gani watauvamia mji wa maadui ili waweze mshinda adui kwa wepesi. Kila jenerali anataka jua atakapovamia atapata msaada toka kwa jenerali mwenzie ili kupunguza idadi ya majeruhi na kushinda vita, pamoja na kujua mbinu watakayo itumia kumvamia adui (kumbuka byzantine war
Inahitajika mpeleka taarifa awepo ili kutoa taarifa upande mmoja hadi mwingine lakini kutokana na uwepo wa maadui na umbali wa kuzunguka mji ili kufika upande wa pili ni njia gani itatumika?. Kufikia hapo jenerali mmoja inabidi aamue muda wa kuvamia pamoja na plan nzima ya jinsi gani watavamia then aipeleke ndani ya muda muafaka.
fikiria hakuna simu wala internet access
JENERALI HUYO ATATUMIA MBINU GANI KUFIKISHA UJUMBE KWA JENERALI MWENZIE KUHUSU PLANI NZIMA?
 
Fikiria hakuna simu wala internet!..Hiyo ni mbinu iliyotumika miaka hiyo!
Swali lingeulizwa kwa muktadha.

Jeshi linatakiwa kuwa na codes zake, kuna milio ya ngoma, bendera zenye rangi mbalimbali, mizinga ya mfululizo fulani. Encrypted codes with predetermined keys, hizi mbinu zilitumika tangu enzi za Julius Caesar na kabla.
 
Back
Top Bottom