The things women do.............(usihofu ni kiswahili)

Heading inasema "things women do" lakini ndani kumejaa vitu avifanyavyo mwanamme!

Sasa mwanamme kumkana mama yake hicho amekifanya mke pia?

Umeona eeh! Ukianzia kwa Adamu, alilishwa kwa nguvu hilo tunda?? Mimi naona tukubaliane tu Leo kuwa wanaume ni weakbeings na ndio maana hutumia nguvu nyingi (kuwa aggressive) kuprove otherwise.
 
Umeona eeh! Ukianzia kwa Adamu, alilishwa kwa nguvu hilo tunda?? Mimi naona tukubaliane tu Leo kuwa wanaume ni weakbeings na ndio maana hutumia nguvu nyingi (kuwa aggressive) kuprove otherwise.

kiu ya mwanamke ni kumtawala mumewe.........................lakini akifanikiwa kumtawala mumewe anaishia kujipatia laana ya mwenyezi mungu ambayo ilimwajibisha amtumikie mumewe..................hivyo kamwe mwanamke wa aina hiyo hatakuwa na furaha maishani mwake.......................kila siku atakuwa analalamika tu........................hataridhika kwa sababu kumkaidi Mwenyezi Mungu kuna gharama zake.............
 
Rutashubanyuma

Hebu siku nyengine ukishakuandika "kazi" yako, kabla ya kuituma anza kuihariri kwa kufuta hivyo vidoto-doto na badala yake utumie vituo vyengine vya uandishi.

Natanguliza shukrani
 
Hao ni wale wasiokua WANAUME!Nenda kwenye uzi wa Aspirin ndo utajua MWANAUME anatakiwa aweje!
 
Moja hukamia kumtawala mumewe.....................hata Hawa usifikiri alipompelekea Adam lile tunda hakujua yalikuwa ni makosa ila alimtega mumewe kuona kama anampenda Mwenyezi Mungu au yeye mwanamke na hivyo njia ya kumpima Adam mumewe kama ataweza kumtawala..................

pili...wanaumme wengi wapo kwenye dhiki kwa sababu ya kukubali kutawaliwa na matakwa ya wake zao.......................sembuse mke kwani hata mpenzi wa baki kama umetembea naye huyo naye sasa mmekuwa mwili mmoja.............Soma 1 Corinthians 6:16

Tatu.............wanaumme huhangaika kujenga nyumba kubwa, kuwa na magari ya kifahari, vyeo lukuki n.k ikiwemo kujiendeleza.................lakini lengo lao siyo kwa ajili ya mahitaji yao binafsi wanapokusanya utitiri wa mambo hayo.....................bali kumthibitishia mwanamke ya kuwa wana kauwezo wa kuwa mpagasi wa mwanamke..........................na kumtumikia mwanamke kwa utashi na ujasiri wao wote........vilivyo.......

Nne.................mwanaumme humpenda mkewe kulikoni wazazi wake............na hata ikibidi huwakana wazazi tajwa ili kutii matashi ya mkewe...................mawifi hulalama kuwa kaka yao katawaliwa lakini yote hayo huwa yameelekezwa kwa kiziwi na/au bubu............

tano .......................mwanamke hutamba ya kuwa huyu jamaa yake aachiwe yeye maana yeye ndiye humjulia alivyo...................kwa hiyo ajua afanye nini ili apate mradi wake........kutoka kwa dume lake............................

sita.........................pamoja na wazazi wa mwanaumme kumgharimia mtoto wao wa kiumme....................na pamoja kudhania kuwa atawasaidia watakapokuwa wazee....................lakini mweye sauti ya watasaidiwaje ni mwanamke.............mtoto wao wa kiume huwa ni kiwete/ na zezeta vile hapo kwenye maamuzi hana sauti...........na wazazi hushangaa kumbe aliyezaa ni yule aliyezaa mwanamke huyu mwanaumme waliyekuwa wanamthamini sana kuwa atakuwa kimbilio lao uzeeni kumbe siyo fimbo ya mnyonge kabisa wa kabisa.......

saba.....................ndugu wa mwanamke ndiyo hufaidi jasho la mumewe.............na huku ndugu wa mwanaumme hutupiwa virago kuwa waende kutafuta vya kwao....................wao huonekana ni viwavi jeshi lakni ndugu wa mwanamke huonekana wao ndiyo wastahiki wa kulilamba jasho la mumewe.........................

these are the things women love to do.......................ninajua watabisha sana humu jamvini lakini penye ukweli uongo hujitenga..........

ooooh dude, am just speechless.... what is this?? are you desparate with ur marriage life?
ndio saba bu mie ninafanya kazi usiku na mchana najaribu kuwekeza ili my only daughter asijekupata shida ya kunyanyasiwa mali ya mume, atakuwa na vya kwake na mume akitaka kumuoa anaweza hata akahamia kwa mke km akitaka! na itabidi nikae nimsome vema huyo mkwe akiwa na mawazo kama yako hata kwa panga simpi binti yangu... loh mtazamo gani huu na wake zenu?? mnanichosha mie nyie wanaume, kila palipo na shortcoming its mwanamke's fault..... mh shame on you!
 
Ulijuaje au yamekukuta, uko mbali ningekupa 5, hiyo shortlist ya Things women do kama shirikishi vile kwa sababu kumpata mwanamke aliyekosa moja kati ya hayo tisa ni kazi kweli kweli. Yote uliyoyasema ni kweli na yanakatisha tamaa na kuwasononesha wanaume na wazazi wao. Lakini wanawake wanapaswa kujiuliza huyu baba niliyekumkuta ameshakuwa mtu mzima amefikia hali hii baada ya mchakato tena wa muda mrefu. Hebu Mwanamke jiweke kwenye viatu vya mama aliyebeba mimba miezi tisa na machungu yake, kisha akasota na mwanae kumtibu na kumlisha ili kuhakikisha anaendela kuwa hai akakosa usingizi mtoto akiugua,akajinyima yeye ili mtoto wake ashibe. Akapata presha mtoto akipata masaibu yeyote. Mtoto huyu akapelekwa shule, akaandaliwa kila siku asubuhi mavazi, chemsha kimya madaftari na kalamu, sare zilizofuliwa na kupigwa pasi, ada za shule na Tuition, kuanzia nursery hadi chuo kikuu miaka zaidi ya kumi na sita watu wanahangaika na katoto kao kisha unakuja Queen unambadilisha mtoto huyu na kumfanya wa kwako tene wa kwako peke yako na ndugu zako. Humuogopi mungu wewe, hivi unamtakia mumeo mema. Dhulma gani hii ukosefu gani shukrani. Unapaswa kuwashukuru na kuwaheshimu wazazi wa mumeo UKIONA VYAELEA VIMEUNDWA. Tafakari wewe mama unayemmiliki mmeo.
 
Umeona eeh! Ukianzia kwa Adamu, alilishwa kwa nguvu hilo tunda?? Mimi naona tukubaliane tu Leo kuwa wanaume ni weakbeings na ndio maana hutumia nguvu nyingi (kuwa aggressive) kuprove otherwise.

kwa wasomaji wa biblia Mwanzo 2:18 na 21-22. Hata MUNGU mwenyewe alieumba kila kitu alimtazama mwanamume kama kiumbe dhaifu, na akasema si vema akae peke yake, akamfanyia MSAIDIZI ( mara zote msaidizi ni mtu ambaye huwa na uwezo mkubwa kuliko msaidiwa) na pamoja na udhaifu alioubaini akauongezea kwa kutoa mbavu zake ili amuumbe mwanamke, hapa naamini mwanamume akapungukiwa zaidi na mke akapewa nguvu! sijaona mahali Mungu alimfanyia mbwa msaidizi.. alimfanyia binadamu kwa kuwa alijua ni dhaifu. mimi kwangu mwanamume huwa namtizama kama MGONJWA na ninaamini wanawake ni NURSES na hasa nikizingatia Doctors hutibu UGONJWA while nurse anatibu MGONJWA (i.e. mtu) kwa hiyo anauwezo mzuri sana wa usaidizi kwa mgonjwa pengine kuliko dr.
 
Mimi sipo kwenye hoja bali kichwa cha thread ndiyo kimeniacha hoi, usihofu ni kiswahili kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi heeeeeeeeeeh.
 
Mimi sipo kwenye hoja bali kichwa cha thread ndiyo kimeniacha hoi, usihofu ni kiswahili kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi heeeeeeeeeeh.

bora angeandika kiswahili tu, hakuna mwenye hofu na lugha hizo mbili humundani kwakuwa si mtihani kwamba lazima uandike kiswahili au english
 
Pole sana kwa matizo yalo kwenye ndoa yako!pia nkupongeze kwa ujasiri ulouvaa kwa kutujuza tabia za mkeo!ila nkutahadharishe k2 sjumuishe wote kadhan kama huyo alokupa kfungo cha ndoa!hakuna m2 anayepewa pole kwa kujpiga mwenyewe bali husikitiwa!ile imeandika ENYI WAUME ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI SANA!
 
kwa wasomaji wa biblia Mwanzo 2:18 na 21-22. Hata MUNGU mwenyewe alieumba kila kitu alimtazama mwanamume kama kiumbe dhaifu, na akasema si vema akae peke yake, akamfanyia MSAIDIZI ( mara zote msaidizi ni mtu ambaye huwa na uwezo mkubwa kuliko msaidiwa) na pamoja na udhaifu alioubaini akauongezea kwa kutoa mbavu zake ili amuumbe mwanamke, hapa naamini mwanamume akapungukiwa zaidi na mke akapewa nguvu! sijaona mahali Mungu alimfanyia mbwa msaidizi.. alimfanyia binadamu kwa kuwa alijua ni dhaifu. mimi kwangu mwanamume huwa namtizama kama MGONJWA na ninaamini wanawake ni NURSES na hasa nikizingatia Doctors hutibu UGONJWA while nurse anatibu MGONJWA (i.e. mtu) kwa hiyo anauwezo mzuri sana wa usaidizi kwa mgonjwa pengine kuliko dr.
Acha kuendelea kudangany wewe, kama Mungu alikuwa na maana hiyo mbona sehemu kubwa ktk Biblia mmewekwa kundi moja na watoto? Na ktk matukio mengi mlikuwa hamhesabiwi isipokuwa ni wanaume tu. Wewe ni assistant wa mume hebu watafute wajuzi wa kiinglishi wakutafsirie maana ya hilo neno.
 
Back
Top Bottom