The Rise and Fall of CCM

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
411
Miaka michache ijayo tutashuhudia CCM ikiungana na vyama vikongwe duniani kuingia katika vitabu vya HISTORIA, vya kiada na ziada, vya kufundishia shule za msingi na sekondari na vyuo.
Tutashuhudia, kwa mfano, maswali ya kiistoria kama:-
1.Jadili sababu za kukua na kuanguka kwa CCM
2. CCM ni adui wa maendeleo Tanzania. Elezea kwa ufupi.
3....
 
sababu za kukua the role of mwal nyerere,role played by tanu,,the role of bibi titi na wanzake,

sababu za kufa
the role of jk
rushwa
makundi
siasa uchwara
ufisadi
safari za jk
umbea wa nape
........
.......
.......
 
CCM ni kifupisho cha Chama Cha Mapinduzi, kilianzishwa mwaka 1977 baada ya muunganiko wa chama cha TANU na ASP. Mwenyekiti wake wa kwanza alikuwa Juliasi Kambarage Nyerere, maarufu kama baba wa Taifa. Malengo makuu ya CCM ilikuwa ni kuwaunganisha na kuwakomboa watanzania katika umasikini, kwa kusimamamia haki na rasilimali za watanzania.

CCM ilikuwa na kuwa chama imara kwa sababu zifuatazo.
(a) uongozi imara
(b)kuchukia rushwa
(c)kutotishiana bastola wana ccm kwa wana ccm
(d)maskini waliweza kushika nafasi za uongozi katika chama.
(e)first lady hakupita bila kupingwa
(f)upendeleo haukuwepo katika kupata nafasi ya uongozi
(g) na kadharika


zifuatazo ni sababu zilizofanya ccm iangukie pua

(a) uongozi legelege hasa kwa mwenyekiti
(b)kukithiri kwa rushwa katika chama
(c)first lady kupita bila kupingwa pamoja na mtoto wa mwenyekiti
(d)ili upate nafasi ya uongozi katika chama lazima uwe na hela nyingi (fisadi)
(e)makundi katika chama (mtandao)
(f) badala ya kuitwa chama cha mapinduzi(ccm) kikaanza kuitwa chukua chako mapema (ccm)
(g) na kadharika
 
kufa haita kufa lakini itatoka madarakani na kutengeneza kambi rasmi bungeni

Kwa mjibu wa maoni ya Jf ni kweli itatoka madarakani, lakini kwamjibu wa sanduku la kura, haijathibitika kama kweli Ccm itakuwa chama cha upinzani.
 
CCM haita fall hata siku moja.
"Haijalishi ni kiti cha thamani gani ambacho shetani amekukalisha hapa duniani, mwisho wake ni maafa."


Hapo kwenye red, Jitafakari kama sio wewe mwenyewe uliyekalishwa.....????

Masikini Barnabas ungekuwa karibu ningekuwekea mikono nikakuombea upate ufahamu maana sio kwamba umekalishwa tu bali umetekwa na kudumazwa hadi fikra kiasi cha kutokutambua maafa ambayo
tayari yamekufika .

 

Hapo kwenye red, Jitafakari kama sio wewe mwenyewe uliyekalishwa.....????

Masikini Barnabas ungekuwa karibu ningekuwekea mikono nikakuombea upate ufahamu maana sio kwamba umekalishwa tu bali umetekwa na kudumazwa hadi fikra kiasi cha kutokutambua maafa ambayo
tayari yamekufika .


Hahaha, usihofu ndugu, uelewa wangu bado upo vizuri sana. Siwezi nikaamini maamuzi ya walio nyuma ya keyboard zao wakiandika kuwa CCM haitaingia madarakani, nasubiri masanduku ya kura yatakavyotoa matokeo basi. Haya mengine ni porojo za wakoswa kazi tu.
 
Tulishajidili hili sana sema tunangoja anguko lenyewe. Tangu alipoondoka Mchonga wakaingia mafisadi tulijua fika kuwa mwisho wa CCM umefika. Tunachongoja kufanya ni mazishi tu. Na yatakuwa mazishi yasiyo na matanga wala dua zaidi ya sherehe ya kufa mtu.
 
Siri zote za CCM wanaziweka hadharani wenyewe. Jinsi makundi yanavyofitiniana na matumizi ya pesa kununua kura. Nani atakichagua chama cha namna hiyo?
 
kufa haita kufa lakini itatoka madarakani na kutengeneza kambi rasmi bungeni
No No No No ikitoka madarakani lazima ife kwa sababu sasa hivi inabebwa na dola na baada ya kutoka madarakani dola haitakuwa na muda nao tena.
 
Hahaha, usihofu ndugu, uelewa wangu bado upo vizuri sana. Siwezi nikaamini maamuzi ya walio nyuma ya keyboard zao wakiandika kuwa CCM haitaingia madarakani, nasubiri masanduku ya kura yatakavyotoa matokeo basi. Haya mengine ni porojo za wakoswa kazi tu.

Mmmmm!! "uelewa wangu bado upo vizuri sana", Rafiki I doubt it, kama comments kwenye red hapo juu kweli zimetoka kwako basi jitafakari zaidi.
  • Hauwaamini walio nyuma ya keyboard - wapi hao ambao wewe sio sehemu yao au na wewe pia haujiamini kile ufanyacho au wewe uko mbele au juu ya keyboard kaka....?? Sijakuelewa....hapo ndo penye shaka ya kiuelewa.
  • Unasubiri masanduku ya kura...hahahahahaaaa......!! hi imenishutua kwamba mtu mwenye uwezo wa kutumia tekinolojia za kisasa bado uko katika fikra kama hizi, anyway endelea kusubiri, lakini nakuachia ushauri kuwa: Kujitambua ni muhimu sana kwako na hii ni pamoja na kuyatambua mazingira yako, jamii unayoishi na mabadiliko yake ambayo ni muhimu ukawa sehemu yake katika kuyaibua na kuyajenga sio kusubiri, unatakiwa kuyatumia matokeo ya kujitambua kwako kwa sasa kuweza kuyaona ya kesho na kupanga vizuri ya mbele yako, huo uwezo Mungu ametupa kwa sehemu fulani tuweze kuweka mipango na kusubiri yeye athibitishe. Hayo matokeo unayosubiri unatakiwa wewe kuyatengeneza leo vinginevyo......oooooo!!
  • Porojo za wakoswa kazi ...........hii naomba nikuachie wewe mwenyewe maana du!! Mr. Barnabas, unayo kazi kubwa ya kufanya na iko kazi kweli kweli ili uweze kujikomboa kifikra......TAFAKARI, JITATHMINI TENA FIKRA ZAKO.
 
Back
Top Bottom