The Power of Imaginations and Rituals

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
"If you cannot imagine it then it cannot be."
"If you cannot ritualize it then you cannot imagine it"

Key words.Imagination and Ritualization
Meanings:
Imagination-the act or power of forming a mental image of something not present to the senses or never before wholly perceived in reality. 2a : creative ability. b : ability to confront and deal with a problem : resourcefulness use your imagination and get us out of here.

Ritualization-The process by which a normal behavioral action becomes a communication signal representing the behavior or its physiological consequence

Sasa tuendelee;


Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Watu wanapata tabu sana kwa kukosa maarifa.Maarifa huwezesha watu kuwa na imagination.Kwa mfano katika kijiji ambacho hakuna magari ni vigumu sana mtu kufikiri kuwa na gari.Hata hivyo mtu wa kwanza kumiliki gari anaweza kuwa ama alilipata toka nje ya eneo husika au alipata hamasa kutokana na changamto fulani.

Katika maisha watu hutamani mambo mengi na vitu vingi sana.Kuna ambao hutamani kuwa matajiri kama Musk, na kuna ambao hutamani kuwa maarufu,na kuna ambao hutamani kuwa wakuu wa watu(Matamanio ya watu hawa ili yatimie ni lazima yaingie katika imaginations zao)

Kama huwezi kuvuta picha na kujiona wewe ni Rais wa nchi na ukawaza kama rais wa nchi na kutenda kama rais wa nchi na kuenenda kama rais wa nchi hakuna namna unaweza kuwa rais wa nchi.Mifano ipo mingi sana ya watu ambao walitamani kuwa marais.Waliofanikiwa ni wale ambao waliweza ku imagine wao wakiwa marais na wakatengeneza Ritual(Tabia) za Kirais yaani namna ya kuwaza na kutenda kama Rais wa nchi.

Unaweza kutamani mafanikio lakini imaginations zako zika ni za loser na hata mwenendo wako ukawa ni wa loser.Kwa hakika utapata kile ambacho kiko katika imaginations na mwenendo wako.Na hii haiko tu katika mambo makubwa kama ya kutaka kuwa Rais au kuwa na mafanikio makubwa katika maisha bali ipo pia katika mambo madogo kama vile kufaulu mitihani,kufanya kazi vizuri katika ofisi,kufanya biashara vizuri,kilimo na hata ufugaji.

Imagination na Ritualization zinafanya kazi kwa pamoja katika namna ambayo inakuwezesha kuelekeza mental and physical energy katika jambo ambalo lina maslahi makuwa kwako ili uweze kuweza kuweka maximum efforts.

Kwa neno fupi huwa wanasema weka FOCUS kwenye jambo unalofanya na utafanikiwa.

Je utafahamuje iwapo kweli imaginationa zako ziko sawa na rituals zako?

Njia pekee ni kuona matokeo yako,kama unaona maboresho hata madogo kuelekea kule unakotamani basi uko katika njia sahihi ila kama unaona kama vile unaelekea negative basi inabidi ujipime.

Nakutakia wakati mwema.
 
Njia pekee ni kuona matokeo yako,kama unaona maboresho hata madogo kuelekea kule unakotamani basi uko katika njia sahihi ila kama unaona kama vile unaelekea negative basi inabidi ujipime.

Nakutakia wakati mwema.
Ahsante kwa ku_share nasi andiko hili,
 
Back
Top Bottom