The Plot that kept Mugabe in Power | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Plot that kept Mugabe in Power

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Jul 5, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kama Jongwe alikuwa tayari kubwaga manyanga, je Jeshi na Usalama wa Zimbabwe haukuwa tayari kuyaheshimu matokeo dhahiri ya uchaguzi? kwa nini wao Jeshi na Usalama wa Zimbabwe ambao ni walinzi wa Katiba na Uhuru wa Zimbabwe waliamua kugeuka viapo vyao na kulazimisha Mugabe aendelee kuwa Raisi?

   
 2. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bwana/Bibi Kishoka,Habari kama hiyo kwenye gazeti la WP zitakuja nyingi tu na kila siku stori zitakuwa zinabadilika mpaka lengo litakapotimia.Is just Bull shiiit!
   
  Last edited: Jul 5, 2008
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhani ungeziamini kama ungezisoma daily news ya Tanzania au siyo mtu mzima? maana kila wasemalo wazungu kwako ni propaganda sio? Na kweli tutasikia mengi kutoka kwenu mnaoona mauaji kama ni ripoti nzuri.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Jul 5, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..hivi ni kitu gani kinashindikana kumuua Mugabe na mchezo huu ukaisha?

  ..hizi kelele za Mugabe,Mugabe,...it is almost 10 yrs now. wananchi wanateseka bure tu.
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Bwana/Bibi Mtu Mzima,

  Shukrani kwa kuchangia.
   
 6. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe mauaji kwako ni hayo yanayotokea Zimbabwe tu.Mauaji yanayotokea Somalia sio mauaji,mauaji yaliyotokea Kenya hadi watu kuchomwa wakiwa kanisani kwako ni kawaida,mauaji yanayoendelea Sudan na Congo DRC kwako sio kitu, mauaji ni yale yanayotokea Zimbabwe.Lazima uelewe kwamba mauaji hata kama ni ya mtu mmoja lazima yakemewe lakini inapotokea watu wanakemea mauaji sehem moja na kubaliki mauaji sehem nyingine ni unafiki na ubinafsi wa wazi.
  Wewe endelea kumeza kila unachopewa sikukatazi na wala sikulazimishi uamini ninachoamini.
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kishoka, hii kali.

  Nimekukubali.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mtu mzima nani anasema mauaji yanayotokea kwenye nchi zingine hayawi reported? hivi unasema kweli?
  Nataka kukwambia kwanza kabla hayaja ripotiwa na vyombo vya habari vya nyumbani huwa tumeshasikia toka kwa vyombo hivyo unavyovikandia. Pole ka sababu hakuna jinsi mambo ya Zimbabwe yanatisha na hakuna uhalali wa kuua watu kwa kisingizio cha nchi za magharibi. Hiyo ndiyo shida ninayoiona achilia mbali mambo mengine ya kisiasa. Najali maisha ya watu wengine hata kama tunatofautiana msimamo kisiasa.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jul 6, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Hata mimi najiuliza kila siku na sipati jibu!! Mugabe ni mtu mmoja against mamilioni ya watu lakini anakuwa na nguvu hivyo na ni wachache mno wanaojitokeza kumpinga. Kingine ambacho hakiingii akilini kabisa ni hao so called wafuasi wa Mugabe wanaotembeza kibano kwa wanaotuhumwa kutokumuunga mkono. Hao wafuasi wa Mugabe kwanza na wenyewe njaa kali na choka mbaya. Wanachukua amri za kijinga na za kinyama halafu wanaenda kuwapiga na kuwaua watu wasio na hatia (as far as I'm concerned). Hawa wafuasi wa Mugabe hawana akili kabisa!!!! Zero IQ!! Common sense yao iko wapi? Kwa nini wasikatae kutii hizo amri za kwenda kutenda mambo ya kinyama? Kwani wakikataa kwa umoja nini kitawatokea? Mimi binafsi labda niko tofauti. Hata kama ikiwa baba yangu au mama yangu mzazi aniambie nikafanye mambo ya unyama kwa binadamu wengine pasipo na haki nitagoma. I'm just principled like that and my principles come ahead of my loyalty to anyone or anything. Sasa hii minyama ya Mugabe sijui ni mijitu ya aina gani tu.....inaambiwa ikawapige watu wasio na hatia na yenyewe bila hata kuhoji inaenda kutekeleza amri.......Haya bana nadhani mnajua hitimisho langu ni nini......
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nyani,
  Mugabe si mmoja tu. Ameshakuwa kama network. Umesikia wanajeshi wanavyoogopa kupoteza utajiri wao na mamlaka waliyopata chini yake? Hilo ndilo tatizo la Zimbwabwe. Askari akishawekwa kwenye position ya kuamua mambo ya siasa anasema kuwa kura ni karatasi tu. Mugabe was willing to go, but his cronnies were not.
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nyani Ngabu...

  ...nina amini unafahamu kuwa hata gate la concentration camp la manazi lilikuwa na walinzi wake wa kijerumani.

  ...kule ujapan pia, prisons of war walikuwa na ma prison guard wao.

  ...kwa milosovic, bosinia, serbia na yugoslavia nao walikuwa na wanajeshi wao waliosaidia kukamata watu, kuwaua na kuwafukia kwenye massgraves.

  ... kule wa watusi na wahutu, pia raia na wanajeshi walishiriki

  ...kule colombia ma militia na raia wanashiriki na kuhusishwa

  ... iraq, raia na militia wanashiriki na kuhusishwa katika mauaji ya wenzao

  ...n.k. n.k.

  Kwenye swala hili la mauaji na vita, Binadamu wakiwa desparate na kushinikizwa na wenzao wengi ndivyo walivyo!!

  SteveD.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jul 6, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  I still belive him and his thugs don't outnumber the good folks. I believe the thugs are far outnumbered. I believe if they (the good folks) are willing to sacrifice their blood, they can do it. I don't see a reason why they can't. At some point one has to say enough is enough....come what may, we are going to kick you out.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jul 6, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  At this point I don't care who goes and kicks his a$$....be it the US...the UK....the UN....the AU....the World Comuunity...I really don't care. He needs to go. The world community said enough is enough to Hitler and his allies....Nato said enough is enough to Milosevic.....I don't care who does it...Mugabe needs to go, period.
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Amina.....Amina......Amina
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MCHUKIA FISADI na REV KISHOKA wamekupata ila hapa hatakwambia 'shukrani kwa kuchangia'
   
 16. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asante.
  Nategemea next time utakemea kwa nguvu hizo hizo nchi zinazofadhili vikundi vya uasi huko Congo,Sudan na pia utakemea kambi za mateso na mauaji zinazoendeshwa na Marekani.Lakini hata kama utaona kwamba hilo sio muhimu ni sawa, ni mojawapo za tofauti zetu.

  Mugabe kwa kura umri wake sasa wa miaka 84 tu unatosha kuonyesha kwamba hana muda mrefu kwenye siasa za Zimbawe lakini maisha ya Wazimbabwe wa kawaida yataendelea kuwa duni na hatarishi hata bila Mugabe kwa kuangalia historia.Nitakupa mifano michache tu hapa kwenye nchi ambazo kunakuwa na maslahi ya wakubwa:Somalia tangu dikteta Siad Bare atimuliwe Somalia hadi leo maisha yamezidi kuwa mabaya zaidi, tangu dikteta Mengistu atimuliwe Ethiopia leo waethiopia hakuna mabadiliko kwenye uwanja wa demokrasia,wapinzani wanaendelea kuuwawa na kutupwa gerezani,Congo DRC tangu kuondolewa kwa dikteta Mobutu ambaye naye aliwekwa na hao wakubwa, bado vikundi vya kijeshi vinaendelea kupokea silaha toka nchi hizo hizo zinazomshutumu Mugabe kwa hiyo hata kama Tsvangirai wanaemtaka wao (Kulingana na Matamshi ya Ufaransa) atakamata madaraka atakuwa mzuri iwapo atatimiza matakwa yao na atakuwa adui iwapo atatimiza matakwa ya Wazimbabwe au ataingilia maslahi ya Magharibi
   
  Last edited: Jul 6, 2008
Loading...