ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Umeme ni jambo linalosumbua sana katika bara la Afrika na pia katika nchi za kimaskini kwa ujumla. Hii sio hali katika jengo la The Pearl River Tower, jengo bora kimazingira Duniani ambalo linajitegemea kuzalisha nishati lenyewe bila ya kutumia aina yoyote ya mitambo au nguvu za umeme kutoka nje ya jengo. Ni jengo pekee kubwa Duniani lililofikia kiwango cha Zero Energy Building (ZEB), yaani hali ya kujitegemea kwa kuzalisha nishati.
Jengo hili halipo New York wala London, bali lipo kwenye mji wa Guangzhou nchini China. The Pearl River Tower ambalo lina maana ya mnara wa mto wa lulu lina urefu wa mita 309 kwenda angani. Jengo hili linajizalishia nishati kwa njia mbali mbali huku likitumia teknolojia za kisasa na za hali ya juu.
Njia ya kwanza ya kuzalisha nishati katika jengo hili ni kwa kutumia upepo. Upepo hukusanywa na kuingizwa kwenye mitambo maalum (wind turbines) ambayo iko kwenye ghorofa ya 24 ya jengo hilo, upepo huo hutumika kuzalisha umeme, lakini pia upepo huo hupelekwa kwenye mfumo wa uingizaji hewa na kutumika kulipoza jengo na kuingiza hewa safi, hivyo jengo hili halihitaji viyoyozi vya gharama vyenye kula umeme ili kuliweka katika hali ya ubaridi wa wastani unaohitajika.
Jengo hili zima limejengwa likiwa na kuta mbili, ambapo ukuta wa nje huruhusu kuingiza joto litokanalo na jua lakini kuta za ndani haziruhusu joto kupita, hivyo joto linaponaswa baina ya kuta mbili hizi nalo hupelekwa kwenye mitambo maalum inayoligeuza joto hilo kuwa nishati na kutumika katika kwa matumizi mbali mbali katika jengo.
ia ili kupunguza matumizi ya nishati katika kuliweka jengo kwenye hali nzuri baina ya joto na baridi madirisha ya jengo hili yametengenezwa kwa namna yake (perforated metal windows blinds) madirisha hayo yana uwezo wa kujifunga na kujifungua ili kuzuia uwepo na utokaji wa joto ndani ya jengo kuhakikisha kwamba joto halizidi sana wala kushuka mno. Pia madirisha hayo yamewekewa photovoltaic cells ambazo zinauwezo wa kugida nishati inayotokana na jua. Vile vile jengo hili limewekewa solar pannel sehemu za juu ambazo kama tunavyojua zinazalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua.
Ingawa jengo hili limetumia gharama kubwa kutengenezwa mkandarasi wa jengo aliliambia shirika la habari la BBC kuwa jengo hili linatarajiwa kurudisha gharama zake za ziada katika kipindi cha miaka mitano tu, baada ya hapo jengo hili litaanza kuingiza faida. Jengo la The Pearl River Tower lina jumla ya ghorofa 71.
Huenda itafika siku na sisi tutaweza kujijengea nyumba zitakazojitegemea kwa nishati na maji ili kuepukana na maudhi ya mgao wa umeme na ukosefu wa maji katika nyumba zetu.
Chanzo: Gajetek Habari: The Pearl River Tower: Jengo Linalojitegemea Kwa Nishati