The New Dr Shein's Cabinet


Kwa hiyo Shamsi Vuai Nahodha Imekula Kwake MAsikini wee ndiyo maana alikua hataki serikali ya umoja wa kitaifa! Kumbeeee!
 
Du! Africa sijui tuna laana? Nchi kenye watu 900,000 mawaziri 25 ???????????????? And yet mambo mengine ya Zenj yanashughulikiwa na mawaziri wa muungano! This is ridiculous, just absurd period.
 
Kwa namna hii bora Shein angeliteua waziri kutoka kila familia moja!! Hahahaha. Halafu anataka kuinuna uchumi wa ZNZ. Kodi yote tutakayokusanya igharimie mawaziri, halafu tuende nje kuomba msaada ili kuwalipa wafanyakazi mishahara yao. Ukweli nimeanza kupoteza imani.
Haijawahi kutokea baraza kubwa kama hili katika historia ya miaka 46 tangu Mapinduzi. Tena tukiambiwa Waafrika tumelaaniwa tunahamaki. Spain yenye watu karibu milioni 45 ina mawaziri 15 - 8 wanaume, 7 wanawake. Hakuna Naibu Waziri, wa nini wakati waziri yupo.
 
Hii serikali ni kubwa sana. Ina wizara 16. Manaibu waziri 6 na mawaziri wasiokua na wizara maalum 3. Jumla 25.
 
Ingelikuwa ni uwezo wangu ningeteua mawaziri sita tu billa ya manaibu hapo Zanzibar ili kuokoa fedha..............
 
Du! Africa sijui tuna laana? Nchi kenye watu 900,000 mawaziri 25 ???????????????? And yet mambo mengine ya Zenj yanashughulikiwa na mawaziri wa muungano! This is ridiculous, just absurd period.
very much amazed, hivyo marekani population ni kiasi gani na masecretary of state ni wangapi?????? Mwenye data tafadhali.
 
kaunda serikali ndogo ya mawaziri 16...

una wazimu

Kuna watu wachache Zanzibar kuliko Mtwara (Milioni 1.1, sensa ya 2002).

Zanzibar kieneo inaingia Newala na Masasi mara kumi!

Nchi ya ki-Wilaya yenye mawaziri 19 si serikali ndogo, ni mtindio wa vichwa!
 
Zanzibar tupeni mchanganuo wa majina na wizara na vyama wanavyotoka waheshimiwa!
 
Kinachonichanganya ni kile kile hivi kuna haja gani ya kuwa na manaibu waziri wote hao? Am totally confused!
 
Kenya hivi sasa wamekata mzizi wa fitina na kuhakikisha ya kuwa kwenye katiba yao mpya wameweka ukomo wa idadi ya wizara za serikali ili kumzuia Raisi kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwajaza maswahiba wake ili kukidhi mahitaji yake mwenyewe.......sisi huku CCM yasema katiba mpya siyo sera yao........................lakini kututawala wanataka hata kwa kuchakachua matokeo..................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…