The New Dr Shein's Cabinet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The New Dr Shein's Cabinet

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Sera za Chadema za serikali ndogo sasa yaelekea CCM wamezivalia njuga na yeye Dr. Shein leo ITV wametuhabarisha kaunda serikali ndogo ya mawaziri 16................7 kutoka CUF na 9 kutoka CCM na manaibu wao 6..........................

  Sikulisikia jina la waziri kiongozi wa zamani............nafikiri panga la kugombea uraisi na kuuokosa limempitia.................
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JK nae atacopy na kupaste
   
 3. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana jf, nimesikia kwa mbali tbc 1 kuwa rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar ameteua baraza lake la mawaziri, mwenye habari zaidi atujuze, na hasa kama shamsi vuai nahodha kapata nafasi yoyote kwenye baraza hilo maana yeye alikuwa msitari wa mbele kupinga maridhiano ya wazanzibar.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Yaelekea hiyo ndiyo sera ya kimyakimya ya CCM kuiba sera za Chadema huko majukwaani wanawaponda........kuwa ni fotokopi kumbe ni wao CCM ambao sasa ni fotokopi.............................Hii ndicho ambacho nilikisema awali ya kuwa JK atatawala lakini Dr. Slaa ataiongoza nchi kwa maana ya kuwa JK atatekeleza matakwa yote ya Dr. Slaa ili kutafuta kukubalika lakini hatakubalika hadi pale atakapokiri hadharani ya kuwa uchaguzi wa 2010 haukuwa wa huru na wa haki................
   
 5. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Je ameweka wapinzani wangapi kwenye baraza lake?
   
 6. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Hongera Shien kwa kuteua wapinzani (kama kweli ni wapinzani).
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  wapinzani 7 na CCM 9
   
 8. M

  Mwera JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye data atupe majina yamawazir ila mm nimeliskia juma duni wazir wa afya na abuubakar khamis wazir washeria,nimeipata tbc1 habari ila ilikua mwisho sikuipata kamili habari hii,mwenye data kamili atupatie please.
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbona imeshaletwa habari hii na Ruta?
  News Alert: Dr. Shein atekeleza sera za Chadema..ateua....mawaziri 16 na manaibu 6......

  Started by Rutashubanyuma, Today 09:40 PM
   
 10. n

  njeru Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni baraza la serikali ya mapinduzi ya zanzibar
  1. Waziri wa nchi afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk mwinyihaji makame
  2. Waziri wa nchi afisi ya rais fedha uchumi, mipango na maendeleo, mhe omar yussuf mzee.
  3. Waziri wa nchi afisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora. Mhe haji omar kheir
  4. Wizara ya nchi afisi ya makamo wa kwanza wa rais waziri ni mhe fatma abdul habib fereji na waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais ni mhe mohd aboud mohd.
  5. Wizara katiba na sheria mhe abuu bakar khamis bakar,
  6. Wizara ya miundombinu na wawasiliano mhe hamad masoud hamad na naibu wake mhe issa haji ussi
  7. Wizara ya elimu na mafunzo ya amali mhe ramadhan abdalla shaaban, naibu wake mhe zahra ali hamad
  8. Wizara ya afya mhe juma duni haji naibu wake dk sira ubwa mamboya
  9. Wizara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya wanawake na watoto mhe zainab omar mohd.
  10. Wizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo mhe abdilahi jihad hassan, naibu wake.
  11. Wizara ya ardhi makaazi, maji na nishati mhe ali juma shamhuna, naibu wake mhe haji mwadini makame
  12. Wizara ya kilimo na maliasili mhe mansour yussuf himid,
  13. Wizara ya biashara viwanda na masoko mhe nassor ahmed mazrui, naibu wake mhe thuwaiba edinton kisasi.
  14. Wizara ya mifugo na uvuvi mhe said ali mbarouk
  15. Wizara ya kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika mhe haroun ali sleiman.
  16. Mhe sleiman othman nyanga, mhe haji faki shaali na mhe machano othman said ni mawaziri wasio na wizara maalum.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Shein huwa namwamini bse hana mawaaaaaaaaaa
   
 12. n

  njeru Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baraza la serikali zanzibar ni hili
  1. Waziri wa nchi afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk mwinyihaji makame
  2. Waziri wa nchi afisi ya rais fedha uchumi, mipango na maendeleo, mhe omar yussuf mzee.
  3. Waziri wa nchi afisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora. Mhe haji omar kheir
  4. Wizara ya nchi afisi ya makamo wa kwanza wa rais waziri ni mhe fatma abdul habib fereji na waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais ni mhe mohd aboud mohd.
  5. Wizara katiba na sheria mhe abuu bakar khamis bakar,
  6. Wizara ya miundombinu na wawasiliano mhe hamad masoud hamad na naibu wake mhe issa haji ussi
  7. Wizara ya elimu na mafunzo ya amali mhe ramadhan abdalla shaaban, naibu wake mhe zahra ali hamad
  8. Wizara ya afya mhe juma duni haji naibu wake dk sira ubwa mamboya
  9. Wizara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya wanawake na watoto mhe zainab omar mohd.
  10. Wizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo mhe abdilahi jihad hassan, naibu wake.
  11. Wizara ya ardhi makaazi, maji na nishati mhe ali juma shamhuna, naibu wake mhe haji mwadini makame
  12. Wizara ya kilimo na maliasili mhe mansour yussuf himid,
  13. Wizara ya biashara viwanda na masoko mhe nassor ahmed mazrui, naibu wake mhe thuwaiba edinton kisasi.
  14. Wizara ya mifugo na uvuvi mhe said ali mbarouk
  15. Wizara ya kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika mhe haroun ali sleiman.
  16. Mhe sleiman othman nyanga, mhe haji faki shaali na mhe machano othman said ni mawaziri wasio na wizara maalum.

  Wengine ni walewale walewael
   
 13. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  coloured; mbona sioni ile kitu "wanawake" ndo zamu yao?
   
 14. M

  Middle JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ningefurahi kama unenitajia na vyama wanavyotoka
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [FONT=times new roman, new york, times, serif][FONT=times new roman, new york, times, serif]Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:[/FONT]

  [FONT=times new roman, new york, times, serif]1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
  Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame

  2. Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo)

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
  Mhe. Omar Yussuf Mzee

  3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
  Mhe. Haji Omar Kheri

  4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
  Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.

  5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
  Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

  6. Wizara ya Katiba na Sheria

  Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.

  7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

  Mhe. Hamad Masoud Hamad

  8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

  Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban

  9. Wizara ya Afya


  Mhe. Juma Duni Haji

  10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto

  Mhe. Zainab Omar Mohammed

  11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo


  Mhe. Abdilahi Jihad Hassan


  12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-


  Mhe. Ali Juma Shamhuna

  13. Wizara ya Kilimo na Maliasili


  Mhe. Mansoor Yussuf Himid


  14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

  Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

  15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi


  Mhe. Said Ali Mbarouk

  16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika


  Mhe. Haroun Ali Suleiman

  17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum


  Mhe. Suleiman Othman Nyanga

  18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum


  Mhe. Haji Faki Shaali

  19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum


  Mhe. Machano Othman Said

  Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

  1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

  Mhe. Issa Haji Ussi

  2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali


  Mhe. Zahra Ali Hamad

  3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya


  Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya

  4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,


  Mhe. Bihindi Hamad Khamis

  5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati

  Mhe. Haji Mwadini Makame

  6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,

  Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi


  Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa hapo kesho jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.


  NOTE: Wenye red ndio wa CUF-niliowagundua haraka haraka
  [/FONT]
  [/FONT]
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nahodha wapi jamani? au katupwa kapuni na kuondoka na Karume? Serikali hii haina kujuana na kulindana? hahahahahahaha
   
 17. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Shamhuna ni kimeo specialised in ng'ang'anizi! Haking'oki hata kwa maji ya moto? Kazi kweli kweli
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Jamani Vuai Nahodha kulikoni? Ana bifu gani na Shein? Mbona mimi nilikuwa namuona kuwa ni mtendaji makini sana? Au Shein naye ni mtu wa visasi?
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanza sio sahihi kwamba baraza la SMZ lina mawaziri 16. Nimesoma list yote nimekuta namba 5 kuna mawaziri 2, mmoja wa Makamu wa Kwanza wa Rais na mwingine wa Makamu wa Pili wa Rais na wote ni mawaziri kamili.

  Namba 16 kuna mawaziri 3, ambao ni wasiokuwa na wizara maalum. Hii title ni ya siku nyingi sana na ilikuwa imepotea, naona imeibuka tena.

  Hivi majukumu ya Waziri asiye na wizara maalum ni nini? Mawaziri 3, hawana wizara maalum, hatujui wanafanya nini na bado wanaendelea kulipwa kwa kazi ambazo hazijulikani?

  Takwimu zangu zinaonyesha kwamba Mifugo ni sekta ndogo sana Zanzibar. Kwa hiyo kuna wizara 2 ambazo zinaweza kuunganishwa na bado kusiwe na tatizo kiungozi. Wizara ya Kilimo na Maliasili ingeunganishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

  Bado Baraza la Mawaziri ni kubwa. Nilitarajia kwamba Jussa angekuwa mmoja wa mawaziri, naona imekula kwake.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wakatui mwingine ukongqwe nao unahitajika-Utuuzima dawa bwana
   
Loading...