The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Tetesi
Kipa wa England na Manchester City Joe Hart, 30, hataruhiswa kumaliza mkopo wake huko Westham mwezi Januari. (Sunday Times - subscription required)
 
Tetesi
MAN CITY NA LIVERPOOL ZAMWANIA SERI


Manchester City na Liverpool zinapambana kuipata saini ya kiungo wa Nice Jean Michael Seri, kwa mujibu wa Daily Mail .
Muaivory Cost huyo alihusishwa na tetesi za kutaka kutua Barcelona majira ya joto, lakini kwa sasa yupo tayari kutua Uingereza.
 
Pep Guardiola anaamini kuwa atahitaji kumsaini mlinzi mwezi Januari la sivyo Manchester City watakuwa matatani. (Guardian)
 
Imeripotiwa kuwa Manchester City inakaribia kukamilisha mkataba mpya na mshambuliaji Gabriel Jesus
Mchezaji huyo wa kimataifa Kibrazili amekuwa akichuana kwenye Ligi Kuu Uingereza tangu Januari, lakini kiwango chake cha 2017 kimemshawishi Pep Guardiola kumtunuku mchezaji huyo kwa mkataba mpya.
Kwa mujibu wa The Telegraph, City wamejipanga kumpa mchezaji huyo wa miaka 20 kitita cha £100,000 ambalo ni ongezeko la 30% na ataongeza mkataba kutoka 2021 hadi 2023.

Katika kipindi chake Etihad, Jesus amefunga magoli 17 katika mechi 34 za michuano yote, ingawa miezi yake ya awali klabuni hakuweza kucheza kwa sababu ya majeraha.
Jesus amefunga magoli 10 katika mechi 21 Ligi ya Uingereza na Ligi ya Mabingwa msimu huu, na mchezaji huyo alipewa nafasi kubwa mbele ya Sergio Aguero wikiendi iliyopita kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United.
 
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amemwelezea David Silva kama kiungo aliyekamilika baada ya kufunga magoli katika mechi za hivi karibuni.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania ameweka kimiani katika ushindi mwembamba dhidi ya West Ham United na Manchester United kwenye mechi zilizopita, kadhalika mabao mawili aliyofunga dhidi ya Swansea City Jumatano.
Guardiola amemsifia Silva kufuatia kiwango chake maridadi, akidai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 sasa ni "mnyama" anapokuwa akiwinda goli mbele ya lango.
"Ana kila kitu, hasa anapokuwa dhidi ya wapinzani wakuu." alikiambia BBC Sport. "Kila mmoja anazungumzia ufundi wake, hakuna shaka katika hilo. Hata kipofu anaweza kuona.
"Lakini huwezi kufikiri ni kiasi gani alivyo mahiri dhidi ya wapinzani. Anaonekana kama mtu wa aina tofauti lakini, wow, ni mnyama katika kipengele cha kushinda mech.
"Mara zote tumekuwa tukizungumzia hilo: 'Unahitaji kufunga magoli, David. Unaweza kufanya hivyo. Unahitaji kufunga magoli ili kushinda mechi. Unaweza kufanya hivyo.' Katika kipindi kilichopita goli dhidi ya West Ham na Old Trafford na dhidi ya Swansea ni muhimu sana."
Silva amehusika kwenye magoli 13 Ligi Kuu Uingereza katika mechi 17 msimu huu - tayari amezidi kile alichofanya 2016-17
 
habari zenu wapendwa? Nina shida ninahitaji kuuliza hasan kuhusu Ligi ya england inayoendelea .swali langu ni je kati ya Man u, Asernal, Chelsea, na Totenham, ni timu ipi ambayo haijakutana na man city bado? kuna siku nilikuwa nabishana na rafiki yangu. Naomba mnjuze tafadhari
 
Pep Guardiola amelazimika kuwashawishi mabosi wa Manchester City kuingia sokoni kusaka beki mpya wa kati katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

Kocha huyo anataka libero mpya baada ya nahodha Vincent Kompany kuwa nje ya uwanja muda mrefu akiuguza jeraha la misuli na John Stones ni majeruhi.

Guardiola amelazimika kumtumia beki wa akiba Eliaquam Mangala katika mechi za hivi karibuni kujaza nafasi ya Stones. Kocha huyo anataka mchakato huo kukamilika mwezi ujao.

Macho ya kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich yametua kwa libero wa Southampton, Virgil van Dijk au Jonny Evans wa West Ham Bromwich.

Van Dijk alishindwa kutua Liverpool majira ya kiangazi msimu uliopita baada ya kuwekwa sokoni kwa Pauni 70 milioni, hivyo Man City italazimika kuvunja benki.
 
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amemkosoa hasimu wake Jose Mourinho kocha wa United na kuimwagia sifa tele Tottenham.
City wanaongoza kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza kwa tofauti ya alama 11 baada ya kushinda mechi 16 kati ya 17, ikiwa ni pamoja na mechi ya Jumapili jijini Manchester.
Timu ya Guardiola itaikaribisha Tottenham Jumamosi na ushindi mwingine utawawezesha kuwa mbele ya Spurs kwa tofauti ya pointi 21.
Akiwasifia wachezaji wa Mauricio Pochettino na Chelsea, Guardiola alionekana kumchambua tena Mourinho na United.
"Nadhani Tottenham na Chelsea ni timu nzuri zinazotaka kucheza mpira," Muhispania huyo alisema, akinukuliwa na Mirror.
"Hawawategemei wengine [kucheza], wanataka kutengeneza mchezo wao wenyewe, na ni mtihani mwingine kwetu siku tatu baada ya kucheza Swansea.
"Baada ya hapo, tutaikabili Leicester Kombe la Carabao. Hakuna muda mwingi wa kupumzika lakini tupo tayari kuikabili Tottenham na kuendeleza kiwango ambacho tumeonyesha mara ya mwisho."
City wamefunga magoli 52 kwenye mechi 17 msimu huu, wakipewa sifa tele kwa mfumo wao, wakati United ya Mourinho inakosolewa kwa namna ya uchezaji wa timu yake licha ya kushika nafasi ya pili.
 
FA imemuuliza meneja wa Manchester United kuelezea kauli zake alizosema kabla ya mechi ya Ligi Kuu Uingereza dhidi ya City uwanjawa Old Trafford
Jose Mourinho ametakiwa na Shirikisho la Soka kuelezea kauli alizosema kwenye vyombo vya habari kabla ya mechi kubwa ya Manchester.
Mreno huyo alishuhudia timu yake Manchester United ikinyukwa 2-1 na mahasimu wao Manchester City kwenye mechi ya Ligi Kuu Uingereza Jumapili ambapo baada ya mechi kulikuwa na tafrani nyingi kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo Old Trafford.
FA tayari imeshaziuliza klabu zte kuhusu mtazamo wao katika tukio hilo, ambapo kwa mujibu wa habari Mourinho alimwagiwa maziwa.
Hata hivyo Mourinho amejikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kauli zake alizosema kabla ya mechi, alipoishutumu City kwa kutumia ujanja kwenye mchezo, akisema: "Wakipulizwa kidogo na upepe wanaanguka."

Mourinho pia alidai kuwa City wanatumia "mbinu ya faulo" kuvuruga mchezo alipokuwa akizungumzia mechi dhidi ya hasimu wake wa siku nyingi Pep Guardiola.
Tangazo la FA inasomeka: "FA imeomba uchunguzi wa kauli za Jose Mourinho kwenye vyombo vya Ijumaa Disemba 8, kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester City.
"Amepewa muda wa kujibu hadi saa kumi na mbili jioni Disemba 18 Jumatatu."

City walitoka kifua mbele, shukrani kwa magoli kutoka kwa David Silva na Nicolas Otamendi walioongeza pengo la pointi kuwa 11 kileleni mwa msimamo wa ligi.
Lakini klabu zote mbili zinaweza kuwa matatani, na huenda FA ikawashughulikia kufuatia tafrani iliyozuka kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo ambapo wachezaji walikuwa wakitofautiana.
Inasemekana Mourinho aliingia kwenye chumba cha City cha kubadilishia nguo, akiwa hajafurahishwa na muziki uliopigwa baada ya timu ya Guardiola kuibuka na ushindi.
City na United zimepewa muda hadi Ijumaa jioni kutoa majibu kwa FA kuhusu mtazamo wao kwa tukio hilo.
 
habari zenu wapendwa? Nina shida ninahitaji kuuliza hasan kuhusu Ligi ya england inayoendelea .swali langu ni je kati ya Man u, Asernal, Chelsea, na Totenham, ni timu ipi ambayo haijakutana na man city bado? kuna siku nilikuwa nabishana na rafiki yangu. Naomba mnjuze tafadhari
Totenham juma mosi
 
Tetesi
Hata hivyo, Manchester City wanataka kumuongeza beki wa kati kwenye kikosi chao Januari na huenda pia wakawasilisha ombi la kutaka kumnunua Van Dijk, ingawa viongozi hao wa Ligi ya Premia pia wanataka kumnunua mchezaji wa Real Sociedad Inigo Martinez, 26. (Goal)
 
Back
Top Bottom