The hijacking of the Kaabah-1979

tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
496
604
Habari Wapendwa!

Ilikua ni siku ya kawaida katika mji wa Makkah, ambapo mahujaji siku hii walikua wakiendelea na pirika zao za kuikamilisha ibada ya Hija ifanyikayo kila mwaka mara moja. Ni alfajiri ya tarehe 20 November mwaka 1979 adhana ya alfajir ilikua ikisomwa huku majeneza nayo yakiingizwa mskitini kwa ajili ya kuswalia Kisha kuzikwa katika ardhi iliotukufu kwa waislam.

Pia njiani kulionekana sura ngeni huku magari yakiingia ambapo wageni hawa waliambatana na wake pamoja na watoto wao ili wasiweze kujulikana kwa tukio zito ambalo wangetarajiwa kulifanya. Ulikua ni mwanzo wa tarehe ya kiislam mwezi wa Muharam sawa na mwaka 1400 hjiria ikiwa sasa ni mwaka 1439 hijiria.

Adhana ilipomalizwa kusomwa na watu wakaanza kuswali, baada ya swala Imamu alievalia vazi la joho akasimama mbele ya watu wafikao takriban laki moja kusiliza kile ambacho atakizungumza.

Alikuwa sheikh Muhammad ibn Subayyid ndio alieongoza hio ibada ya suala, mara milio ya KALISHNIKOV ASSAULT RIFLE iliotengenezwa Belgium ikaanza kusikika ndani ya eneo la mskiti.

Hapo vurugu likaanza kutokea huku mtu mmoja akichomoka kutoka mstari wa mbele na kushika microphone ambayo imam alikua akiitumia. Walinzi walimtazama tu kwani hawakua na silaha ila fimbo tu zajuwekea ndidham kwa wale mahujaji ambao wangetarajiwa kuleta vurugu.

Hapo hapo, kuna kikundi cha watu pia nao wakainuka na kuwazidi nguvu wale asakari waliokua mbele ya safu. Matangazo yakaanza kutoka kwa yule mtu aliempkonya microphone sheikh Subayyid, akazungumza kuhusiana na kuporomoka kwa maadili sambamba na kutokuwa na uadilifu katika utawala wa kiflme wa Saudi Arabia, pia akaongezea kuwa nyingi katika dalili za kumalizika ulimwengu zimekwisha kutokea tena mbele ya macho yao. Na akanukuu maneno ya Mtume Muhammad swala na salam ziwe juu yake ya kuwa alisema kuwa Allah anamleta mtu ambae atakuja kuihuisha dini ya kiislam kila baada ya miaka 100,naam na kweli siku hio ya tukio ilikuwa ni karne mpya kwa upande wa tarehe ya kiislam yaani mwaka 1400A. H, Kisha mzungumzaji akanukuu maneno mengine juu ya Mahdi ambae atakuja kuijaza dunia uadilifu pale uadilifu utakapotoweka na kuondosha uovu uliokithiri kama ilivyokua mwaka huo 1979 Akaongezea tayari huyo Mahdi tupo nae hapa. Hapo akamuita mtu alie mbele yake huku akiupasha Umma uliopo hapo na kuwaeleza" hamuoni amesimama katika makam Ibrahim, jina lake ni Muhammad ibn Abdullah AlQhtani, jina Sawa Sawa na lile la Mahdi alietajwa na Mtume Muhammad swala na salam ziwe juu yake, tena anatokea katika kabila la Quraish!?

Mpendwa msomaji, naomba nikueleze baadhi ya vitu ili tuweze kwenda sambamba.
Ni kweli Mtume Muhammad swala na salam ziwe juu yake alitabiri kuwa atakuja Mahdi kama alivyotabiri kuja kwa nabii Issa,. Ni nan haswa alie kuwa akiwapa khabari hizi watu?

Si mwengine bali ni kijana wa miaka 43 wakati huo, anaitwa Juhayman ibn Muhammad ibn Seif Al Utaybi, yeye ndiebaliekua mastermind wa tukio zima la utekwaji wa Mskiti mtukufu zaidi duniani. Alizaliwa tarehe 16 September 1936 katika kijij cha Al sajri nchini KSA, alikua mzuri katika masuala ya kivita tokea yupo mdogo, alimaliza skuli pasi na kutokuwa na uwezo mzuri wa kuandika bali alipenda sana kujisomea maandiko ya kidini. Alihudumia vikosi vya Saudia Arabia kuanzia mwaka 1955-1973.Alikua mwembamba mwenye urefu wa 187cm. Alijuana na Muhammad ibn Abdullah AlQhtani wakati alipokua Madina, mji jirani na Makkah.

Waislam waliokuwepo hapo wengi wao walichanganyikiwa hali ya kutokuelewa kinachozungumzwa mana walikua ni watu kutoka pande tofauti za ulimwengu, bali Juhayman alikua na watu wengine kama 2 mmoja alikua a nafanaya interpretation kwa kingereza, mwengine kwa kiurdu. Hakuna alieruhusiwa kuingia wala kutoka katika eneo la mskitini kila mlango ulikua umefungwa na kulikuwa na wanajeshi waliojihami kwa Ak-47, ilipofika siku ya 4 Juhayman na wenziwe waliwaruhus baadhi ya watu kutoka kwani hawakua na uwezo wa kuwalisha.

Inasemekana Juhayman alikua na kikosi cha wanajeshi 200,ila baadhi ya wanahistoria wanasema walikua 1000. Siku hizi Kaaba ambapo ilikua mateka ibada zilisimamishwa katika eneo hili tukufu, hapakuswaliwa swala za pamoja wala hapakufanyika twawaaf, yaani kile kitendo cha kuzunguka Al kaaba.

Siku ya tukio yaani November 20 1979, mnamo nyakati za adhuhuri jeshi la Saudia pamoja na askari wake hawakua wakijua nini kinaendelea ndani ya mskiti wa Haram, ilikua ni mara yao ya kwanza kukabiliana na kitendo cha kigaidi, bali hapo nyuma limeshawahi kutokea tukio lifananalo na hili ambalo lilisababishwa kuibiwa kwa jiwe jeusi (the black stone) hivo iliwachukua siku nzima yote ili kuweza kuchanganua kitu gani kilikua kikiendelea ndani ya mskiti kuwa kulikua na Mahdi feki ameteka mskiti. Walipo jaribu kupeleka wanajeshi watembeao kwa miguu kuingia eneo la mskiti waligundua kuwa katika minara ya mskiti yenye urefu wa futi 292 Juhayman alikua amewapanga snipers wakutosha ili kumtungua risasi kila atakaejichomoza.

Mpendwa msomaji, hivi Juhayman aliwezaje kupitisha silaha nzito, na nini alikipanga kabla ya tukio?
Unakumbuka yale majeneza yaliokua yakiingiza maiti ndani ya mskiti, basi zile jeneza zilitumika kubebea silaha za KALISHNIKOV ASSAULT RIFFLES, BELGIUM made FN FAL GUNS BULLET belts, kwani jeneza hazikuwa zikisachiwa. Na silaha zote hizo zilikusanywa katika eneo moja na once baada ya swala kila mtu alitakiwa akae katika position ambayo alitakiwa kukaa ili kufanikisha mpango mzima wa kutekwa kwa Kaabah.

Matakwa yao ilikua kuitaka serikali ya kifalme iachie madaraka licha ya matakwa mengine zaidi jambo ambalo lisingeweza kutokea na kukubaliwa si unajua Ile ya kwenye movies "we can't negotiate with terrorists" sasa hio ndio iliotokea. Tukumbuke kuwa kupigana vita ndani ya eneo la mskiti huu mtukufu ni haramu yaani haifai.

Hivo basi wanachuoni yaani wasomi wa kiislam na wanaotegemewa hapo Makkah na dunia nzima katika ulimwengu wa kiislam walitoa Fatwa kuhusu huyu Mahdi feki, na wakasema kuwa hachua zichukuliwe zidi yake kwani the prophecies Mahdi asingeweza kuiteka Kaaba na kusababisha vita baina ya safu za kiislam, kwani Mahdi anaetarijiwa atakuja kuleta uadilifu na amani katika dunia hapo itakapochafuka.

Ilipofika day 9, vikosi vya Saudia walichukua vifaru na kuvipandisha katika eneo la ngazi kuingia katika eneo la tukio, na kuweza kuwakimbiza wanajeshi hao wa Juhayman na kukimbilia katika basement ya mskiti na hii pia ilikua tactics yake kwani ilikua ni one way in hivo mwanajeshi yoyote ambae angeingia eneo hilo basi angepigwa risasi.

Ila wanajeshi wa Saudia wakagundua mtego huu na wakaamua kuingiza matairi yaliochomwa moto ili wale jamaa wa Mahdi feki wae chocked na moshi ambao ilienea ndani ya basement ili kuwafanya watoke nje na kuwamaliza. Mbinu hii haikusaidia sana hivo ikatumika plan nyengine ambayo ndio ilileta ushindi, ilibidi itumike physics ya primary nayo ni walijaza maji katika eneo hilo la basement na kuingiza live electrical wires na kupelekea wanajeshi wengi kufariki pamoja na Juhayman mwenyewe, na wengine walikamatwa na wakawa excuted publicly yaani waliuwawa hadharani.
Ila nitakuwacha na masuala ya kujiuliza.

Kwanini jeshi la Juhayman halikuangamizwa kama walivyoangamizwa wanajeshi wa Abraham kwa ndege waliobeba vijiwe vya moto? Usikose sehemu ya pili ili kuweza kuja kujua sababu ya kutokuangamizwa wanajeshi wa Juhayman directly kama ilivyokua kwa wanajeshi wa Abraham au kama wajuoikanavyo THE ELEPHANTS ARMY.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
tilmikha, Ingawa Uzi huu ulivutwa kitambo na Mimi napenda kuongeza kuwa kiongozi utekaji wa AL-KAABA TAKATIFU MWAKA 1979 JUHAYMAN AL-OTAYBA, alijisalimisha na baadae akauwawa na mamlaka ya Saudia.

Juhayman.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie unenishagaza uliposema kuwa muhammadi alitabiri ujio ya Nabii isa ambaye ni Yesu(According to Islam doctrine) kitu ambacho ni uongo. Yesu alikuwepo kabla ya Mohammad na baadae yesu akawa amekufa na kufufuka.
Kingine cha kushangaza, Jiwe jeusi liliibiwa Yawezekana lililopo sio jiwe halisi.


Happy dude
 
Mie unenishagaza uliposema kuwa muhammadi alitabiri ujio ya Nabii isa ambaye ni Yesu(According to Islam doctrine) kitu ambacho ni uongo. Yesu alikuwepo kabla ya Mohammad na baadae yesu akawa amekufa na kufufuka.
Kingine cha kushangaza, Jiwe jeusi liliibiwa Yawezekana lililopo sio jiwe halisi.


Happy dude
Yaani katabiri ujio wa yesu mara ya pili Kama MASIH(MASIA)anae subiriwa Hilo nadhani hata wa Kristi ujio huo wanauamini na kuusubiria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie unenishagaza uliposema kuwa muhammadi alitabiri ujio ya Nabii isa ambaye ni Yesu(According to Islam doctrine) kitu ambacho ni uongo. Yesu alikuwepo kabla ya Mohammad na baadae yesu akawa amekufa na kufufuka.
Kingine cha kushangaza, Jiwe jeusi liliibiwa Yawezekana lililopo sio jiwe halisi.


Happy dude
Hukufaham mkuu, nilikusudia ujui wa Yesu wa mara ya pili labda niwe nimeandika makosa ila kusudio ni ujio wa mara ya pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ah nilihisi hauna wasomaji nikaona tabu kujichosha ila kama mpo mnaotaka niendeleze basi nitafanya hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapoandika jambo humu jua unaacha alama ya kudumu. Kuna baadhi ya nyuzi humu unakuta iliandikwa mwaka 2016, lakini inakuja kupata michango mingi mwaka 2018. Mfano, mimi kuna wakati napata nachokihitaji kupitia nyuzi za mwaka 2008 huko. Maandishi huwa hayafi mkuu!
 
Unapoandika jambo humu jua unaacha alama ya kudumu. Kuna baadhi ya nyuzi humu unakuta iliandikwa mwaka 2016, lakini inakuja kupata michango mingi mwaka 2018. Mfano, mimi kuna wakati napata nachokihitaji kupitia nyuzi za mwaka 2008 huko. Maandishi huwa hayafi mkuu!
Ahsante mkuu kwa kunielewesha, nitafanyia kazi ushauri wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sijui uelewa wako ulifikia wapi, Mohammad hakutabiri hivyo, yeye alisema kua katika zama karibu na kiama basi masii Issa mwana wa mariam atarudi kupambana na masii dajjal huko Mashariki ya kati.
Mie unenishagaza uliposema kuwa muhammadi alitabiri ujio ya Nabii Issa ambaye ni Yesu According to Islam doctrine) kitu ambacho ni uongo. Yesu alikuwepo kabla ya Mohammad na baadae yesu akawa amekufa na kufufuka.
Kingine cha kushangaza, Jiwe jeusi liliibiwa Yawezekana lililopo sio jiwe halisi.


Happy dude

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom