Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mr Acky

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
234
313
MTUNZI : AKIDA S. RAMBAO
Contact : 0658328596
email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 1 (A) : JINAMIZI LA SIKITIKO.
Kijiji cha kishanje, Makaburini, Bukoba-Kagera.

Dodoso:
Ni maumivu yanayo ukoroga moyo wake na kuutibua tibua, moyo unatibuka
unachafukwa anajikuta akilia kwa uchungu anatamani abadilishe ukweli uwe uongo
lakini yameshakuwa. Nini kimemkuta, atafanya nini na ataamua nini? Ni ukweli upi huo? Yeye ni nani?

Alibaki kasimama akitazama makaburi manne ya thamani kubwa, yaliyojengwa kwa kufanana na kufatana, akafumba
macho huku akikunja sura kama mtu anayejitahidi kupingana na hali inayomkabili. Punde machozi yakaanza kumtoka aliyaacha yamwagike kwa mfatano huku sauti ya kilio cha chini chini iliyobanwa isitoke ikisikika ikiomboleza kichwa kikinesa nesa kwa uchungu. Mwisho kitambaa kikapita kati ya macho yake na kuyakaushia mbali. Akavuta kamasi lililokuwa likizengea zengea kuchungulia katika tundu ya pua likitaka
kutoka na kukirudisha kitambaa mfukoni.

“Uuuuuuhuu…”
alizishusha pumzi “Nimewamisi sana…baba, mama, dada na kaka Pater…niko mpweke sana” aliongea kwa kuachia achia maneno akijishika kichwa mara kiuno na tena kichwa kana kwamba ni mtu asiyeamini au kuchanganyikiwa.

Mara alijikuta akiishiwa nguvu akayakita magoti ardhini na kuanza kulia kwa sauti kama mtoto. Alilia bwana huyo kwa kupiga nduru kadri alivyoweza huku akitweta jasho likimtoka.

“Kiongozi inatosha utaumwa kichwa unajua, alafu jua ni kali…” ilikuwa ni sauti ya kiume nyuma ya mgongo na mkono ukagusa bega lake kumaanisha, akageuza shingo na kumtazama hasira ikijidhihirisha machoni pake “Lau kama
Ungeliniacha ungelikuwa bora kuliko kuniingilia” aliongea huku sura ikiwa imekunjamana haswa kiasi cha
kumuogopesha aliyemuongelesha mara moja mkono ukatolewa begani mwake na kurudi alipokuwa. “…nakumbuka
mengi sana yaliyopita tukiwa pamoja, zaidi ninachoweza kuwaambia nimekuja kwa kuwa nahitaji Baraka zenu juu ya
kazi ambayo naenda kuifanya naamini itawapa amani huko mlipo na nafsi zenu zitatulia” aliongea kisha akasimama
“Majaliwa nipatie maua yangu tafadhari” aliongea tena, Majaliwa akampatia, huyo akasogea hadi katika kaburi la kwanza “Julius Ebariki Emmanuel Mkwasi” aliyasoma kwa sauti ndogo maneno yaliyoandikwa katika jiwe kubwalililojengwa kichwani mwa kaburi lililonakshiwa kwa Granite muundo huo hujulikana kama Memorial Granite tombstone na kisha akaweka moja ya maua aliyoyakumbatia. Alifanya hivyo
kwa makaburi yaliyosalia akageuka na kuondoka zake.

“Nipatie simu yangu nataka kupiga” aliongea akapandisha mguu baada ya kufunguliwa mlango wa gari kwa heshima.

Baada ya kupatiwa akabonyeza namba zenye usajili wa nchi ya kigeni “Hallow what’s news…will please give him his cash in cash and transport him by Private plane to Tanzania without being denied and make sure he does not escape” aliongea kisha akatabasamu “Majaliwa tuondoke” Gari ikawashwa na kuondoka

Kijiji cha Kyakailabwa, Bukoba-Kagera
“Sijaja hapa kwa ajili ya kupoteza muda Mzee Ishengoma nipo serious nipatie majibu ya maswali yangu tafadhari laa sivyo…” kabla hajamaliza Mzee Ishengoma akadakia “Fanuel mwanangu kwanza umekuja bila taarifa na ukapitiliza katika
makaburi na sasa usiku huu mzito unanishambulia kwa
maneno nikueleze ukweli!? ni ukweli upi kijana wangu unaniweka katika wakati mgumu mbona…” Mzee Ishengoma
alijikuta akishindwa kumalizia kauli yake nakujiinamia akisikitika kwa kichwa “…nimekulea na nimekusomesha na
sasa una wadhifa mkubwa mwanangu hebu tulia achana na
hayo mambo ni mambo makubwa mwanangu” Mzee
Ishengoma aliongea tena, “Mzee hujajibu maswali yangu” aliongea Fanuel Emmanuel sasa sura yake ikiwa imekunjamana kwa hasira akimkodolea kwa macho yaliyotumbuka, “Kijana sikia sitakuwa tayari kwa hilo nilipokusaidia panatosha” aliongea Mzee Ishengoma huku akinyanyuka toka sofani “ooh sawa watu kama nyinyi dawa yenu ndogo sana” aliongea Fanuel na kutoa bunduki ndogo
nyuma ya kiuno aina ya Girsan M1911SC akaifunga kiwambo wakati huo Mzee Ishengoma macho yakiwa yamemtoka
akishuhudia bunduki ikimtazama haraka akanyanyua mikono wasiwasi ukimzidi “Hapana mwa…mwanangu” aliongea Mzee Ishengoma akitetemeka, lakini hakuwa na bahati teyari risasi
ilisharuhusiwa na kukutana na paji la uso wa mzee huyo akiwa kwenye Taharuki mwili ukisikilizia maumivu alifyatuliwa risasi nyingine ya kifua iliyomyumbisha hadi katika sofa alilokuwa amekalia wakati wa mazungumzo, masikini akaacha Mkono.

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu-Dar es Salam.
Yowe la furaha lilisikika pindi tu Mheshimiwa Jaji bwanaCharles Pascal Kunambi alipoipiga nyundo yake ya haki juu ya meza kusisitiza kile alichokisema awali kisha akanyanyuka
katika kiti chake akiliacha joho pana lililo mzidi kwa wembamba likienda huku na kule akilizuia kwa kulishika
akiwaacha watu wakiwa wamesimama toka kwenye kitiwakitia gumzo za hapa na pale wakishikana mikono wengine
wakitoka kimya kimya huyo. “Hongera sana Richardwasamehe bure ni roho mbaya na wivu wa maendeleo ndio
umetutawala watu wengi na tunakosa ubinadamu” Mzee mmoja aliyekakamaa kwa utuuzima aliongea huku akiwa
kashikilia kiganja cha mkono wa Mheshimiwa Richard
“Asante sana Mzee Boni namshukuru Mungu kwa huruma zake na kumuongoza wakili wangu rafiki yangu bwana
Ferdric Shaka Dodo ambaye alikuwa nami bega kwa bega katika kesi hii” aliongea Richard huku akimshika bega mtu
aliyevalia joho jeusi pembeni yake akitabasamu mkononi akiwa ameshikilia lundo la nyaraka “Ooh vizuri sana kijana
kazi nzuri sana huo ndio urafiki wa kweli haya naondoka” Mzee Boni akauachia mkono huyo akashika njia akipishana na
watu walioendelea kuja kumpa hongera.

“Mheshimiwa… mheshimiwaaa” ilisikika sauti ya kike ikiwa inakuja na kupotea Richard akaacha matembezi ya taratibu aliyoyaanza akiwa karibu kabisa kutoka nje akiongea na Wanahabari
akatulia kidogo akionekana kutegesha masikio “Kuna sauti naisikia kwa mbali” alijisemea “Baada ya madai ya ufujaji wa
mali za Young Trader Company unalipi la kuwaambia wananchi?” hatimaye sauti ilisikika vema na kumfanya Richard kukutanisha macho na mwanahabari akiwa kashikilia kinasa sauti chake akiminyana na watu, akatabasamu
“Naomba utulivu tafadhari” aliongea Mheshimiwa Richard kwa sauti yake ya besi na watu wakatulia “Naomba mumpishe huyo dada asogee karibu ana swali muhimu sana…binti rudia
swali lako tafadhari” aliongea Mheshimiwa Richard na binti akarudia na Mheshimiwa Richard akaanza kujibu huku
akiwaacha wanahabari wakiendelea na jukumu la kuchukua kila kinachowafaa “Kila mtu anapitia changamoto mbalimbali katika maisha yake lakini zote zipo kwa ajili ya kumfanya mtu
akue, nashukuru Mungu nimeshinda kama ilivyo kawaida lazima atokee mshindi na mshindwa, na ninacho weza
kukisema ni kuwa sita rudi nyuma japo biashara zangu zimeathirika kwa kiwango kikubwa na siwezi kuwakasirikia
na nimewasamehe washindani wangu, zaidi ya yote ni kuwa hakuna sehemu iliyoandikwa kuwa ni dhambi kujitafutia cha kwako isitoshe kufanikiwa au kufeli ni jitihada zako, asanteni”
alimaliza Richard na kutoka katika mkusanyiko akifatwa na jamaa zake huku waandishi wa habari wakimfata na maswali lukuki hakujishughulisha nayo akaingia kwenye gari hao wakatimka.

“Unajua mpaka sasa sielewi imekuwaje Richard akashinda hiikesi kwa kishindo jamani tena akiwa na vidhibiti vya kutosha
mbona nashindwa kuelewa hapa” ilisikika Sauti ndani ya chumba cha ofisi mlangoni kukiwa na kibao chenye maandishi
makubwa meusi Ofisi ya Wakili binafsi “Ndugu yangu hata mimi nilibaki mdomo wazi sikutegemea kabisa, wakili hata wewe ulishindwa kuligundua hili? hela zetu zimepotea, alikuwa kila kitu kwetu msimamizi wa kila jambo unajua, akajitoa na mara from no where anakuwa mfanya biashara mkubwa kutuzidi akituacha na madeni na mikopo isiyoeleweka na
bidhaa zilizopitwa na wakati inawezekanaje hili?” “Ndugu
sikia ngoja yameshatokea wacha tujipange upya hakuna atakae skia kilio chetu hapa tumezidiwa kete tumeshajifunza
japo inaumaa” mara mlango ukafunguliwa na wanaume watatu wakatoka wakiwa na nyuso zilizo sawajika,wanahabari waliwaona wakawakimbilia lakini
hawakusikilizwa wakaingia kwenye gari na kuondoka.

Julius K. Nyerere Road, Dar es Salam.
Kimya kilikuwa kimetanda ndani ya gari kila mtu akiwa na lake “Mzee ilikuwaje nikashinda hii kesi kirahisi hivi mihuri
nyaraka kibao, hati miliki, barua sijawahi ziona, taarifa nyingi mpya nimezisikia pale kizimbani zilinishtua ila nilijikaza tu
kama ulivyoniambia, nini kinaendelea hapa?” Richard aliongea “We ni mtu mkubwa bwana, Mheshimiwa Rais
bwana Meza anahitaji kukutana na wewe hayo ndiyo maagizo niliyopewa kwa kweli, maana hata mimi vithibiti nilivyovitoa
mahakamani nililetewa jana home tena na watu nisiowafahamu nikabaki mdomo wazi nani ameziandaa na kwanini ukiniuliza sijui…nakuomba uwe makini naona kuna kitu hakipo sawa mahali au wewe kuna kitu umenificha si
bure au unatakiwa kurudi kazini wanakutafutia sababu”
aliongea Ferdrick huku akiuma meno yake macho yakiwa na wasiwasi Richard akabaki kumtazama akiyapima maneno
aliyoyasikia,Ferdrickakaendelea
“Kingine naonelea uwatafutie pesa kidogo uwape kama shukrani kwa Mungu
maana tulikuwa tunakupoteza ungeshikwa na ndoto zako za biashara na Siasa zingekufa leo kwa kifungo cha miaka ishirini au pesa taslimu, ungezitoa wapi...hata kama tulikuona
ukipambana mengine ni siri yako jaribu kuwapoza na msameheane tu maisha yaendelee pesa zinatafutwa ndugu
yangu” Richard alibaki kumtazama “Na nina wasiwasi na kuvuja kwa siri kuhusu umiliki wa Mzalendo web”
“Inawezekanaje hilo! ni mimi, wewe na Swai tunaojua kuhusu Mzalendo web nani mwingine anaweza kujua bila kuambiwa
na sisi” Richard aliongea kwa wasiwasi “Aah mi nimesema tu haya hayo tuyaache Je, nambie nani unaenda kumuoa kati ya
wale wasichana wawili? Inabidi ufanye maamuzi na tukio mapema” aliongea tena Ferdrick na kumfanya Richardajiinamie huku akiibana midomo yake akalitoa tabasamu la kujilazimisha “Sipo tayari kuingia katika matatizo tenanitatangaza ndoa soon…” Richard akaanza kujisikitikia
akishika kichwa chake machozi yakimlenga lenga. “Maamuzi
mazuri, we ni mwanaume na una bahati hivyo hupaswi kulia utajitia nuksi bure jikaze na usimame kila mmoja akuone,
ujenge na kuziboresha imani za watu upya hilo ndilo jambo la msingi” alidakia Ferdrick

Itaendeleaaaa...wakati ujao

Mijadara inaruhusiwa
IMG_20210320_131445_046.jpg
 
Goma litaaendeleaa msijali
Muendelezo unaambatana na comments zenu pia, Ni riwaya nzuri na ya tofauti sana haichagui lika, hadhi au watu waina fulani pekee. MTUNZI amejaribu kugusa Kila sehemu ya maisha yetu ya Kila siku. Tunaposoma tusiache kukoment na kufikilia Sana kwa sababu inahitaji utulivu mno.
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

MTUNZI : Akida Siri Rambao
Contact : 0658328596
Email : akidasiri@gmail.com

SEHEMU 1 (B): JINAMIZI LA SIKITIKO.
Msasani, Kinondoni-Dar es Salam

BAADA YA MIAKA MITANO

Hakuacha kulia kimya kimya mkono mmoja ukiwa umeshikilia tumbo na mwingine ukiwa umeshikilia picha kubwa akiitazama, kwenye picha alionekana kijana mtanashati na msichana mrembo akiwa amebebwa mikononi mkono wake ukiwa umerusha hewani mawaridi
yaliyochanganywa rangi za kuvutia matabasamu ya haja yakiwa nyusoni “Ooh ndoa yangu, mume wangu, ikowapi
furaha yangu?” Maneno yalimtoka mdomoni na kumpeleka miaka kadhaa ya kumbukumbu ya vifijo, nderemo na
vigeregere vilivyotokea ndani ya kanisa la Kibangu Katolikimaeneo ya Kinondoni miaka ile. Vifijo viliambatana na shamla
shamla kutokana na furaha iliyosheheni miongoni mwa watu wote ambao walikusanyika kwenye hafla hiyo na kushuhudia kwa macho na sio kusubiri kusimuliwa na watu ambao hawaishi kuongeza chumvi na vidokezo kibao kutokana na sifa ya waswahili. Siku hiyo adhimu iliwakutanisha vijana wawili waliotoka mbali kimahusiano na hadi kuamua kuwa mwili mmoja katika maisha yote yaliyo salia ndani ya ndoa yao, ilipendeza mno.Siku hiyo ilikuwa siku ya aina yake maana ilivunja rekodi kwa kuwa na umati mkubwa wa watu waliohudhuria, watu walifurika kanisa likaonekana dogo lisilo tosha kumeza wingi wa watu hao. Hivyo wengi walibaki nje wakisikiliza kupitia spika kubwa.

Baada ya ndoa kufika hitimo lake sherehe ilihamishiwa kwenye moja ya Hotel mashuhuli iliyopatikana katika moja ya
fukwe tulivu maeneo ya Mbezi ambapo wanafamilia na marafiki waliona ndiko sehemu sahihi ya sherehe yao kuishia.
Watu walisombelewa wakitangulizwa katika Hotel zamu kwa zamu mpaka wakaisha. Sherehe ilisuuza nyoyo za watu kwakufana sana kila mtu alikuwa ni mwenye kuridhika,haikuchambua watu, wenye pesa zao walikuwepo na wasio
kuwa nazo pia walikuwepo. Watu ziliwajaa furaha si kwa ajili ya sherehe hiyo maalumukwao laahasha! bali kule kufika sehemu ya hadhi kwa mara ya kwanza ilitosha kuongeza furaha zao maradufu, wengi walikuwa wakiisikia toka midomoni mwa watu tu kuwa ina hili na lile basi siku hiyo wakajionea maana walisafisha macho haswa. Sherehe iliwafanya watu wote kuonekana wapo sawa,haikuwa rahisi kuwatambua wenye nazo na wasio kuwa nazokwa muonekano wa macho tu bila kupata fununu na nyepenyepe zinazowahusu maana waliulamba viwaro vya heshima na kunukia manukato mazuri waliyopeana huko walipo toka, waswahili husema umaridadi huficha umasikini.
Siku hiyo watu walikunywa vinywaji vya kila namna, lakini ndo hivyo huwezi pata kama utakavyo bali kwa kuridhika upatacho ndio uungwana na ukitaka ukitakacho kwa wakati uutakao basi fanya chako, ndivyo ilivyo kuwa kwa wapenzi wa pombe za asili chang’aa, chibuku na mataputapu
hazikuwepo siku hiyo hivyo walikubaliana na mazingira kwakupozwa na chupa za konyagi zilizo jaa maboksi kwa maboksi. Wanywaji hao walibaki kukenua meno wakatulia na chupa zao na kusahau kiu za vinywaji wavipendavyo, basiwalikunywa baadhi yao waliserebuka kumwaga shoo ya kucheza kwa zamu kwenye jukwaa, ilifurahisha nyoyo zao na kupendezwa sana.

Wachamungu wenye kuheshimu imani zao kutokana na makatazo ya dini zao juu ya unywaji wa pombe wao walikaa chonjo wakinywa vinywaji laini visivyo na kilevi.
Watu walijichagulia vyakula kwa kupanga mistari wake kwao na waume kwao kwa nidhamu ya hali ya juu hii nikutokana na
kusimamiwa na watu mahususi, watu walichagua vyakula na matunda mbalimbali kwa uhuru na kujaza sahani zao. Walala hoi wengi walishangazwa walishazoea kukaa kwa pamoja na
kugombaniana sahani za pilau zilizo bebwa na waandaaji katika harusi zao za mitaani tena hata kuambulia kula bila
kunawa ilikuwa kawaida kwao na hata siku nyingine kuondoka bila kula kabisa, lakini walichokiona kwao ilikuwa Pepo. Nyama zilichomwa vizuri, zingine zilikaangwa na
zingine ziliungwa mchuzi kwa viungo vilivyo pangiliwa kitaalam na wapishi wa hoteli hiyo, basi ikawa za kuchomwa
twende za kukaangwa twende za kuungwa mchuzi twendewatu walijichukulia kwa kurudia.Upande wa ndugu walifurahia sana kuona utulivu wa sherehe nzima,walibaki kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuwashukuru watu wote waliohudhuria kuonesha mapenzi mazito kwa vijana wao. Moja ya mambo waliyoyapa
kipaumbele ni pale baadhi yao walioshika kipaza sauti na kuwaombea dua wengine kutoa chochote kitu walicho jaaliwa
na kuwapatia wanandoa kabla ya kutawanyika, imebaki kumbukumbu tu haiwezi kujirudia tena siku hiyo.

Taratibu akajinyanyua kitandani na kusimama na kuiachanguo ya kulalia fupi iliyo mwilini mwake kutoa siri ya yaliyo
hifadhiwa kwa namna ya uwepesi na uundwaji wake wa uwazi. Urefu usio kera, Umbile la miinuko, kiwiliwili cha
kushangaza, maeneo yaliyogawanywa sehemu zilizojaa kujaa
na zilizo achia kuachia na kumfanya kuwa mwanamke mwenye mvuto usio isha hamu kana kwamba alishushwa toka
Peponi. Huyo moja kwa moja kwa kujivuta akiacha mitikisiko ambayo hakuijali akalikabili kabati lilioshikizwa ukutani
akavuta mtoto wa droo na kutumbukiza mkono wake wa kuume na kukutana na Flash disk akaitazama kwa muda
akigeuza geuza kinyonge “Kuna nini ndani yake humu mbona nasita kuitazama, itabidi niirudishe mahala pake kabla
haijatafutwa” alijisemea na kuirudisha huku akiifunika na vitabu juu aliporidhika “mbaah” akafunga droo kisha
akageuza shingo akauma midomo yake huku viganja vya mikono vikifata kupangusa machozi machoni taratibu
akasogea kitandani na kujibwaga chali kitandani macho yakiwa juu.

Baada ya masaa mengi kupita majira ya saa sita usiku yule mwanamke mrembo akiwa kajiegemeza ubavuni mwa
mumewe alivuta pumzi kwa nguvu na kuzitoa kwa kujizuia na mkono wake wa kulia “Mke wangu…” Mume alimshika bega mkewe na kujiweka sawa “…sikia, lazima tutafute njia ya kutatua tatizo hili…” kisha akaanza kuupitisha mkono wake
wa kuume hadi kwenye mashavu ya mkewe na kuanza kuyafuta machozi kwa vidole vyake taratibu. “…unajua mke
wangu sisi sote hapa hatujui ni nani kati yetu anamatatizo inabidi twende Hospitali tukajitambue tu hamna kukwepa,
tumesubiri sana…” Mume aliongea huku akiikuna pua yake na akamtazama mkewe kwa jicho la wasiwasi. Mke akajinyanyua
kishida shida akijitoa ubavuni mwa mumewe akamtazama mumewe kama mtu anaeomba kitu muhimu alichokipoteza na mara akaangua kilio cha kwikwi kubwaa tena kwa sauti huku
akiongea kwa shida shida “Naogopa mmu…mumme waanguuuuu…aaah…” Mume akamtazama mkewe kwa
huzuni, “Usijali mke wangu kila kitu kitakuwa sawa tu” aliongea mume kisha akamvuta zaidi kwake na kumkumbatia.
“Kwa kuwa kesho ni jumamosi tuitumie vizuri kwenda Hospitali mke wangu” Richard alijinasua kwenye sofa na
kumnyanyua mkewe taratibu akamueka kwapani nakumuongoza kwa hatua fupifupi kwenda ghorofani.
Tangu siku ile ambayo ilikuwa ngumu kusahaulika vichwani mwa watu wengi, familia ya mheshimiwa Richard ilivamiwa
na Jinamizi la sikitiko, likatawala na kuanza kuifubaza tamu ya ndoa. Furaha iliaanza kuzorota siku hadi siku. Wanandoa hao waliwaza na kuwazua walikuna vichwa vyao wakifikiri kuhusu atakae kuja simamia mali zao, hawakumuona
mwingine zaidi ya mtoto wao ambae atatokana na ushirikiano wa maungo yao kuja kumiliki majumba, mahoteli, magari na maduka ya jumla yaliyo sheheni sehemu nyingi nchini. Kila mmoja wao alitamani sana kumuita mwezie mama fulani na huyu baba fulani, lakini haikuwa.
Baadhi ya familia zimejaza watoto wanaongezeka kila uchwao huku mifuko yao ikiwa mitupu haina kitu hali hohe hahe.

Familia nyingi za mafukara huwaacha watoto wao kutanga tanga mitaani na mijini wakiomba kwenye magari, wengine
wakitafuta mikate majalalani na hata kufanya kazi ngumu kwa ajili ya kukidhi haja za matumbo yao wengine wakiishia
kuwa wezi waliokubuu na hata kuishia kwenye ulevi na biashara ya madawa ya kulevya ndio shughuli za watoto
wengi huko mijini huku mabinti wadogo kubeba mimba kutokana na changamoto za ubakaji, kuwa malaya na vijana
wa kiume kuishia kulawitiwa na kupelekea kuwa mashoga sababu ikiwa ni maisha duni. Hatari kubwa inayokithiri siku
hizi ni wamama wengi wenye vizazi ambao huwatelekeza watoto wao wakiwa bado wachanga wengine kuchoropoaujauzito kwa sababu tu ya kutokuwa na uhakika wa kula, umasikini kweli mbaya. Hakika ni jambo la kustaajabisha kimtazamo na kuona nguvu ya mwenyezi Mungu ilivyochukua nafasi katika ulimwengu kila alifanyalo huwa lina sababu hasa
pale anapogawa riziki kwa waja wake.
Migeuzo na minyoosho ya mwili ilimtawala kishaakajinyanyua kitandani uso ukiwa na wenge la usingizi akifinyafinya macho na kupikicha kwa vidole vyake
kujichangamsha haikutosha akaupeleka mkono mmoja magharibi na mwingine mashariki akanyonga mgongo kushoto na alafu kulia akiacha milio ya viungo vilivyokaza “Taat…tat…tat” akaenda mihayo mfululizo akimtazama mumewe aliyekuwa kajilaza nyuma yake fii! hajijui hajitambui akatabasamu akasogeza uso wake karibu zaidi na kumbusu mumewe shavuni “Mume wangu, mumeeee amka babaaa kumekucha ivooo” huku akimtikisa bega taratibukumuamsha.
Mume akafumbua macho yakakutana na ya mke “Ooh mke wangu, za asubuhi…” aliachia tabasamu jembamba na
kujinyanyuaa taratibu “Salama mume wangu…kumekuchawajionaje na hali?” mke aliongea kwa pozi akirembua macho
yake makubwa “Sipati maradhi wala uchovu kando yako, nashukuru kwa kunijali…ila leo umeonekana mrembo zaidi
mamaa Rich” Winifrida alijikuta anatabasamu bila kupenda
“Acha bwanaa, hauishi visa kila siku naizidi jana kwa miaka yote hii haya ukaswaki uoshe mwili upate kifungua kinywa
alafu…” Mke alisita akatulia akajikuta anameza fundo la mateuso ukabadilika dhahiri wasiwasi ulimjaa ghafla akanyanyuka na kusimama, Mume uso ukasawazika alielewa kitu akanyanyuka na kumkumbatia kwa nyuma “Haya haya
twende Habib wangu tukaoge…alafu lile sime nimelitoa juu ya kabati nimehamishia chini ya uvungu maana wewe…”
aliongea mume “Ooh sawa afadhari umeliweka karibu” aliongea mke na kufungua mlango wa bafu.

Baada ya dakika kadhaa, Mume alionekana kuwa bize akijiweka sawa kimavazi, kipindi hicho mke akiwa anajipodoakatika meza ya mavazi akijiburudisha na kanyimbo alikokuwa akikaimba nusu nusu bila kumalizia. “Khoo! khooo!” alijikoholesha Mume kitendo kilichomfanya mke kugeuka kumtazama kwa macho ya kulikoni “Mke wangu hebu nambie
nivae tai gani hii au hii itakayonitoa bomba?” aliongea huku akijiwekea aina mbili za tai kifuani zamu zamu macho yakiwakwa mkewe pembezoni mwa kabati kubwa la kahawia lenye kioo kikubwa cha kujitazama. Mke akiwa na vazi lake la
kinaijeria (Mama Afrika) macho makini akimkagua mumewekwa makini huku akiendelea kulichanua tabasamu mkononi akiwa kashikilia wanja wa macho “…mi naona uvae hiyo yenye mistari ya brown” aliweka wanja mezani na
kumsogelea karibu akaitoa tai moja wapo mikononi mwa mume na kumfunga shingoni “Sasa unaonekana kuwa ni
mume wa mtu, na sio tu mheshimiwa pekee” Mume akatabasamu na kukitupia macho kioo akijihakiki huku akitingisha kichwa kukubali na kuachia tabasamu pana “Asante hakika nimepata mke makini sana lazima nijivunie” mume aliongea na kutabasamu akiitazama taswira yake
katika kioo.

Baada ya muda mchache.
“Fatuuuu…fatumaaa…” “Abee dada Wini naja” sauti ilisikika tokea jikoni, punde Fatuma akawa mbele ya meza ya chakula
“Shikamoo dada Wini…shikamoo kaka Rich” alisalimu “Marahaba” kwa pamoja waliitika, “Vipi leo haunywi chai
nasi?” aliuliza Wini “Hapana dada endeleeni nitakunywa tu kuna kazi ndogo naimalizia jikoni” akatabasamu tena, “Ooh
sawa sisi tunatoka tutarudi baadae pika chakula kiasi unajua hivi sasa hatupo wengi kama zamani na uhakikishe hakuna mtu tofauti anaeingia nyumbani” “Naelewa dada” alijibu Fatuma, “…alafu lile Baibui lako leo tukipata muda nitaenda
kukuchukulia” “Sawa dada asante” Fatuma alitika kwa furaha huku akikutanisha viganja vya mikono yake kushukuru kisha
akaondoka “Mume wangu unajua siamini kama kweli umekubaliana nami kuacha mambo ya siasa siamini kabisa”
aliongea mke huku akikoroga sukari kwenye kikombe “Yaahwacha niwe huru tu mke wangu niwaachie wengine
waendelee tu.” Aliongea mume huku akikusanya mikono kifuani “Ni kweli japo wananchi wanakuhitaji sana lakini
hapana sitaki kukupoteza mume wangu hasa katika kipindi hiki cha upweke na haya mambo ya Uchaguzi” aliongea
Winifrida akikisogeza kikombe karibu na mumewe “Ni kweliwacha iwe hivyo nitabaki katika biashara tu pekee kama
nilivyoongea na waandishi wa habari jana katika ofisi kuu” Mume aliongea tayari kikombe kikisogelea mdomo. “Vizuri…umepunguza walinzi na wafanyakazi hapa nyumbani na hujanambia kinachofata” aliongea mke “Ooh my God…pole,
nimeghadhibika tu mke wangu ni hivi kuna kijana atakuja nafikiri ni leo jioni atakuwa mlinzi na msimamizi wa mambo yote ya usalama juu yetu ni mtu makini” aliongea Mume na kurudisha kikombe mezani na kuanza kudokoa vitafunwa sahanini.
Baada ya muda kidogo wakawa wameshamaliza kifungua kinywa, tayari kwa safari huku wakienda
wamekumbatiana hadi katika sehemu kubwa iliyokusanya magari sita ya kifahari.

Winifrida ni msichana mwenye uzuri wa kipekee sana, sura yake ndefu kama mtusi, umbile lake la kama samaki nguva
urefu wa haja haukuchosha mboni za macho kumtazama msichana huyu wa Kisambaa. Winifrida ana kila sababu ya
yeye kuitwa mrembo ngozi yake nyeusi ya mng’aro isiyozoea vipodozi ilibaki kusifiwa na marafiki zake pamoja na watu
waliopata bahati ya kuonana nae japo mara moja walienda wakinong’ona kumjadili. Marafiki wa karibu walibaki
kumuuliza kila uchwao kuhusu siri ya urembo wake walau awatajie mkorogo wajaribu kunusuru ngozi zao, majibu
waliyopewa yaliwaacha midomo wazi mafuta ya mgando haya haya ya mia mbili ndio mafuta ayatumiayo kila siku “Mmmh
huu sasa uongo” walijisemea katika makundi. Watu wengi walibaki kumchukulia kuwa ni mchoyo wa maendeleo ya afya za watu asiye penda wenzake wawe warembo kama yeye
lakini hayakuwa sawa na wanao kumjua undani wake ambao walibaki kusema amependelewa sana na mwenyezi Mungu
maana hakuwa muongo wala tabia ya uchoyo bali ngozi yake tu ilikuwa na shukrani haikuwa na hila za uchaguzi wa
mafuta.

Mandal Hil Hospital, Kinondoni -Dar es Saalam.
“Mke wangu tumeshafika” Mume alimshika bega mkewe baada ya kuegesha gari sehemu ya maegesho, Winifrida alizukwa na mshituko na macho yakamtoka mfano wa mtu ashitushwapo toka usingizini. Baada ya kutuliza akili na
kutafakari kutokana na kuwehuka akaonekana kama mtu mwenye kujishauri kushuka na kutoshuka mwishowe
akafungua mkanda wa kiti cha gari na kuteremka kichovu chovu huku macho yakiwa ardhini kwa wasiwasi. Taratibu zote za awali zilifanyika na mwishowe wakabaki katika viti kwa ajili ya kuonana na Daktari, si mume wala mke aliyethubutu kumuongelesha mwenzie, kila mmoja alikuwa na la kwakwe analoliwaza. Foleni ilipungua kuwakaribiamwishowe ikawadia zamu yao ya kuingia. “Ohooo
mheshimiwa Richard habari zenu…karibuni sana” alisimama daktari akiwapatia mkono kwa zamu alafu akakaa
“Nzuri…asante dokta” Richard aliitika. Winifrida aibu machoni iliyochanganyika na wasiwasi iliendelea kumtawala mikono
ikiwa imekusanywa kwa mbele mgongo kaupinda akitazama miguu ya meza iliyopo mbele yake. Daktari aliiweka miwani yake vizuri machoni na kupokea karatasi alizopatiwa na Richard. Takribani dakika mbili zilipita huku pakiwa kimya
pasina mazungumzo yoyote. Baada ya daktari kupiga mafundo kadhaa ya maji toka katika chupa ya maji ya Kilimanjaro iliyokuwa upande wake wa kulia juu ya meza akawatazama kwa zamu “Ndio mheshimiwa, naomba nipate ushirikiano wenu, bila kusahau kupatiwa majibu sahihi ya maswali nitakayo wauliza ili tuweze kupata suluhu nzuri tena kwa muda mfupi” wanandoa wakatazamana “Hakuna shida
dokta endelea tu” Richard alijibu kwa kujiamini “Asante” dokta alitabasamu na kuanza mahojiano kwa zamuu huku
akiandika andika vitu muhimu.

Ndani ya dakika kumi daktari alikwisha maliza mahojiano kwa wote “Vizuri asante kwa ushirikiano mzuri…naomba
muelekee chumba namba tisa alafu kuna maelekezo mtayapata huko kisha mtarudi tena kwangu” aliongea dokta
“Sawa” Richard alipokea karatasi toka kwa daktari wakanyanyuka na kutoka.
Dakika zilikata na masaa takribani mawili yaliyoyoma na wao bado waliendelea kutulia kwenye viti kama watu wengine
wakitazama kwa kuibiana hofu ikiwatafuna ububu ukiwawaandama. Hatimaye muuguzi akiwa na makaratasi
alionekana kusogea akasimama na kuanza kuita majina kwa zamu huku akirudia kwa wale ambao hawakusikia, waliosikia majina yao walinyanyuka na kuchukua majibu na kuweka foleni ya kwenda kwa daktari kwa mara nyingine “...Winifrida Gorge…Richard Edward…” Richard chapu akanyanyuka na kuzichukua karatasi zote na kwenda kuketi katika foleni.

Wakati huu hali ilizidi kuwa mbaya maana hata mheshimiwaRichard ujasiri wake ulianza kuvuja maana kwenye kiti
hapakukalika kabisa palikuwa pamoto Winifrida alionekana kubadili mikao kila baada ya dakika kadhaa huku mumewe
akiwa ni mtu wa simama kaa simama kaa na safari za chooni zisizokwisha nenda rudi nenda rudi hadi ilipofika zamu yao
wakaingia kwa daktari na kukaa tena baada ya kumpatia makaratasi ya majibu.

Daktari aliendelea kusoma kwa makini kila kipengere, akamaliza. Daktari akavua miwani yake na kuiweka mezani,
“Ndio, vipimo vimeenda vizuri kwenu nyote na kwa msaada wa historia zenu fupi za maradhi na mahusiano, kutokana na
kupata kuchukua vipimo vya mkojo kwako bwana Richard ili kutambua kama una maradhi ya kaswende japo historia
inaonesha hukuwahi kuugua,kitaratibu tumeamua kujiridhisha kwa hilo, tumechukua vipimo vya damu
kutazama vichocheo vyako na uhai wake kwa kweli umeonekana upo salama na hauna shida yoyote ile” alimaliza
kuongea Daktari na kumeza mate na kuacha furaha ikichepuka na kutawala usoni mwa bwana Richard lakini
alipomtazama mkewe alijikuta anapoteza furaha yake maana sura ya Winifrida haikuwa na hata lepe la furaha zaidi ya
wasiwasi hivyo ikambidi atulie. “Ndio…” Daktari alivunja ukimya na kuendelea “…upande wako mama pia tumechukua
vipimo vya mkojo, na tumetazama muda wa kupevusha mayai kitaalamu confirmation of ovulation, kipimo cha damu kuhakiki kama una kisukari kuangalia shinikizo la damu na
joto la mwili, hormone level…” Daktari akaiweka vizuri miwani yake kisha akaendelea “…nah tumepima post coital
test ili kujua uwezo wa kukaa kwa mbegu za kiume kitaalamu tunaita examination of sperm survival in cervical mucus na
kutazama kama sperm zina safiri vizuri into female reproductive system baada ya kusema mlikutana tena hivi karibuni, tukapima pia utra sound kwa ajili ya kuangalia upana wa ukuta wa uterus kama unaruhusu mimba kujishikiza na mwisho tumefanikiwa kupima HSG kuangalia kama mirija ipo sahihi imeziba au laah! na je imeziba kwanini na imeathirika kwa kiwango gani…” daktari aliivua miwani na kuiweka katika meza huku akiwa bado kashikilia karatasi la
Winifrida kisha akaendelea “Majibu kidogo yameenda tofauti na historia yako mama” Winifrida moyo ukamlipuka Puuh!
daktari alimtazama Winifrida, Winfrida akajikuta akifumba macho kwa nguvu huku moyo ukimzidi mapigo akaanza
kulegea huku mikono ikishika tumbo lake la mshtuko.

Itaendeleaaaa.....

Mijadara inaruhusiwaView attachment 1733928
Ndugi Kama simulizi haifai tuache kuituma maana mtunzi haoni mjadala wowote. Hata comments ya bahati mbaya
 
Daktari atapindisha majibi na atasema mwenye matatizo ni Mwanamke wakati ukweli Mh. Richard ndio mwenye tatizo... Ndoa itaanza kuwa chungu kwa WINI, lakini kwa Mbele Winifrida atashika Mimba... utabiri wangu
 
Hahahaaa nimefurahi haya ngoja tuone kalamu ya Mwandishi Akida inasemaje.

Ila feedback Kama hizi zinatia moyo wa kutuma riwaya.
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)
MTUNZI: Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 1 (C): JINAMIZI LA SIKITIKO.

Mandal Hil Hospital, Kinondoni -Dar es Saalam

Ilipoishia

... daktari aliivua miwani na
kuiweka katika meza huku akiwa bado kashikilia karatasi la Winifrida kisha akaendelea “Majibu kidogo yameenda tofauti na historia yako mama” Winifrida moyo ukamlipuka Puuh!daktari alimtazama Winifrida, Winfrida akajikuta akifumba macho kwa nguvu huku moyo ukimzidi mapigo akaanzakulegea huku mikono ikishika tumbo lake la mshtuko...

Tuendeleeee....

Mheshimiwa Richard akamtupia macho mkewe akionekana kutokuelewa sentensi ya daktari, daktari akauma midomo
yake na kuiachia kwa pamoja, “Mama kizazi kinaonekana kimeathirika sana, na sababu kuu ya uathirikaji huu ni
utolewaji wa mimba kadhaa katika maisha yako hii ni mbaya sana” Winifrida alichukua kitambaa chake kidogo katika
mkoba wake na kujiwekea usoni akilia taratibu. Richard macho yakamtoka asijue la kufanya mapigo ya moyo yakaanza kubadili kasi yake ya kawaida “…na kitu kingine ni kuwa kizazi chako kwa sasa kimelegea, hizo ndio kesi mbili ambazo zimepelekea kutokushika mimba kwa muda wote huo mlio ishi pamoja” aliongea daktari. Richard akashika kichwa
kana kwamba amefiwa na mtu muhimu katika maisha yake, hasira zikampanda maradufu macho yakawa mekundu huku
kajiinamia hakujua afanye nini, ‘Mke wangu kwanini hukuniambia siri hii ya kutoa mimba jamani fedheha gani hii’
Richard alijiwazia, ‘Mume wangu nisamehe sikujua kama itafikia hatua hii mimi najuta bora ningekwambia mapema…lakini ningekwambia usingenipenda nani angenithamini, nani angenisomesha mimi, nani Richard wangu?' walikuwa wakiongea kupitia nafsi zao bila kutambua.

Winifrida alihisi kizunguzungu kwa taarifa hiyo mwili ulishindwa kujizuia kichwa kikiendelea kumuuma na kuwa kizito moyo wote ulichakaa kwa huzuni ya moyo na wasiwasi, daktari akaendelea “Lakini nitamuandikia dawa ambazo atazitumia kwa kipindi huku mkihudhuria maonano na daktari husika mara kwa mara kujua maendeleo yake huendasiku za usoni akapata ujauzito nani anajua, maana Mungu ni mkubwa sana na tuzidi kumuomba maana ni mwingi wa huruma na mwingi wa msamaha” aliongea kwa masikitiko.

Winifrida alitamani ayeyuke atokezee ulimwengu mwingine kabisa kwa uchungu aliokuwa nao na aibu maana aliona
amemvua nguo mumewe mbele ya ulimwengu. ‘Fadhira zote ulizonifanyia mumewe wangu leo nakulipa madudu hivi
maumivu ya aina hii, kwanini nisife?’ Winifrida alijiongelea nafsini, daktari akaendelea “Lakini nawaomba jambo moja msije mkaleta mfarakano kutokana na tukio hili wengi sana wakishamaliza na kuondoka hapa mapenzi na wanandoa wao yanapotea wengi wanaachana, wanasalitiana na hata wengine kujiua kwa sababu tu hawezi kuzaa…” Winifrida alinyanyua kichwa na kumtazama dokta kwa huzuni, ‘Ulijiuaje dokta kuhusu hisia zangu’ alijiongelea tena Winifrida “…Mkaemkijua watoto ni baraka toka kwa Mola, yeye ndiye humpa anaemtaka na humnyima anaemtaka na kumpa wakati anaotaka yeye mwenyewe, vipimo na madawa vipo ilikurahisisha mambo na uchunguzi ili kuweza kujua jinsi ya kutatua matatizo na kuyajua matatizo kama ilivyotokea, hivyo nawasihi sana nyinyi bado ni vijana tena ni watu maarufu
muende na mkawe mfano” dokta Abdi alimaliza, Richard akanyanyuka na kumpa mkono dokta bila kusema kitu akapokea karatasi alimtazama mkewe sekunde kadhaa kama mtu anae tamani kusema jambo huku akiwa kasimama
“Nyanyuka tuondoke” aliongea Richard huku akiwa wa kwanza kutoka, usoni akiwa na hasira ya waziwazi.

Nelson Mandela Road – Dar es Salam.
Ndani ya gari ya aina ya Mitsubish Lancer Winifrida alikuwa ni mtu wa kulia tu alilia mfano wa mtoto mdogo aliye na njaa
na kiu kikali japo hakutoa sauti lakini kilio chake cha kimya kimya kilileta hisia kuwa amezidiwa uchungu. Kilio chake
kilimpelekea macho kumvimba na kuwa mekundu. Richardyeye alionekana kama mtu asiye jali hali ya mkewe wala
hakujigusa, hakujipa nafasi ya kumtazama wala kumuongelesha mkewe tangu walipo toka hospitali na kuitiagari yake funguo, hakutia neno hata moja katika safari hiyo
yeye alikuwa macho mbele kama tochi huku akijinyusa nyusa tu kila wakati. Sura ya Richard ilionekana kukunjamana kama
karatasi iliyo kosa kazi na kukunjwa au kumfananisha na mtu aliyelamba ndimu au kunusa kitu chenye harufu mbaya.
Winifrida mara moja moja alimtupia macho mumewe kiwiziwizi lakini alichokutana nacho aliuona upweke na kuzidisha uchungu unaochoma ndani kwa ndani usioisha wala kupata nafuu huku tumbo likimsokota haswa.

PURPLE in Hotel, Temeke, Kurasini - Dar es Salam.
Kipindi Winifrida akiwa kaegemeza kichwa kwenye kioo cha mlango wa gari akashtushwa na breki kali sana iliyomfanya mwili kusukumwa mbele “Paaap” ilikuwa ni msaada tu wa mkanda wa usalama laa sivyo chochote kingetokea. Baada ya mshituko akaanza kuangaza kupitia katika kioo cha gari na
kuanza kuzirudisha kumbukumbu vizuri mwisho akaishia kusoma kibao kikubwa kilicho kaa pembeni mwa bustaniupande wa mbele ya gari walilopanda, “PURPLE in Hotel …mmh” alijigunia kwa sauti huku akiwa na wasiwasi na mshangao. Richard mikono ikiwa imeshikilia usukani wa gari
kichwa kakiinamisha akihema hovyohovyo, taratibu akatoa mikono katika usukani akajishika kichwa chake nakujiegemeza katika kiti alichokalia, macho akayafumba, zikapita dakika tano nzima pakiwa kimya ndani ya gari. “Naomba unifate tafadhali” Richard aliuvunja ukimya akaufungua mkanda na kutoka katika gari, Wini yeye hakuwa na lakufanya zaidi ya kufata amri ya mumewe huku maswali yakiendelea kumtawala ‘Purple in Hotel kuna nini? kwaniniisiwe nyumbani, na kwanini’ alijiuliza nafsini, Usilo lijua ni
usiku wa giza.

Richard alisogea hadi katika sehemu ya mapokezi huku akipokea salamu za watu waliomfahamu na wasio mfahamu
mahala hapo, baada ya kufika na kuongea maneno mawili matatu na mhudumu akatoa kiasi cha pesa taslim toka
kwenye waleti na kumpatia Mhudumu aliyekuwa mahala hapo akaegema na kuanza kuandika kitu, Mhudumu na yeye
akaikabili simu na kuiweka sikioni akiongea kitu kisha akarejesha sehemu yake. Richard akiwa mwingi wa mawazo
mkewe akiwa hatua kadhaa nyuma akimuangalia kwa kujiiba akiwa “Habari Mheshimiwa…” ilisikika sauti mgongoni mwa Richard na kumshitua akageuka na kumtazama kijana mtanashati aliyevalia sare za Hoteli hiyo “Ooh salama” alijibu “Mnaweza nifata tafadhari” aliongea tena kijana huyo na kuongoza njia huku akifatwa nyuma na Richard pamoja na
mkewe.

Richard aliendelea kujifuta maji kichwani na taulo huku akiwa anaufunga mlango wa bafu kipindi hicho Winifrida kajikalisha
na kujiinamia kwenye kona ya kitanda akiwa kama alivyo kuwa hakuvua wala kuvaa chochote. Richard akamsogelea
mkewe na kukaa karibu yake kwa huzuni kubwa, akamtazamamkewe kwa kumkagua vizuri kana kwamba ni mtu mwenye kumfananisha akabaki kutingisha kichwa chake kuonesha anakataa hali anayoiona au kuihisi kuwa sikweli “Samahani naomba nikuongeleshe tafadhari” alijikuta akiyatoa maneno hayo toka katika kinywa chake huku akimuangalia mkewe.

Winifrida aliyasikia maneno hayo akaunyanyua uso wake na kumtazama mumewe kwa aibu huku akikwepesha macho yake yasikutane na mumewe. “Hivi ni wewe kweli, niWinifrida wangu kweli wewe? Unajua umenikosea sana mke wangu!” maneno hayo yalipenya na kuingia kwenye masikio moja kwa moja hadi katika sakafu ya moyo wa Winifrida na yakatibua fukuto la uchungu lililokuwa limepoa poa kwa vijidakika kadhaa tangu wafike Hotelini hapo yakaleta mchafuko wa moyo. Winifrida alianza upya kulia yani kiasi cha kumshangaza mumewe ambae ndiye aliyekosewa “Wewe una nini unanikejeli au vipi?” Richard alishindwa kuzuia hasira zake alipaza sauti yake nzito juu na kumtazama kwa mshangao akanyanyuka alipo kaa na kusimama huku kajishika kiuno, Winifrida aliteremka taratibu na kukaa katika sakafu huku akilia kimya kimya akayasimamisha magoti yake huku kichwa kakiinamisha, “Nisamehe mume, Rich naona aibu, naona haya mimi kukuita mume wangu kwa dhambi nilizofanya nyuma ya mgongo wako sikukwambia mimi…” winifrida alijifuta machozi na kujikaza kuongea, “Sikujua kama yatafikia hapa, nikweli nilikuongopea historia ya maisha yangu asilimia hamsini sio ya kweli” Richard alimtupia macho ya hasira mkewe “…ila tangu umenioa miaka minne iliyopita, sijawahi kukudanganya nimekuwa nikiishi ndani ya ukweli na uwazi wa kila jambo kwako hiyo ndio ahadi niliyoiweka katika maisha yangu na wewe ni shahidi ” Winifrida akaangua kilio cha chini chini bila kunyamazishwa na mumewe aliye jisimamia pembeni akiwa kampa mgongo “Nipo tayari kuyakubali maamuzi yako mume wangu na hiyo itakuwa ndio adhabu inayo nifaa…” Richard alishtuka na kugeuka kumtazamaa mkewe kwa mshangao, “Ila kabla hujaamua chochote nataka kukupa ukweli mmoja kuwa sijawahi kumpenda mwanaume yoyote zaidi ninavyokupenda… nashukuru nimeweza kufurahia na kuridhika kwa mara ya kwanza ndani ya ndoa yangu”aliongea Winifrida kwa sauti ya mtetemo machozi yakimwagika macho ya Richard yalionekana kupata wingu la machozi uso sasa ukafunguka toka katika mikunjo kunjo ya ndita kwenye paji la uso, “Nilipata ujauzito mara kadhaa na wote walionipatia walipotea wote na kila mmoja alikuja na uongo wake na mimi nilikuwa muhitaji wa pesa kama ulivyokuta hali ya uchumi kwetu haikuwa shwari mzee wangu alivyokuwa mgonjwa gonjwa ningefanyaje?” aliongea tena Winifrida akiwa kapiga magoti akajifuta kamasi na machozi sasa yamekata na sauti imekauka inatoka kama mtu anae
nong’ona akaendelea “Mimi nilikupenda mwenyewe na nilikuvutia mwenyewe na wala sikuwa na tamaa na pesa zako,
na nilitamani uwe wangu maisha yote, sikupenda ughalimike kwa ajili yangu ila uliamua ukanisaidia, nilikufurahia sana
asante kwa hilo” Richard picha ikamjia jinsi alivyomkuta siku za mahusiano yao machanga alipokuwa anahudhuria siku za mwisho wa wiki katika mji wa Tanga, kumbukumbu ilimchosha akatingisha kichwa kuivuruga maana ilimuumiza
taratibu akajikuta anarudi kujikalisha katika kitanda kama zigo lililotupwa kwa kususwa “Puuuh”. Wini akaendelea
“Nilitamani nikuambie ukweli lakini uchafu wangu ungeujua ingekuwaje isingekuwa rahisi kunioa ungenitelekeza tu kama
wale wengine, niliogopa sana kukukosa niliogopa kukwambia niliogopa mimi” Winifrida alijikuta anatingisha kichwa
kusikitika, “Wewe ni mwanaume wa kipekee sana mume wangu, najivunia kuwa nawe, sasa nasubiri hukumu yako na nitaikubali bila kinyongo” Winifrida aliongea nakunyamaza shingo imeinama kama mtu anayesubiri kuchinjwa, Richard
alibaki kuwaza na kuwazua aamue lipi, saa zima na nusu likapita akiwaza tuu. ‘Ni mwanamke uliyenifunza nini maana
ya kupenda na maana ya penzi la dhati sasa mbona umeniumiza kiasi hiki, sijawahi jua uchungu wa penzi kumbe
inauma kiasi hiki?’ alibaki akijiwazia. Ushauri wa dokta kuhusu hali halisi na kukabiliana ilianza kuranda randa katika
kichwa chake ikijirudia rudia ‘Mungu wangu nifanyaje mimi siwezi kumuacha mke wangu siwezi’ Richard alijisemea
moyoni na kunyanyuka haraka haraka na kumkumbatia mkewe kwa masikitiko makubwa sana kiasi cha kumshangaza
sana Winifrida, wote wakaanza kuangua kilio cha huzuni huku wakiwa wamekumbatiana, ama kweli penzi ni kitu kisicho na mfano katika ulimwengu wote. Mabembelezano yalienda na walikuja tahamaki saa tatu usiku, wakaamua kuondoka zao.

Msasani, Kinondoni -Dar es Saalam
Mke na mume wakiwa kitandani wamejilaza kila mmojaakiwa na lake aliwazalo mke akajipindua na kuanza kuongea“Mume wangu unajua nina hofu na uoga sana juu ya dada zako, mama yako, jamaa zako na hata marafiki zako
watanichukuliaje maana dunia hii haina siri” aliongea Winifrida akageuka na kumtazama vizuri mumewe, “Mke
wangu sisi ndio tulio oana sawa? halafu kama Mungu ameamua tusipate hatutapata na kama amepanga tupate
tutapata, tena sasa huwenda tukapata mtoto mzuri mwenye hekima na busara hapo baadae” Richard aliongea na kuachia tabasamu jembamba na kukaza macho kuashiria kumaanishamaneno yake. Winifrida akatabasamu na kujivuta zaidi kwa mumewe, kwa pamoja wakajiweka sawa kuukaribisha usingizi.

Kijiji cha Mtamba, Matombo - Morogoro.
Majira ya saa nne asubuhi hivi, nje ya nyumba ya kisasa kwenye baraza walionekana wanawake watatu, wawili
walikuwa bize wakitembea kwa kupishana huyu akienda na huyu akirudi mikono kiunoni kichwa sakafuni mara wamekaa
mara wamesimama, walionekana wazi vichwa vyao vimebeba mzigo wa hasira kutokana na jazba walizokuwa nazo nyusoni, Lakini watatu wao mama wa makamo ya miaka hamsini mpaka kwenye siti yeye alikuwa kajiegemeza ukutani katika kibaraza hicho, kiganja chake cha mkono wa kuume alikigandisha shavuni mwake mguu mmoja kaukunja na
mwingine kunyooshwa. Mama huyo mtu mzima alibaki kujisikitikia tu aliwatazama wanawake hao waliokuwa mbele
yake kwa wakati huo walikoma kutembea wakabaki wamesimama na kuanza kunesa nesa kama wasoma ngonjera
waliokuwa wakitambiana kwa zamu.“…Mama sisi kesho piga ua lazima twende Dar”, ukimya wa muda mfupi ulivunjwa na
mmoja wao, mama wa watu alitoa kiganja cha mkono shavuni na kunyanyua uso wake kuwatazama kwa zamu wanawake
hao walio mbele yake “Sawa ila nawaomba sana wanangu msiende bila kumtaarifu kaka yenu” mama huyo mtu mzima
alikunjua mguu wake na kuunyoosha kwa mbele, “Nani?..sisi?...aaah mama hilo sahau” mwingine alidakia, alikuwa pande la mwanamke wa maji ya kunde, alionekana kufanana sana na mama huyo, maana alimchukua kila kitu.

“Hakuna cha taarifa wala nini sisi tumeshaaga waume zetu na wewe tumekuletea taarifa tu na sio kutaka ushauri au ruhusa, mwanamke mbaya sana yule bila shaka amempa limbwata
kaka yetu” alimaliza na kugeuza shingo kutazama pembeni mikono kiunoni huku akichezesha mguu kwa hasira. “Sawa
wanangu ila tu nawaomba msiende kumfanyia fujo wifi yenu sawa Ester?” Mama wa watu akageuka kumtazama mwanawe mkubwa aliyekuwa kachukizwa mno amejitazamia pembeni “Mama sikiliza, mimi na dada Ester tumekuletea wajukuu wangapi mpaka sasa je vipi mwanao wa kiume? Je! unajiskia raha sio mtu mheshimiwa eeh anasifa kubwa nchini kazi kumwaga hela za misaada tu kwa watu nani atazirithi mali zake? Sisi tumeshaamua ukitaka ni hivyo usipotaka ni hivyokwaheri” aliongea Ester kama cherehani akashika njia huku akiifunga vizuri kanga yake kiunoni, Eva nae hakukaa akafata nyuma na kumuacha mama huyo akiwasindikiza kwa machoya mshangao wakiingia ndani. Mama wa watu mawazo yakamchukua na kumkumbuka mumewe mzee Edward Kobero, kumbukumbu hizo hazikumuacha macho makavu mama huyo akajikuta akijifuta michozi na utuuzima wake kweli “Ukimuona mtu mzima analia ujue kuna jambo” Mama huyo akiwa bado jamvini alinyanyua kichwa kutazama nyumba anayoishi, ilikuwa nyumba ya kipekee sana na nzuri kuliko nyumba zote kijijini hapo, “Eeh Mungu msaidie mkwewangu dhidi ya shambulio la wanangu” alijisemea.

Ni kweli kilikuwa ni kitu cha kuhuzunisha sana kwa mama huyo wa watoto watatu, masikini alibahatika kupata mtoto
mmoja tu wa kiume kama wa dawa vile ambaye alimsomesha kwa pesa za kuungaunga tena kipindi kile alipo kuwa analimamboga mboga na matunda na kwenda kuuza Morogoro mjini,
alimkumbuka sana marehemu mumewe. Mumewe mzee Edward Kobero alikuwa anajishughulisha na kazi ya ulinzi
alishikwa na umauti baada ya kukosa matibabu stahiki ya jeraha la mguu lililotokana na shambulio la majambazi katika harakati za kujaribi kulinda mali ya bwana Mohammed Seifalijikuta akipigwa risasi ya paja, kwa uhaba wa hospitali na
pesa za kutosha kwa kipindi kile na kesi iliyomkabili toka kwa muajiri wake kwa kuhusishwa na wizi huo ikampelekea
kupatwa na umauti akiwa chumbani kwake.

Msasani, Kinondoni -Dar es Saalam.
Sauti za magari na milio ya ndege wakiimba nyimbo za kushukuru kuingia kwa siku mpya zilisikika kwa mbali toka
katika nyumba ya kipekee mfano wa kasri iliyokuwa ikitajwamiongoni mwa nyumba nzuri kuwahi kutokea nchini, kila apitaye aliishia kuitupia macho ya matamanio na kuishia na ndoto za alinacha. Wapendanao hao wakiwa sebureni pahala pa meza ya chakula Winifrida alilichukua koti la suti lililoegemezwa kwenye kiti kimoja wapo na kumvalisha mumewe ambaye alikuwa kasimama huku mdomo ukicheza cheza kumalizia chakula “Mke wangu basi usisahau kunywa dawa tafadhali sawa” Richard aliongea huku akiendelea kupitisha mkono huu na mkono ule katika mikono ya koti la suti alilokuwa anavalishwa na mkewe “ Usihofu mume wangu nitakunywa” Winifrida aliongea kwa tabasamu pana huku akiendelea kumuweka kola sawa mumewe, “...alafu kama kawaida yako umeacha chai kwenye kikombe” winifrida aliukunja mdomo kwa juu huku macho yakiwa katika kikombe katika meza ya chakula iliyokuwa karibu nao na kusitisha zoezi. “Mmh haya nipatie” aliongea Richard huku
akitabasamu na kukichukua kikombe mkononi mwa mkewe fundo moja tu akamliza chai yote akaitupia macho saa ya mkononi mwake “Saa mbili na robo sasa” aliongea kishaakamsogelea mkewe na kumpiga busu shavuni. “Unajua
siamini kama leo tumeikosa ibada hivi hivi mume wangu”“Wala usihofu sina budi kuufanya huu mkutano ni muhimu
sana… tena leo niandalie ugari wa dona nimeumisi sana,”Richard aliongea huku akiwa tayari ameshaufikia mlango
mkubwa wa kutoka nje. “Haya sawa take care Honey” “You too”. Winifrida akasogea hadi katika mlango akatoa kichwa
kumuangalia mumewe akiondoka, alibaki akitabasamu tuhuku paji la uso likiegemea mlango.

Baada ya Masaa kazaa.
“Habari za Ulimwenguni toka katika izaya ya kiswahili ya DeutscheWellemjini Boni mimi ni Ukhty Zukheirah Abdallah, Katika tarifa ya habari mchana huu, marekani yasitisha mashirikiano yake na Urusi juu ya Syria, wakati Uturuki ikiongeza muda wa hali ya hatari hadi mwakani na ripoti
ya Amnesty International ikifichuwa kwamba ni mataifa kumi tu duniani
yenye uchumi usiozidi asilimia mbili nukta tano...” sauti hiyo ilitokea katika redio ndogo iliyopakatwa kwenye mapaja na
bwana aliyevalia sare macho yakiwa
yameikodoloea redio masikio yamemsimama yakitega kila neno toka redioni akiwa juu ya kiti cha plastiki. Mara
akashtushwa na sauti ya geti ikigongwa kwa nje bira mpangilio kiasi cha kumfanya kukunja sura na kulitupia jicho la hasira geti lakini uso ukiwa hauna uhakika maana si kwa kugongwa huko, akatulia na kutegesha masikio shingo kaipindisha mkono ukiwa katika redio akipunguza sauti kuhakikisha kelele hiyo ya geti anaisikia vizuri, alipotambua kuwa ni kweli kuna mtu anagonga geti sura ikazidi kukunjamana. Akatazama katika kifaa maalumu kwenye ukuta kikionesha wanawake wawili na mabegi yao, alitulia
akabonyeza kitufe pembeni yake “Nyinyi kina nani na mna shida gani? Kwani hamja ona kitufe cha kengere mnagonga
hodi kama kuna ugomvi” aliongea na kusikilizia “Dada zake mheshimiwa Richard tufungulie au sio hapa” ilisikika sauti ikitokea katika kifaa hicho ukutani. “Subirini kidogo…" aliongea bwana huyo na kugeuka tayari kuondoka “Jumaa
kuna nini hapoo” Wini akiwa anarejesha mlango na kusimama aliongea kwa sauti “Kuna wanawake wawili wanasema ni
dada zake kaka Rich…” Wini akiwa amesimama moyo ukamlipuka kiasi cha kupeleka mkono kifuani akijizuia “…Je!
Niwaruhusu?” aliongea Jumaa ‘Mungu wangu wamefata nini tena?’ Wini alijiongelea nafsini, kabla hajapata jibu la swali lake Jumaa akaongea “…niwaruhusu waingie?” Wini akameza fundo la mate la uchungu lililopita kwa tabu kooni, mkono
ukiwa bado katika kitasa “Waruhusu” aliongea na kurudi ndani kinyonge. Juma akabofya sehemu na geti likajifungua
kwa umeme mambo ya teknolojia, wadada wawili hao wakaingia, “Hivi wewee kisa cha kutuweka masaa muda wote
nini hasa” Eva aliongea kwa ukali huku macho yakiwa kwa Jumaa hii ni baada ya kupiga hatua kazaa ndani ya uzio wa
ukuta wa matofali ulio nakshiwa vizuri na kupendeza.“Samahani mnisamehe siwatambui mimi ni mpya hapa
nilikuwa nauliza kwanza” Jumaa alijitetea “Alafu unaonekana mshamba mshamba imekuwaje kaka akakuweka mtu kama
wewe hapa mtu simple simple tu khaa!” Eva aliongea akimtazama kwa dharau, Jumaa kwa makini alibaki kumtazama wazi akionekana kuchukizwa machoni “Wote wapo?” Eva aliuliza “Aliyekuwepo ni dada Winifrida kaka Richard yeye alitoka tangu asubuhi” Jumaa alijibu akificha
macho yake asibainishe hasira zilizomuandama wakati huo,
“Shoga twende zetu” Eva alimgusa bega ndugu yake na kuongoza njia kuufuata mlango. “Ooh mawifi hao karibuni
jamani” Winifrida aliiweka rimoti katika meza akanyanyuka kwa furaha kuwasogelea wageni wake. Ester akamuangalia Winifrida kwa jicho la dharau huku kasimama, akampandisha
akamshusha “Fsyuuuuu…naona unajitanua tu kwa raha zako” Ester aliongea kwa majivuno. Winifrida alihisi mwili kupatwa
na baridi alihisi shari ikimnyemelea lakini akajizuia “Eeh bibi si unajua tena…” Wini alichombeza akinyoosha mkono
kulichukua begi la Ester macho yakiwa kayainamisha chini.‘Eeeh Mungu nipe usalama’ Winifrida alijisemea katika nafsi
yake “Fatuma njoo uchukue begi lingine unifate tafadhari”aliongea Wini huku akianza kulivuta, wakati huo Fatuma
akimfata alipo. Kisha akarudi, “Karibuni wifi zangu jisikieni mpo nyumbani” Wini alisogea pembeni na kukaa “Hivi we
mwanamke kwa kaka yetu ulichokikosa ni nini” Wini alishtushwa “Wifi Ester una maana gani sijaelewa” “Huelewi?
huelewi nini we mwanamke mchawi sana wewe” Ester safari hii aliamua kusimama kwa ghadhabu jicho limemtoka kwa
hasira kidole kakinyoosha kwa Wini, Wini alibaki kabung’aa tu kama mtu asiejielewa. “Sikiliza wewe kinyago cha mpapule tumekuvumilia tumechoka sawa tunataka utuambie kwanini umemroga kaka yetu, unachotaka hasa nini?” Eva nae alijinasua kwenye sofa na kumsogelea Wini akampiga singi
takatifu lililomfanya Wini kuinamia mto wa Sofa uliokuwa pembeni yake. Wini bado alikuwa hajang’amua kitu aliwaza
na kuwazua kipindi akiwa bado kajiegemeza kwenye mtokwenye sofa machozi yakimlengalenga kinachomaanishwa na wifi zake hakukipatia jawabu.

Fatuma alionekana kujiminya katika ukuta akishuhudia kila kitu juu ya mawifi
wakimshambulia Wini, alionekana kujiskia vibaya sana alitamani kwenda kumsaidia kulipiza mashambulizi lakini moyo ulimzuia “Eva mbona unazunguka zunguka tu…” Ester alimsogelea Wini karibu na kumuweka kati kama mwanamke
anae sutwa “…Sikiliza wewe mwanamke sisi tumechoka tunahitaji kuitwa mashangazi haiwezekani miaka kibao hii
umejikalia kama jiwe tu hujiskii vibaya mwanamke wewe” Winifrida alijivuta vuta kichovu na kukaa kitako, alijiinamia,
alijishika kichwa akiwaza maana safari hii tayari alishaelewa maana ya ujio huo nyumbani kwake. Uchungu uliendelea
kumjaa aliona wazi mwisho wake tayari ushafika hana msaada dunia sasa imeshaanza kumtazama alihisi kuchekwa
na kuzomewa na watu wengi, “Mwanamke jeuri huyu halafu hana haya huoni aibu? Hivi hujui Kama thamani ya mwanamke ni mtoto unajua nina hasira sana na wewe na tumekuja kistaarabu tunataka utulete watoto uliowafichamchawi wewe sisi kwetu tuna uzazi ukae na ulijue hilo”. Eva aliongea kwa uchungu sana karibia kutoa machozi, “Hebu fikiria ingekuwa wewe ndio dada yake ungejiskiaje eeh…” Ester aliongea nakumtia singi wifi yake lililopindisha shingo ya Winifrida “Tunachokiamini ni kuwa wewe ni mchawi habari zako tunazo kwa hiyari yako chagua kuondoka au laa sivyo…” Winifrida alinyanyuka kabla Eva hajamalizia kuongea akatoka mkuku mkuku akaziparamia ngazi kupanda juu kwa kasi kiasi cha kuwashangaza wifi zake wakabaki kutazamana.
“Na safari hii utaondoka tu na bado alaaaa” Eva alimrushia maneno na kweli yalimfikia Wini kabla hajaingia chumbani
kwake yalishadakwa na masikio yalikuwa kama mkuki maana yalimuingia moyoni akahisi kuna kitu kimekaa katika koo lake
kinamzuia kuhema aliufungua mlango na kuingia.

Masikini dada wa watu nguvu zilionekana kumuishia alijiona ni mtu aliyepoteza kitu cha thamani katika maisha yake na kutokana na kupoteza kwake basi nae thamani yake imeshuka daraja,hana thamani alijitupa kitandani na kuanza kumwaga kilio, kitanda hakikufaa alijinyanyua na kusogelea kioo cha kabati
huku akiendelea kulia na kujitazama alivyo umbwa “Masikini mimi nimeshajiaribu mimi ooh Mungu wangu” alijisemea kwa
uchungu mara likamjia wazo, alionekana kuanza kuhema hovyo hovyo alikurupuka na kukimbilia katika droo za kabati alitoa kila kitu na kutupa chini hakuambulia kitu akarudi katika nguo alizitoa na kuzikung’uta ili apate kitu ambacho
kinaweza kusaidia kutoa uhai wake. Baada ya kuambulia mikono mitupu akagutuka akasogelea kwenye dressing table
akachukua kisturi na kusogelea kabati akapanda juu yake na kuanza kupapasa papasa kwa makini akatoa tabasamu la
uchungu baada ya kukishika kitu alichokitarajia akashuka huku mkononi akiwa ameshikilia bastola akaiweka kitandani na kusogelea droo ya dressing table akachukua peni na Notebook alishusha pumzi nzito na kuanza kufikiria kidogo kisha akajituliza kitandani na kuanza kuandika huku machozi yakimtirika. Baada ya kufika tamati na kuridhika akaamua kuusoma kwa sauti.

Mume wangu Mpendwa,

Sioni sababu ya Mimi kuishi kutokana na sababu ya kutokuzaa najiskia vibaya sana mume wangu lakini sina jinsi, mawifi zangu ninaowapenda nao hawanipendi tena wananisema vibaya, sitaweza kuwa na amani kuishi na hali hii, kwanini nikupe maisha magumu mimi sitaki uishi kwa masononeko wakati ukweli ni kuwa mimi ndiye niliyekudhurumu hivyo basi sifai kuishi. Buriani mume wangu maisha mema.”

Wini alimaliza kuyasoma kwa sauti, ‘Inaniuma mume lakini haina budi najua hata nikiishi nitakuwa ni kama mti usio nafaida hautoi kivuli wala matunda wala kuni wala mbao wala majani na mizizi isio ponya hata ndege wataukimbia’ Wini
alijongelea nafsini kisha akasimama akaichukua bastola kitandani akaiweka karibu na sikio, jasho jembamba likaanza
kumtoka nyuma ya shingo huku akiwa kafumba macho.

Kipindi chote hicho mawifi hawakuwa na walijualo juu ghorofani, sebuleni sauti ya redio ilipandishwa ikawa juu wakawa ni wenye kucheza taarabu na kurusha maneno ya vijembe kwa wifi yao huku wakipongezana, Fatuma akiwa jikoni chakula hakipikiki kwa raha roho ilimuuma alitamani apande ghorofani akamliwaze dada ake lakini hakuweza kufanya hivyo.

Ghorofani Winifrida wazo la kujiua bado lilikuwa limeutawala mwili, akili na nafsi “qataa” huo ndio mlio pekee uliosikika
masikioni akatulia sekunde kadhaa kusikilizia maumivu ya risasi itakayopenya katika kichwa na kuvuruga ubongo,

Je Nini kitajiri?????

Itaendeleaaaa....

Mijadara muhimu

Mijadara muhimuView attachment 1741102
Iko poa sn
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom