The Godfather

Call him godfather or mother the true has been reveal and the ccm party has come to the end, they will soon be a opposition party in this country you will see it. The only one big problem that facing CCM followers, they never accept the true.

Duh! Hii serenge ni ya kiyunani au?
 
mleta uzi umetumwa tuuu ila umechelewa....
kama unamlengaaa reginald mengi umechemsha mkuu
 

Mkapa alimdhibiti vizuri tu huyo Mengi
 

Mpaka hatua hii hatujaelezwa makosa ya Waziri Muhongo ni yepi. Raisi Kikwete alipomuweka kiporo kwa ahadi ya siku mbili baada ya uchunguzi, ilitegemewa angemfukuza kazi ktk muda huo iwapo angethibibitisha makosa. Ukweli kwamba kajiuzuru mwenyewe baada ya kukaa kiporo mwezi mzima ni ushahidi tosha kuwa hana makosa.
Muhongo amewachalenji waandishi wa habari wathibitishe kama kapokea rushwa wamekaa kimya. Mhariri wa Mtanzania anadai eti hakufanya due dilligence ya makabidhiano ya mitambo ya IPTL kana kwamba hiyo mitambo ni mali ya serikali kama ilivyo ya Kidatu na Mtela! Nadhani dhambi kubwa za Muhongo ni kusitisha malipo ya mabilioni kwa Mkono na kuingilia vitalu vya Mengi na kuwakatalia mabepali kweka sera ya gesi walivyotaka wako. Ni muhanga wa Kangaroo Court ya PAC na upotoshaji wa makusudi vyombo vya habari.
 

Asante mkuu kwa kunipa elimu mujarabu ya umeme na gharama zake za uendeshaji,Now you have successfully changed my mind over Muhongo and his power development projects.
 
----,

kwa iyo ulitaka wezi watetewe, kisa tu ni watendaji wazuri??? poor mind



Sio kwamba ni watendaji wazuri bali ni waongo.
Muhongo ni muongo sana na anawadanganya watanzania kwa sera ambazo hazitekelezeki.
Watu ambao hawajawahi kifanya biashara wanamwamini sana muhongo.

Lakini kwa mfanyabiashara kwa mazingira ya CCM lazima alalamike.

Iko rushwa kubwa sana kwenye suala la wawekezaji toka nje.
Wa ndani wanaitwa madalali lakini anasahau kuwa hata hayo makampuni makubwa ni madalali wanapoona fursa za kuwekeza kwenye nchi maskini.
Na Muhongo anafikiri ni rahisi kufanya biashara au kuwa dalali nje ya ofisi na mgongo wa serikali basi ajaribu kujitegemea kwa kuwekeza kwa lengo la kunufaika yeye na familia yake kama anavyodanganya umma .

Muhongo anadanganya watu kuwa yeye ndio ameleta umeme vijijini.
Hivi Tanesco ilianzishwa na Muhongo?.Hivi REA imeanzishwa na Muhongo?
Huu mpango uko Muda mrefu wa umeme vijijini.Tangu utawala wa Nyerere. Bahati nzuri mpango wa REA ukaongeza nguvu.
Leo Muhongo anaongopea watu kuwa amepunguza bei ya umeme vijijini. Wapambe wake nao wanamshabikia ili bosi wao asije akakosa ajira huko nje walikomtuma .


Na pia huyu mleta mada hana jipya kwani Mhongo na uprofesa wake inabidi sasa awe kama gaidi au ajiunge na makampuni ya kitapeli mana haaminiki tena kwenye taasisi zenye usafi na uadilifu za kimataifa.Labda aendelee kutumika kama dalali na kibaraka wa wanyonyaji wa wakizungu.Na ISIS wakimgundua watakitaka kile kichwa chake kilichojaa utumwa wa kizungu.
 
Ndiyo maana nimesema ningekuwa na uwezo, sasa sina uwezo huo, nchi haiwezi kuburuzwa na wapuuzi wachache kama MENGI. yeye mwenyewe katajirika kwa kukwepa kodi.

Yaani hapa ni kama vile unasema CCM na serikali yake wamewekwa mfukoni na Bw. Mengi? Kwamba, akimwambia Rais mfukuze Prof. Muhongo, basi Rais anatekeleza. Jamani, tumefikia hatua ya kukidharau chama na Rais wetu kiasi hiki? Kwamba Rais na CCM wanatekeleza maelekezo ya Bw. Mengi? Siamini. Tunaweza kukosoa serikali lakini hili la kusema Mengi ndiye anatoa maelekezo ya namna ya kuendesha nchi ni dharau kubwa kwa serikali na chama tawala. Kipindi cha nyuma kuna watu (Mwakilishi wa Pope hapa nchini?) waliwahi kusema serikali ya Nyerere imewekwa mfukoni wa mafisadi, cha moto walikiona. Sasa leo thatha, ambaye ni kada maarufu wa CCM, anafikia hatua ya kumdharau Rais na CCM kwa kiwango cha hali ya juu na hakuna hatua zinazochukuliwa. Kweli waliosema Rais ni dhaifu hawakukosea.

Kwamba serikali inafahamu fika kuwa Mengi anakwepa kodi na haichukui hatua (thatha wa JF anafahamu hivyo na ushahidi anao)? Jamani, kuna serikali dhaifu zaidi ya hii ya CCM kweli? Serikali inashindwa kukusanya kodi. Serikali hiyo ya nini? Si bora tubaki bila serikali na kila mtu ajifanyie lake? Wakati wa mabadiliko ni sasa: Kataa Katiba inayopendekezwa, Kataa CCM, Boresha Maisha!
 
Mengi na Escrow wapi na wapi?
Muhongo kaingizwa Kingi na JK nae kaingia kichwakichwa kwa ujinga wake, kang'ang'ania kiti mpaka kaona aibu mwenyewe akatoka.

Suala la Godfather CCM ndiyo wanalitaka wenyewe, CCM ina Godfathers kila mkoa ktk nchi hii, uchaguzi unapokaribia barua za mchango wa fedha zinaletwa ofisi mbalimbali za wafanyabiashara binafsi na wengine wanakuwa wamepewa kiwango cha kuchanga.
Kwa maani hiyo CCM inajilazimisha kuingia mfukoni kwa mfanyabiashara at the end mfanyabiashara lazima arudishe fedha zake tena kwa kukupangia wewe serikali(mwenyekiti wa chama ndiyo mfanyakazi mkuu wa serikali).
So CCM itajikuta haiwezi kujiendesha yenyewe ila itaendeshwa na Godfathers the way wanavyotaka.
GODFATHERZZZ WA CCM:

Rugemalira
Harbinder Sing
Mpaka sasa wako safi hamna anayewabugudhi, hata Rais(Nwenyekiti wa Chama) alisema hela zile za Escrow ni za hawa watu not za umma.
Habari hiyo ikiripotiwa na ITV TZ mnaanza maneno kwamba Mengi yuko against serikali ya chama, ikiripotiwa na TBC mnaufyata kuliko Muongo.
Hivi watu wa chama chetu cha mapinduzi mna akili timamu kweeeeli.
 
Kigezo cha ajira ni elimu na uaminifu
Ukikosa uaminifu hupati kazi.
Kuna wazungu pale azam
Kuna financial advisor wadosi hindus pale tena anawasikilza sana.
Mnataka kazi mkaukate mchume haraka mshazoea escrow wote watoto wa kondoo



Bora umesema ukweli watu wameamua kurithi uongo wa Kipofu wao Muhongo.

Hivi kweli mtu haoni umuhimu wa Bahressa. Makampuni yake yameajiri watu kwa maelfu utamlinganisha muhongo anaekula kwa kuajiriwa na laptop mkononi.
Yani Mhongo hata akiwekwa gerezani hakuna mtu wa kuathirika zaidi ya familia yake.

Eti mleta mada anasema Bahressa ameajiri waislam tu !!!
Hivi waislam sio watanzania?
Kama muislam ana sifa zinazohitajika kwa nini asiajiriwe ili aendane na mazingira ya kazi zake?

CCM kazi yake ni kuwatumia watanzania maskini wenye elimu ndogo na uelewa mdogo kutetea mafisadi wanaokwapua mali za umma.
 

Nimesoma maoni ya wengi humu ndani lakini ukweli ni kuwa wengi wetu bado hatujaijua CCM na Serikali yake na ndy maana mashambulizi yanaenda kwa Dr Mengi ila niwaombe tu kuwa wapole na ipo siku sote tutajajua kuwa siasa za Bongo ni usanii wa sarakasi zisizo.za democrasia hata kidogo. Kwa muda wa sasa haya tuendelee kuaminishwa kuwa GODFATHER lengwa ni Mengi R. kama ilivyoletwa na mtoa mada.
USILO LIJUA NI SAWASAWA NA USIKU WA GIZE NENE!
 

Asante sana mkuu. Prof. Muhongo akiulizwa kuhusu escrow, anasema hahusiki kwa kuwa mikataba ilisainiwa kabla hajakabidhiwa Wizara. Akiulizwa kuhusu umeme vijijini, anahusika sana na jitihada zake zimepelekea maelfu ya vijiji kupata umeme. REA na miradi ya umeme vijijini iliandaliwa kabla Prof. Muhongo hajakabidhiwa wizara na ingetekelezwa hata kama Waziri wa Nishati angekuwa Hawa Ghasia badala ya Prof. Muhongo. Kwenye umeme vijijini, hasemi kuwa miradi iliandaliwa kabla hajafika Wizarani kama ilivyo kwa mikataba ya IPTL. Iweje mafanikio ya Wizara yanamhusu lakini mapungufu ya Wizara hayamhusu?

Na huyu anadai ni msomi aliyebobea. Msomi aliyebobea haogopi kukosolewa na hukubali inapothibitishwa kuwa amekosea. Kwa mfano, mtu msomi hukubali pindi inapothibitishwa kuwa utafiti wake ulikuwa na makosa fulani fulani. Hakai kung'ang'ana kujitetea kwa kuorodhesha utitiri wa vyeti alivyonavyo na kazi alizowahi kufanya.
 
Asante mkuu kwa kunipa elimu mujarabu ya umeme na gharama zake za uendeshaji,Now you have successfully changed my mind over Muhongo and his power development projects.

Na Prof. Muhongo ni mtaalamu wa miamba. Sasa, utaalamu wa miamba na energy systems (pamoja na gharama zake) haviendani. Prof. Muhongo ni researcher na si kiongozi au manager anayeweza kutuletea umeme wa uhakika na bei nafuu. Prof. Muhongo hajawahi kuuza hata juice, ataweza kweli kusimamia biashara ngumu kwenye sekta ya nishati? Prof. Muhongo ni msomi mzuri sana na mtaalamu anayeheshimika wa miamba. Ni vyema akaendelee na kazi aliyoisomea na anayoimudu vilivyo kuliko kung'ang'ania vitu asivyoviweza.
 

Kwa maoni yako kuna mambo ambayo sijaelewaz intention yake hasa kwa public.

Huyo Godfather unayedanganya uma siyo sahihi. Yeye amekuwa mwiba kwa wezi kwa kujaribu kufungua wananchi macho. Kwa mtu kama wewe ambaye ni mnufaika wa syndicates za Wizi, ufisadi (Mapapa), madawa ya kulevya (Nzowa issue), watapanya mali zaumma ikiwemo ardhi, na wasiotaka jamii ielewe mambo viongozi washenzi wa CCM wanaifanyia nchi mko sahihi kumuana ni adui wenu. Vyombo vya habari vya huyu unayemhadaa kwa umma vimesaidia sana kuleta uelewa wa mbambo yaliyofichika ikiwemo midahalo huru, taarifa za pande mbili kueleweka vizuri. amefichua maovu mengi na kusababisha CCM kuaibika na kutafuta mbinu nyingi chafu za kudhuru vyombo hivi vya habari. Uzuri huyu ndugu awe na tabia gani ila Kupitia kwa vyombo vyake vya habari taifa limekomboa raslimali nyingi, limejengea wazalendo uzalendo wa kweli na kuimarisha confidence ya wananchi.
KUPITIA VYOMBO HIVI VYA HABARI HUYU NDUGU MBALI NA KUTENDA HAKI NA KUAJIRI WENGI, amesaidia sana kukuwa kwa uhuru wa vyombo vya habari, kuamsha ari ya wanahabari kutngeneza habari sanifu, za kimaendeleo, makala constructive na ripoti mbalimbali maalumu ambazo ni matukio ya kweli wananchi wanafanyiwa na hakuna uwajibikaji kuwaadhibu wahusika. mfano migogoro ya ardhi.

Naona wanaosupport mawazo yako mufilisi ni wezi wenzako ambao walitaka wakishaiba waitwe heros kama Chenge (Mwaandaaji wa katiba ya CCM) ambao hawataki kabisa kuwajibika. Kiburi cha Muhongo, majidai, mbwembwe, dharau, dhihaka, uongo na kujiona anajua kila kitu ndo kilimuondoa kwenye uwaziri. fedha kama hazikukwapuliwa, kwa nini ajiuzulu?? Viongozi wenu CCM wezi na walafi ndio wanaosababisha maisha ya wananchi yanakuwa magumu na wanaichukia chama chenye serikali kwakuwa kimekosa kutoa sera zenye tija zaidi ya kujikita kwenye wizi, ufisadi, kuuwa aldino , na kuuza nchi kwa mafungu na rasilimali zake kwa wawekezaji wezi.

Kwa taarifa yako inaonesha una bifu binafsi ila jamii inaelewa fika muuaji wa Chama chenu cha wizi ni viongozi wachafu ikianzia kwa mwenyekiti mpaka kwa watendaji wadogo katika chama. mha husda mna hadaa na mnafanana kabisa na ibilisi mwaribifu. mfsno ni njia CCM inazotomua kuwadhuru waaduilifu wa chama na kuwainua waovu. Kuna waliolishwa sumu na wengine kuuawa au kudhuriwa kwa kusababishiwa ajali. mfano mzuri tu ni recent incidence ya Mgimwa na Dr. Mvungi. Jamii inaelewa fika unyama CCM inaoufanya kwa raia wema kupitia polisi na vyombo vya usalama. wapinzani wanajua uchungu wa kuwepo CCM kwa jinsi walivyotumia fedha na madaraka kukandamiza wapinzani mpaka kuanzisha hujuma ya kudhuru raia wakisingizia wapinzani. mfano ni Mwigulu nchemba na wengine.

Tumeshuudia rafu za chaguzi mbalimbali zikifanywa na CCM ba sio ripot za TV, tumeona rafu ndani ya chama, tumeona hujuma kwenye elimu, viongozi wasio na weledi wakipewa nafasi nyeti, maisha kuzidi kuwa magumu huku kina masaburi na viwanda vya ARV faki wakizidi kuneemeka, mahospitalini dawa shida na huduma mbovu, elimu ndio changa la macho, vyuo vikuu mikopo inatolewa kama dawa, sasa utamlaumu Godfather ndio kasababisha haya?????? Ufisadi, Wizi, tafakari na chukua hatua, muuanyi wa CCM ni UFISADI KIKWETE na Syndicate iliyomuweka madarakani. Udhaifu,hadaa, fedha, umasikini, visasi na umimi ndio vinaiharibu CCM.

God father anafanya ligal businesses ila CCM wanafanya illegal business kuanzaia madawa ya kulevia, pembe za ndovu, madini, warumwa (wanapelekwa uarabuni kiagent wakilaghaiwa kazi nzuri) na ndio in ayoharibu nchi.
Tutafakari pamoja.
 
kumjadili baba wawili ni kupoteza muda tu.!! ccm wanatapatapa wanatafuta mchawi.wamerikologa walinywe tu..!!
 

vibaraka wa ccm mna kazi kubwa kiwango cha uchafu wa ccm ni mkubwa sana hamuwez kuusafisha kwa kusingia mara MENGI mtatajana wengi tu msimu si ndo huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…