dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,476
- 2,087
Habari zenu marafiki?
Kwa kuamini busara hekima na weledi wa wanajamvi mliosheheni humu ndani, Wake kwa waume, Wazee kwa vijana, Magwiji kwa Mamanju, Wezi wa Mapenzi.
Kwa taadhima na mhemko uliojawa na mshawasha wa kupata mchepuko waukweli uliohamia hapa mtaani kwetu.
Naomba kuwasilisha ombi langu rasmi muweze kunipa mchango wa mbinu za namna rahisi za kuniwezesha kumpata mrembo wa ukweli aliehamia hapa jirani kabisa na nyumbani.
Kifupi, Si kuwa naogopa kumtongoza, ila, Sitaki kubahatisha na kwa kuwa naamini ninayo hazina kubwa ya wadau wanaoweza kuni-push naazimia nimuingie nikiwa na zana zote muhimu ili asichomoke.
Si mnajua mtu watu? Sasa watu ninao nafanzaje? Nawashirikisha kama ifuatavyo:
Mdada huyu namuona zaidi ya mwaka sasa mtaani kwetu, ila tunagongana mara mojamoja sana tena kwa mbali kutokana na mishemishe zake na zangu kutofautiana katika kusaka Tonge la kila siku.
Kiumbo ni mrembo haswa, dizaini zile za ma-miss, rangi nzuri ya ngozi ni maji ya kunde na mrefu wa wastani.
Nampendea kitu kimoja anaoneka yupo simpo san, ana upendo kwa watu.
Yupo nadhifu kila nimuonapo na pia asiependa Uswahili kwani hana zile za kuzagaazagaa sana mtaani kupiga umbea.
Mwenzenu baada ya kurogwa na mvuto wa huyu kiumbe nimejikuta nikifanya ujasusi wa kutaka kumjua zaidi.
Nikajipanga kwa kuweka mashushu wangu kila kona ili mradi nimjue kiundani nijiridhishe.
Mirejesho ninazopata kutoka kwa timu yangu makini ya upelelezi, ikimjumuisha mdada wa kazi wa binti huyu, ni kuwa mrembo huyu anafaa kabisa kuwa wifi yenu au Shemeji kwa baadhi yenu.
Baada ya kumjua, Kazi rasmi ya kumfukuzia inaanza sasa.
Lakini kumbuka yeye akitoka kazini yupo kwenye gari yake, akiingiza gari ndani kutoka ni nadra sana.
anaonekana ni mtu na kazi yake nzuri na bila shaka mwenye kipato cha kuridhisha.
Juzi kati bahati iliyoje;
Nikiwa natoka mazoezini jioni, mwenyewe nimejichokea baada ya kuvirigwa na mazoezi makali,
Hamad! 'Wifi yenu mtarajiwa' huyu hapa mbele yangu,
Yupo pekeyake tena kwa miguu akielekea dukani na tumeongozana,
wakati namkaribia pembeni ya nyumba moja upo mti wenye maua nikaona anachuma ua moja kisha akaanza kulinusa,
Mimi sasa nikawa nimemkaribia kabisa nipo nyuma yake,
Nikapata ile 'Breaking the Ice-point'
Nikamwambia, Afadhali unipatie mimi hilo ua'
Yeye akawa kama kastuka, Hakutegemea kuwa kuna mtu nyuma yake.
Kisha akageuka, Huku akiachia tabasamu nakunijibu,Sio wewe ndiye apaswae kunipatia mimi ua?
Mkware wenu, Mungu anipe nini tena? (Moyoni nikaachia cheko la furaha)
Nikamjibu-Nikamwambia, Usihofu siku moja nitakupatia-Tena UA halisi linalofanana na wewe.
Au unasemaje?-Nikamuuliza.
Nikaona binti kaachia tabasamu likinionyesha kwa ukaribu Mashavu yake yenye mvuto na macho yenye bashasha, kisha akaondoka zake namimi nikawa nimeshafika geti la nyumbani.
Kiukweli ule uchovu wangu wote wa mazoezi nikahisi kama umetoka baada ya kuongea na huyu binti.
Basi, nikajisemea moyoni sasa kazi inaanza rasmi.
Ni kama ninayo bahati na huyu mlimbwende kwa siku za karibuni,
kwani jana tena wakati natoka kuelekea kwenye mishe zangu mida ya asubuhi namuona tena huyoo akielekea dukani tukawa kama tunapishana.
Mwanenu nikataka niweke kumbukumbu vyema na kumfanya asinisahau haraka,
Nikamwambia, Mambo?- Kabla hajajibu salamu yangu nikaunganisha,
Swala lako nalifanyia kazi-nakuahidi sitakuangusha.
Binti akaniangalia kisha akasema,"Nini"? Ooo.. akawa kama amenikumbuka,Akaachia tabasamu tena "UA ee?"
Okay I'll be waiting", akiwa anatabasamu tena.
Nikaondoka zangu, nae akielekea uelekeo wake.
OMBI
Sasa wadau mimi huu utamaduni wa kupeana Maua na wapenzi sina na sijauzoea.
Pili, Huyu binti namhitaji kiukweli nimuweke kwenye himaya yangu ya mapenzi.
Mpaka sasa bado sijamtamkia kuwa nampenda lakini kwa mtu mzima kama yeye nafahamu wazi kuwa atakuwa anafahamu kuwa mimi nina langu jambo juu yake.
Ombi langu kwenu ni kushea na mimi mbinu sawia zitakazorahisisha mchakato huu kufikia tamati njema na kusudiwa.
KWA WANAUME WENZANGU:
Nafahamu wengi humu ni wajuzi na matajiri wa ufahamu wa kumshawishi mwanamke aweze kuchojoa 'Kifuko cha asali' kiurahisi.
WADADA:
Najua mtaurahi sana kupata Wifi wa ukweli,
Pili, Mnafahamu mnawezaje kunasa kiurahisi,
Hivyo basi, si vibaya mkaniwezesha kimbinu ili niwaletee Wifi wa ukweli.
Cc. miss. Chagga:
Wewe ni mjuvi wa Maua nichagulie aina nzuri ya ua la kumtongozea Wifi yako mtarajiwa fasta na wapi naweza kulipata
nifahamishe pia.
NAWASILISHA.