The Fastest Internet Connection in the World | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Fastest Internet Connection in the World

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by sijui nini, Jul 12, 2012.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Internet speed is measured in kilobits per second (Kbps) or megabits per second (Mbps). Generally, higher speed services attract higher monthly rental fees. The bandwidth you can get is only limited by your budget. How much do you want to pay? Some of the sites claim that users can increase the web browsing speed by using their Booster, Accelerators, or some programs such as Download Managers.

  Internet connections are fastest in South Korea. South Korea boasts the world's highest average connection speed at 14.6 Megabytes per second. Japan had the second highest average connection speed of 7.9 Mbps, followed by the Chinese territory of Hong Kong with 7.6 Mbps. South Korea has six of the top ten fastest cities in Asia, all with average speeds above 15 Mbps. In South Korea, 74 percent of Internet connections were high broadband, the world's top rate, while the figure was 60 percent in Japan, followed by Hong Kong with 46 percent. Asia, thanks to the growing number of fiber-based broadband connections in countries like China, Japan and South Korea accounts for 59 of the top 100 fastest cities in the world. The United States came twelfth, with just 24 percent of internet connections at 5 Mbps or more.

  https://sites.google.com/site/worldfastcar/internet-connection
   
 2. leh

  leh JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  average speeds za top ten cities in the world (over 5MBps) ni almost impossible kupata isp hapa bongo atakupa that kinda speed. na the select few wanao hizo speeds wanapiga price za hatari. tsk tsk tsk. makes me wish nilizaliwa ulaya at times :(
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zote hizo cha-mtoto yenyewe hii hapa:

  Qatar's Qtel trials 100mpbs Internet speeds for consumers

  From 18 May 2011, Qtel is enabling customers within the company's trial fibre footprint to receive home Internet broadband at speeds of up to 100 Mbps. As Qtel's next generation fibre network continues to extend, the company will be well positioned to offer this service to customers throughout Doha and other urban areas.

  Source: Qatar's Qtel trials 100mpbs Internet speeds for consumers | t-break: Tech @ Its Fastest
   
 4. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  heheheheee...afu tunajisifia maredioni ... pata internet ya kasi kutoka *!@#@$()&....
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  TTCL wanajibaraguza na 8Mbps ambayo sina uhakika kama inafanya kazi kwa spidi hiyo. Inakuwaje tusipate hata 10Mbps tu hapa TZ?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Bongo Bingo!
   
 7. The Tan-talizer

  The Tan-talizer Senior Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 155
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Daah kwa hapo hata me wish same
   
 8. Paje

  Paje JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 24, 2010
  Messages: 1,198
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  jamani tusichanganye kati ya MBps na Mbps. capital B maanake ni byte na small b ni bit. moja ni mara nane zaidi
   
 9. Mr Kicheko

  Mr Kicheko JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  somo bado gumu kwa wadau labda udadavue upya pajeeee
   
 10. leh

  leh JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  umeona eh?? was]huni hapa bongo wanatoa 8mb/s (1MBps) ambapo hata hiyo 1MBps mpaka upate labda uishi chini ya mnara
   
 11. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Scientists has discovered fastest Wi-Fi which can transmit up to 2.5TBps (yes it's Tela Bytes) but for now it under development and it can only transmit at 1 meter range, Je Ni lini wata maliza hii kitu ili niache kununua hivi vi bluray disk.
   
 12. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  ishu sio ni lini tu watamaliza maana hata wakimaliza leo huku bongo hadi ifike ni balaa na bado kuna wachakachuaji...zis is bongo bana!!
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Teknolojia ya bongo imeanza kukuwa kwa haraka sana lakini hatuitumii ipasavyo, tuna mkonga wa fibre optic unazunguka nchi nzima, tunau under utilize so far.
   
 14. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  tatizo ndo hilo..uchakachuaji..kila mtu ndo anataka kushibia hapo pila kujali utendaji kazi wa hiyo technolojia..unadhani nini kitafuata zaidi ya kupewa maneno meengiiiii...!!
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siyo uchakachuaji, ni watu kutokujuwa hii teknolojia waitumie vipi.

  Kinachotakiwa kufanywa ni aidha hawa ma service providers watumie huo mkonga na kuwafikishia watumiaji wa kawaida, au kuibukuka kwa service providers wengine wataoweza kuitumia hiyo teknology na kuifikisha inapotakiwa.

  Kuwa na mkonga wa fibre optics wa taifa ni kama kuwa na bomba kubwa la maji, ambalo inabidi ukaunganishe mabomba madogo yatayosambaza hayo maji kwa watumiaji. Inabidi kuwe na uwekezaji wa makusudi.

  Kwa sasa, ma service providers hawana ushindani mkubwa wa kibiashara na wanatengeneza pesa kwa zana walizonazo sasa hivi kuliko matarajio yao, kwanini waingize pesa zingine? inabidi waje wajitokeze wengine kuimarisha ushindani ndipo tutakapoona speed zikiongezeka kwa kasi.

  Factor nyingine ni kuwa watumiaji wako happy na spidi za sasa na hakuna demand kubwa ya kuwa na spidi kali za teknolojia.
   
 16. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,801
  Likes Received: 2,572
  Trophy Points: 280
  Bongo ni zaidi unavo ijua LTE network tayari imezinduliwa hapa . Hata SA hawana hii kitu. Tatizo inapatikana uzunguni tu. Google 4G LTE network dar es saalam
   
 17. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  GHALAMA ya kuvuta hiyo fiber optics itakua ni sawa na kuvuta umeme wa TANESCO
   
 18. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hapana mkuu mi nakukatalia kwa hili..si kweli kuwa watumiaji hawajui matumizi ya hii technolojia..Tanzania ya sasa tofauti sana na tanzania ya miaka michache nyuma juu ya matumizi ya technolojia..saiz watumiaji wa hii tcholojia ni wengi mno..na bado wapo wengi sana wanaihitaji lakini wanaipata kwa taabu saana..na hata hao tunaoipata si kweli kuwa tuko happy..mfano mrahisi we angalia tu humu jamvini watu wanayolalamika juu ya hizi internet zetu za kibongo..matatizo matupu..basi tu tunavumilia! we unadhani aiktokea mtu mwenye akili akaamua kuwekeza kwenye hili na kutoa intenet safi nani atabaki kwenye hii mitandao ya kijinga?? na si kweli kuwa wanashindwa kutoa huduma bora tatizo ni uchakachuaji tu..kila mtu anaangalia tumbo lake..bajeti ikitolewa inaishia juu kwa juu..mtu akishashiba hajali tena technolojia yenu hii..itamsaidia nini yeye wakati kila kitu anacho na anamaisha mazuri..thats the problem!! kama ni watumiaji wapo wengi tu hata kama gharama zikiwa juu ni bora lakini tupate kitu cha uhakika..si kuzinguana kama hivi..watu wanajisifu na 3G wakati spidi yake hata 0.5G hamna!!!
   
 19. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Unaona eeh..we unadhani ni kwanini wamejitenga uzunguni huko...hawataki ubabaishaji wa kibongo bongo..!!ukitaka kuamini system hiyo hiyo wangechukua mtandao wa kibongo ungeona kama hata wangeweza kusupply hata huko uzunguni tu kwa speed hiyo wanayopata saiv..
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kujuwa kuitumia na kujuwa kuitumia kwa kuzalisha ndio tofauti usiyoielewa bado. Kuna kitu kinaitwa "technology economics" kama una teknoloji ambayo haijilipi kifaida hakuna mwekezaji awe wa ndani au awe wa nje ataewekeza.

  Mkonga tunao, nani ataewekeza kuunganisha na unapotumika ili ulete faida? anza wewe unangoja nini? kama huwezi kuanza niambie kwa nini? utakuta jibu ni economy hairuhusu. Kama una jibu lingine nifahamishe.
   
Loading...