The End of The World: Sleepy Hollow

Stavros Myles

JF-Expert Member
Jun 7, 2020
350
390
Ikiwa ni majira ya usiku na kuisindikiza weekend yangu leo nimeanza kutazama series ya Sleepy Hollow iliyokuwa 'produced' na Fox.

Kongole za kutosha ziwaendee waandishi wa series hii ambao ni Roberto Orci, Alex Kurtman na Mark Goffman

Ni series inayohusu watu wanne wapanda farasi ambao wanaongozwa na Lucifer. Miaka 250 iliyopita askari mmoja aliyekuwa kipindi cha George Washington akiwa vitani alikumbana na mtu aliyekuwa na alama ya upinde (Bow) mkononi.

Mtu huyo aliyevalia mavazi ya kijeshi (ya miaka hiyo) mekundu alimsogelea Ichabod Crane (mhusika mkuu) ili amuangamize, Ichabod alijitahidi kupambana na jitu hilo lakini kwa bahati alifanikiwa kulikata kichwa..


Muda umeenda Ichabod anajikuta ameamka kutoka kwenye pango, akiwa njiani anakamatwa na polisi akiwa kama mshukiwa namba moja wa kifo cha sheriff Corbin aliyeuawa karne hii ya 21 baada ya headless man kurudi duniani. Sheriff Corbin aliuawa na yule jamaa aliyekatwa kichwa miaka 250 iliyopita ambaye amerudi karne ya 21 kuwainua wapanda farasi wenzie watatu ili wawe wanne kama ilivyotabiliwa kwenye kitabu cha ufunuo (Revelations).

Bahati mbaya nikwamba kiumbe asiye na kichwa anatafuta kichwa chake ili aungane na wenziwe watatu walete maafa duniani. Na bahati njema ni kwamba wakati ule miaka 250 iliyopita damu ya Ichabod na jitu lile zilikutana ivyo wote wakawa bound under the same fate. Akija yule kiumbe Ichabod anakuwepo.


Ichabod alikuwa na mke aliyefahamika kama Katrina aliyeuawa miaka 250 iliyopita. Lakini Katrina alipokuwa anamtokea Ichabod ndotoni(karne hii ya 21) alikuwa anamsisitizia kuhusu mipango ya headless man.


Maofisa wa polisi hawamuamini Ichabod na wanadhani ameweuka kwa kumtaja G.Washington aliyefariki miaka mingi iliyopita. Kama bahati Ichabod anakutana na Lieutenant Abbie ambaye hapo awali aliwahi kukumbwa na mkasa wa ajabu.

Ilikuwa hivi majira ya mchana wakiwa na dada yake aliyefahamika kwa jina la Jenny (ingawa bado alikuwa hai) wakiwa wanatembea maeneo ya msituni walishangaa ghafla miti minne iliyokuwa na rangi nyeupe inajitokeza nyuma yao. Wakiwa hapo mara ghafla sauti ya ajabu inasikika..Baada ya muda wanaokotwa na watu wakiwa kando ya balabala, kama ilivyokawaida watu wanawaona ni vichaa (insane at that point).

Lieutenant Abbie anakubali kufuatana na Ichabod licha ya mkuu wake wa kazi kumtia vitisho kila siku.

Lucifer mwenyewe anamtokea mmoja wa watu wake aliotaka wasaidiane na headless man kupata kichwa chake na kumnyonga kichwa, lakini katika hali ya kushangaza mtu huyo ana 'survive' na ndiye anayetumika kumuinua mwanamama mmoja mshirikina ambaye ili awe mzima anahitajika mtu wa kumuua. Lieutenant akiwa na Ichabod wanapata kushuhudia mtu mwenye mapembe akiwa anatokomea kwenye kioo cha cell aliyouawa mfuasi yule wa Lucifer.


I recommend this series kwa wale wanaotaka wajifikirie na kutafakari mambo ya imani zao au hata wale wanaoangalia for fun.

I wish ningekuwa natupia popcorn mdomoni kuiendesha siku ya leo mpaka kitisa tisa (03:00 AM).


UPDATES:
UPDATE : 01
Kwa siku ya leo nimefanikiwa kufika episode ya 10 ya season one. Mambo naona yanazidi kutamalaki na kuwa interesting. Sema inaonekana main character alianza kuzidiwa waandishi wakaona wamuongezee msaidizi. Msaidizi naye alifanya kazi nzuri hapa namzungumzia mzee Henry.

Henry huyu ni mzee wa makamu aliyekuwa na cheo chau 'sin eater', muibua mizimu na mengine mengi ya ushirikina.

Hapa wadau nitaendelea siku nyingine leo weekend imeisha vyema tu.

Sun, Oct 24 ,2021
7:26 PM
 
Iko interesting napenda anavyo ongea ascent English yake ya miaka 500 nyuma na
Jinsi anavyo unganisha matukio kutoka , kwenye kitabu cha revelation .. ila session
Za mwanzo ndio nzuri
 
UPDATE: 02

Hatimaye nimefanikiwa kuimaliza season one ya Sleepy Hollow, ninasubiri kuanza season ya pili weekend ijayo.

Aisee tasnia za muvi katika nchi nyingi wana chakujifunza kutoka Marekani. Waandishi walitulia kutengeneza stori ya aina hii.

Licha ya season one mpaka inaisha bila kupata full view ya moloch bado season inaelekea kuzuri.

#sleepyhollow👹
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom