IGP Mwema, UWT, na JWTZ yetu chini ya kiongozi wetu Denis Mwamnyange mpo mpaka hapo.
Raia tunapolalamikia mambo mbambali ya nchi yetu na hata kufikia mahala tukasukumana, kamwe haiwapi a disciplined professional force in uniform or plaincloth haki ya kutuona raia wenzenu maadui na kuingiza ushabiki wa kupenda kwenu binafsi itikadi fulani fulani kutugonganisha.
Hapo ndipo uzalendo wa dhati unapojiibua yenyewe tu na kumea kama maua mazuri porini kipindi cha mvua kubwa na jeshi husika kupata heshima kubwa na ushirikiano mbele ya macho ya jamii yake.
Nchini Misri ilikua ni utamaduni wa aina yake kuona askari anapotimiza wajibu wake KIKATIBA kumlinda Bosi wake (Mlipakodi) hata pale ambapo ni wazi bosi kachukia hakuna mfano wake.
Hapa kweku majeshi yetu hawatambui kwamba sisi ndio mabosi na watu kma Mubarak au Kikwete ni watumishi wetu tu. Si ajabu hapa kwetu Bosi lazima tungeuaua kama kule Arusha na mtumishi wetu namba moja (Kikwete) na timu yake wakalindwa!!
Jamani kila mara tuwe tunajikumbusha wajibu wetu, kutambua washikadau wetu wote na jinsi gani KATIBA inavyotuelekeza kuhusiana naye katika sura mbalimbali; tuache kufanya tu kazi kwa mazoea.
Jeshi la Misri heko, Polisi wao warudi shule baada ya kupata aibu ya mwaka mbele ya macho ya ulimwengu.