The doubts of love | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The doubts of love

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The dirt paka, Apr 13, 2011.

 1. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanasema tu mapenzi huja na kukaa au kuondoka yakitaka.
  Na akupendae mpende lakini hii hutegemea na type yenyewe.
  Mimi nashangaa, najiuliza sipati jibu.
  Ninapoishi kwasasa nimezungukwa na wasichana wengi mno. Ila binafsi ni kijana mkimya sana nazaidi kwa wanawake hasa ambao sina jambo linalotuunganisha hata salamu kuitoa huwa shida muda mwingi huwa namambo yangu sina habari na mtu na kimotion changu cha haraka na katabasamu maramojamoja. Sasa nashangaa wasichana hawa wanaponiona kuna baadhi huniangalia sana hadi nahisi aibu naweza hata kujikwa na kila nikipishana nao huwa wanajadilijadili vitu fulani. je humaanisha nini?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Labda wanakushangaa..labda ni hobby yao kuangalia wapita njia..labda unavutia kwahiyo wanajiburudisha!Wanayojadili unayajua?Kama sio hamna cha ajabu hapo..unawakuta tu katikati ya maongezi yao.Imewahi kunitokea..kuna sehemu karibu na nyumbani vijana walikua wanakaa mida ya mchana hivi mpaka jioni!Wanapiga story zao huku wakiangalia wapita njia.Ilikua nikifika pale napita haraka ila sikuwahi kua na mawazo kwamba wananiangalia na kuniƱgelea nikipita mpaka nilipokua rafiki na mmoja wao...
   
 3. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wanamaanisha wewe ni The Dirt Paka - ambapo it has to read - The Dirty Paka - Yaani Paka Mchafu............
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Chukua chako mapema zubaa mwishowe uje kuanza kupost sredi za natafuta mchumba
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mmmh! Unaona aibu ya nini mtoto wa kiume! Pole.
   
 6. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Juzi nilikua nimevaa simple shoes zangu nilipokutana nao nikainamisha kichwa, nilipowapa mgongo wakaanza kudiscuss vile viatu kwasauti ambayo walihisi siwasikii ila nikapotezea maana sina mazoea nao. Jana nimekuta na wawili mmja alishawahi kuwa rafiki yangu mwaka jana almanusura tuwe wapenzi tulisalimiana nikachapa mwendo nikamsikia akimwambia mwenzie neno kama "ANAAIBU..., ANAISHI..., anaitwa..." nikapotezea huyo maana siku hizi alishakuwa paka wa mpishi. Hapo ndo nikawa najiuliza kunani? Leo nimekutana na wengine wawili ambao sina mazoea nao ila miezi kadhaa tumekuwa tukionana mmoja wao huwa akiniona ananitazama sana hata kutabasamu, mwezi wa 12 mwaka jana rafiki yangu aliniambia nimsindikize kwa rafiki zake kufika walikuwa wasichana hao walichobase nikujua jina langu huku huyo ambaye hunizoom sana na tuliwahi kusoma nae kozi moja chuoni akiniambia "leo mchana nilikuona ukichota maji juu ya ghorofa tankin nikatamani nikuombe unisaidie na mi nikaogopa", mara akaanza kunikumbusha sehemu tulizowahi kukutana kila mtu akiwa na tisin zake. Akanambia sehemu niliyokuwa sikumbuki eti tuliwahi kukutana library mi nikiwa na rafiki yangu tulichagua kitabu tukakosa sit nikatoa uamuz wakuondoka yeye ndiye tukampa kitabu hicho. Nilishangaa kuona anajua detail zangu nyingi hata nisizokumbuka. Baadae nkaambiwa na rafiki yangu huenda mrembo huyo ananiadmire sana si bure ila nikapotezea.
  Leo mchana nimekutana nao sehemu akaniangaliaa nakumnong'oneza mwenzie jambo mwenzie akamjibu kwasauti "usinambie mtajuana wenyewe" lakini nikapotezea wakapita mbele yangu huku akilazimisha kunitingishia urojo wake nikajisemea maybe next time we gonna work together.
   
 7. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  hehe...
   
 8. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  We Husninyo! hata shujaa huingia vitani huku kabeba silaha maana anajua kunakufa.
   
 9. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwikwikwikwiiiiiiiiii

  sasa nimepata picha..yani ni kwamba unataka tujue kuwa wewe unavutia mtaani hakukaliki wanawake kila kukicha wanakuangalia

  wanakusema wanatamani kuongea na wewe etc...duuh!

  kumbe huna shida ya kutafuta
   
 10. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Weee! Usinitanie..!
  Lakini mimi simpi mtu mkuki na sime hadi nimchunguze ndio awe malikia.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Amekuzimia...sasa amua kumzindua au kumpotezea!
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Wewe kila kitu una POTEZEA???? Utaendelea hivi mpaka lini??? At the same time inaonyesha HUPOTEZEI bali unasumbuliwa na hayo mawazo mpaka ukaleta thread kabisa hapa JF.

  Kwa staili hii ya KUPOTEZEA itakufanya uonekane unawaogopa wanawake, na unafanya kila mbinu uendelee kuwakwepa.
  Hakuna sehemu utakayokwenda utaishi bila kuonana na wanawake. Jaribu kujichanganya nao kimaongezi, wachukulie kiurafiki kama unavyowachukulia wanaume wenzako. Jichanganye na jamii.
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hii story mie hoi bin taabani, 2lkutana mchana..,..... Yaonekana unawarusha roho hao mabinti wanashndwa kukwambia coz co utamaduni we2, ila kweli cna mbav na haya maelezo yako.
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haha haaa mkuu, hawajakuomba vocha? maana sikuhizi vocha zipo juu! But anyway Usiwe serious saaana hawatakubaka ni makubariano tu, kuhusu kucheka huenda wanayao tu, usijihisi sana, be simple broda!
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  we lizzy c ashasema huwa ANAPOTEZEA??? Tena haswa akivaa simple shoes??? Acha bana! Mi hata cjamwelewa anataka kusaidiwa nini manake naona anatupigshia story za mtaani kwao tuuuuuuuu!
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Pole sana. kupungua Self esteem (kujiamini) husababisha uonekane kituko mbele ya watu. Lakini hilo halitawezekana mpaka pale utapoonekana unafanya vituko, mfano kujikwaa kila unapoangaliwa na hao mabinti.
   
 17. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kaka umemaliza, tuko pamoja!
   
 18. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Umeona eee!
   
 19. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Usinitanieee!
  Hata kama ni mvuto sa ndo wananing'inia hadi madirishani wanazuga network inasumbua, ilimradi nisikie sauti mara nikipita usiku wanapiga miluzi, "ksiiiii" sijisifii hata kidogo this is a sign of dangerous... ilimradi yangu masikio yangu macho.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Alianza kwa kusema haelewi kinachoendelea kumbe anaelewa...nimeona nimpe samari kwa lugha nyepesi!
   
Loading...