Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,262
- 2,191
Ukiniuliza ungependa tuwe na serikali moja ya ulimwengu, mimi ningesema ndiyo kwani ingeweza kupunguza political instabilities ulimwenguni na kuongeza umoja na mshikamano. Mboki na Gaddafi waliona mbali kwa kuweza kuunga mkono agenda ya kuwa na serikali moja ya Africa yaani, United states of Africa, ila ikashindikana, lakini muda sio mrefu tutakuwa na serikali moja ya ulimwengu yaani "one world government".
Kamati ya watu 300, ndiyo jamii ya siri yenye ushawishi mkubwa kuliko zote duniani kwa sasa kwani imefungamana na agenda za jamii nyingine zenye nguvu duniani kama vile BOHEMIAN GROVE, ILLUMINATI, FREEMASONRY, SKULL&BONES, SOCIETY OF JESUITS, COUNCIL ON FOREIGN RELATIONS, KNIGHTS OF TEMPLAR, HASHSHASHINS, serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za ujasusi kubwa duniani kama vile CIA, MOSSAD, KGB,FBI. Hii imepelekea kamati hii kusimama kama "muhandisi" wa "one world government" agenda, ambayo muda sio mrefu itaenda kutekelezeka kama walivyokusudia.
Mwana viwanda wa kijerumani Welther Rathenau mnamo mwaka 1909 alinukuliwa akisema hivi "watu mia tatu, ambao wote wanafahamiana, wanaendesha uchumi wa mabara na kuchagua viongozi wa kuendeleza mpango wao kutoka miongoni mwao".
Mwaka 1727 ilianzishwa almashauri ya 300, ambayo ilikuwa chini ya mwanvuli wa kampuni ya kibiashara ya British India Trading Company, kampuni hii ilikuwa chini ya malkia Elizabeth wa I. Lakini kampuni hiii ilikuja kudidimia kibiashara mnamo miaka ya 1874. Pamoja na yote hayo kampuni hii ya kibiashara ilikuwa imeshakuwa na ushawishi mkubwa kwenye masuala ya uchumi na biashara ulimwenguni, hali hii ilipelekea kampuni hii kutengeneza familia 300, watu 300 wenye nguvu na ushawishi pamoja na taasisi 300 zenye nguvu na ushawishi duniani kuanzia karne ya 18 hadi karne hii 21, ambayo imekuja kupewa jina "committee of 300" kama "muhandisi" wa serikali moja ya ulimwengu "one world government" inayotarajiwa siku zijazo.
Almashauri hii ya watu 300 imeanzisha taasisi nne binafsi zenye mlengo wa ushawishi katika nyanja zote hususani siasa za ulimwengu, taasisi hizo ni hizi zifuatazo;
Chatham House,the Royal Institute of Affairs, makao makuu London.
Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1920 ikiwa na mpango wa kuhakikisha inahusisha serikali zote,taasisi binafsi,jamii na wanachama wake kwenye midahalo ya wazi na majadiliano ya kimkakati kuhusu umuhimu wa maendeleo kwenye mambo ya kimataifa.
The club of Rome
Ilianzishwa mwaka 1968 na Aurelio Peccei na mfalme Alexander in Rome, ikiwa na mpango wa kuhakikisha inakuwa kichecheo cha mabadiliko duniani kupitia kutambua na kufanya upembuzi wa matatizo sugu yanayowakumbu binadamu na kuwasilisha matatizo hayo ya watu kwa viongozi wa serikali na sekta binafsi wenye mamlaka ya kuchukua maamuzi au kuamua kwa ajili ya watu wote.
The Tavistock Institute on Human Relations
Ilianzishwa mwaka 1947 chini ya udhamini wa Rockefeller ikiwa na mpango wa kuhakikisha inasoma mahusiano ya watu kwa ajili ya kufanya maisha ya watu na hali zote za watu kwenye taasisi, jamii na kuchochea mabadiliko ya mazingira kwenye nyanja zote za maendeleo ya watu duniani.
The council on Foreign Relations
Hii ndiyo taasisi ya mwisho iliyoanzishwa na committee of 300 kwa ajili ya kutimiza agenda na mipango yao.
MALENGO YA KAMATI YA 300
Malengo ya kamati ya 300 kwa namna moja hama nyingine yanashabiana na malengo ya jamii nyingine za siri zenye nguvu ulimwenguni. Jamii hizi zote zinashirikiana kwa pamoja huku kila jamii ikilinda maslahi yake zaidi, lakini kwa kushirikiana na committee of 300, kamati hii iliweza kuja na malengo yafuatayo kwenye hii dunia
1.Serikali moja ya ulimwengu (one world government ), kuhakikisha dunia inakuwa na serikali moja ya ulimwengu yenye kutumia noti na sarafu moja ya pesa, chombo kimoja cha ulinzi na usalama, na mamlaka moja isiyowajibika kwa mtu yeyote. Hapa ndipo jamii zote zenye nguvu duniani zinakutana kimtazamo.
2. Kuondoa utambulisho wa utaifa. Hii itachochea kuundwa kwa mamlaka au tawala moja ya ulimwengu kwa kuhakikisha tunakuwa na utambulisho mmoja tu dunia nzima. Cheti cha UVIKO19 ni ishara moja wapo.
3. Uanzishwaji wa maendeleo ya kiteknolojia katika kuendesha akili ya binadamu na kucontrol idadi ya watu duniani.Hapa ni kuhakikisha kabla ya mwaka 2050 zaidi ya watu billion 3 wawe wamefariki duniani.
4. Kuhakikisha kuna kupungua kwa mapinduzi na maendeleo ya viwanda na uzalishaji wa nishati ya nuclear, ambayo inajulikana kama "the post industrial zero-growth society ".
5. Kudidimiza maendeleo ya kisayansi na kitabibu isipokuwa kwa yale yenye mlengo wa kuinufaisha kamati. Target kubwa ikiwa uzalishaji wa nishati ya nuclear kwa ajili ya matumizi sahihi na ya amani duniani.
6. Kusababisha vita visivyo kuwa na mwisho kwenye nchi zilizoendelea, majanga, njaa na magonjwa kwa nchi zinazoendelea, kwa kuhakikisha watu zaidi ya billion 3 wanafariki kote duniani kufikia 2050. Hapa unaweza kuona janga la UVIKO19, kama ishara moja wapo ya lengo hili ndani ya miaka 20 ijayo.
7. Kuzorotesha maadili ya nchi ulimwenguni kwa kutumia vyombo vya habari, muziki na muvies na kudidimiza wafanyakazi kwenye sekta ya ajira kwa kutengeneza idadi kubwa ya watu wasio na ajira duniani "Mass unemployment " kwa kuanzisha teknolojia mpya za uzalishaji zisizohitaji nguvu kazi ya watu. Hii itapelekea machafuko zaidi duniani ili kutimiza agenda no 6,5 na 4.
8. Kusababisha uangukaji wa jumla wa uchumi wa dunia hili kutimiza agenda yao ya kisiasa. Mtikisiko wa uchumi wa dunia wa mwaka 2008 utegemewe tena kwenye miaka ijayo.
9. Kuwa na nguvu na maamuzi kwenye sera zote za mambo ya kimataifa,kigeni na ya ndani ndani ya Marekani. Deep state ya USA ipo chini ya committeeof 300.
10. Kuzipa sapoti ya kutosha taasisi zote za kimataifa duniani, kama vile UN, IMF,BIS,WORLD COURT, na kuhakikisha taasisi za ndani za mataifa haziwi na nguvu na ushawishi wowote duniani kwa kuziweka chini ya umoja wa mataifa.
11. Kujipenyeza na kugawa serikali zote, na kufanya kazi kutoka kwenye hizo serikali kwa kuharibu uimara wa nchi kupitia viongozi wa nchi wanao wawakilisha. Hapa tunakutana na viongozi vibaraka duniani wasio na ukomo.
12. Kuunda chombo kimoja kikuu cha ugaidi duniani. Kuibuka kwa vikundi vya ugaidi kama ISIS, AL-QAEDA, BOKO HARAM, AL-SHABAAB n.k si kwa bahati mbaya.
UANACHAMA
Wanachama wa kamati hii ni wengi sana wengine walishafariki, wengine wapo na wengine wanazidi kuongozeka kila kukicha. Ili uwe mwanachama lazima uwe mtu mwenye nguvu ya pesa au ushawishi duniani, viongozi wakubwa duniani, wafanyabiashara wakubwa, vyombo vya habari vikubwa duniani ni mojawapo ya wanachama wa kamati hii.