The committee of 300

Hakuna hicho kitu, hakitawezekana kuwa na serikali moja. Serikali moja inayowezekana ni ya Mungu mwenyewe. Hizo ni hadithi zako za kutunga tu
Ndoto ya mfalme kwenye Daniel 2 imeelezea vizuri mfululizo wa tawala za kibinadamu hapa ulimwenguni hadi mwisho ambapo mungu mwenyewe atatawala milele.
Daniel alionyeshwa sanamu ambayo ilikuwa imejengwa kwa madini mbalimbali ,ikianzia kichwani ambacho kilikuwa cha dhahabu, mwisho wake ilikuwa kwenye vidole na ukisoma Daniel 2:42 inasema
''Kama ulivyoona, vidole vyake vya miguu vilikuwa nusu chuma na nusu udongo wa mfinyanzi, na hii inamaanisha kwamba ufalme huo utakuwa na nguvu kiasi fulani na udhaifu kiasi fulani. 43Hii inamaanisha kwamba watawala wa ufalme huo watachanganyikana kwa kuoana na watu wasio wa taifa lao, lakini hawatafaulu kuchanganyikana kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi''

44Wakati wa wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao kamwe hautaangamizwa. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, bali ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele.

Kwa upande fulani kunaweza kuwa na jitihada za kuinganisha dunia , kwa kulazimisha , kama walivyojaribu kufanya akina hitila, lakini kwa mujibu wa neno la Mungu hazitafaulu

Nakuomba usiogope Mungu yupo

Daniel2:36“Hiyo ndiyo ndoto yako, ee mfalme. Na sasa tutakupa maana yake. 37Wewe, ee mfalme, mfalme wa wafalme! Mungu amekupa ufalme, uwezo, nguvu na utukufu! 38Amekupa mamlaka juu ya wanaadamu wote, wanyama wa porini na ndege wote wa angani, kokote kule waliko. Wewe ndiwe kile kichwa cha dhahabu! 39Baada yako utafuata ufalme mwingine, lakini ufalme huo utakuwa dhaifu. Huu utafuatwa na ufalme wa tatu unaofananishwa na shaba; huo utaitawala dunia yote. 40Baada ya falme hizo, utafuata ufalme mwingine imara kama chuma. Na kama vile chuma kivunjavyo na kupondaponda vitu vyote, ndivyo ufalme huo utakavyovunjavunja na kusagilia mbali falme zilizotangulia. 41Uliona pia kuwa nyayo na vidole vya sanamu hiyo vilikuwa nusu udongo wa mfinyanzi na nusu chuma. Hii ina maana kwamba ufalme huo utagawanyika; lakini utakuwa na kiasi fulani cha nguvu za chuma kwa sababu kulikuwa na chuma kilichochanganyikana na udongo wa mfinyanzi. 42Kama ulivyoona, vidole vyake vya miguu vilikuwa nusu chuma na nusu udongo wa mfinyanzi, na hii inamaanisha kwamba ufalme huo utakuwa na nguvu kiasi fulani na udhaifu kiasi fulani. 43Hii inamaanisha kwamba watawala wa ufalme huo watachanganyikana kwa kuoana na watu wasio wa taifa lao, lakini hawatafaulu kuchanganyikana kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi. 44Wakati wa wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao kamwe hautaangamizwa. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, bali ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele. 45Uliliona jiwe lililongoka lenyewe toka mlimani, bila kuguswa, na jinsi lilivyoivunja vipandevipande ile sanamu iliyotengenezwa kwa chuma, shaba, udongo wa mfinyanzi, fedha na dhahabu. Ee mfalme, Mungu Mkuu amekufunulia mambo yatakayotukia baadaye. Mimi nimekusimulia. Ndoto yako ni ya kweli na maana yake ni halisi.”
 
Biblia imeandikwa na nani? na imetafsiriwa kutoka lugha gani na watu gani?
 
These are stupid and luciferian questions which are aimed at bringing about endless,unbeneficial and unnecessary debates.Such questions do not deserve my attention.
Sikulaumu kwa sababu kila mtumishi wa Mungu ninayemuulizaga swali hili sipewagi majibu na wanaishia kupanic kama wewe na hakuna theologian ambaye anapendaga kujibu hili swali.Hili swali nilimuuliza padre wakati nipo seminary nayeye alishindwa kunijibu na hadi naondoka tulikuwa maadui kwahiyo nilitegemea labda wewe unaweza kuwa theologian uliyeiva unipe majibu.
 
hahahahahaha aisee Hawa watu ni wendawazimu sana Bora nimeona comment Yako Kuna thread huyu huyu bwana Mathanzua nilimhoji swali hili hili akaishia kunijibu Kwa style hii hii
😁😁😁😁
 
Ningeweza kukujibu,ila watu wanaouliza maswali ya hivi huwa ni watu ambao huwa wameshapotoka spiritually,na nia yao huwa si kujifunza, ila kuleta useless and endless arguements,kwa hiyo busara na hekima ni kuwaepuka.Naukomboa wakati mkuu,sitaki kufanya kitu kisicholipa.
 
Ok . Ila kingine mtu anapouliza sio kwamba hana imani bali muda mwingine anataka kufahamu kwa kina kile anachokiamini.
 
Serikali moja inawezekana endapo mfumo wa wenye dunia yao yaani mataifa yenye nguvu yatakubaliana nao.

Changamoto kubwa ni wanasiasa, je watakubali kunyang'anywa ulaji na ile pride ya mimi ndiye rais au mfalme wa nchi hii then wakubali kuwa sawa na magavana?

Wananchi siku zote hawanaga noma maana utawaliwa na hawa wanaowazid akili yaani wanasiasa so hata likija hili la serikali moja ya dunia propaganda sikishaenezwa, wananchi watapangwa na wataeleweka.

Swali ni je, uwepo wa serikali ya namna hii ni strength na suluhisho la matatizo tuliyonayo au ni majanga matupu bora na tulivyo sasa.

1. Je, serikali hiyo itaweza kumaintain amani ya dunia kuliko ilivyo sasa?

2. Je, serikali hiyo itaweza kufutilia mbali kabisa umasikini nakuondosha matabaka?

3. Je, serikali hiyo itadumisha usawa kati ya nchi zote pasipo kupendelea upande wowote kati ya mataifa yale tajiri zaidi na maskini?

4. Je, serikali hiyo itaweza hakikisha inathibiti uzalishaji wa silaha za maangamizi na kuwajibika kikamilifu kwa dosari zake?

5. Je, serikali hiyo itawajibishwa na chombo kipi endapo ikienda ndivyo sivyo?

6. Je, itatumia muundo upi kuongoza watu ambao hauna dosari?

7. Ikiwa sasa hivi chanjo ya corona tunalazimishana, viwanda vimekuwa kero kwenye athari za kimazingira na tabia ya nchi au waamiaji toka Afrika na Asia wanawekewa vizuizi wasiingie Europe, je siku wakitawala wao kwa asilimia 100% maamuzi yao yataiathiri vipi dunia?

8. Kwa miaka yote dunia imeendelea sababu ya ushindani, sasa tukiondoa nchi tukazibadilisha kuwa na cheo cha mikoa/states, je uhakika wa maendeleo upo au yale yale tu kama tulivyo sasa?

9. Je, usalama, uhuru, usawa, haki, maamuzi ya haraka,kuheshimu imani za watu wote na tamaduni zao utadumishwa kwenye nyanja zote za kijamii na kiuchumi ikiwemo biashara?
Mfano; Leo wewe ni mfanyabiashara umekuja bongo tumezingua unaondoka na kutafuta eneo lingine kuwekeza, pata picha ni serikali hiyo hiyo hata kama imekuminya hapa hamna pa kuchomokea hata uende wapi.

10. Je, serikali hiyo itaruhusu upinzani? Vp ikitokea waliopo madarakani wakagoma kutoka nani atawaondoa? Na kama ni jeshi la dunia limepindua uongozi wa dunia nani atawachomoa?

11. Je, serikali hiyo ikiamua kuingilia uhuru wetu wa maamuzi,afya,faragha,imani,n.k au kutuongoza kidikteta au ukatokea mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali hiyo moja nini hatima yake?

12. Je, utawala huo utatofautiana vipi na tawala zakishenzi zilizopita kama ajemi,mesopotamia,rumi na nyinginezo ambazo licha ya kutawala dunia ziliishia kulipisha kodi kubwa, kuishi luxury, kupendelea mabara yao na kudumisha ubaguzi wa rangi,utamaduni mpaka imani?

Kiufupi kuna maswali mengi nahisi yanapaswa kujibiwa kabla ya kuunga sera ya serikali moja ambayo badala ya kuwa na faida inaweza ishia kuwa jehanamu kwa dunia yetu.
 
Kwa kiwango kikubwa Dunia inaenda kuendeshwa, kwenye mfumo mmoja kiutawala..
 
Mpumbavu tu ndio anaweza kuamini huu upuuzi.
 
Matumizi sahihi ya akili...
 
Sio kweli,umedanganywa,you are suffering from delusional psycosis.Zipo kambi mbili,ya Shetani na Mungu wa Israel.Halafuu,mimi sijifanyi mjanja,ni mjanja kweli kweli,sidanganyiki.
Mkuu, Mungu wa Israel ndio yupi?
 
Sio kweli,umedanganywa,you are suffering from delusional psycosis.Zipo kambi mbili,ya Shetani na Mungu wa Israel.Halafuu,mimi sijifanyi mjanja,ni mjanja kweli kweli,sidanganyiki.
walioandiandika bible ndio hao hao unao wapondeaga kila s4
 
walioandiandika bible ndio hao hao unao wapondeaga kila s4
Si kweli,you are suffering from misinformation.Ninao waponda ni NWO.Naomba uelewe kwamba ufalme ukijifitini hauwezi kusimama.You can't preach love and at the same time practise depopulation/eugenics/euthanasia,things which the NWO is advocating.That is hypocrisy,characteristic of the Devil.The B ible on the other hand presches love of one another.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…