The best place to live in dar..

sehemu nzuri ni Boko national housing....kumepimwa,kuna maji,kuna umeme,kila nyumba ina access ya barabara ya molamu,hakuna msongamano,hakuna kelele za baa
 
Bongo kote kubaya tu, labda uniambie sehemu zenye 'kujitahiditahidi'

ndugu yangu wewe, we si ulisema utabakia bongo tu? leo unasema bongo ni kubaya tena? mwe! sikusomi!

bongo kuzuri sana; tembelea Tegeta, Wazo Hill, Madale, Bunju, Mbweni etc! karibu kwetu Goba ndg. Abdul, utakula sana matunda ila usisahau kwenu sijui wapi, usiniambie ni shimo la udongo!!!
 


uzoefu wa kuishi maeneo ya ovyo tu??
Huna uzoefu wa kkuishi kwa wastaarabu?
 
boko-bunju ndo penyewe sasa!😀
 


sio mikogo...
Napenda eneo lenye nightlife iliyochangamka
ndo maana makumbusho napaona pazuri
mimi naishi tegeta,utulivu mkubwa mno...
Hadi naboreka sometimes.
 
Napenda uswazi, ambako ninapata fursa ya kuona Mwali anachezewa ngoma za Kizaramo usiku kucha. Maeneo ya Kiwalani yanafaa sana na nilienjoy wakati naishi kule, ila tatizo ni vibaka na roba za mbao.
 
Sinza ndio poa.....

Vigezo...
Baada ya Nyumba 4 unakutana na Grocery,Pub,Bar na Nightclub Hamna vibaka (wakabaji),Maji ya Uhakika (Line ya Ikulu),Jirani na Mlimani City ambayo ni One stop Shop,Madada poa kwa saana.... Etc Bar ukiamua kujilipua mpaka asubuhi kuna Meeda Night Club,Corner Bar etc...
 


sinza mori kwa kweli pazuri...
 
hizi huduma hata suka zipo!CHAWOTE BAR INAKESHA MARA KIBAO!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!
 
hizi huduma hata suka zipo!CHAWOTE BAR INAKESHA MARA KIBAO!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!

Hali kadhalika Basihaya campsite, Boko View Hotel, Tegeta By Night, Zero pub. Unakula bia huku unaangalia watalii wanaenda kushangaa bagamoyo. Karibuni kwetu Boko.
 
hizi huduma hata suka zipo!chawote bar inakesha mara kibao!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!

mkuu buffalo usiisahau, kuna KILIMANI pale napo pazuri, halafu pale kilimani huwezi amini kuna bavaria 8.6, hii bia naisakaga sana bar nyingi hawana hii kitu
 
mwamba ngoma uvutia kwake, popote kambi ilimradi nina pa kulala, misosi napata na mavazi hayanipigi chenga bila kusahau afya bora!
 
Hali kadhalika Basihaya campsite, Boko View Hotel, Tegeta By Night, Zero pub. Unakula bia huku unaangalia watalii wanaenda kushangaa bagamoyo. Karibuni kwetu Boko.


Boko napo kumevamiwa cku hizi, enzi zile hata hawajatengezeza road nilikuwa naona kama natokea dar kwenda kigoma...lol, cku za Eid ndio balaa na road yaani vurugu tupu na waendao bagamoyo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…