The best leaders ever in Tanzania

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
DR. Augostino Lyatonga Mrema na Edward Ngoyai Lowasa, ni miongoni mwa viongozi ambao, wamefanya mambo makubwa yanayo waletea watanzania manufaa mpaka sasa.

1. DR. (PHD) Mrema ndie alieneza vituo vya polisi nchi nzima kwa siku saba tu, bila bajeti wala tume au blaa blaa za wataalamu wowote. The best qoute of Lyatonga " C C M SIO MAMA YANGU, C C M SIO BABA YANGU............"

2. Leo hii watoto wote wa walala hoi, angalau wanapata fursa ya kufika sekondari, washindwe wenyewe.
Mnyonge Mnyongeni Haki yaki mpeni. Nadhani mpaka sasa watanzania mmesha jua ukweli kuhusu RICHMOND. The Best quote of Ngoyai " Nimedhalilika sana,.........................................."
 
Huyo Mrema mbona kawa comedian siku hizi?

Mwaka juzi chama chake kiliweka mgombea wa urais lakini yeye alikuwa akimkampenia JK!

Halafu kumsifia kiongozi kujenga vituo vingi vya polisi ni fikra finyu, hivo vituo vingi vya polisi huweza pia kutumiwa kwa kukandamiza raia.
 
Umetumwa jf kupost umbea? Wakati tuliona si wakati wa kuzungumzia historia. Tunatakiwa tutafakari nini cha kufanya kutokana na hali na mazingira tuliyonayo. Uchumi unazidi kushuka kwa kasi speed 200 we unaleta mambo ya historia ili watu wasahau kujadili mambo ya msingi! Kweli mungu ana watu wengi sana!
 
I know for a fact that my father is always among the best leaders in Tanzania.Aliahidi angehakikisha chakula kiko mezani mpaka leo nimesimama mwenyewe kimaisha sikuwahi kukosa chakula enzi za utawala wake,aliahidi atanipa elimu bora mimi mwenyewe ni ushahidi wa hilo,aliahidi angehakikisha napata matibabu pindi nikiwa mgonjwa leo niko hai na mwenyewe afya,the list goes on.
Usijaribu kuweka majina ya wanasiasa mbele ya macho yangu na kunielekeza kuwa wao ni viongozi wazuri na bora,kura yangu itaenda kwa yule atakayekuwa na uwezo wa kumtimizia mtanzania wa kawaida japo mahitaji yale muhimu na msingi kama alivyojitahidi mzee wangu ambaye sasa ametupwa mkono na umri.Na mpaka sasa bado sijamuona anayeweza.
To hell with dirty politics,what we need is sustainable development.
 
Aisee!! EL kweli anajituma kuutafuta U-RAIS, amejisifu amemaliza sasa anakosa aseme lipi... hadi 2015 tutasikia mengi!!!!!!!
 
Huyo Mrema mbona kawa comedian siku hizi?

Mwaka juzi chama chake kiliweka mgombea wa urais lakini yeye alikuwa akimkampenia JK!

Halafu kumsifia kiongozi kujenga vituo vingi vya polisi ni fikra finyu, hivo vituo vingi vya polisi huweza pia kutumiwa kwa kukandamiza raia.

Mkuu njaa haina baunsa!
 
Inawezakana hii ni fikira finyu, kama jamii itakubaliana na mimi kua, tuache kulima ngano, maana hutumika kutengezea pombe. Kama mawazo yako polisi ipo au imeundwa kukandamiza raia?, kaka nadhani upeo wa kufikiria ................. . Watanzania kama nyinyi sijui mtanchangia nini katika katiba. Itabidi wachangiaji katiba angalau wapewe interview ya maswali ya darasa la saba.
 
Umetumwa jf kupost umbea? Wakati tuliona si wakati wa kuzungumzia historia. Tunatakiwa tutafakari nini cha kufanya kutokana na hali na mazingira tuliyonayo. Uchumi unazidi kushuka kwa kasi speed 200 we unaleta mambo ya historia ili watu wasahau kujadili mambo ya msingi! Kweli mungu ana watu wengi sana!

Duuh! Kaka nadhani hata haustahili kusema chochote humu kama hujui maana ya Historia katika kufanya Maamuzi ya jayo. Kama hujui unapotoka, kaka siume potea wewe. Utajuaje unako enda. Je hata hapo ulipo unajua uko wapi?
 
Naunga mkono hoja Lowasa Fisadi lakini alikuwa na moyo wa kujaribu, alianzisha barabara tatu dar, alianzisha shule za kata na angeendelea angejua walimu wangepatikana wapi kaja kilaza Pinda hajui lolote kwanza anatuzalilisha wakulima. Hivyo ambao wamefanya vitu tangible ni hao kwa kweli. mnaowataka nyie semeni wamefanya nini? au kamusheni kuwa hao hawakufanya wao. Lowasa angekuwepo serikalini kungekuwa na displine ya kutosha. mgomo wa madaktari usingefikia hapo ulipo.
 
naunga mkono hoja lowasa fisadi lakini alikuwa na moyo wa kujaribu, alianzisha barabara tatu dar, alianzisha shule za kata na angeendelea angejua walimu wangepatikana wapi kaja kilaza pinda hajui lolote kwanza anatuzalilisha wakulima. Hivyo ambao wamefanya vitu tangible ni hao kwa kweli. Mnaowataka nyie semeni wamefanya nini? Au kamusheni kuwa hao hawakufanya wao. Lowasa angekuwepo serikalini kungekuwa na displine ya kutosha. Mgomo wa madaktari usingefikia hapo ulipo.

aliilia
 
I know for a fact that my father is always among the best leaders in Tanzania.Aliahidi angehakikisha chakula kiko mezani mpaka leo nimesimama mwenyewe kimaisha sikuwahi kukosa chakula enzi za utawala wake,aliahidi atanipa elimu bora mimi mwenyewe ni ushahidi wa hilo,aliahidi angehakikisha napata matibabu pindi nikiwa mgonjwa leo niko hai na mwenyewe afya,the list goes on.
Usijaribu kuweka majina ya wanasiasa mbele ya macho yangu na kunielekeza kuwa wao ni viongozi wazuri na bora,kura yangu itaenda kwa yule atakayekuwa na uwezo wa kumtimizia mtanzania wa kawaida japo mahitaji yale muhimu na msingi kama alivyojitahidi mzee wangu ambaye sasa ametupwa mkono na umri.Na mpaka sasa bado sijamuona anayeweza.
To hell with dirty politics,what we need is sustainable development.

Sasa tukusaidieje mtanzania, Yaani hayo nilio ya andika hapo yana hitaji nini kuya verify au kuyaelewa. Amakweli tatizo la watanzania ni watanzania wenyewe. JUDGE PEOPLE FOR WHAT THEY DO, AND NOT WHAT THEY SAY. AU WANACHOSINGIZIWA. AU BADO HUJAJUA UKWELI KUHUSU RICHMOND. JAMANI, MNATUCHOSHA SANA. TUNATAKA MABADILIKO SIO TAARABU AU BONGO FLEVA KWENYE KUJADILI MAMBO YA NCHI. ALAAA!
 
Kila kiongozi ana mapungufu yake.Wewe taja wako uone watakavyomshukia.Ukweli upo kwamba kwa utendaji hakunaga kama lowasa.Mponde mpendavyo lakini ukweliu nabaki hivyo
 
I know for a fact that my father is always among the best leaders in Tanzania.Aliahidi angehakikisha chakula kiko mezani mpaka leo nimesimama mwenyewe kimaisha sikuwahi kukosa chakula enzi za utawala wake,aliahidi atanipa elimu bora mimi mwenyewe ni ushahidi wa hilo,aliahidi angehakikisha napata matibabu pindi nikiwa mgonjwa leo niko hai na mwenyewe afya,the list goes on.
Usijaribu kuweka majina ya wanasiasa mbele ya macho yangu na kunielekeza kuwa wao ni viongozi wazuri na bora,kura yangu itaenda kwa yule atakayekuwa na uwezo wa kumtimizia mtanzania wa kawaida japo mahitaji yale muhimu na msingi kama alivyojitahidi mzee wangu ambaye sasa ametupwa mkono na umri.Na mpaka sasa bado sijamuona anayeweza.
To hell with dirty politics,what we need is sustainable development.

Hajakosea kabisa yeye ameweka kiongozi wake halafu ametoa hoja zilizo na mashiko kutetea uhalali wa kumuita best leader in Tanzania kama wewe ulivyowaorodhesha viongozi wako halafu haujaweka hoja yoyote zaidi ya kauli zao ambazo walizitoa zamani.JF we speak openly,namuunga mkono.
Tatizo letu nchi hii tunatamani miujiza kutoka kwa mtu ambaye hata hawezi kutatua matatizo madogo madogo.Kipindi ambacho Lowassa alikuwa mtendaji wa serikali(Waziri Mkuu) alimfanyia nini mtanzania wa kawaida???
 
Huyo Mrema mbona kawa comedian siku hizi?

Mwaka juzi chama chake kiliweka mgombea wa urais lakini yeye alikuwa akimkampenia JK!

Halafu kumsifia kiongozi kujenga vituo vingi vya polisi ni fikra finyu, hivo vituo vingi vya polisi huweza pia kutumiwa kwa kukandamiza raia.

Umesema kila kitu hapo kwenye red. Shule za kata ni Dampo la watoto wa walala hoi ambao mstakabali wao umeamuliwa na wenye madaraka waendelee na watoto wao, vijukuu na vilembwe kufanya watakalo kwa sababu fursa zao si sawa na za shule za kata.
 
umesema kila kitu hapo kwenye red. Shule za kata ni dampo la watoto wa walala hoi ambao mstakabali wao umeamuliwa na wenye madaraka waendelee na watoto wao, vijukuu na vilembwe kufanya watakalo kwa sababu fursa zao si sawa na za shule za kata.

amakweli nabii kwao hupigwa mawe. Bora kumfadhili punda kuliko mtu asie jitambua.
 
Back
Top Bottom