CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA ULUGURUNI…
Utangulizi:
LEO NI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, JAPO KWETU SISI ULUGURUNI KILA SIKU NI SIKU YA MAZINGIRA, kwani kijadi ulinzi na uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila siku la kila mwanajamii.
Changamoto
Milima ya Uluguru inakabiliwa na changamoto nyingi za kimazingira, ikiwa ni pamoja uchomaji moto, ukataji miti hovyo kwa baadhi ya wanajamii, mmomonyoko wa udongo, uchafuzi wa maji, na athari za shughuli za binadamu kwenye mazingira asilia unaoathiri pakubwa eneo hili; zikichochewa sana ongezeko la watu, kilimo kinachokiuka kanuani asilia za mazingira, na mahitaji ya ujenzi na nishati.
Suluhisho:
Wadau wa mazingira, wamejitahidi kila mmoja kwa wakati, rasilimali na fursa alizonazo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira; ingawa jitihada njia shirikishi za pamoja zinahitajika kuliko kila kundi kufanya kazi kinyake, hivyo kutawanya nguvu na kufanya jitihada za kuirejesha ULUGURU YA ZAMANI kuwa za taratibu mno.
Ushauri Muhimu na Hitimisho:
Tunazishauri mamlaka husika serikalini kuona umuhimu wa kushirikisha jamii za wenyeji na viongozi wao wa jadi wakiwemo machifu wote wa Uluguru bila kubagua, katika harakati za usimamizi wa mazingira na utawala wa rasilimali, hivyo kukuza hisia ya umiliki na uwajibikaji wa uhifadhi wa maliasili zao. Suala la Uboreshaji wa miundombinu hasa barabara za milimani ni jambo la kupewa kipaumbele cha kwanza, lakini pia suala la uasisi miradi mbadala itakayozaa ajira nje ya ya utegemezi wa misitu ni muhimu sana; na uwepo wa nishati mbadala itakayowaondoa wanajamii kuwa wategemezi wa misitu nalo ni jambo la kutafakari. Kwa wakulima, suala la elimu ya kilimo endelevu na cha kisasa, ufufaji wa vyama vya ushirika, na upatikanaji wa masoko ya uhakikika ya mazao yao ya kilimo, linaweza kuongeza fursa za kiuchumi na kupunguza athari mbaya kwa kimazingira. Mwisho ni kuongeza ufahamu kwa wanajamii wa maeneo husika kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
NAOMBA KUWASILISHA
CHIEF LUKWELE COMMUNITY BASED ORGANIZATION,
WEBSITE:
CHOMA TRADITIONAL KINGDOM (ULUGURU)