Kwako wewe nani mwenye uamuzi wa mwisho endapo kuna mpangaji anataka kupangisha nyumba yako? Maandishi mekundu una maana gharama za ujenzi si mkopo bali ni zawadi? Kwamba kama ni zawadi basi mtoaji ana hiari ya kukuambia nakupa zawdi lakini nitaondoka na mkeo!!!!???
Yote kwa yote, uamuzi wa kutoendeleza bandari zilizopo ili zilete ushindani wa kibiashara na bandari nyingine nje ya nchi, ni uamuzi wa kulihujumu taifa hili.
Kanundu, sio kweli hata kidogo kwamba kuna uamuzi wa kutoendeleza bandari nyingine sababu ya uwepo wa bandari ya Bagamoyo. Kwa taarifa yako, tayari mpango wa kuendeleza bandari ya Mtwara upo na fedha zake zimeshapatikana. Bandari ile ya Mtwara ndio itakuwa bandari kuu ya kuhudumia gas industry nchini. Pia ndio itakuwa bandari ya kusafirisha bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vikubwa vinavyotarajiwa kujengwa Mtwara kama kile kiwanda kikubwa cha Cement cha Dangote na viwanda vya Mbolea vitakavyojengwa na wawekezaji wengine. Aidha, bandari ya Lindi nayo itaendelezwa kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa katika soko la ndani.
Bandari ya Dar es salaam nayo haijabaki nyuma. Mpango mzima wa kuijenga upya reli ya kati katika viwango vya standard gauge kutoka Dar-Isaka-Kigali-Musongati unalenga kuiwezesha bandari ya Dar es salaam kuhudumia mizigo kutoka nchi hizo. Mpango wa kujenga gati mpya 13 na 14 una lengo la kupanua bandari hiyo kumudu idadi ya mizigo itakayoongezeka kutokana na reli hiyo mpya.
Bandari ya Tanga, kuna initiative inaitwa MWAPROC, ambayo inaendana na ujenzi wa EPZ ambayo tayari Wakorea wameshaonyesha interest ya kuijenga. Vilevile Uganda na Tanzania kwa pamoja zinakamilisha mpango wa ujenzi wa reli ya Tanga itakayoifanya Bandari ya Tanga itumike kusafirisha bidhaa za Uganda.
Hivyo kusema, kuna uamuzi wa kutoendeleza bandari nyingine sio kweli.