The 'Bagamoyo deal'

The 'Bagamoyo deal'

Mheshimiwa Meles Kijakazizenawi mwanaukumbi yeyuote wa JF anatakiwa awe na uwezo wa kujadili hoja kwa Kiswahili au Kiingereza. Naona una uvivu wa kusoma Kiingereza hata huwezi kusoma sentensi moja. Pole sana - kazana la sivyo utaachwa nyuma1
 
Salaama,asante kwa majibu!! Tatizo tulilonalo Tanzania ni kuamini kuwa kila mtuanayetoa hoja ya kuboresha au kueleza wazo tofauti aidha ana mawazo mgando auanafanya hivyo kwa sababu za kisiasa.
FoleniDar es Salaam: Foleni ya Dar es Salaam haichangiwi na malori yanayotoka bandarini peke yake kama unavyodai.Kwanza Malori yanayotoka bandarini na kuingia hayapiti katikati ya jiji. Tatizo kubwalililoko Dar, kama ilivyo miji mingine ya Afrika kusini mwa Sahara ni mipangomiji. Huwezi kuwa na mji ambao huduma zote kuu zinapatikana eneo moja audirection moja. Miji mikubwa ya Ulaya na Asia ina settilite cities na unakutamiji mipya inajengwa ili kupunguza pressure ya miji ya zamani (Go to London, Beijing,Tokyo, Paris, Abuja, etc). Kwa jinsi tunavyokwenda na jinsi mji wa Darunavyokuwa kiholela, tatizo la foleni halitakwisha. Hata mabasi ya kasi yanayokujahayatamaliza (Moro – City centre) tatizo. Ukweli ni kuwa plan za mji wa Dar unafanywakisiasa au wenye uwezo wa kuupanga hawana vision. Pamoja na kuupanua mji wa Darkuwa wa kisasa kuelekea Kigamboni – Kimbiji, Master city Plan for modern cityingefanyika pia eneo la Pwani kuelekea Msata. Hii ingehusisha upimaji wa maeneoya makazi, ofisi, viwanda etc. Kwa jinsi inavyofanyika sasa hivi, mji waBagamoyo utakuwa kijiji kimoja kisichokuwa na mpangilio wowote. KujengaBandari, Uwanja wa Nidege etc katikati ya maeneo yaliyopangwa kihohela ni kukosamaono ya wapi tutakuwa 50 years to come. Tunahitaji kufanya maamuzi magumuyaliyo juu ya fikra finyu za kisiasa (5 years election plan).
Competingports: Ni ukweli usiofichika na muda utakuwa shahidi, Bagamoyo Port haitakuwana msaada mkubwa kwa Bandari ya Dar. Kama umesoma project Document ya mpango waujenzi wa Bandari mwambao wa Bahari ya Lindi, Bandari ya Bagamoyo ni kwa ajili yaku-handlevessels ndogo ndogo na si kubwa. Hii, kama ilivyo kwenye Bandari nyinginezinazoendeshwa na wachina ulimwenguni, itakuwa na jukumu la kurahisishabiashara ya China na Mataifa inayofanya nazo biashara. Ukumbuke kuwa, Singaporeiliamua kujenga Bandari nyingine na kuicha ile ya zamani si kwa sababu yafoleni kama unavyotaka kutuaminisha, ni kwa sababu, Singapore kama free port nanchi ndogo ,723.2 sq. km(almost the size of Mafia Islands which is 886.03 sq km) na kukua kwa sekta ya viwanda ilikuwana haja ya kufanya hivyo. Sisi, kimsingi ni net importers wa almost kila kitulakini tuna bahati ya kuwa na majirani wasiokuwa na Bandari. Ujue pia kuwaSingapore kama kisiwa na kama free port ina-justify kuwa na bandari hata ndaniya Kilometa moja kwa kuwa wao wanatoa service kwa nchi zinazoizunguka. Hapakwetu hatuna budi kuangalia kila kitu tunachokifanya kwa maana ya macho yamiaka 50 hadi 100. Uboreshaji wa Bandari ya Tanga kwa mfano, ingekuwacompetitor mkubwa wa bandari ya Mombasa kwani ingerahisisha usafirishaji waMizigo ya Uganda, Rwanda, Burundi na Kanda ya Kaskazini. Mtwara, pamoja nauwekezaji unaofanyika huko, ungerahisisha usafirishaji wa mizigo ya Malawi,Zambia, E. Congo na hivyo kuwa competitor wa Bandari za Beira na Durban. Ujue,kuna nchi kama Djibout inaendesha uchumi wake kwa kutumia bandari kwa asilimia80.
Maoniyangu:
1. Mjiwa Bagamoyo ufanyiwe urasimishaji kuanzia inapopakana na Kibaha, Kinondoni hadiWami. Kwa kuwa Wachina wameshaingia mkataba na hakuna namna ya kuuvunja kwasasa (whether huo mkataba uko kisiasa au kimaslahi ya wachina), Urasimishajihuu utaufanya mji wa Bagamoyo kuwa wa Kisasa kama ilivyo Abuja na kupunguzapressure ya Dar.
2. Bandariza Tanga na Mtwara ziwe ni agenda yetu kuu kwa miaka 10 ijayo. Hii ijumuisheujenzi wa barabara na reli kama mwandishi alivyopendekeza.
3. Tutafutevitu kama nchi vitakavyotuwezesha kuwa na competitive advantage kwenye eneo laAfrika Mashariki na kwa ubora wa maisha ya wananchi wetu.
4. Tuacheku-copy na kupaste programs za maendeleo ya nchi za wenzetu kabla ya kuangaliamazingira yetu, tunataka nini, na tutafaidika vipi (swala Singapore kujengabandari kila kilometa kumi au tano for that matter halina uhusiano wa moja kwamoja na mazingira ya nchi yetu). Nchi ya Singapore ni tofauti kabisa na sisi,uchumi wake ni tofauti na utendaji wa taasisi zake kuanzia mwanzo ulikuwatofauti pia.
5. Tujitahidikuviimarisha kwanza vile vilivyopo kiufanisi kabla ya kudandia projectsnyingine. Hii itatufanya tuwe competitive, kutumia resources kidogo zilizopo vizuri na kufaidika zaidi. Nina uhakika, kama mpango wa utekelezaji wa upanuzi wa Bandari ya Dar na Mtwara ungefanyika kama ilivyokusudiwa miaka 20 iliyopita ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa ufanisi wa reli tungalikwa tunashindana kibishara na bandari bora ukanda wetu kwa sasa.

Babatunde walau this time umeandika sio kuponda tu, bali pia umepotoa mawazo mbadala ya kujenga na kuboresha harakati za kuendeleza nchi. Kwa mantiki hiyo nafuta comment yangu juu ya mawazo mgando....hai apply kwako.

Nikirejea kwenye hoja zako nzuri.
N kweli kabisa,mipango miji ya halmashauri za jiji na manispaa wamechangia kwa kiasi kikubwa katika sokomoko la foleni za jiji. Hili ni tatizo na linahitaji kuchukuliwa hatua. Uzuri mmoja hata Mkuu wa nchi wakati fulani akihutubia wananchi kule Mabwepande, alisemea suala hili, hasa umuhimu wa kuwa na satelite cities....zenye huduma zote muhimu ili kuepusha misongamano. Wewe umeongeza hoja nzuri zaidi, natumaini wahusika watasoma na kuzingatia maoni mazuri uliyotoa. Bandari ya Dar nayo ina mchango katika ongezeko la foleni mjini.....sio tu kwa maroli yanayotokea kule, bali magari madogo ya wananchi wanaoelekea kufuata huduma kule. Pengine with modernization ya bandari na matumizi ya Teknolojia.....itaweza kusaidia kutolazimu wananchi kwenda kule physically. Kuhusu mji wa Mpya wa Bagamoyo, mpango wa kuujenga kwa kuzingatia mradi mpya wa bandari na EPZ, ni sehemu ya mpango mzima wa mradi huo. Kama umewahi kufika Shenzen.....jinsi ilivyo develop, ndivyo Bagamoyo itakavyokuwa miaka 15 ijayo.

Kuhusu competing ports......wewe una make reference to documents za mpango wa ujenzi wa TPA ambazo haziku take on board other projects zitakazofanywa chini ya makubaliano na mwekezaji...ambayo inajumuisha EPZ, Railways na Expressways toka Dar mpaka Bagamoyo. Pia mpango ule wa TPA ulikuwa unafikiria bandari ya Bagamoyo ni ya ku handle vessels ndogo, wakati mpango wa sasa ni bandari hiyo kuwa ni 4th generation port yenye uwezo wa kuhandle meli kubwa kubwa ambazo kwa hivi sasa haziwezi kuingia bandari ya Dar

Umesema bandari hii ikijengwa kazi yake itakuwa ni kurahisisha biashara ya wachina na mataifa inayofanya nayo biashara. What is wrong with that? Mbona bandari ya Dar hivi sasa inatumika kurahisisha biashara ya Rwanda, Burundi na Zambia na mataifa mengine? Kuna dhambi? Sisi si tunachotaka ni bandari ifanye biashara....kodi zilipwe, ajira zizalishwe, shughuli nyinginezo za kiuchumi ziongezeke? Kama bandari hiyo itatumika kusafirisha bidhaa kwenda china au mahala pengine popote......si ndio biashara imeingia hapo? What more do we need?

Mawazo yako juu ya kuboresha bandari ya Tanga na Mtwara ni mazuri kabisa. Nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Bahati nzuri hata serikali nayo inatambua potential iliyopo kwenye bandari hizo na inayo mipango ya kutekeleza
 
Katika karne hii ambayo kila nchi inafukuzia uwekezaji.......kipindi hiki ambacho Djibuti inawakimbilia wawekezaji wajenge bandari kwao; wakati wakenya nao wanawavutia wawekezaji wajenge bandari mpya kwao..... Leo akija mwekezaji anataka kujenga bagamoyo, wewe ukadai hapana aende Tanga.....mwekezaji huyo ataenda Kenya au dijbuti kama sio Msumbiji......that will be an opportunity lost.

Sijasema ujenzi wa bandari hiyo ni zawadi.

Yes, Serikali haiendi kukopa popote kwa ajili ya mradi huo......hivyo hakuna cha riba, wala grace period......pesa yote itatoka kwa mwekezaji kwenye utaratibu wa PPP. Mfano uliotoa wa hiari ya kuondoka na mkeo hauna relevance yoyote, popote katika context hii tunayozungumzia

Swali la msingi, je!!!? mtanzania atanufaika vipi!!!? na maslahi ya nchi mbona yana kificho!!!? Unavyoandika its as if ulihisishwa kwenye hii deal. Inawezekana kuna mambo unayajua, hebu yaweke wazi zaidi ili tutoke kwenye porojo tuwe na data zinazoeleweka, tafadhali, endelea kutiririka na baada ya huu wito na uache hasira!

Muhimu: watu wana uchungu na rasili mali 'ZA NCHI' kuchezewa kwa faida ya wachache kwa muda mfupi kwa kupoteza uwekezaji wa muda mrefu wenye tija kwa taifa na wananchi
 
Umeuliza swali zuri dukebrain....nilishatolea majibu swali hilo, ngoja ni cut and paste majibu ambayo nilishatoa:

mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo la viwanda utakuwa na manufaa mengi from day one utakapoanza. Wananchi wapatao 3000 watapata ajira za muda za moja kwa moja katika ujenzi wa bandari na EPZ, wananchi wengine wapatao 2000 na zaidi watapata ajira zisizo za moja kwa moja kama vile Mama Ntilie watakaouza chakula, wenye nyumba zao watakaowapangisha wajenzi, wauza vinywaji, watoa huduma za usafiri-daladala, taxi, maroli ya kusafirisha mizigo n.k

Faida nyinginezo za mradi huo ni kwamba mara utakapokamilika, thamani ya properties zilizopo eneo la mradi na maeneo ya jirani kama vile Bunju,Boko, Mbezi, Tegeta n.k yatapanda thamani na kuwafaidisha wamiliki endapo watahitaji kukodisha property zao au kuzitumia kuwekea rehani kupata mikopo benki n.k

Faida nyingine ni za moja kwa moja kwa Serikali......ukubwa wa bandari maana yake volume ya mizigo itakayopitia hapo itaongezeka ambapo Serikali itaongeza mapato kupitia IMPORT DUTY, customs Duty......bandari itakapokamilika itaajiri wafanyakazi wasiopungua 1000; eneo la viwanda litakapomilika-litawezesha viwanda vingi kujengwa (by the way Mwekezaji ndio atavutia viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuweka viwanda vyao kwenye eneo hilo na tayari ameshapata wawekezaji walio tayari kuwekeza provided kuna efficient port) na viwanda hivyo vitatoa ajira kwa wananchi wasiopungua 50,000 na zaidi.

Kwa faida ya wasiojua kwanini viwanda vingi vitakuja kuwekeza katika eneo hilo:
1) bidhaa zitakazozalishwa hapa Tanzania katika eneo hilo la viwanda zitaweza kufaidi misamaha ya kodi inayotolewa kwa Nchi masikini huko Marekani (Chini ya AGOA); Ulaya (Everything but Arms EBA), Japan (TICAD consession), na China yenyewe iliyotoa msamaha wa kodi kwa asilimia 95 ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania

2) Cheap labour- ukweli ni kwamba toka China uchumi wake umekua, factors of production zilizokuwa zinawa favour zimetoweka....Afrika ndio ina fursa ya kuziba pengo hilo la China

3) Kwakuwa viwanda vingi lengo lao ni kuzalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi- uwepo wa bandari kubwa yenye mtandao mkubwa duniani inakuwa ni kivutio kikubwa kwao.....mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo anao mtandao wa bandari kadhaaa ulimwenguni....wao ndio wanamiliki bandari tano kati ya bandari kubwa kumi duniani....ikiwemo bandari ya Hongkong, Schenzen n.k

Ukiachilia ajira etc.....serikali inaweza kufaidika pia kwa kupata mrahaba (royalty) katika kipindi chote ambacho mwekezaji ataendesha bandari ili kurejesha uwekezaji aliofanya.

La muhimu hapa ni wataalam wetu watakao negotiate mkataba huo kuwa makini na kuhakikisha serikali inapata WIN-WIN deal na hao wawekezaji. Kwenye nchi nyingine kama Singapore, India, Ulaya, Marekani...zipo specialised firms zinazotoa huduma ya kuguide serikali zinazo negotiate na wawekezaji complex transactions za aina hii. Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa ku procure services za firm za aina hiyo.
 
Babatunde walau this time umeandika sio kuponda tu, bali pia umepotoa mawazo mbadala ya kujenga na kuboresha harakati za kuendeleza nchi. Kwa mantiki hiyo nafuta comment yangu juu ya mawazo mgando....hai apply kwako.

Nikirejea kwenye hoja zako nzuri.
N kweli kabisa,mipango miji ya halmashauri za jiji na manispaa wamechangia kwa kiasi kikubwa katika sokomoko la foleni za jiji. Hili ni tatizo na linahitaji kuchukuliwa hatua. Uzuri mmoja hata Mkuu wa nchi wakati fulani akihutubia wananchi kule Mabwepande, alisemea suala hili, hasa umuhimu wa kuwa na satelite cities....zenye huduma zote muhimu ili kuepusha misongamano. Wewe umeongeza hoja nzuri zaidi, natumaini wahusika watasoma na kuzingatia maoni mazuri uliyotoa. Bandari ya Dar nayo ina mchango katika ongezeko la foleni mjini.....sio tu kwa maroli yanayotokea kule, bali magari madogo ya wananchi wanaoelekea kufuata huduma kule. Pengine with modernization ya bandari na matumizi ya Teknolojia.....itaweza kusaidia kutolazimu wananchi kwenda kule physically. Kuhusu mji wa Mpya wa Bagamoyo, mpango wa kuujenga kwa kuzingatia mradi mpya wa bandari na EPZ, ni sehemu ya mpango mzima wa mradi huo. Kama umewahi kufika Shenzen.....jinsi ilivyo develop, ndivyo Bagamoyo itakavyokuwa miaka 15 ijayo.

Kuhusu competing ports......wewe una make reference to documents za mpango wa ujenzi wa TPA ambazo haziku take on board other projects zitakazofanywa chini ya makubaliano na mwekezaji...ambayo inajumuisha EPZ, Railways na Expressways toka Dar mpaka Bagamoyo. Pia mpango ule wa TPA ulikuwa unafikiria bandari ya Bagamoyo ni ya ku handle vessels ndogo, wakati mpango wa sasa ni bandari hiyo kuwa ni 4th generation port yenye uwezo wa kuhandle meli kubwa kubwa ambazo kwa hivi sasa haziwezi kuingia bandari ya Dar

Umesema bandari hii ikijengwa kazi yake itakuwa ni kurahisisha biashara ya wachina na mataifa inayofanya nayo biashara. What is wrong with that? Mbona bandari ya Dar hivi sasa inatumika kurahisisha biashara ya Rwanda, Burundi na Zambia na mataifa mengine? Kuna dhambi? Sisi si tunachotaka ni bandari ifanye biashara....kodi zilipwe, ajira zizalishwe, shughuli nyinginezo za kiuchumi ziongezeke? Kama bandari hiyo itatumika kusafirisha bidhaa kwenda china au mahala pengine popote......si ndio biashara imeingia hapo? What more do we need?

Mawazo yako juu ya kuboresha bandari ya Tanga na Mtwara ni mazuri kabisa. Nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Bahati nzuri hata serikali nayo inatambua potential iliyopo kwenye bandari hizo na inayo mipango ya kutekeleza[/QUOTE)

Salama, Thanks for this! Elaboration yako iko poa. Gd day!
 
Mlipaji wa mpiga zumari ndiye mchaguaji wa muziki. Hivi sie wenyewe hatuna vipaumbele hadi aje Mchina kutuonyesha? Kwa utegemezi huu tumeangamia
 
Rais yoweri mseveni ameikaribisha china ikawekeze uganda.sie bado tunamlalamikia kikwete wakati majirani wanatamni kuwapokea wachina.
watanzania ni watu wa ajabu sana.....tukienda ulaya tunasifia sana gatwick na heathrow, au, washington dulles na reagan

lakini hao hao, wanapiga perepete, dar is no longer sufficient kwa mahitaji ya leo, meli zijazo si za kitoto nk
 
Ungeandika kwa KISWAHILI ingeeleweka vema kwa wengi na mchango wako ungekuwa hauna chembe za unafiki kama wale wanaowaambia waumini wao wasile nyama ilo chinjwa na waislamu lengo lao nyuma yao waje wa wale nyama. Ukisema kitu kimaanishe.

Let us look at the Bagamoyo deal in a wider scheme of things.

The choice of building a the largest port in Bagamoyo raises more questions than it answers. Of the three main seaboard ports – the two that is Tanga and Dar have rail access connecting the hinter land and neighboring countries. Mtwara is a natural harbour and is the deepest of the Tanzanians’ seaboard harbours. Mtwarahad a rail which was removed and the materials used to connect central and Tanga lines.

Mtwara port and its hinterland lags behind in terms of development as compared to the hinterland behind Tanga and Dar. Mtwara area is the nave of the now discovered future wealth of the nation. I it is here one begin to question the wisdom of building nation’s biggest port in Bagamoyo.

Recently we heard Statoil of Norway had discovered enough gas to raise considerations for building LNG processing for export purposes. Mtwara being the nave in the gas extraction it would be assumed that gas processing industry would be established in Mtwara necessitating the deepening and expansion of Mtwara port to accommodate large LNG carriers.

Other than gas processing Mtwara is also the logical port of export when the nation start to exploit iron ore and coal deposits in southern Tanzania. It can be added here that with the re establishment of Mtwara rail and its extension to join Tazara railway , this would also ease transportation of Chinese copper from Zambia and/or DRC.

Bearing the above in mind one can see the building of gas pipeline from Mtwara to Dar in a different light. We were told this was for production of electricity in Dar.

This argument fails because:
1)producing electricity near gas source would have cut down the overallcosts,
2)Electricity produced in Mtwara could easily be distributed to surrounding districts accelerating REA activities and joined to the national grid.

The other argument we were given was supply of energy user in Dar. This too can be shown not to carry weight. The current industrial gas users could continue be serviced by current gas providers. The government could provide incentives for future industrial gas users to establish in Mtwara/southern areas thus extending the industrial nodes in otherwise forgotten parts of Tanzania. Future gas needs of Dar, Bagamoyo and Tanga could be accommodated by use of LNG ships and building of gas depots at designated ports. This is what is done everywhere else i.e. Mombasa.

After what has been said one can see the Mtwara-Dar gas pipeline as the first stage in the Mtwara-Dar-Bagamoyo-Tanga (with possible extension to Mombasa) pipeline.

As you are reading this the grapevine is abuzz with construction of JMK airport in Bagamoyo.

IMHO Mtwara other than Bagamoyo deserved the EEZ/bandari deal.

Wonders never cease, but on the Bagamoyo deal, we as Tanzanians have bought a pig in a sack.
 
Naona JK anataka akumbukwe na watu wa kwao kwa kuwaletea bandari!
But a wise man would have deveolped Mtwara port in view of the current oil and gas explorations also find ways on how to use the same port for Iron and Coal projects at Mchuchuma and liganga.
Main factors towards establishing this port is totally selfishness
 
Mshindo ni kweli kabisa katika taifa lolote ipo miradi ambayo lazima itekelezwe na serikali yenyewe, na ipo mingine inayofaa kuvutia uwekezaji. Mfano ulioutoa wa Ethiopia ni sawa kabisa. Labda nikukumbushe tu kwamba hata Tanzania ipo miradi mingi tu mikubwa inayotekelezwa na Serikali bila kusubiri wawekezaji. Mfano ni mradi mkubwa wa kusafirisha bomba la gesi wa usd 1.2 billion. Sambamba na mradi huu, ipo miradi mikubwa ya uzalishaji na usambazaji wa umeme ambayo utekelezaji wake utaanza muda si mrefu. Miradi hii inafanywa na Serikali yenyewe bila kusubiri wawekezaji. Vilevile ipo miradi ya Mkonga wa Taifa iliyotekelezwa kwa fedha za serikali. Leo hii, Serikali ina miradi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 3000 nchi nzima ambazo zote zinajengwa kwa fedha za Serikali bila kusubiri wawekezaji. Ili upate picha tu, urefu wa kilomita 3000 zinaweza ku cover nchi nzima ya Rwanda, Burundi na Kenya combined.

That said, kuhitaji uwekezaji kutoka nje sio dhambi. Nchi zote zilizopiga hatua leo hii....uwekezaji una mchango mkubwa. Angalia Qatar, UAE, Afrika ya Kusini.....hizi ni nchi zimepiga hatua kutokana na mitaji ya uwekezaji kutoka nje. Wote hawa wana rasilimali nyingi tu, bado wamehitaji wawekezaji kupiga hatua. Nchi kama Singapore, imeweza kutoka kuwa nchi ya dunia ya tatu hadi ya kwanza kwa kipindi cha miaka 50 tu kwasababu ya uwekezaji kutoka nje. Ulaya yenyewe, baada ya vita kuu ya pili ya dunia......ilishuka kabisa kiuchumi, lakini uwekezaji wa marekani ndio uliwanyanyua.

Jambo muhimu la kuzingatia ni kuweka sheria, mifumo na taratibu za kuhakikisha uwekezaji unaofanyika unakuwa win-win kwa Serikali na mwekezaji. Na win-win yenyewe kwa upande wa Serikali ni kodi zitakazolipwa, ajira zitakazotengenezwa n.k

Asante tena kwa maelezo mazuri sana. Tunaelekea kukubaliana in principle, lakini shida yangu moja kuu ni hapo kwa RED hapo. Trend ya taifa letu inanishtua sana na kufanya nijiulize hivi ni kwa bahati mbaya, kwa kutokujua au ni kwa makusudi fulani ambayo mimi na wengine wengi hatuyajui?
Waweza kunitajia katika mataifa hayo ya mfano uliyoyataja, ni lipi ambalo lilimpa mwekezaji Reli, Bandari, Migodi ya madini (kwa fasheni ya mrabaha kama yetu), Uzalishaji mkubwa wa nishati, Mabenki (kama NBC),Manufacturing industry (kwa mtindo wa mpe kiwanda chote afanye atakalo) n.k...(nazungumzia njia KUU za uchumi) ? Mwishoni mwa siku nani anaendesha uchumi wetu? "Win-win" situation yetu hii mbona ya kipekee sana? Napata shida!
 
Adili

Theory yako ni nzuri academically, lakini the bottom line ni investor anayeamua kuwekeza, anachoangalia sio factors ulizojikita wewe. Anachoangalia ni mahala ambapo atakapa returns.

Muhimu ieleweke ni investor ambaye ameamua pesa yake awekeze Bagamoyo na sio Tanga, au Mtwara, au Kilwa, au Dar es salaam.

Ingekuwa zinachukuliwa pesa za walipa kodi kujenga bandari.....then hoja zako zingekuwa na mashiko.

What matters ni return of investment....and nothing else

Mkuu Salaama, pengine huelewi kinachozungumziwa.
Investor ni nani na mtaji anautoa wapi?

Tuelimishane kidogo kuhusu Bagamoyo deal.
1)Muwekezaji ni sirikari ya Tanzania.
2)Mtaji wa kuwekeza ni hizo $10b tunazokopa kutoka kwa mchina.
3)Ni walipa kodi watakagharamia mkopo huu
3)Zaidi ya riba juu ya mkopo, masharti mengine ya mkopo huo ni mkandarasi kuwa kampuni ya mchina.

Kwa hiyo sirikari kama mwakirishi wetu (investor), kwa dili hii naona imetuingiza mjini. Bado nasisitiza Mtwara deserved and was better placed for this enomous undertaking.
 
Mshindo......kwahiyo wewe hautaki uwekezaji huo sio? Faida zake hatuzitaki kweli? Nikusaidie ufahamu faida ya uwekezaji huu.......

mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo la viwanda utakuwa na manufaa mengi from day one utakapoanza. Wananchi wapatao 3000 watapata ajira za muda za moja kwa moja katika ujenzi wa bandari na EPZ, wananchi wengine wapatao 2000 na zaidi watapata ajira zisizo za moja kwa moja kama vile Mama Ntilie watakaouza chakula, wenye nyumba zao watakaowapangisha wajenzi, wauza vinywaji, watoa huduma za usafiri-daladala, taxi, maroli ya kusafirisha mizigo n.k

Faida nyinginezo za mradi huo ni kwamba mara utakapokamilika, thamani ya properties zilizopo eneo la mradi na maeneo ya jirani kama vile Bunju,Boko, Mbezi, Tegeta n.k yatapanda thamani na kuwafaidisha wamiliki endapo watahitaji kukodisha property zao au kuzitumia kuwekea rehani kupata mikopo benki n.k

Faida nyingine ni za moja kwa moja kwa Serikali......ukubwa wa bandari maana yake volume ya mizigo itakayopitia hapo itaongezeka ambapo Serikali itaongeza mapato kupitia IMPORT DUTY, customs Duty......bandari itakapokamilika itaajiri wafanyakazi wasiopungua 1000; eneo la viwanda litakapomilika-litawezesha viwanda vingi kujengwa (by the way Mwekezaji ndio atavutia viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuweka viwanda vyao kwenye eneo hilo na tayari ameshapata wawekezaji walio tayari kuwekeza provided kuna efficient port) na viwanda hivyo vitatoa ajira kwa wananchi wasiopungua 50,000 na zaidi.

Kwa faida ya wasiojua kwanini viwanda vingi vitakuja kuwekeza katika eneo hilo:
1) bidhaa zitakazozalishwa hapa Tanzania katika eneo hilo la viwanda zitaweza kufaidi misamaha ya kodi inayotolewa kwa Nchi masikini huko Marekani (Chini ya AGOA); Ulaya (Everything but Arms EBA), Japan (TICAD consession), na China yenyewe iliyotoa msamaha wa kodi kwa asilimia 95 ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania

2) Cheap labour- ukweli ni kwamba toka China uchumi wake umekua, factors of production zilizokuwa zinawa favour zimetoweka....Afrika ndio ina fursa ya kuziba pengo hilo la China

3) Kwakuwa viwanda vingi lengo lao ni kuzalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi- uwepo wa bandari kubwa yenye mtandao mkubwa duniani inakuwa ni kivutio kikubwa kwao.....mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo anao mtandao wa bandari kadhaaa ulimwenguni....wao ndio wanamiliki bandari tano kati ya bandari kubwa kumi duniani....ikiwemo bandari ya Hongkong, Schenzen n.k

Ukiachilia ajira etc.....serikali inaweza kufaidika pia kwa kupata mrahaba (royalty) katika kipindi chote ambacho mwekezaji ataendesha bandari ili kurejesha uwekezaji aliofanya.

La muhimu hapa ni wataalam wetu watakao negotiate mkataba huo kuwa makini na kuhakikisha serikali inapata WIN-WIN deal na hao wawekezaji. Kwenye nchi nyingine kama Singapore, India, Ulaya, Marekani...zipo specialised firms zinazotoa huduma ya kuguide serikali zinazo negotiate na wawekezaji complex transactions za aina hii. Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa ku procure services za firm za aina hiyo.
Nakubaliana na hoja yako. Bagamoyo ipo kati ya Dar na Tanga - yenye maendeleo makubwa sana ukilinganisha na Mtwara. Basi ingekuwa busara kama mradi huu ungepelekwa Mtwara ili nao wenzetu waanze kufaidi tunda - kama wanaofaidi wa maeneo uliyoyataja.
 
Kwani umejuaje kama mwekezaji alitaka Bagamoyo specifically? Hiyo ya kwamba mwekezaji amechagua Bagamoyo ni assumption ambayo imetolewa na mmoja wa wachangiaji hapo juu. Mimi sisemi kwamba kuna kitu kibaya sana kujenga Bagamoyo ila kama lengo la viongozi wa juu ni maendeleo ya Tanzania as a whole, Mtwara ni logical zaidi kuendelezwa kwa sababu ya mambo yanayotarajiwa kutokea pale kwa kipindi hiki na miaka michache ijayo. Mtwara inatakiwa iendelezwe ipasavyo na itatuvuta sisi Watanzania wa sehemu nyingine, kama ambavyo raslimali zilizoko sehemu nyingine za Tanzania zinavyoisaidia Mtwara sasa hivi. Aliyeanzisha mada ameangalia pure logic na wala sio kwamba yuko against maendeleo ya Bagamoyo kama wachangiaji wengine wanavyofikiria. Watanzania walio wengi ambao wametoka mbali kabisa na Mtwara kama mimi watakubaliana na mimi kuwa it's time tutafute maendeleo ya Tanzania nzima na siyo sehemu chache tu kama ilivyo sasa.
hasante mkuu seacliff,
Tukishauri keki ya maendeleo isambazwe kote, tunaambiwa tumetumwa na EU.
 
Hivi mtu akija na kusema anataka kununua nyumba Kinondoni, wakati wewe unanyumba unazouza Kawe, utamlazimisha anunue ya Kawe? Akiamua kununua Kinondoni, atakuwa amemuweka rehani muuza nyumba, simply because hakununua kule unakoona wewe kunafaa?
Hii ni rahisi mkuu namtumbo, mimi nina nyumba Kawe naziuza, mnunuzi anataka nyumba Kinondoni. Itabidi awatafute wanaouza nyumba Kinondoni.
 
Mkuu Kiligo,

Umesema, "Kumbuka kwamba China wana Mkataba wa kuchimba mafuta Sudani ya Kusini na kwa sasa baada ya kuwepo taifa la sudani ya kusini, kuna mgogoro wa kusafirisha mafuta hayo kwenda bandarini mwa Sudani ya Kaskazini" . Hilo tatuzi yake limo ndani ya LAPSSET.
Siamini unamaanisha kutakuwa na pipeline ya kutoka Sudan mpaka Bagamoyo ili crude ipakiwe kwenye meli:smile-big:
 
Ungeandika kwa KISWAHILI ingeeleweka vema kwa wengi na mchango wako ungekuwa hauna chembe za unafiki kama wale wanaowaambia waumini wao wasile nyama ilo chinjwa na waislamu lengo lao nyuma yao waje wa wale nyama. Ukisema kitu kimaanishe.

mooduke sikuelewa hoja yako. Nifafanulie tafadhali.
 
[/QUOTE] :Ni ufafanuzi mzuri ulioutoa kuhusu sekta ya uwekezaji. Si kila kitu serikali inafanya ni kibaya.Inatakiwa serikali iwe wazi kuwaelimisha wananchi nini makusudio yake,faida na ustawi wa jamii.Si wote wako karibu na Ikulu au wamebobea katika uchumi.Kwa maana hiyo uwazi na weledi ndio utayaangaza maisha ya mtanzania.Mifarakano namintafaruku inaletwa na viongozi wanaoshindwa kutetea hoa za serikali, wako katika cabinent kama sanamu.Naunga mkono tubadilike mawaziri wasichaguliwe tu kutoka katika wabunge ila ujuzi wake.
 
Katika karne hii ambayo kila nchi inafukuzia uwekezaji.......kipindi hiki ambacho Djibuti inawakimbilia wawekezaji wajenge bandari kwao; wakati wakenya nao wanawavutia wawekezaji wajenge bandari mpya kwao..... Leo akija mwekezaji anataka kujenga bagamoyo, wewe ukadai hapana aende Tanga.....mwekezaji huyo ataenda Kenya au dijbuti kama sio Msumbiji......that will be an opportunity lost.

Sijasema ujenzi wa bandari hiyo ni zawadi.

Yes, Serikali haiendi kukopa popote kwa ajili ya mradi huo......hivyo hakuna cha riba, wala grace period......pesa yote itatoka kwa mwekezaji kwenye utaratibu wa PPP. Mfano uliotoa wa hiari ya kuondoka na mkeo hauna relevance yoyote, popote katika context hii tunayozungumzia

sidhani kama ni sahihi kumkimbilia mwekezaji asiyefuata matakwa na mahitaji yetu kwavile tu majirani zetu wanamhitaji. ni jambo la busara kujua nchi yetu itanufaika vipi na uwekezaji wa "Serikali haiendi kukopa popote kwa ajili ya mradi huo......hivyo hakuna cha riba, wala grace period......pesa yote itatoka kwa mwekezaji kwenye utaratibu wa PPP" tukumbuke Onyo la mwl nyerere na uwekezaji kwenye madini yetu.
 
Back
Top Bottom