The Arab spring... Mageuzi ya utawala nchi za kiarabu

Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Mkuu siyo arab spring, ni arab uprising. asante.
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?
the very best lesson learned from the arab uprisings ni kwamba... oh! kumbe inawezekana kuviondoa/kuwaondoa madarakani vyama/marais vinavyo/wanao ng'ang'ania madarakani!!.....haswa pale wanaposhindwa kwenye sanduku la kura na kuiba kura...au kusaidiwa na vyombo vya dola/usalama......Pia tunajifunza kuwa nguvu ya umma ina sauti kuliko vyombo vya dola/usalama......kama ambavyo ccm imekua inashinda chaguzi kwa hila nchi hii ya TZ.....Hata wewe ulishasemaga kuwa TZ ina wenyewe..na wenyewe ni CCM.....hili si kweli kwani the arab uprisings zimeonyesha the opposite.....do you get me!!!!..then go tell your seniors..... kwamba its high time they change their old mentalities......let them learn from the arab uprisings........
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Mabadiliko tunayoyaona kwenye nchi ulizotaja ni mazuri kwa wananchi wa nchi husika. Nasikitika umetaja Libya na Misri tu bila kutaja Morocco au Tunisia au hata Algeria ukipenda maana nao **** reforms wamefanya kutokana na kinachojiri kwa majirani zao.

As for Libya na Egypt tunayoyashuhudia ndicho kile tutakachokishuhudia CCM watakapong'olewa madarakani. CCM ni chama dikteta kama alivyokuwa dikteta Gadafi na Mubaraka. Hawa walidhoofisha organs zote muhimu za serikali. Badala ya organs hizo kama Police kufanya kazi za kulinda raia wao walikuwa wakilinda dikteta na vibaraka wake wanaomzunguka kama vile jeshi la IGP mwema linavyolinda chama dikteta cha ccm na wezi wa mali ya umma na wale wanaonufaika na mfumo huo na wewe Nape ukiwemo.

Kule Libya na Misri tuliona hata Benk kuu ya nchi ilikuwa mali ya madikteta kama Gadafi. Hawa waliweza hata kuchota pesa toka hazina ya taifa ili kufadhili uchaguzi wa rais wa ng'ambo kama Sarkozy na hata kutoa bakshishi kwa vyuo va ngambo kama London School of Economics walivyopewa hela na Saif al-Islam. Jiulize alipata wapi hela za kugawa kama hakuchota toka hazina ya taifa.

Siku CCM ikiondoka maumivui itakayotuachia ni mengi lakini ni lazima iwe hivyo kama tunataka kurudi kwenye mstari sahihi. CCM imelea uchafu,wizi, uonevu, undugu, kupendeleana kwa muda mrefu zaidi ya miaka 33 hivyo usitegemee eti ikitoka mambo yatakuwa mororo. Si ajabu tukapita kipindi kigumu kuliko hata Libya au Egypt na lazima watu kadhaa walipie hiyo gharama.

Hivyo Bw. Nape usitutishe kwa mifano ya Libya ama Misri...kinachotokea huko ni sahihi kabisa. Kama nyie mkitaka hayo yasitokee hapa Tanzania bado muda mnayo wa kutuondelea uoza mwingi mlioulea kwa miaka mingi
 
Kwa libwa ni obvious, hali ni mbaya sana baada ya kumuua ghadafi,

Utoroshaji wa mali umekuwa mkubwa sana, wamagharibi wamekuwa wakilinda sehemu za kuondolea mafuta tu, nchi

imegawanyika vipande kuwana baadhi ya maeneo yanataka kujitenga na serikali kuu. Hakuna amani tena na hakuna tena

coverage za vyombo vya magharibi. In short yale ni majuto makubwa kuwahi kutokea.

Kwa upande wa misri bado jeshi lina nguvu na linaendelea ku-manipulate lile vugu vugu la mageuzi, hatuwezi kucomment

much hadi watakapofanya uchaguzi.
 
Viongozi wao walikuwa ni wezi na wasiofuata haki. Misri bado wanatawaliwa na jeshi, Libya ukanda na ukabila unawamaliza na kuwa na amani 100% itachukua muda sana. Tunisia ni mfano mzuri wa jinsi ya kung'oa udikteta. Algeria wamegawanyika nusu kwa nusu na utawala uliopo bado una support kubwa kulinganisha na wanamageuzi.

Bahrain na Syria ukandamizwaji ni mkubwa na inaonyesha jinsi nchi za magharibi zilivyo wanafiki.Morocco na Yemen wana mifumo tofauti ila changes zitakazofanyika nazo bado zitakuwa nusu nusu kutokana na Cultures zao kuwa superior to the government apparatus (Monarchy and Tribal leaders respectively).

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ghafi, Demokrasia yetu inabidi iimarishwe kwa kubadilisha katiba na mfumo wa uongozi (Power of the executive) na kuboresha mahakama zetu kwa kuzipa uhuru kamili na kuhakikisha mahakama kuu inateuliwa na rais na kupitishwa na bunge (mawazo yangu tu), kuuimarisha muungano kwa kuwa na serikali moja, au kuuengua muungano kabisa kwani hii kitu itakuju kutugharimu sana tukikaa kimya. Tusitegemee jeshi au polisi kuzima ari ya wananchi kutaka kujua hatma ya muungano.

Tunachojifunza watu wengi hasa wa CDM hawatakwambia, viongozi wenye mvuto wa CDM wameonyesha si chini ya mara mbili, kutaka kujaribu mabadiliko ya nguvu. Hawana support ya umma kwa hili, na mawazo yao ya kujitenga (divide and rule) hayana mashiko kwa watanzania wengi. Wasubiri uchaguzi wa 2014? na 2015, ila tuhakikishe tuna katiba iliyokubalika na uchaguzi huru utaosimamiwa na tume huru wakati tuna mahakama zinazoheshimika na kukubaliwa na wananchi.

Militancy wanayojaribu kina Lema, Heche, Nassari, Slaa (na Lissu kidogo ingawa ameacha) hazitaatufikisha popote pale. Nitukane unavyopenda ila usinishikie silaha, kwani hujui what I'm packing. Hata mitaani kuna watu wanaanza kuwa too aggressive wakijua wewe ni CCM, let's just stop this nonsense, it's not gonna work.
 
Mkuu siyo arab spring, ni arab uprising. asante.
Ni Arab Spring.

spring (spr
ibreve.gif
ng)v. sprang (spr
abreve.gif
ng) or sprung (spr
ubreve.gif
ng), sprung, spring·ing, springs
v.intr.1. To move upward or forward in a single quick motion or a series of such motions; leap.
2. To move suddenly on or as if on a spring: The door sprang shut. The emergency room team sprang into action.
3. To appear or come into being quickly: New businesses were springing up rapidly. See Synonyms at stem[SUP]1[/SUP].
4. To issue or emerge suddenly: A cry sprang from her lips. A thought springs to mind.
5. To extend or curve upward, as an arch.
6. To arise from a source; develop.
7. To become warped, split, or cracked. Used of wood.
8. To move out of place; come loose, as parts of a mechanism.
9. Slang To pay another's expenses
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?
Fumbo mfumbie mjinga...mwerevu ung'amua. Kwa taharifa yako tumeelewa unakusudia kutoa ujumbe gani.
Sasa ni hivi...watanzania wa sasa hasa vijana,chakwanza tunachokitaka ni kuona nyinyi (CCM) munaondoka
madarakani hayo mengine mungu ataongoza....so acha kuwatishia watu nyau
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Somo tunalojifunza kutokana na Arab spring ni kuwa, daima watawala dikteta/wenye hila (kama wa CCM) hutumia kila mbinu kung'ang'ania madarakani huko wananchi wakiwa hawana la kufanya mpaka wakati watakapokusanya nguvu zao yaani, nguvu ya umma. Kutokana na watawala kupenda kutawala hujenga IMANI POTOFU kuwa wao ndiyo wenye hati miliki ya kutawala. Hili husababisha hata kupindisha matokeo ya kura ili waendelee kutawala. Nguvu ya umma inapochukua nchi daima mvutano huwepo kati ya watawala wa zamani na wapya kama unavyoona Misri na Libya.

Mwisho wa siku mabadiliko haya ni mazuri sana kwa wananchi. Katika nchi kama Tanzania ni wazi kuwa CCM itakapoangushwa nchi hii itakuwa bora sana katika kipindi cha muda mfupi kabisa. Angalia Michael Satta wa Zambia alivyofanya ndani ya siku 100 za utawala wake. Kisha angalia Ghana walivyofanya kuhusu namna ya kutumia vizuri mafuta yao halafu linganisha na uozo wa watawala wa Tanzania kuhusu dhahabu na gesi. Watawala wa Tanzania ya sasa kazi ya kubwa ni kushangaa kwa nini nchi ni masikini!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwani Keil kuna mtu au mahali umekatazwa wewe kuweka hayo ya Senegal na Kwingineko? Ugonjwa wa kutaka niwaze kama unavyowaza umeanza lini? Fungua thread nyingine anzisha hoja yako, kama ina mashiko watachangia, hapa kwa mujibu wako, umesema hatuna tulo jifunza kutoka nchi za kiarabu, period!

majibu yako yanaonesha kuwa kweli umefilisika kichwani. Mbona huendi kwenye hoja wanazotoa wachangiaji unakurupuka kufoka na povu viganjani mkuu? heshima yako iko wapi Nape? Aaagh! Utamu wote wa thread unauharibu mkuu. Mie nilitaraji kuwa utawaacha watu wacomment nawe uangalie usahihi wa mawazo na maoni yao, kumbe unaajihami kiasi hyiki? Your are too weak Nnauye. Too low to be you.
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Nape,
You are being disingenuous. Aren’t you? The people who are supposed to learn from the Arab spring are those who cling to power through corruption and deceit. Please ask them if they have learned anything.Z-10.​
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?
Kwa waarabu nadhani hii ni hatua yao ya kwanza ktk kuutafuta UHURU kama tulivyokuwa sisi enzi za Ukoloni japokuwa wao wamekuwa wakikoloniwa na wafalme wenye asili za kwao. Hivyo kinachotufundisha hapa ni kwamba mkoloni sii lazima awe mgeni, hata jamaa yako anaweza kuwa mkoloni na mbaya sawa na mgeni kiutawala. Kwa mara ya kwanza waarabu wataweza kuchagua viongozi wao kupitia sanduku la kura, kuwawajibisha na kwamba hakuna mtu yupo juu ya sheria. Binafsi naamini itafikia muda hata Malkia wa Uingereza na watawala wengine wote wenye kudai Umungu mtu watapigwa chini. Hii ndio demokrasia tuitakayo hata kama itagharimu maisha ya wapambanaji.
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Japokuwa ni vigumu sana kulinganisha yaliyotokea kwenye nchi za Kiaabuni na yanayoweza kutojea hapa Tanzania, still kuna mengi tuu ya kijifunza. Lakini la muhimu tunalojifunza kutoka Arab Uprising ni kwamba the sovereinty lies in the people and not the government. Kwamba wananchi wana mamlaka juu ya nchi na sio serikali iliyo madarakani. Serikali imewekwa tuu madarakani na wananchi ambao wanaweza kuindoa wakati wowote ule wakitaka.

Tatizo linakuja pale ambapo wananchi wanataka ku-exercise their sovereignty lakini serikali iliyo madarakani inadai ndiyo inayomiliki sovereignty ya nchi. Kama alivyosema JFK "Those who make peaceful revolution impossible, make violent revolution inevitable". The people will use whatever means to exercise their sovereignty kama serikali inawakatalia.

Kwa hiyo cha kujifunza hapa ni kwamba japokuwa serikali inaonekana kama ina madaraka makubwa, wananchi wanayo mamlaka makubwa zaidi tena ya kuondoa hiyo serikali madarakani. Kama ilivyo serikali kuwa tayari kuua ili kuendelea kuwa madarakani, wanannchi nao wako tayari kufa to exercise their sovereignty.

Lingine watu wanataka kuwa na "viongozi" na sio "watawala" kama ulivyoandika kwenye post yako. Waarabu got tired na "watawala" waliodhani ni wanamiliki sovereignty ya nchi husika. Tanzania tunabidi kujifunza hapo, tena kwa kuanzia na maandhishi yako. Hatutaki "watawala" bali "viongozi" ambao wata exercise our sovereignty on our behalf. Wakishindwa tunawandoa bila zengwe na kuwakabidhi "viongozi" wengine. Vinginevyo, a "violent revolution will be inevitable".



Is the change we are seing for better?

Nafikiri madhumuni ya kuanzishia hii thread yako kwenye hii sentensi. What better changes unazoziongelea? People can exercise their sovereignty for good or bad. Ni haki yao. Wape tu haki yao. How they are going to use their rights, is none of your business. They can do whatever they want to do with their sovereignty. Kama alivyosema jmushi1 hapo juu "Listen to the people, period. Kama wako wrong ama right, hilo ni juu yao na Taifa lao" na sio wewe kiongozi.

What you may see as not a better result of the peoples' exercise of their sovereignty, wao wanaweza kuiona ni better change. Kwa mfano, huyo mama Mtunisia kwenye video hapo chini, kwa sisi wabongo tunaweza kumwona kama ni kichaa fulani hivi, lakini kwake, anachofanya means a lot to her. Kwa miaka zaidi ya 20, she has never been able to stand on the pavement of her street road in her own country to exercise her freedom of expression. That in itself is a better change for her.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom