Thanks Rubi,....Thanks God!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Thanks Rubi,....Thanks God!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Eng. Smasher, Jan 20, 2011.

 1. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kutoa maada kuhusu dawa ya KIKOHOZI tatizo lililokuwa linamsumbua ndugu yangu!
  Rubi alitoa ushuhuda wake mwenyewe na kuanza kuufanyia kazi!!

  Kwa kweli MUNGU ametenda miujiza sasa hivi huyu ndugu yangu ameanza kuacha kukohoa bila kutumia dawa zaidi ya KUNYWA MAJI MENGI awezavyo na MATUNDA!!

  Ahsante Rubi MUNGU akubariki na wana JF wote!!!
  BIG THANKS kwa GREAT THINKERS!!!
   
 2. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi ndo RUBI alivyonielekeza!!

  hUYO INAWEZEKANA AKAWA ANA ALEJI AU MZIO. SO inabidi ajue ni kitu gani knasababisha hiyo hali. binafsi niliwahi kupatwa na tatizo la kikohozi balaa tena kile kikavu haswa, karibia miaka miwili mfululizo si usiku si mchana, si natembea si nimekaa nilikuwa nanijona si mimi maana nilikuwa nakohoa mpaka kutapika nikipanda kwenye daladala Naomba Mungu nikohoe lakini niisitapike hiyo shida niliyokuwa napata nilikuwa siachani na mitandio kila niendapo nikiwa kwenye public sina amani kwa ajili ya kikohozi ila nilichoshukuru Mungu Kifua kilikuwa hakiumi kila nikohoapo na mwili wangu ulikuwa mzuri tu na shughuli zangu nafanya kama kawaida kazini shuleni n.k Shida ilikuwa ile kukokoa bila breki kama ningekuwa na maumivu ya kifua basi ingekuwa ni stori nyingine.

  Nilipimwa kila aina ya vipimo unavyojua lakini nilikuwa niko ok. Watu waliokuwa karibu ndo wanajua mateso niliyokuwa nayo ila pia niligundulika na aleji kali ya vumbi. Sasa dawa za hospitali nilikunywa za kila aina kuanzia za aleji, vikohozi za maji, vidonge lakini wapi mwishowe nikasema aah dawa zitaniua maana hakuna mabadiliiko wala nafuu nikaamua kuacha kunywa dawa na kujikabidhi kwa Mungu nilisema ndiye awezaye binadamu tumeshindwa. na Dk. mmja akanishauri kunywa tu maji kwa wingi uwezavyo ili koo liwe linalainika ila sasa nikaamua kitu kimoja kuwa nakula matunda kwa Wingi kila aina ya matunda ninayoweza kupata.

  Lazima kila siku nihakikishe nimekula matunda i.e, mapapai, mananasi, matango, machungwa n.k tena yote nayachanganya nakula mpaka najisikia nimeshiba matunda chakula nakula baadaye. Kitu kingine nakunywa maji kwa wingi kila siku nahakikisha maji hayapungui lita mbili na zaidi kwa siku mpaka tatu, juisi ya vitunguu swaumu, saladi ya vitunguu maji, asali ndimu n.k yaani ili mradi nihakikishe hivi vitu kila uchao navipata. Basi taratibu ile frequent ya kukohoa ikawa inapungu wakati mwingine ikawa naweza shinda asubuhi mpaka jioni labda nimekohoa mara moja au mbili na usiku ni hivyo hivyo nikaanza kulala vizuri na kujitahidi usafi wa ndani kusafisha mavumbi kila siku niwezavyo mara nikaona tu Kikohozi kimeacha sikohoi tena yaani nakwambia niliona kama miujiza kwa kweli Mungu yu mwema. siwezi kusahau.

  Ndo mana nimeguswa na tatizo lako binafsi siwezi kujua kipi ndo kiliniponyesha ila mchanganyiko wa mboga na matunda naamini kwa Uweza wa Mungu vilinisaidia sana. Pengine wakati pia unapokea ushauri wa watu na wataalamu hapa janvini nami ushauri wangu ni huu:-

  Kama huyo rafikio hana TB mwambie aende kwa specialist apimwe aleji then akijua na aleji ya nini inakuwa ni rahisi kijilinda mwenyewe maana kuna watu huwa wana aleji ya vumbi kama mimi, nyama ya aina fulani au aina moja wapo ya chakula ambacho pia hupelekea mtu kukohoa sana. Pia ajitahidi kula mtunda na mboga kwa wingi kadri awezavyo ili kupata vitamini C kwa wingi bila kusahau maji mengi kila siku. Amtangulize Mungu ndiye kimbilio letu daima. Atapona tu kwa uweza wake.
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  nice being grateful.......big up for ya!
   
 4. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Safi sana, Mungu na JF washukuriwe. Ingawa wengine wanafikiri JF ni sehemu ya porojo na siasa, actually kuna faida nyingi sana ktk kila sector na hasa hii muhimu na nyeti ya afya. Ni baada ya kusoma faida za vitu kama asali, nilianza kubwia asali kama mwendawazimu, na you can tell the difference, mafua, kichwa, tumbo (unakunya kwa raha mustarehe bila kutoka mijasho na kuguna kama unatoa mawe) na magonjwa madogo madogo kwishnei. Unalala na kuamka so fresh !! again, big up all JF members...
   
 5. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu,JF ni kweli ma GREAT THINKERS!!

   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni wachache sana wanaorudi kushukuru!
  Engineer, ithink thats Social Engineering!
   
 7. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Yeah PJ, Engineering sio Solid Mechanics na thermodynamics tu, siku hizi Engineers wako social sana.
   
 8. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Maandiko PJ, "SHUKURU KWA KILA JAMBO"
  Hata Engineers 2naamini maandiko ingawa sio WATUMISHI!!!

   
 9. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yap hapo umenena M!! kuna Soft Engineers siku hizi!!

   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  INJINIA SMASHA,
  unaniudhi sana vile unavyojifananisha na ST. RR kwa kila kitu
   
 11. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh!! Huyo ST.RR ndo nani TEAMO??!!
  Najifananisha vipi na huyo mtu??!! Hebu rudi UDADAVUE hapa!!!

   
 12. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Eng. Smasher. Mungu ashukuriwe. Na namuombea huyo nduguyo Mungu ajiinue kwake na amponye kwa uweza wake arudi katika afya njema. Vile vile asiache kumshukuru Muumba maana ndiye muweza yote na kimbilio letu sote.

  Ushauri kwa nduguyo ajitahidi sana kuwa makini kwa vyakula na mazingira yanayomzunguka. akiweza kupunguza matumizi ya vitu kama sukari na akawa anatumia asali mbichi ni vizuri sana pia kupunguza mafuta mengi kwenye chakula na apendelee kutumia mafuta ya mimea kama soya, alizeti n.k, na pia kupendelea kula vyakula halisi (visivyozindikwa)kama matunda fresh, juis fresh, n.k nafikiri ataona mabadiliko mwenyewe.

  Asante sana kwa kurudi kutupa 'feedback' ya maendeleo ya nduguyo. Ubarikiwe.
   
 13. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanks Rubi!!
  Nashukhuru kwa msaada wako wa mawazo,nitaendelea kuutumia ushauri wako.
  MUNGU ametenda MIUJIZA sasa hivi hasumbuki kukohoa sana.
  Anasema anaendelea KUPONA kabisa.
  UBARIKIWE NA BWANA.

   
Loading...