Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,805
- 43,230
Habari za weekend tulivu wapendwa, tumemaliza kupata staftahi nimepitia magazeti ndo nagundua kumbe leo ni Nyerere Day.... So happy Nyerere Day to everyone out there.
Iko hivi kuna kazi nilikuja kuifanya mwanzo wa wiki hii na jumatano ilikuwa nirudi kazini. Sijui kilichonichelewesha nikajikuta hadi alhamis bado niko Dar, usiku wa kuamkia ijumaa saa sita na nusu napokea simu kwa namba ya bongo ambayo sijaisave.... Napokea ni sauti ya mwanaume ananiambia mambo Kasie, hujalala kumbe hadi saa hizi, sikumuuliza wewe ni nani maana sauti ilikuwa tamu kuendelea kuisikiliza.... Akasema niko getini hapa kwa walinzi njoo uwaambie wanifungulie mmhh nilivopigwa na butwaa nikawa naelekea getini nikamtambue huyo mgeni wangu wa usiku huo ni nani, nikamjibu haya nashuka in few minutes ntakuwa hapo.
Akanitukana na tusi kubwa tuu kama mara tatu hivi kisha akaniambia ndo ameingia usiku huo na hapo yuko hotelini sio getini kwangu kama nilivoamini na hapo ndo nikagundua ni nani......
Nikajikuta napiga uyoweee mkubwa wa kufurahia ujio wake, bad you sasa unakuja ghafla what if ningekuwa kazini SA, akaniambia asubuhi ningechukua SAA na tungekutana Cape Town Fish Market..... Hapa nikaangua kicheko kikubwa na tusi juu maana kuna kahistoria kuhusu Cape Town. Sasa Papitoo ujio huu wa ghafla hivi niaje, au baba mkubwa Madata ameshakutafutia mke kijijini ndo umekuja kimya kimya kuchukua jiko lako uachane na ukapera? Najua baba mkubwa siku nyingi anakusumbua kuhusu kuoa....
Akaniambia hii safari nimekuja mahsusi kwa ajili yako, nimekumiss Kasie na sikujua kama uko Dar, hapa niko hotelini na nikasema nikupigie namba yako ya TZ usipopatikana ningekucheki wasap kisha asubuhi ningekufata SA. Daaah nikahema kwanza, akaniwahi saa hizi wee lala ila saa tano asubuhi ijumaa ambayo ni jana niende hapo Hyatt Hotel zamani Kempisk.
Hehehehheheee Babacitaaaa, Kasie adores you, acha nianze kusimulia kilichotokea....
Saa tano niko pale mapokezi Kempisk nampigia anakuja kunipokea tunakaa yale makochi ya pale chini kwa salamu na habari hoja mchanganyiko kedekede...
Basi maongezi yakanoga muda wa mlo wa mchana ulipofika tukapanda juu kushiriki pamoja....
Ndani ya Oriental Cuisine bufee na desert zilinifurahisha.... Nnavopenda kula sasa ...... Papito akaniambia wee kulaa unone baadae na mie nile nifaidi aahahahahahahaa yaani Papito anapenda matusi kunizidi looh.
Basi baada ya mlo wa mchana tukakaa eneo la juu pembeni ya Oriental Restaurant maongezi ya hapa na pale huku ka wine kanashuka hadi mida jioni hivi.
To cut the story short, hapa ndo tunajiandaa ku check out.... Babacita anaondoka leo kurudi alikotoka. Kiukweli asante sana Papito kwa huu mtoko, ma care yako yameniacha hoiii....
Wapendwa mtusamehee tuu, Kasie na Babacita tuna element za kihaya....
Sio hela nyingi ukizibadili kwenda kwenye hela ya kitanzania, ila hela ya kigeni ukiishika na ukiwa nayo kwenye pochi yako ina raha yake....
Pesa ya malkia.....si kuwa ndo nazishika mara ya kwanza au sijawahi kushika zaidi ya hizi hapana, ila zawadi au pessimistic ya kupewa ina utamu na raha yake hata ikiwa shilingi mia tano....
That's not all, of course there's more...
Thank you Babacita Papitoo.... Mmuahh!!
Kasie loves you more and more.
Kasie Mahaba Matata.