Thanatophobia: Hofu ya kifo na sababu zake

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
23,326
69,565
ArtTfEc9_400x400.jpg

Thanatophobia ni neno la kitaalamu lenye maana 'hofu ya kifo' (fear of death). Ukweli ni kuwa watu wengi kama sio karibu wote wanaogopa kufa. Baadhi wanaogopa ile hali ya kuwa mfu wakati wengine wanaogopa kile kitendo cha kufa (actual act of dying).

Hizi ni sababu mbalimbali zinazochangia kwa kiasi kikubwa binadamu kuwa na thanatophobia.

1. Mchango wa Imani/Dini.

Kwa watu wengi thanatophobia inahusishwa zaidi na dini/imani zao. Baadhi ya watu wanafikiri kuwa wanatambua ni nini kitatokea baada ya kufa kwao, lakini mda mwingine wanakuwa na mashaka kuwa labda hawajui ukweli. Wengine wanaamini kuwa wenye 'dhambi' watahukumiwa milele kwa kuchomwa moto jehanamu.

Kwa upande huu mtu hujikuta akiwa njia panda kutokana na kukosekana kwa ushahidi juu ya habari zinazohubiriwa kwa watu wenye kuamini masuala ya 'mungu', shetani pamoja na mbingu na moto.

2. Hofu ya Yasiyojulikana (Fear of the Unknown)

Thanatophobia inaweza kuwa na mizizi pia katika hofu ya mambo yasiyojulikana. Kiasili binadamu sisi ni wadadisi na tunapenda kufahamu ukweli juu ya mambo na nadharia mbali mbali zinazotuzunguka. Lakini mpaka leo hii hakuna yeyote aliyeweza kueleza kwa ushahidi wa kisayansi ni nini hutokea baada ya kifo, ni jambo ambalo hakuna binadamu awezaye kulieleza akiwa hai bado.

Zaidi kumekuwa na dhana zakufikirika ambazo zimekuwa zikienezwa kulingana na imani/dini za waamini. Mfano imani nyingi zinafundisha kuhusu moto na paradiso kwa watenda mabaya na mema respectively.

Hivyo hali ya kutojua kuwa hatima yako ni nini baada ya kuondoka hapa duniani hufanya wati wengi kuwa na uoga sana juu ya kifo.

3. Hofu ya Kupoteza Udhibiti (Fear of Loss of Control)

Kama tujuavyo mara nyingi binadamu hupenda kuthibiti matokeo ya mambo ayafanyayo, kwamba anajua kuwa akifanya jambo fulani matokeo yake yatakuwa kitu fulani. Anaweza kupanga kuwa wakati fulani nile, wakati fulani nilale, wakati fulani niingine JF n.k.

Lakini kitendo cha kufa ni kitu ambacho hakuna binadamu mwenye uwezo wa kukidhibiti. Hii nayo inakuwa ni sababu kubwa inayofanya watu kukiogopa kifo kwakuwa hawawezi kujua kitawafika sangapi na kwa style gani.

Tutofautishe uwezo wa wanasayansi wa kutibu maradhi na kusaidia kuongeza siku za kuishi na uwezo wa kupanga siku au wakati wa kufa na aina ya kifo. Pamoja na kuwa juhudi na rasilimali nyingi zinaweza kutumika kukikimbia kifo lakini mwisho kifo hushinda na hakuna ambae ameweza kukiepuka na ambae ataweza kukiepuka.

4. Maumivu na Magonjwa

Baadhi ya watu wenye uoga wa kufa hawaogopi kifo kama kifo lakini mazingira yanayopelekea kifo yaweza kuwa ndio sababu kubwa ya hofu. Wanaweza kuwa wanaogopa maumivu makali watakayopata wakati wa kufa (mfano katika ajali mbaya kama za moto au kuzama katika maji) au kuugua magonjwa yasiyotamanika na yanayoua kwa haraka (mfano ebola).

Watu wengi wa namna hii huathiriwa pia na nosophobia ambayo ni uoga wa kuambukizwa magonjwa, hypochondriasis ambayo ni uoga na obsession juu ya uwezekano wa kupata magonjwa ambayo hayatibiki (undiagnosed medical conditions).

5. Hofu Kuhusu Familia, Ndugu na Jamaa

Inasemekana pia kuwa watu wengi wenye hofu ya kifo hawakiogopi zaidi kifo bali wanaogopa hali watakayo waachia wapendwa wao ikiwa ni pamoja na familia, ndugu na jamaa zao.

Hali hii huwatokea sana wazazi wapya (walipata mtoto siku sio nyingi), single parents na walezi wakutegemewa. Hofu kubwa huwa labda watakaowaacha watapata shida (financially) au labda hakutakuwa na mtu wakuwasaidia pindi wao watakapofariki.

Hali hii pia kwa mazingira yetu ya watu weusi jinsi tusivyo na utu inachochea zaidi kutokana na jinsi tunavyoona mayatima wakinyanyasika kila mara au ndugu kugombea mali za watu waliokufa na wale waliostahili kunufaika nazo wakikosa haki zao.

Baadhi Ya Hofu Nyingine Zinazohusiana na Kifo

Ni kawaida pia kwa watu wanaoogopa kufa kuwa na uoga na vitu vinavyohusiana na kifo kama vile maiti, makaburi, majeneza, magari ya kubebea maiti, mortuary, picha za watu waliokufa n.k. Hii ni kwasababu vitu hivi huwakumbusha zaidi hofu yao kuu ambayo ni kifo. Aina hii ya uoga kitaalamu inaitwa necrophobia.

Hitimisho

Kuna msemo maarufu unasema "the only two certainties in life are taxes and death" kuwa kuna vitu ambayo hutaweza kuvikimbia navyo ni kifo na kodi. Haijalishi kama utavipenda au hautapenda lakini you have to come to terms with them either way.

Nadhani kitu kikubwa ni kukubali kuwa kama tulizaliwa basi kuna siku tutakufa na kifo hakikwepeki. Kutokana na kifo kuwa hakiepukiki na hakijulikani kitatokea mda gani ni vizuri kujiaanda kisaikolojia na kiimani pia. Kujiandaa ni kukubali kuwa lazima wewe au hata wale unaowafahamu lazima mtaonja umauti wakati fulani usiojulikana.

Kwa wenye imani ni vyema kufuata mafundisho ya imani zenu juu ya kifo. Kama ni kutubu na kutenda mema kwa ahadi ya kurithishwa pepo na uzima wa milele mtu ukiwa umejiandaa wala hutaogopa kifo. Kwa mtizamo huu utagundua wengi wanaaogopa kufa ni watu waovu ambao kwa namna moja ama nyingine hawajajiandaa kabisa na safari yao ya mwisho.

Katika Buddhism tunaamini kuwa matendo yako wakati ukiishi (karma) ambayo unayafanya kwa kusudi (cetana) ndio yata determine hatma yako mbeleni katika (samasara) cycle ya kuzaliwa upya 'reincarnation' mpaka utakapokuwa enlightened na ku achieve "nirvana" (blowing out).

Hivyo namna unavyoishi maisha yako ya sasa ndivyo itategemea samrasa yako itakuaje. Kwamba ukiwa na karma nzuri (kutokana na maisha mema na matendo mema hapa duniani) basi huna haja ya kuhofia kifo kwakuwa una uhakika wa maisha mazuri zaidi kwenye after life.

Mafundisho haya kwa uelewa wangu wa imani nyingine hayatofautiani sana zaidi labda kwenye life after death. Imani zote zinafundisha waamini wake kutenda wema na kujilibikinzia thawabu jambo ambalo litawafanya kurithishwa paradiso huko mbinguni.

Kwa mtu yoyote mwenye maisha mema hapa duniani hana haja ya kuogopa kifo bali ni kujiandaa tu na kuwa tayari kuondokewa na wale uwapendao au hata wewe mwenyewe wakati wowote na kwa nja yoyote.

Je wewe ni sababu gani inayokupelekea kukiogopa kifo?

Memento Mori - Remember You Must Die.
 
Watu wenye uelewa na mambo ya spiritual huwa hawana kabisa hofu ya kifo kwa sababu wanaelewa exactly kifo ni nini. Namkumbuka mentor wangu mmoja, Munga Tehenan, alikuwa akisema raha ya nafsi inapoingia kwenye blissful state (kuonja mauti) huwa inaizidi raha unayoipata unapofikia mshindo wakati wa tendo, total peace, total freedom and great state of the spirit.
 
Ni kweli mkuu, na hofu hii ni wachache sana wanaweza izuia. Nina rafiki yangu mmoja wa kike anaogopa kufa balaa..basi mimi huwa namtania, basi anakosa amani hadi machozi yanamlenga.
Sasa je kwanini usimsaidie ili aweze kukubaliana na ukweli kuwa kuna siku tu atakufa. Afate maelekezo ya imani yake ili awe tayari amejiandaa wakati wote?
 
Watu wenye uelewa na mambo ya spiritual huwa hawana kabisa hofu ya kifo kwa sababu wanaelewa exactly kifo ni nini. Namkumbuka mentor wangu mmoja, Munga Tehenan, alikuwa akisema raha ya nafsi inapoingia kwenye blissful state (kuonja mauti) huwa inaizidi raha unayoipata unapofikia mshindo wakati wa tendo, total peace, total freedom and great state of the spirit.
Hapo kwenye raha wakati wa kuingia umauti ndipo penye utata kwakuwa sidhani kama Tehenan anaweza kuthibitisha hilo.
 
View attachment 1043896

Naogopa kufa kwa sababu, hakuna proof inayothibitisha 100% kwamba binadamu akifa anaenda wap? Ni kama Mche unavyochipua kutoka kwenye Mbegu, hauwezi tena kurudi na kuwa Mbegu. Hivyo hivyo kwa Mwanadamu, maadamu amezaliwa basi atakufa.
 
Watu wenye uelewa na mambo ya spiritual huwa hawana kabisa hofu ya kifo kwa sababu wanaelewa exactly kifo ni nini. Namkumbuka mentor wangu mmoja, Munga Tehenan, alikuwa akisema raha ya nafsi inapoingia kwenye blissful state (kuonja mauti) huwa inaizidi raha unayoipata unapofikia mshindo wakati wa tendo, total peace, total freedom and great state of the spirit.
Kuna kitu umenikimbusha kuhusu huyu guru
 
Naogopa kufa kwa sababu, hakuna proof inayothibitisha 100% kwamba binadamu akifa anaenda wap? Ni kama Mche unavyochipua kutoka kwenye Mbegu, hauwezi tena kurudi na kuwa Mbegu. Hivyo hivyo kwa Mwanadamu, maadamu amezaliwa basi atakufa.
Mkuu kwani wewe huna dini? Huna imani na mafundisho yanayotolewa na dini yako?
 
Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom