Thamani ya Upekee

David Mabullah

New Member
Jul 14, 2021
1
0
THAMANI YA UPEKEE

Jiwe alifanya mara zote kitu cha kipekee hakuwa na hali ile ya kupenda kufanya jambo ambalo wengi walijaribu kufanya au kufanikiwa. Watu wengi upenda kufata njia ya wengi ila sio kwa Jiwe alikua wakipekee sana, tokea wakati alipokua akisikia juu ya njia ile wapitao wengi nakujaribu ipita na asipate anacho itaji.

Wakati Jiwe alipo anza safari ya utafutaji mali na kipato alijihusisha na shughuli mbalimbali. Alianza kwa kufanya biashara tofauti-tofauti ambazo wengi walikua wamekwisha anza zifanya nakuwanufaisha na wengine wakiendelea kujiunga akiwemo Jiwe, tena kwa imani kubwa atafanikiwa kama ilivokua kwa watungulize wake, zaidi alijikuta akiweka mtaji unapotelea kwenye hiyo biashara. Jiwe ulifika wakati ule wa wengi wakukata tamaa na kujikuta akitawaliwa na maswali Mengi yakiitaji majibu.

Jiwe alipokua amewekeza kwenye kilimo alianza kupata baadhi ya majibu ya maswali yaliokua yamemtawala, likiwemo kwanini sipati kufanikiwa ilihali najitahidi kupita/kufanya kile wengine wamefanya na wamefanikiwa.

Jiwe alipata rafiki alieitwa Kigozi, ambaye alishirikiana naye katika mengi ikiwemo ushauri, na msaada. Siku moja Kigozi alimsauri Jiwe walime mazao ambayo soko lake sio kubwa au hayaitajiki sana sokoni, ukilinganisha na la mazao mengine wakati huo wanapanga kulima, wakaafikiana kulima kwa uchache zao hilo, ulipo fika wakati wa mavuo zao walilokua wamelima wao tena kwa uchache lilikua na bei nzuri sokoni tena linaitajika sana.walipo panga kulirudia kulima kwa wingi awamu nyingine ili wanufakie nalo zaidi walikuta soko limeshuka yani bei aikuwa kama awali na kujikuta aliwanufaishi tena kama Mara yakwanza.

Jiwe baada ya hicho kilichomtokea awali kwenye kilimo cha mazao akiwa na Kigozi aliamua kufanya kitu cha kipekee ambacho hakuna aliewahi kifanya au kukiwaza kwa wakat huo tena alioneka kanakwamba amepoteza akili. Alilima matiki-maji hekali mbili za shamba ambalo alikua anamiliki yeye pasipo kuweka zao jingine lolote, kwa wakati huo Jiwe akitegemea soko hilihilo dogo analolijua akitegemea litamlipa hata kwa hela kidogo, wakati wa kuvuna alivuna nakuuza rejareja kwa kukata vipande vipande, mteja mmoja baada yakununua kipande kimoja kisha kukila, akauliza unatoa wapi tikiti-maji hili nimevutiwa nalo sana,

Jiwe akajibu akisema nimetoa shambani kwangu,

Mteja akauliza waweza niuzia yote haya pamoja nayalioko shambani?

Jiwe akajibu akisema bila shaka twaweza fanya biashara kama tukiafikiana vyema.

Baada ya hapo Jiwe na Mteja walienda shambani kwa Jiwe, ndipo Mteja akamwomba jiwe kuyanunua matikiti-maji kwa bei ambayo akutarajia Jiwe, ilikua ina mlipa Mara dufu ya ile aliokua anaitarajia yeye ataenda kuuza sokoni anapopajua.

Mwaka ulofuata watu wengi waliekeza kwenye matikiti-maji wakitegemea wanufaike kama Jiwe, ila Jiwe kwa kua aliona thamani ya upekee aliwekeza katika kilimo cha vitunguu maji ambavyo apakua na mwingine alikua analima kwa wakati huo pale alipokua amewekeza na kujikuta akinufaika tena zaidi na kumfanya kumiliki mali nyingi na kujihakikishia kipato cha uhakika

Kwahiyo Jiwe anajivunia sana katika kufanya jambo au kupiga hatua ya kipekee nakuweka alama kama mfano wakuigwa kutokana nakupenda kufanya jambo kwa upekee. Kuna thamani na faida katika upekee wakati wakufanya jambo haijailishi ni wakati gani.

*Asante

#toteachistolearn
 

Attachments

  • Thamani ya upekee story.docx
    8.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom