Thamani ya mwanamke

Love Doctor

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
726
786
Thamani ya mwanamke

Mwanamke ni mtu wa thamani katika jamii. Kuachwa kwa majukumu muhimu ya mwanamke kumechangia mahali pakubwa kwa kudorora kwa maadili ambayo tunayalalamikia leo jamii inaharibika au kujengwa kutokana na aina ya wanawake katika sehemu hiyo.

"Taifa ambalo wanawake wako nyuma kielimu ni wazi kwamba Taifa hilo halina maendeleo," Hayati Mwalimu Nyerere mwaka 1984.

Ni muhimu mwanamke kupata elimu ili kutengeneza familia na jamii inayojitambua

Mwamke ndio mlezi mkuu wa familia
Hakuna familia bila mwanamke, yeye ndio mlezi mkuu wa familia. Wahenga husema "Mtoto mbaya ni mzigo wa mama yake," leo tumeacha utamaduni huu na matokeo yake familia zetu zimekosa malezi bora kwa kubeba sera na tamaduni zisizotuhusu.

Mama ametukuzwa na vitabu vyote kwa malezi yake;

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾

Na tumemuusia ihsani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; Kwangu ndio mahali pa kuishia. [Luqmaan: 14].

Mwanamke ndio mchunga
Mwanamke ndio mchunga wa mali za mume wake na nyumba, hapa siku hizi kumekuwa na biashara ya kuolewa na kurithi mali, wengine huua hadi waume zao! Wanawake wao ni wachunga na asili yao ni kulazimiana na nyumba zao kwa amri za waume zao.

Mwanamke ni mshauri
Mwanamke humshauri mumewe katika mambo mbalimbali, akili ya mwanamke huwa tulivu tofauti na mwanaume, nyumba ya wasioshauriana hawawezi kufaulu.

Mwanamke ni kitulizo kwa mwanaume
Mwanamke ndie pekee wa kumtuliza mwanaume awe katika ghadhabu, huzuni au furaha. Mwanamke anaweza kuleta mapinduzi makubwa kutokana na nguvu kubwa ya ushawishi aliyonayo.

Mwanamke ni msaidizi
Mwanamke ni msaidizi kwa mwanaume katika huduma mbali mbali kama kumpikia, kumfulia n.k.

Thamani ya mwanamke ni kubwa na wala hatuwezi kuipima kwa mambo hayo pekee. Unapotaka kutengeneza jamii yoyote tengeneza mwanamke na unapotaka kuharibu jamii haribu mwanamke pia.

Abuuabdillah
0744883353
 
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾
Ni nini hiki?
 
Back
Top Bottom