TGNP, TAMWA, katika usingizi mzito wa pono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TGNP, TAMWA, katika usingizi mzito wa pono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by che wa Tz, Jan 6, 2012.

 1. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Habari zenu waungwana.
  ":..........Saudi Arabia yapiga marufuku wanaume kuwauzia na kuuza chupi na sidiria kwa wanawake kama njia ya kutunza maadili na heshima ya wanawake..." Hii ni katika habari iliyonifurahisha sana asubuhi ya leo. Waungwana najua mnajua kuwa hapa nchini kwetu kuna vyama na mashirika mengi ya kutetea haki za wanawake, na kwa hakika mashirika haya kwa kiasi kikubwa yamefanya kazi wanayostahili kufanya. Pamoja na mashirika, na NGO's hizi kujitahidi kutetea haki za mama zetu na kutunza heshima zao, lakini wakati mwingine mashirika haya kwa kiasi fulani yamekuwa kama vipofu na kusahau mila na desturi ya WaTz na Afrika kwa ujumla haswa juu ya maadili na heshima kwa mama zetu hawa na kushindwa kutetea heshima yao katika jamii na kuachwa wakidhalilishwa na wafanya biashara wa nguo pale kkoo na penginepo kwa kutumia MIDOLI ambayo huwaacha uchi dada zetu, bibi zetu na mama zetu kwa namna MIDOLI hii inavyorandana na maungo halisi ya mwanadamu mwenye jinsia ya kike. Waungwana, si ajabu sana siku hizi kupita kkoo na kukuta MIDOLI hii ikiwa imevalishwa nguo za ndani za kike kama chupi na sidiria pasipo kusitiriwa na vazi lingine. Wakuu, nadhani mnajua ni kwa kiasi gani haya mamidoli yalivyo tengenezwa na kuwa na mvuto midhili ya binadamu wa ukweli na mbaya zaidi Maduka mengi pale kkoo yanahudumiwa na jinsia ya ME. Waungwana sitaki kuongea mengi mno kwasababu huwa siku zote naumia kwa kufikiri ni wapi wadogo zetu na watoto wetu wanapelekwa, na je kizazi chao kitakuja kuheshimu na kuwathamini wanawake kama walishaanza kuwaona walivyo tangu wakiwa wadogo? TGNP, TAMWA , wizara ya jinsia na wanawake, hebu amkeni bhanaaaaa na kupinga huu udhalilishwaji wa hadharani wa mama zetu..............."kusoma hamjui!, hata picha pia hamuoni!"
  Natoa hoja
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,471
  Likes Received: 4,747
  Trophy Points: 280
  Hii siyo hoja ya kisiasa mkuu
   
 3. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wako bize wanaandika proposal ili wapate pesa
   
 4. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mwenye mamlaka ya kupinga na kufungia matumizi ya MIDOLI hii ni wenye mamlaka kisiasa
   
Loading...